Mufti aomba mapumziko mwaka mpya wa kiislamu,naam uislamu ni dini ya haki

Mufti aomba mapumziko mwaka mpya wa kiislamu,naam uislamu ni dini ya haki

Zee la madawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,895
Reaction score
4,478
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakari Zubeir Ally, amemuomba Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, kumshawishi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili siku ya mapumziko ya Mwaka Mpya wa Kiislamu (Hijriyya) itambuliwe Tanzania nzima.

Mufti Zubeir ametoa ombi hilo leo Juni 15, 2026 wakati wa maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu visiwani Zanzibar, akieleza kuwa Tanzania ni nchi moja hivyo mapumziko hayo yanapaswa kuwanufaisha Waislamu wa pande zote za Muungano.

Amesema hatua ya Rais Mwinyi kutangaza siku ya mapumziko kwa Zanzibar ni jambo la kupongezwa, huku akionesha matumaini kuwa ushauri huo unaweza kufikishwa kwa Rais Samia ili utaratibu huo uweze kuenea nchi nzima.

Awali, Rais Dkt. Mwinyi alitangaza kuwa Jumatano Juni 17, 2026 itakuwa siku ya mapumziko Zanzibar kwa ajili ya kuadhimisha na kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1447 Hijriyya.
 
Ni vizuri pia ila tahadhari iwe kubwa maana kila dhehebu na dini zikitaka kutambuliwa mwaka wao mpya tutakuwa na maadhimisho mengi.
Lau ingewezekana siku kuu zote za kidini zingefutwa ibaki siku moja ya taifa ambayo ni uhuru .
 
Dunia ipo mwaka wa 2026 halafu kikundi cha dini kiko mwaka wa 1447, hii wapi na wapi wakati hii si nchi ya kiislam? Wasubiri iwe jamhuri ya kiislam ndio wajaze mambo yao kwenye public holiday
 
Upumbavu mtupu, eti mwaka mpya ilhali katika maisha mnatumia kalenda tofauti pumbavu zenu na Allah.
 
Mufti yuko sahihi, tupumzike, ndugu zetu waislam washerekee siku kuu yao
 
Back
Top Bottom