Mimi ni muislamu lakini kuna hoja hapa na tuongee bila kubezana. Hii issue hata nchi za kiarabu zimechukuwa hatua na sio kwa nia mbaya ila wameweka utaratibu. Adhana inakuwa moja tu na sauti iko regulated. Lakini adhana ikiisha tu basi speaker za ndani tu zinawashwa za nje zinazimwa na huu ni utaratibu wa kiungwana. Sisi hapa ni lazima tu copy huu utaratibu sababu ni jambo zuri sana. Lakini pia kwenye makanisa hizi kwaya zisikike ndani tu na mahubiri ndani tu. Tujenge utaratibu mzuri, kumbuka humu mitaani tuna wagonjwa, kuna watoto.