Mufti Mkuu Dkt. Abubakar: Tusisumbuliwe na fikra za Watu au kikundi cha watu. Muislamu haambiwi jambo akaenda tu, msifuate mkumbo

Mufti Mkuu Dkt. Abubakar: Tusisumbuliwe na fikra za Watu au kikundi cha watu. Muislamu haambiwi jambo akaenda tu, msifuate mkumbo

Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania Alhaji Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally Mbwana amewataka Waislamu kote Nchini kuendelea kuhubiri amani na kuachana na vitendo viovu vitakavyopelekea uvunjifu wa amani ya Nchi.

Mufti amesema hayo katika Sherehe za Maulid ya Kitaifa iliyofanyika katika Viwanja vya Kalangalala Mjini Geita ambapo maelfu ya Waisalmu wamehudhuria akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela pamoja na Viongozi mbalimbali wa Dini.

Mufti amesema “Mtume alikuwa Mtu wa subra, alikuwa Mtu wa pole, alikuwa akifundisha amani, Mungu alimtayarisha akawa ni Mtu wa namna hiyo hakufanya mambo ya kipuuzi hata siku moja”

“Na Mungu ametueleza katika Quran juu ya masuala ya amani ni ajabu Umma huu leo ikawa hawa ndio wanaovunja amani wao ndio wanaoharibu ulimwengu, msilete uharibifu, msieneze uharibifu katika Nchi, Mungu ametukataza na Muislamu hatakiwi kila jambo ambalo linafanywa na anafanya na yeye”

“Tusisumbuliwe na Watu, kikundi au fikra za baadhi ya Watu kwa makusudio yao au zile mambo wanayokuwa nayo, rudi katika uislamu, je, uislamu unaniamlisha Mtume kasema yafaa kufanya jambo hili ?, haiwezekani Muislamu unaambiwa jambo unakwenda unauharibu uislamu na unatoka katika mafunzo ya uislamu na uislamu hauko huko, Muislamu ndio Mtu wa kwanza kuchunga mazingira, usiwe kama Mtu ambaye ana tabu ya afya ya akili, sasa unaona Watu wanapita barabarani wewe unaingia ‘eeh hatukubali Bwana’ haukubali nini sasa!?”

“Tutumie akili zaidi, Muislamu haambiwi jambo halafu anakwenda, anaanza kufikiri, ukiambiwa jambo unalitia katika mizani kwanza kisha ndio unakwenda, sio unaambiwa jambo unakwenda tu ‘hatutaki hatutaki’ asili yake unaijua?, lazima tulinde amani Nchini hatuna Nchi nyingine Nchi yetu ndio hii, tusisumbuliwe na fJwapikra za Watu au kikundi cha Watu, jiulize hakuna mambo mengine hapa?, lakini Muislamu unaambiwa jambo unakwenda unauharibu uislamu”

Unafiki ni kitu hatari sana.
Hawa wanufaika wa pesa za misaada ndio wanaosababisha ugaidi duniani.

Amesahau kuwa Kule Kibiti polisi na viongozi na Makada wa CCM waliuawa sana bila kujali dini na wale waliodhaniwa kuwa ni magaidi wanaofungamana na waliokuwa wanafadhiliwa na matajiri wa kutoka nje kuingiza ugaidi wa Alshabab Tanganyika.
Kama sio uimara wa serikali Kuzuia pesa haramu za kusapoti ugaidi na NGOs za mashoga leo nchi ingekua kama Somalia.

Watanganyika hatukuwa watu wa kunyamazia uonevu lakini kutokana na misaada toka nje uhalifu dhidi ya binadamu unanyamaziwa na taasisi zinazonufaika kama zile za ushoga n.k.
Kule Zanzibar Nyumba za Ibada zilichomwa moto kutokana na hasira zinazotokana na dhulma wakati wa uchaguzi . Wizi wa kura ulisababisha wananchi wa Zanzibar kuichukia Seikali na kuichukia dini ya Kikristo mpaka kusema kuwa nchi hii inaongozwa na mfumo Kristo kisa ni dhulma zinazofanywa na Serikali ya CCM. Na CCM ikaitwa kuwa ni cha cha kikatoliki kilichoanzishwa Vatican kwa maana ya Christian Council Motion.
Dhulma zilizofanywa na CCM kushirikiana na Majeshi kule Zanzibar wakati wa Chaguzi zote ulipelekea Visasi na vinyongo na waathirika wakubwa wakawa ni Polisi na Wakristo ambapo Mapadri walimwagiwa tindikali na makanisa kuchomwa moto.
Hata watoto waliozaliwa pamoja watakua na chuki endapo mzazi atakua anampendelea moja na kumlinda mwingine hata pale anapomchokoza mwingine. Yaani mmoja anampiga mwenzake halafu mzazi anamficha mgongoni basi ni lazima ataanza kuviziana kwa visasi na vinyongo.
Mufti anadhani kuwa anaibabea CCM bila kujua kuwa mbeleko ya CCM imebaki kwenye Mauaji na vitisho na Rushwa zinazotokana na pesa za dhamana na wizi wa mali za umma .
Wananchi hawana tena furaha na CCM wala Bakwata na KKKT mana hakuna mtu anayekubaliana na mauaji popote duniani . Nyerere akiwa mkatoliki na Mwasisi wa CCM alifunga ubalozi wa Israel Tanganyika kupinga uonevu na mauaji ya wapalestina . Leo Taasisi kubwa kama Bakwata inakaa kimya na kuangalia Watu wakiwapotezwa na kuacha watoto yatima na wajane.
Hii haikubaliki .
Hii ni roho mbaya sana inayojengwa Tanganyika na hawa Watu waovu.
Itafikia mahali hata mtu akivamiwa na wezi Watu anapiga picha badala ya kupambana na wahalifu eti mpaka polisi waje wenyewe mana nisije nikaumizwa bure.
Nani analindwa kwenye haya mauaji ?
Kule Rufiji Mpaka leo hatujaambiwa nani walihusika na yale matendo maovu. Bila shaka wangepelekwa mbele ya mahakama siri kubwa ingegundulika mana ni kweli nyuma yao palikua na wakubwa ndani na nje na pia misukumo ya kisiasa na kidini.

Je ,Mufti wa BAKWATA haoni kuwa bado kuna hali ya watu kuuawa na kutekwa kwa sababu zile zile za kisiasa walizokuwa wanafanyiwa wanachama wa CUF kule Zanzibar huku watu wakialbiwa Kuwa ni wachochezi kwa sababu ya kupinga dhulma wakati wa uchaguzi.
Je, Bakwata kama taasisi ya kidini inaruhusu watu kutekwa na kuuawa kwa sababu ya kukosoa utendaji na sheria za kidunia ambazo zisiposimamiwa vizuri na watu wenye kujali utu zinageuka Kuwa dhulma na uharibifu mkubwa.

Je,Mufti haoni Kuwa kuna sheria zinazowagandamiza watu na kuwaumiza hata Bakwata wenzake wasio na madaraka au wasiofungamana na CCM.
Je , mufti haoni Kuwa haki ya damu za watu waliotekwa na kupotea inatakiwa idaiwe na watu waliobaki hai ?
Au anafikiri siku wakifanikiwa kuwamaliza Wapinzani Dini zitakua salama ?

Kwa taarifa yake huyo Mufti siku wakiwamaliza wapinzani basi ndiyo siku utawala wa Tanzania utaanza kupatikana kupitia dini hapo watu wataanza kuwamaliza wale wa dini nyingine maarufu na kuwatisha ili dini nyingine ibakie madarakani kwa manufaa ya wanasiasa waliopo juu kuendelea kuifanya nchi kuwa shamba lao. Tunaona uchaguzi unaokuja ulivyofadhiliwa na matajiri wa kutoka nje .
Hapa kuna yanayokuja kwa mkono wa pesa haramu za misaada.

Kama Rais mwenyewe alikemea utendaji wa kukamata na kutesa watu tangu mwanzo mpaka akaunda tume ya haki jinai. Akitoa mfano jinsi yeye mwenyewe alivyowahi kukamatwa na kunyanyaswa kule Zanzibar lakini bado tu Mufti haoni Mapungufu. Basi hiyo taasisi ina kiongozi kipofu asiyeona mabaya yanayofanyika kwenye jamii.
Au Mufti taasisi yake inaruhusu watu kuuawa bila kosa lililothibitishwa na mashahidi mbele ya Hakimu au kadhi??

BAKWATA kama taasisi ya dini yenye muongozo wake ndani ya Qorani na Hadithi za Mtume inawakataza watu kuua hata mnyama yeyote bila sababu iweje Siku ya kuzaliwa Mtume BAKWATA wasitoe hata ushauri wa namna ya kudhibiti hili suala la watu kutekwa bila kuathiri amani ya nchi.

Au Mufti anataka tuamini Kuwa kuna siri inayotembea chini kwa chini ikiwaalinisha BAKWATA Kuwa Chadema ni chama cha wale wanaoipinga Bakwata kumpinga Samia na eti wakati wa Magufuli wasio Bakwata walikaa kimya jambo ambalo ni uzushi na unafiki mkubwa!!
bAu tuamini Kuwa BAKWATA wamekatazwa chini chini wasijiunge na Chadema.

Nilikua siungi mkono maandamano ya tarehe 23 ila nimegundua kuwa hayo maandamano ni muhimu sana . Yalifanyika kwa nguvu kubwa yataondoa hali mbaya inayotengenezwa na wazee walizokalia madaraka na wenye mishahara na maslahi manono huku vijana wakiwa na maisha magumu mpaka wengine wanashindwa hata kuoa.
Lakini pia maandamano yataondoa hali fulani ya Udini inayotumika kuzimika viongozi wasio na uzalendo na nchi . Maandamano yatawaunganisha watanzania na watanganyika wote bila kujali hali inayojengeka ya kikabila na kivyama
.
Maandamano yatawafanya CCM na serikali yake waone umuhimu wa kusimamia haki na utawala bora na pia kuwajibika kwa wananchi kama waajiri wao.

Mufti na wanaofanana nao wanapopata previllage kutoka serikalini wanasahau kuwa ni kodi za wananchi na huyo anayewapa wala halipi Kodi zaidi ya yeye kunufaika na kodi za wananchi.
Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania Alhaji Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally Mbwana amewataka Waislamu kote Nchini kuendelea kuhubiri amani na kuachana na vitendo viovu vitakavyopelekea uvunjifu wa amani ya Nchi.

Mufti amesema hayo katika Sherehe za Maulid ya Kitaifa iliyofanyika katika Viwanja vya Kalangalala Mjini Geita ambapo maelfu ya Waisalmu wamehudhuria akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela pamoja na Viongozi mbalimbali wa Dini.

Mufti amesema “Mtume alikuwa Mtu wa subra, alikuwa Mtu wa pole, alikuwa akifundisha amani, Mungu alimtayarisha akawa ni Mtu wa namna hiyo hakufanya mambo ya kipuuzi hata siku moja”

“Na Mungu ametueleza katika Quran juu ya masuala ya amani ni ajabu Umma huu leo ikawa hawa ndio wanaovunja amani wao ndio wanaoharibu ulimwengu, msilete uharibifu, msieneze uharibifu katika Nchi, Mungu ametukataza na Muislamu hatakiwi kila jambo ambalo linafanywa na anafanya na yeye”

“Tusisumbuliwe na Watu, kikundi au fikra za baadhi ya Watu kwa makusudio yao au zile mambo wanayokuwa nayo, rudi katika uislamu, je, uislamu unaniamlisha Mtume kasema yafaa kufanya jambo hili ?, haiwezekani Muislamu unaambiwa jambo unakwenda unauharibu uislamu na unatoka katika mafunzo ya uislamu na uislamu hauko huko, Muislamu ndio Mtu wa kwanza kuchunga mazingira, usiwe kama Mtu ambaye ana tabu ya afya ya akili, sasa unaona Watu wanapita barabarani wewe unaingia ‘eeh hatukubali Bwana’ haukubali nini sasa!?”

“Tutumie akili zaidi, Muislamu haambiwi jambo halafu anakwenda, anaanza kufikiri, ukiambiwa jambo unalitia katika mizani kwanza kisha ndio unakwenda, sio unaambiwa jambo unakwenda tu ‘hatutaki hatutaki’ asili yake unaijua?, lazima tulinde amani Nchini hatuna Nchi nyingine Nchi yetu ndio hii, tusisumbuliwe na fikra za Watu au kikundi cha Watu, jiulize hakuna mambo mengine hapa?, lakini Muislamu unaambiwa jambo unakwenda unauharibu uislamu”
 
walikuja na kuwachukua wanasiasa, nikasema hayanihusu mimi si mwanasiasa.
Wakaja kwa waandishi wa habari, nikasema hayanihusu mimi si mwandishi wa habari.
Wakaja kwa wanaharakati, nikasema hayanihusu mimi si mwanaharakati.
Wakaja kwa wakristo, nikasema mimi si mkristo siendagi kansani.
Wakaja kwa Waislamu, nikasema mimi si mwislamu.
Waliponiijia mimi, hakukuwa na mwingine wa kunitetea.

copy and paste
Lema alisema hakuna aliye salama, bdo....
 
Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania Alhaji Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally Mbwana amewataka Waislamu kote Nchini kuendelea kuhubiri amani na kuachana na vitendo viovu vitakavyopelekea uvunjifu wa amani ya Nchi.

Mufti amesema hayo katika Sherehe za Maulid ya Kitaifa iliyofanyika katika Viwanja vya Kalangalala Mjini Geita ambapo maelfu ya Waisalmu wamehudhuria akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela pamoja na Viongozi mbalimbali wa Dini.

Mufti amesema “Mtume alikuwa Mtu wa subra, alikuwa Mtu wa pole, alikuwa akifundisha amani, Mungu alimtayarisha akawa ni Mtu wa namna hiyo hakufanya mambo ya kipuuzi hata siku moja”

“Na Mungu ametueleza katika Quran juu ya masuala ya amani ni ajabu Umma huu leo ikawa hawa ndio wanaovunja amani wao ndio wanaoharibu ulimwengu, msilete uharibifu, msieneze uharibifu katika Nchi, Mungu ametukataza na Muislamu hatakiwi kila jambo ambalo linafanywa na anafanya na yeye”

“Tusisumbuliwe na Watu, kikundi au fikra za baadhi ya Watu kwa makusudio yao au zile mambo wanayokuwa nayo, rudi katika uislamu, je, uislamu unaniamlisha Mtume kasema yafaa kufanya jambo hili ?, haiwezekani Muislamu unaambiwa jambo unakwenda unauharibu uislamu na unatoka katika mafunzo ya uislamu na uislamu hauko huko, Muislamu ndio Mtu wa kwanza kuchunga mazingira, usiwe kama Mtu ambaye ana tabu ya afya ya akili, sasa unaona Watu wanapita barabarani wewe unaingia ‘eeh hatukubali Bwana’ haukubali nini sasa!?”
 
Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania Alhaji Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally Mbwana amewataka Waislamu kote Nchini kuendelea kuhubiri amani na kuachana na vitendo viovu vitakavyopelekea uvunjifu wa amani ya Nchi...
unaambiwa jambo Fulani ni haramu, wewe unakaidi na unakwenda kulifanyika,

hakika huo sio uislamu 🐒
 
Mufti uchwara huyu. Mufti halisi wako Mecca.
 
Back
Top Bottom