Mufindi: Watu 18 wamefariki katika ajali ya Coaster na lori

RPC na RTO wawajibike kabla ya saa 4 Leo asubuhi. Otherwise IGP akapumzike tu. Tume tumechoka kupoteza ndugu zetu​

Yaani ulevi wa madereva ndio ufanye hao viongozi wawajibike, yaani mtu katoka nyumbani kwa lengo la kuua watu halafu awajibike/wajibishwe mtu mwingine
 
Mkuu 'kicheche' ina maana gn?

kicheche ni neno la kihuni linatumiwa na madereva dhidi ya magari yanayoharibika barabarani na kutokuwa na alama yeyote...

kwa hiyo huyo mwenye Coaster alipiga kicheche na mwenye lori tena akaja akapiga vicheche viwili....

ukisikia kupiga "kibuyi" nayo ni ajali ya uso kwa uso.. hahahahaha maneno ya wahuni hayo barabarani huko..
 
Jiwe hz mambo alizipunguza kibabe haswa...!! R.I.P wote
 
Dunia inachangamoto sana hasa Afrika, maisha yamekubana inabidi upambane unajitoa tena unakutana na ajali kama hizo zinakatisha uhai wako, na familia yako inaanza kuteseka, kama sivyo basi zinakupa ukilema pamoja na hivo bado maisha yanakutizama tena ni vipi utakula, na ni vipi utaweza kulipa kodi na kulisha familia. Yani dunia hii sometime ukianza kuifikiria unaona hata ni bora usingezaliwa. Maana maisha yanatesa na yana changamoto nyingi mno. All in all Mungu awape mapumziko mema wameumaliza mwendo japo kwa uchungu na maumivu makali
 
Daah pale Changarawe panashida nadhani,hata Majinja ilichinja pale pale
 
Kama ni kutafuta chanzo halisi basi ni mwenye lori. Sidhani kama aliweka warning signs umbali unaotakiwa kabla magari mengine hayajafika pale. Nadhani unajua tahadhari za kuchukuwa iwapo gari imeharibikia barabarani!
 

Watu 18 wamefariki katika ajali ya Coaster na lori Rais Hana habari na hajatuma Hata salami Za Rambi Rambi kwa wafiwa na majeruhi? Nchi ya ajabu sana hii​

Kikanuni huwa anatakiwa atume baada ya dakika ngapi toka ajali itokee? Na akija kutuma baada ya kupokea taarifa rasmi atakuwa amekosea bado?
 
hayo maneno tu ukishakuwa mzoefu wa barabara utaovertake tu .halafu ajali nyingine kama hizi sababu sio kuovertake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni kutafuta chanzo halisi basi ni mwenye lori. Sidhani kama aliweka warning signs umbali unaotakiwa kabla magari mengine hayajafika pale. Nadhani unajua tahadhari za kuchukuwa iwapo gari imeharibikia barabarani!
Inawezekana Mkuu; ila najaribu kuzingatia kwamba dereva yeyote awapo barabarani huongoza vyombo vitatu: chombo chake mwenyewe, chombo kilicho mbele yake; chombo kilicho nyuma yake. Lakini pia dereva anatakiwa azingatie kwamba wenzake wanaoendesha vyombo sio wote ni madereva; wengine ni washika uskani tu na kunyoosha barabarani- hawajui kwa undani kazi ya udereva kwamba njiani wapo walevi, vichaa, watoto, wanyama, viziwi, wazembe, madereva wakorofi n.k. na wate hao wanatumia barabara pamoja na yeye. Sasa kama mwenzake(lori) ni mzembe kwa kutoweka alama, kwa nini yeye ajitumbukize kwenye kundi la Wazembe?Ni umbali gani mbele dereva anatakiwa aangalie kwa mwendo alokuwa nao? e.g. angekuwa speed ya 40 -50 Km/hr. ajali hiyo ingegharimu maisha ya watu wote hao? Mwendo wa 80- 90km/hr ni pale barabara imenyoka na dereva anauhakika wa meta 300 au zaidi mbele yake na anaona vizuri na hakuna chombo au alama za barabarani e.g vivuko vya watoto wa shule, mifugo, matuta hakuna wala katazo la mwendo i.e. speed limit au onyo e.g. upepo mkali, kona n.k. dereva mwangalifu sio kwamba hapati ajali la hasha, ila ajali yake inakuwa sio ya kiwango cha hiyo coaster. Watu 18 on the spot Inasikitisha sana.
 
hayo maneno tu ukishakuwa mzoefu wa barabara utaovertake tu .halafu ajali nyingine kama hizi sababu sio kuovertake

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli Mkuu. Siku za mwanzo-mwanzo madereva wanakuaga waangalifu sana. Kadri siku zinavyoenda wanarudi mdogo-mdogo kulekule kama ulivyosema. Mbona hata hapo kwenye ajali wapo wadereva wamepita na wameona lakini wakishapita kidogo tu ngoma iko palepale mwendo mkali...hawakujifunza kitu hapo.
 
"Innalillahi wainnailayhi rajiuun" hakika sisi niwa Mwenye-ez-Mungu na kwake yeye tutarejea.
 
Ajali imetokea pale pale ambapo Majinja ilinyonga watu 40.
 
Doh!! Hivi huku ndio kwa wakinga au?
 
POLE WAFIWA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…