Watu 18 wamefariki dunia papo hapo, katika ajali ya gari Wilayani Mufindi katika barabara Kuu ya Iringa-Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema kuwa Coaster ilikuwa inatokea Dar kwenda Mbeya
Aidha, amesema kwa taarifa za awali chanzo cha ajali hiyo ni kulikuwa na lori lililoharibikia barabrani na dereva wa Coaster hakuchukua tahadhari akaligonga lori hilo hali iliyosababisha kupatikana kwa majeruhi
Ameongeza kuwa wakati majeruhi wanaokolewa likaja lori jingine likawagonga tena waliokuwa wameanza kuokolewa na hivyo ajali ikawa mara mbili
Kuhusu majeruhi amesema wapo ila hajapata idadi kamili
View attachment 2255971
View attachment 2256046
Source:
ITV
====
Eneo ambalo ajali hiyo imetokea, ndilo ambalo basi la
Majinja liliangukiwa na lori mwaka 2015 na kuua zaidi ya watu 40