Muft mkuu wa waislamu tusaidie kudhibiti misikiti mtaani, uhuru umezidi kwenye vipaza sauti

Muft mkuu wa waislamu tusaidie kudhibiti misikiti mtaani, uhuru umezidi kwenye vipaza sauti

Mawaidha yanatakiwa yasikike kwa walio ndani tu. Mbona kuna misikiti mingi mjini lakini sijawahi sikia hizo kelele. Misikiti ya uswazi ndio ina hayo mambo
Mawaidha yanayozungumziwa sio ya Mchana wala jioni mkuu ni Mara baada ya adhana ya 1 Fajir (Subuh)
 
"Kitanda ni jeneza, shuka ni sanda, amka muislamu wewe ukaswali, adhabu ya kabri....". And stuffs like that[emoji23]
Chumba ni kaburi, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Bas wakianza mawaidha hapoo, woiiiih
 
ninacho ona hapa watu wanaogopa mawaidha ya baada ya adhana ya asubuhi kisa ni waovu sasa yale maneno yanawachoma. na waovu wanaogopa kifo balaaa

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Kuna Rafiki yangu pale MABIBO - MAKUTANO anapoishi Kuna "kijikanisa" Cha Mpendwa mmoja hivi ndio anaibukia kwenye huduma nadhani, pembeni Kuna Pub (anasema wanakesha) then MITA kama 50 hivi Kuna Msikiti.
 
"Kitanda ni jeneza, shuka ni sanda, amka muislamu wewe ukaswali, adhabu ya kabri....". And stuffs like that😂
Kumbe Daawah inakuingia umeanza kuhifadhi hata maneno yake in out inakuingia sana na huo ndio ukweli wenyewe.
 
Lakini na kuna yale makanisa ya upepo wa kisulisuli pia ya kukesha alhamisi na Jmosi miziki na maombezi ya makelele ni kero hili nalo waliangalie vizuri
 
Mimi ni muislamu lakini kuna hoja hapa na tuongee bila kubezana. Hii issue hata nchi za kiarabu zimechukuwa hatua na sio kwa nia mbaya ila wameweka utaratibu. Adhana inakuwa moja tu na sauti iko regulated. Lakini adhana ikiisha tu basi speaker za ndani tu zinawashwa za nje zinazimwa na huu ni utaratibu wa kiungwana. Sisi hapa ni lazima tu copy huu utaratibu sababu ni jambo zuri sana. Lakini pia kwenye makanisa hizi kwaya zisikike ndani tu na mahubiri ndani tu. Tujenge utaratibu mzuri, kumbuka humu mitaani tuna wagonjwa, kuna watoto.
Hapa ni sawa mkuu baada ya adhana mic zizimwe na baada ya misa mizike iwe indoor maana eeh hatulali kwa masebene
 
wale wana hekima walishasikiliza maagizo ya NEMC na wametii maagizo yao. Imebaki nyie waislam ni wabishi na wakaidi hamfuati sheria za nchi kutwa kupigia watu kelele na miazana yenu kwenye maspika makubwa. Kule Rwanda mmeshikishwa adabu hakuna hayo makelele
Labda warokole wa mtaani kwenu ndo wana hiyo hekima [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hasa kwenye stori pale, hiyo adhana waendelee nayo ni alam yangu, ila kwenye mastori happy naona huwa wanajiongelesha wenyewe na huku kwetu wanapenda sana mastori ya wanawake
Nipo zangu tandale,muadhini wa alfajir akishamaliza kuadhini,utasikia 'nimekuamsha uje kuswali,we unachukua kapu lako safari kariakoo'
 
Mkuu kinachokukera wewe kuna mwingine kinampa Furaha..
Kwahiyo kumridhisha kila mtu huwa ni vigumu sana..

Kwa mfano akasitisha kumbe kuna watu walikuwa wanapenda hicho kitu..na wenyewe wakaja juu kuomba kirudishwe nao hao tutawaitaje?...

Kuna wakati ukiwa kiongozi lazma uwe unajua kuwa huwezi kumridhisha kila mtu kwa sababu kila mtu aa matakwa yke na mipango yake
Na tunatofautiana texture na maono kwenye almost kila kitu
We jamaa unatumia kwa kufikiria nini sasa mtu anayezitaka hizo kelele si aende akazifuate huko ziliko, uliona wapi kitu chenye madhara kikaruhusiwa kwa kuangalia watu wanaokifurahia badala ya watu wanaodhurika, hizo kelele zikipigwa marufuku itampunguzia mtu asiyezipenda madhara ya kukosa usingizi ila huyo anayezipenda itampunguzia kitu gani
 
Mkuu miskiti kuna madhehebu kama kulivyo na wakrito na kila dhehebu lina Taratibu zake..

Na kumbuka zile unazoita kelele ni kabla ya adhana ya pili ni mawaidha ya watu ambao wako nyumbani...
Kulingana na Qurn binadamu tunahitaji kukumbushwa mara kwa mara hili tuweze kuchukua maamuzi mazuri..

Na ndo maana baada ya mawaidha atapiga adhana ya Pili na baadae watu wakishakuja baada ya adhana ya pili huwwzi kusikia tena maana yake watu wataswali na kurudi makwao
Halafu mkiambiwa kwamba dini yenu haina uvumilivu na dini nyingine na inalazimisha kila mtu awe mfuasi wake mnakuwa wakali, sasa aliyewaambia hayo mawaidha kila mtu anahitaji kuyasikia ni nani kwanini hamheshimu haki za wengine, naunga mkono hiyo adhana yaa kuitana ila baada ya hapo zimeni vipaza za sauti vya nje hayo mawaidha peaneni wenyewe humo misikitini sasa shida ipo wapi hapo
 
We jamaa unatumia kwa kufikiria nini sasa mtu anayezitaka hizo kelele si aende akazifuate huko ziliko, uliona wapi kitu chenye madhara kikaruhusiwa kwa kuangalia watu wanaokifurahia badala ya watu wanaodhurika, hizo kelele zikipigwa marufuku itampunguzia mtu asiyezipenda madhara ya kukosa usingizi ila huyo anayezipenda itampunguzia nini
Tatizo unaandika kwa kupanic na hasira kwa hyo huwezi kuelewa point yangu kwa sababu umesoma maelezo yangu kwa chuki bila kutumia Busara...

Narudia tena unachokiona wewe ni kero kuna mwingine kwake anataman kiwepo muda wote..
Ingekuwa kama kelele hizo zina madhara kama unavyosema bhasi naamini Wazi zisingekuwepo na zingepigwa marufuku..
Sheria haiendeshwi kwa matamanio ya mtu bali kwa matakwa ya taratibu na Kanuni..
 
Halafu mkiambiwa kwamba dini yenu haina uvumilivu na dini nyingine na inalazimisha kila mtu awe mfuasi wake mnakuwa wakali, sasa aliyewaambia hayo mawaidha kila mtu anahitaji kuyasikia ni nani kwanini hamheshimu haki za wengine, naunga mkono hiyo adhana yaa kuitana ila baada ya hapo zimeni vipaza za sauti vya nje hayo mawaidha peaneni wenyewe humo misikitini sasa shida ipo wapi hapo
Mimi sio Muislamu wala sio mkristo bado umeweka chuki na udini na kwa bahati nzuri kwangu na bahati mbaya kwako sipo katika udini..
Nilichojaribu kukiongea kinatokana na utaratibu wao..
 
Back
Top Bottom