Muharami Abdallah (Chonji) na wenzake wahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya

Muharami Abdallah (Chonji) na wenzake wahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya

Unamfananisha chonji na shkuba.
Chonji wa one man army. Pale magomeni makanya, tajiri huyu alijulikana sana na aina za gari zake either gx 100 nyeupe zina mdundo saaana mziki mnene, enzi dicksound ni fundi wa yule jamaa alikufaga, utamkuta pia na verossa.
Nyumba yake inakuta ndefu, nje garage ya magari, na imezungukwa na camera. Humkamati huyo. Akiingia tu ndio utamkamata, sii vinginevyo. Na hutojua yupo ndani au nje muda gani.

Hawa hawakusingiziwa ila walikutwa red handed.
Chonchi ni muuza madawa mkubwa sana magomeni, ajali kazini, Kaka zangu hawa nawaonea huruma kubananishwa maisha. Ila Mwenyezi Mungu awe nao mpaka mwisho wao uwe mwema.
Shkuba ni shkuba na hajawahi toroka popote, shkuba alikamatwa na tikotiko. Watoto wa kinondoni hao.
Ila Mimi nawaambiaje awa watu wanatoka...nchi yetu baada ya mkapa kesi nyingi hata za mauaji wahusika Huwa wanaachiwa...amini ata Hawa watatoka...!​
 
Duh! Sasa kwa nini polisi wasitengeneze mazimgira ya kumuua tuu kama walivyofanya kwa yule don wa colombia
Mie ningekuwa mkuu wa hiyo idara yaani ningesema kabis ahapa sitaki kesi nataka a dead body tena especially mtu ambaye tunajua kabisa anatembea na bunduki
Cheki movie moja ya Elchapo Guzman utaona jinsi hiyo biashara inavyogusa connection nyingi mpaka polisi, siasa na jeshi
 
Yani unamfananisha Pablo Escober na Jamaa wa magomeni haupo siriaz au unatania...yani ufananishe mtu anasakwa na Marekani ( FBI) na huyo mzaramo
Hahahha .....aisee kuna comments zingine mtu unasoma unabaki kucheka tu na kumtafakari huyo aliyeitoa hiyo comment.

Sidhani kama huyu anajua hata historia ya Pablo Escober mwenyewe zaidi ya kumskia skia tu kwenye vijiwe vyao huko magomeni.

Halafu inaonekana anaamini mtu akiwa mjanja mjanja na kuishi kihuni huni hapa bongo na akatoboa, basi huyo ni muhuni na mjanja wa dunia nzima na hakuna mjanja au muhuni zaidi yake.
 
Miaka hiyo, vijana wa Dar wanawaza kwenda Ulaya, vijana wa vijijini wanatamani kuja Dar! Huu mtazamo unaenda katika nyanja mbalimbali za kimaisha!

Watoto wa Magomeni, Ilala, Kinondoni na Kariakoo miaka hiyo ndiyo walikuwa DSM! Sinza walikuja baadaye sana! Weka pembeni wale wa kishua from Masaki, Osterbay na Upanga wale walikuwa next level!

Usishangae sana sekta ya michezo na burudani kutawaliwa na watoto wa hayo maeneo! Halafu kwenye biashara na uongozi wamejaa watoto wa kishua kutoka pande hizo! Unaweza kuta hata wanaotamba huko shamba kumbe alitoka DSM!

Sifa kuu ilikuwa kupendana na kutojiona bora kuliko wengine hata kama umetoboa!

Leo mtu akipata kinyumba na gari anahisi ameyapatia na kuwadharau hata wenyeji waliompkea na kuwaona hawana akili! Ukifuatilia makuzi kumbe alikulia shamba! Siyo wote lakini!
Vijana sahivi wepesi sana
Kila kijana anataka kuwa mkata
Uno

Ova
 
Aliekamatwa na wamarekani Beka Rangers,tena walienda kumkamatia Mauritius kama sijasahau akapelekwa Marekan nahisi kesi yake iliisha
Beka rangers Alifungwa miaka saba Mauritius ila kamaliza,, huyu anamuongelea tiko rasta wa makanya naye alikuja kuchukuliwa na interpool bongo akafungwa marekani nafikiri ni miaka mitatu nae kamwaga
 
Kwa hiyo kwa akili yako unaona hii serikali ya samia ndio ina umadhubuti wa kupambana na vita ya madawa ya kulevya??

Kwamba kukamata hao akina choji ambao hata sio main supplier ndio kunakufanya uwe excited namna hii kiasi cha kubwabwaja maneno ya mipasho kama kimama cha uswahilini chenye asili ya kizanzibari?

Wewe nakuona umevimbiwa asali na haujui kinachoendelea, na kwa taarifa yako tu ni kwamba hakuna kipindi ambacho biashara haramu zinafanyika sana tena kwa uwazi kama awamu hii... weka hilo akilini.
Una ushahidi au ni stori za mitaani.

Mwache Mama akomeshe madawa. Hana roho mbaya ya kubambikia watu Madawa kwa chuki.
 
Back
Top Bottom