Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Kila nikisoma kisa cha Mfalme Suleiman katika Quran tukufu huwa naona kiwango cha juu sana cha utunzi wa sanaa ya masimulizi kwa Mtume Muhammad (PBUH).
Fikiria Muhammad anasema Suleiman alikuwa anaweza kuwasiliana na wanyama wote, ndege mpaka siafu alikuwa anawasikia.
Suleiman anahadithiwa aliweza kuhamisha kiti cha Ufalme wa malkia wa Sheba kutoka Yemen mpaka Israel kufumba na kufumbua. Mtume alikuwa anajua "time travel" enzi hizo
Muhammad anasema Sulemani alikuwa ana amri juu ya upepo (upepo enzi hizo ilikuwa ni kitu muhimu sana kwa jamii za Gulf zinazosafiri baharini)
Suleiman alikuwa ana amri juu ya majini/mapepo na hata aliwatumia kujenga msikiti wa Al-Aqsa.
Suleiman alipokufa majini na watu hawakujua mpaka alipoanguka kutoka kitini mwake na hapo ndipo ilipogundilika kwamba majini hayaoni mambo ya mbeleni.
Hii ni kama riwaya ya kubuni (fiction novel) ya hali juu sana.