Muhimbili yaongeza Gharama za Kuona wagonjwa wa VIP

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
242
Reaction score
1,141
Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Aprili 9, 2024 imesema kutokana na maboresho yaliyofanyika na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili upande wa Kliniki za VIP Jengo la wagonjwa wa nje inayoitwa 'NOPD VIP', bei ya kumwona Daktari kwa Kliniki kwa sasa ni Shilingi 100,000/=.

Mgonjwa wa Malipo Taslimu 'Cash' atatakiwa kulipia kwa Control Namba ya kiasi kama inavyoonyesha kwenye Jedwari. Aidha, Wagonjwa wa Bima watakaohitaji kuonwa kwenye Kliniki hii watalipa kama Jedwali linavyoonyesha hapo chini.

 
Daah Nchi hii watu wanajipangia gharama kubwa kama vile wanaotibiwa sio Watanzania daah na maboresho yote yanafanywa kwa Kodi zao ila kwenye kutibiwa sio jukumu lao.
 
Dr.Janabi futa hiyo kitu Haraka sana.Wakati wa Nyerere saa hizi wewe kazi kwisha ! Ungesharudi Bagamoyo kukwea minazi.

Mama Samia usikubali upuuzi huu. Binadamu wote tuko sawa hakuna cha VIP wala nini.
 
=jedwali.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Dr.Janabi futa hiyo kitu Haraka sana.Wakati wa Nyerere saa hizi wewe kazi kwisha ! Ungesharudi Bagamoyo kukwea minazi !
Mama Samia usikubali upuuzi huu !
Binadamu wote tuko sawa hakuna cha VIP wala nini
Endelea kudanganywa tu usawa upo kwa Mungu sio hapa duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…