MUHIMU: Tuma maoni yako ya Rasimu ya Katiba Mpya, Mabaraza ya CHADEMA

MUHIMU: Tuma maoni yako ya Rasimu ya Katiba Mpya, Mabaraza ya CHADEMA

CHADEMA

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
490
Reaction score
2,471
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kinaanza rasmi kuendesha Mabaraza ya Katiba, ambapo wananchi wote watashirikishwa kujadili na kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba Mpya, kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo;

1. Mikutano ya hadhara, itakayoanza leo katika maeneo mbalimbali ya nchi, ikiongozwa na timu mbili za viongozi wakuu,
Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibroad Slaa.

Mikutano hiyo itafanyika nchi nzima. Ratiba ya mikutano yote, itaendelea kutolewa kwa umma, kupitia vyombo vya habari (mainstream & social media).

2. Kutuma ujumbe mfupi kwa simu. Mwananchi anaweza kutuma maoni yake ya Katiba Mpya kupitia simu ya mkononi, kwenye NAMBA HII YA SIMU; 0789 24 82 24.

3. Email; chademamaoni@gmail.com

4. Kwa kupitia JamiiForums, toa maoni yako kwenye hii thread, ukishatoa maoni; jaza fomu ifuatayo;

Fomu ya maoni juu ya Rasimu Katiba Mpya (CHADEMA) - 2013

ili kukubaliana au kutokubaliana na vipengele vilivyoonyeshwa kwenye Jedwali.

Mfumo huu utatumika kwa facebooks, twitter, group emails, k.m mabadiliko, wanabidii n.k,

====================

[TABLE="width: 942"]
[TR]
[TD]S/N
[/TD]
[TD]IBARA
[/TD]
[TD]MAPENDEKEZO YA CHAMA (CHADEMA)
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1.[/TD]
[TD]2 Eneo la Jamhuri ya. Muungano[/TD]
[TD]Neno Tanzania Bara liondolewe na kuandika Tanganyika kila palipo na neno Tanzania Bara.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]4(1) Lugha ya Taifa[/TD]
[TD]Lugha ya Taifa itakuwa Kiswahili na miswada/sheria zote zitaandikwa kwayo pamoja na lugha zingine[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3.[/TD]
[TD]5 Tunu za Taifa[/TD]
[TD]Viongozwe vipengele hivi demokrasia ya vyama vingi, utawala wa sheria,uwazi na haki za binadamu.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]4.[/TD]
[TD]6(2) Daftari la wapiga kura[/TD]
[TD]Liwe mahali ambapo kila raia akifikisha miaka 18 ana andikishwa wakati wowote.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]5.[/TD]
[TD]17&85 watumishi wa umma.[/TD]
[TD]Mishahara ya watumishi wote wa umma pamoja Rais ijulikane.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]6.[/TD]
[TD]32 (2) haki ya kuandamana[/TD]
[TD]Kila mtu ana haki kwa amani na bila kubeba siraha kukusanyika/kuandamana kuzuia njia na kuwasilisha malalamiko.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]7.[/TD]
[TD]35(e) kugoma[/TD]
[TD]Kugoma au kusitisha nguvu kazi yake mahali pa kazi.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]8.[/TD]
[TD]47 Haki ya kumiliki rasilimali[/TD]
[TD]Iongezwe ibara mpya ya 48 haki ya kumiliki rasilimali za asili zote Ardhi, Madini, mafuta na gesi, maji na misitu na wanyama pori.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]9.[/TD]
[TD]60 (7)nyongeza[/TD]
[TD]Kiongozwe kifungu cha 7 Maadili na miiko ya uongozi na utumishi wa umma, Haki za binadamu na wajibu wa raia. Tume huru ya Taifa ya uchaguzi.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]10.[/TD]
[TD]Serikali tatu (3)[/TD]
[TD]Kuwepo serikali ya Muungano, serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanganyika.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]11.[/TD]
[TD]75(d) Uchaguzi wa rais.[/TD]
[TD]Umri wa mgombea urais uwe miaka kumi na nane[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]12.[/TD]
[TD]83(i) kinga dhidi ya mashtaka ya Rais.[/TD]
[TD]Wakati wowote Rais akiwa madarakani na baada ya kuacha kushika madaraka aweze kushtakiwa.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]13.[/TD]
[TD]105 (2) (b) wabunge wa kuteuliwa[/TD]
[TD]Kipengele hiki kifutwe na badala yake iwe wabunge 20 watakaochaguliwa kutokana na uwiano wa kura zilizopigwa kwa vyama vya siasa.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]14.[/TD]
[TD]117(i) (a) Mgombea Ubunge[/TD]
[TD]Umri wa mgombea ubunge uwe miaka 18 na si 25 kama inavyopendekezwa.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]15.[/TD]
[TD]123(2) uwajibikaji wa mbunge.[/TD]
[TD]Hii ifutwe na kuongeza :mbunge aliyependekezwa na chama cha siasa atapoteza ubunge wake ikiwa atafukuzwa au kuvuliwa uanachama wa chama chake cha siasa.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]16.[/TD]
[TD]123(3) mbunge kuhama/kujiunga na chama cha siasa.[/TD]
[TD]Kuongeza ibara ndogo :endapo mbunge kwa ridhaa yake atajiondoa au kujivua uanachama wa chama cha siasa au kujiunga na chama kama alikuwa mgombea huru basi atapoteza sifa ya kuwa mbunge.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]17.[/TD]
[TD]124 adhabu kwa mbunge[/TD]
[TD]Kuondoa kabisa ibara hiyo na badala yake iseme wananchi wa jimbo au kata watakuwa na haki ya kuwaondoa madarakani kwa sababu na kwa kufuata utaratibu na sheria.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]18.[/TD]
[TD]182 Tume Huru ya uchaguzi.[/TD]
[TD]Kuongeza wajumbe wa vyama vya Mawakili na vyama vya siasa.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]19.[/TD]
[TD]184 Tume Huru ya Uchaguzi[/TD]
[TD]Watumishi wote wa Tume Huru ya uchaguzi wasiwe watumishi wa serikali.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]20.[/TD]
[TD]234 Mkurugenzi wa usalama wa Taifa.[/TD]
[TD]Ateuliwe baada ya kuthibitishwa na Bunge[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]21.[/TD]
[TD]Nyongeza[/TD]
[TD]Kuanzishwa kwa mchakato wa katiba ya Tanganyika, kuundwa TUME ya Katiba ya Tanganyika.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Tunashukuru kwa taarifa bwana Makene. Mie nitaanza ni lile la serikali tatu (nakubaliana na mapendekezo ya wananchi yaliyopitishwa na tume), mawaziri wasitokane na wabunge (kama ilivyo katika rasimu), mgombea binafsi (kama ilivyo katika rasimu) na pia napendekeza wakuu wote wa wilaya wasiwepo na tuwe na serikali za majimbo.

Maoni hayo nitayawasilisha kwa njia sanifu baada ya kutupatia muongozo zaidi.
 
Nachukia hizi tume na Kamati za uchunguzi, hazina Faida Katiba mpya iainishe utekelezaji wa maazimio ya tume na Kamati zinazoundwa, na wenyeviti wake wapitishwe na bunge. Huku kumekuwa Chaka la kuchezea kodi zetu. Vinginevyo tume ziwe za majaji, ili wawe huru
 
Tunashukuru kwa taarifa bwana Makene. Mie nitaanza ni lile la serikali tatu (nakubaliana na mapendekezo ya wananchi yaliyopitishwa na tume), mawaziri wasitokane na wabunge (kama ilivyo katika rasimu), mgombea binafsi (kama ilivyo katika rasimu) na pia napendekeza wakuu wote wa wilaya wasiwepo na tuwe na serikali za majimbo.

Maoni hayo nitayawasilisha kwa njia sanifu baada ya kutupatia muongozo zaidi.


Hapo kwenye red; nakumbuka miaka ya nyuma ilikuwa hivyo (mawaziri hawakulazimika kutoka miongoni mwa wabunge) ila ilikuja kubadilishwa kwa NIA NJEMA kabisa ili kuzuia uwezekano wa Rais kuchagua watu wake aliowataka katika nafasi za uwaziri.

Kwa maneno mengine, nia ilikuwa kwamba angalau mtu akubaliwe na wananchi (kupitia ubunge of course ukiacha nafasi chache za Rais na Viti Maalumu) na kutoka kwenye kapu hilo ndipo Rais aweze kuteua mawaziri. Kwa kweli nia ilikuwa njema kabisa kabisa.

Hata hivyo kutokana na uchu wa madaraka uliokithiri ndipo suala la RUSHWA YA MADARAKA lilipofumuka kwa kasi hasa katika nafasi za ubunge kuanzia kura za maoni na kuendelea kwani mafisadi hawa walijuwa bila ubunge hakuna uwaziri labda kwa huruma ya Rais kupitia nafasi zake 10 za upendeleo na kwa wanaume ndio ilikuwa vigumu zaidi kwani viti maalumu havikuwagusa wao ingawa pia kwa akina mama rushwa ilitwala sana mchakato kwa lengo hilo hilo la kutumia nafasi hizo kama daraja kuelekea nafasi za juu.

HOJA: Kama utaratibu utabadilika ni lazima Katiba Mpya iweke bayana na kuzuia mianya yote haramu ya kupata nafasi za juu ikiwemo ufisadi, kujuana (mteuwaji na mteuliwa), ku-balance dini, makabila, n.k. Watu waingie kwenye nafasi hizo kwa kuzingatia vigezo vya kitaalamu na uadilifu na sio vinginevyo. Hata kwa aina ya Bunge tulilonalo bado sioni umahiri wake katika kutupatia viongozi wanaofaa kutokana na kugubikwa na ushabiki na itikadi za kijinga zisizozingatia maslahi mapana ya nchi na wananchi maskini.
 
Nimekutumia text, ni vyema mkatupa na email account

Rev Masa

Mkuu Rev Masanilo

Noted.

Email ni; chademamaoni@gmail.com & chademamaoni@chadema.or.tz

Namba ya simu; 0789 24 82 24.

Tutume maoni yetu kwa njia ya ujumbe mfupi. Kama nilivyotaarifu, utaratibu wa Jamii Forums, Twitter, group emails n.k, utatolewa muda si mrefu. Lengo ni effectiveness na efficiency ili kupata maoni ya Watanzania wengi kadri inavyowezekana kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu sote.
 
SAMAHANI KWA "UJINGA" UFUATAO:

Mimi nadhani kusiwepo na nafasi za ubunge bali udiwani na urais. Inakuwaje? Inakuwa hivi:-

Kila jimbo la uchaguzi lina idadi kamili ya Kata hivyo idadi ya madiwani nayo inaeleweka. Kwa kuwa mbunge ni mwakilishi wa wananchi Bungeni na kwa kuwa kimsingi ubunge ni ofisi badala ya personalities, utaratibu uwekwe hivi:-

(i) Kila Kata (sitaki kusema diwani) iwakilishe Jimbo husika Bungeni kwa usawa.

(ii) Kata A itawakilisha Jimbo Bungeni kwa kipindi, say, mwaka mmoja then mwaka unafuata inakwenda Kata B, n.k.

(iii) Kama Jimbo lina kata zaidi ya 5 (zaidi ya muda wa uhai wa Bunge - miaka mitano); msimu unaofuata zile Kata ambazo hazikwakilisha Jimbo ndizo zitakazoanza na mzungo unakwenda hivyo hivyo.

FAIDA ZA MFUMO HUU:-

(a) Itaondoa ujinga waliojijengea wabunge wengi wa kuhodhi majimbo kama mali yao hata kama output ni zero.

(b) Madiwani kwa kiasi kikubwa wanaishi karibu zaidi na wananchi hivyo wanajua zaidi shida zao kuliko wabunge wengi ambao wanaishi Dar es Salaam au miji mingine.

(c) Mganwanyo mzuri wa keki ya taifa: Badala ya kipato kwenda kwa mtu mmoja (mbunge) ; kipato hicho hicho kinakwenda kwa watu watano.

(d) Itaondoa uwezekano wa watu fulani kutoka maeneo fulani tu ndani ya jimbo husika kuchaguliwa kama wabunge. Kuwe na usawa kwa kila Kata kuwakilisha Jimbo.

(e) n.k. n.k. (faida ni nyingi sana)

CHANGAMOTO:

Itaendelea ...
 
Serikali ya Tanganyika, Mgombea binafsi, Kufutwa kwa vyeo vya Ukuu wa Mikoa na wilaya, wateule wote wa Rais lazima wahojiwe na kuthibitishwa na kamati husika za Bunge na Mawaziri wasiwe wabunge wa kuchaguliwa
 
SAMAHANI KWA "UJINGA" UFUATAO:

Mimi nadhani kusiwepo na nafasi za ubunge bali udiwani na urais. Inakuwaje? Inakuwa hivi:-

Kila jimbo la uchaguzi lina idadi kamili ya Kata hivyo idadi ya madiwani nayo inaeleweka. Kwa kuwa mbunge ni mwakilishi wa wananchi Bungeni na kwa kuwa kimsingi ubunge ni ofisi badala ya personalities, utaratibu uwekwe hivi:-

(i) Kila Kata (sitaki kusema diwani) iwakilishe Jimbo husika Bungeni kwa usawa.

(ii) Kata A itawakilisha Jimbo Bungeni kwa kipindi, say, mwaka mmoja then mwaka unafuata inakwenda Kata B, n.k.

(iii) Kama Jimbo lina kata zaidi ya 5 (zaidi ya muda wa uhai wa Bunge - miaka mitano); msimu unaofuata zile Kata ambazo hazikwakilisha Jimbo ndizo zitakazoanza na mzungo unakwenda hivyo hivyo.

FAIDA ZA MFUMO HUU:-

(a) Itaondoa ujinga waliojijengea wabunge wengi wa kuhodhi majimbo kama mali yao hata kama output ni zero.

(b) Madiwani kwa kiasi kikubwa wanaishi karibu zaidi na wananchi hivyo wanajua zaidi shida zao kuliko wabunge wengi ambao wanaishi Dar es Salaam au miji mingine.

(c) Mganwanyo mzuri wa keki ya taifa: Badala ya kipato kwenda kwa mtu mmoja (mbunge) ; kipato hicho hicho kinakwenda kwa watu watano.

(d) Itaondoa uwezekano wa watu fulani kutoka maeneo fulani tu ndani ya jimbo husika kuchaguliwa kama wabunge. Kuwe na usawa kwa kila Kata kuwakilisha Jimbo.

(e) n.k. n.k. (faida ni nyingi sana)

CHANGAMOTO:

Itaendelea ...

Mi nafikiri hapa, ubunge uwe na kikomo cha muhura mmoja au miwili tu!
 
Iwepo serikali moja ya Jamhuri ya muungano wa Watu wa Tanzania .Serikali ya Zanzibar ifutwe na kupotea kama ilivyopotea serikali ya Tanganyika...ila majina ya Zanzibar na Tanganyika yanaweza kuitwa baadhi ya Mbuga za wanyama ama kitu chochote cha kudumu kwa ajili ya ukumbusho tu. Katiba iseme kuwa huko mbeleni kusiwepo na uwezekano wa kuanzisha serikali zaid ya JMT. Kama nchi nyingine itataka kujiunga na JMT mfano kama Rwandwa hivi sharti ifute userikali wake na iwe moja ya sehemu ya JMT.

Kwa leo ni haya.
 
Tutashukuru sana endapo maoni ambayo yameanza kutolewa hapa tayari, yatatumwa katika hizo njia ambazo zimeshaelezwa, yaani simu na email, huku tukiendelea kusubiri utaratibu wa maeneo mengine kama JF, twitter, blogs, group emails n.k.

Hili ni suala linalotuhusu Watanzania wote. Tushiriki kujadili Rasimu ya Katiba Mpya na kutoa maoni yetu sote kuamua mstakabali wa taifa letu utakaotokana na mwafaka wa kitaifa. Ni fursa ya 'kujiumba'.
 
Hadi sasa, kutokana na mikutano ya hadhara leo, ambayo imefanyika, Bunda, Mugumu, Tarime na Musoma (timu ya Mwenyekiti) na Same, Mwanga, Rombo na Vunjo (timu ya Katibu Mkuu), maoni yakiendelea kumiminika, mambo yanakwenda vizuri kama ifuatavyo;

Ujumbe mfupi wa simu ya mkononi;

Kutoka Mwanga, hadi sasa sms 214

Kutoka Vunjo, ambako mkutano umemalizika hivi punde, hadi sasa sms 516

Kutoka Rombo, hadi sasa sms 423

Kutoka Bunda, hadi sasa ni 264

Kutoka Tarime, hadi sasa sms 1,226

Kutoka Mugumu, Serengeti, hadi sasa sms 312

Kutoka Musoma ambako mkutano bado unaendelea, hadi sasa ni sms 278
 
Tunaanza kutoa maoni hapa hapa;
Ile ya kuwa na wabunge wawili kila jimbo, mwanamke na mwanaume mimi sipendi.

Kamanda Mjuni Lwambo

Naona una munkari kweli kweli kushiriki Mabaraza ya Katiba Mpya ya CHADEMA. Utaratibu wa hapa utawekwa. Wananchi walioko hapa watawekewa utaratibu wao maalum.

Kwa sasa, kwa kutumia emails na namba ya simu, ni kama ilivyoelezwa hapo juu...

Karibu.
 
Mimi hapa hapa:

1. ondoa hawa wakuu wa mikoa+wa Wilaya. Maana ni kuongeza gharama kwa wananchi , pia vimekuwa ni vyeo vya shukrani kwa wakubwa. Hasa kurubuni wapinzani wahame chama na kuwapa nyadhifa.
2. Dira ya nchi. Nchi iwe na dira mf. kilimo kwanza au ubepari au nn? Kama ni kilimo kwanza tuanze na kusambaza maji kwa wananchi ili watu tuwe Irrigation scheme na c kutatua tatizo kwa Mbolea na matrekta ambazo zote ni miradi za wakbwa na kuwa na manufaa machache kwa wananchi.
3. Serikali 1, kama hawataki 3 na kama pia hawataki basi kila mtu ale chake.
4. Budget ya Matumizi ya Rais iwe na kikomo, iwezekana Maximun no of trips should be mentioned.
5. Rais aweze kushitakiwa na Raia yeyote yule. Pia awapo Ikulu asijihusishe na biashara yeyote ile ikifahamika kabla na baada ya urais apigwe pingu (ashitakiwe).
6. Spika asiwe MWANAMKE na asiwe mbunge. Naona wametudhalalisha sn duniani.

7. Mawaziri wote wateuliwe na wasiwe wabunge. Na neno Chama Cha Mapinduzi lisisike kwenye maneno yao wawakilishapo report au budget au popote kwa lengo la kusifu au nn!!

8. Haki ya kuishi na kulindwa iwe ya 1 . Make noana kwa sasa mtu yeyote anaweza kukutoa pumzi mchana kweupeee!!, dk yeyote ile maisha yako yaweza kukatishwa. Pia haki ya kupata Elimu bora bila matabaka-yaani shule za kata wala nn! Na ikiwezekana Elimu ya awali hadi Elimu ya juu iwe kwa wote na neno mkopo liondoke-kwani migodi na kampuni za cm hazijaguswa hata chembe 1.

Kwa leo nahishia hapo, napenda kuwasilisha maoni yangu japo machache kwenye baraza lenu la mchakato wa katiba Mpya.

Makene msalimie Dr. Slaa, mwambie tupo Pa1 hata kwa risasi.
 
Nipo Arusha

Mkuu suala la ardhi liingie kwenye Katiba

1. Serikali ikitaka kutumia ardhi ninayoitumia tufanye makubaliano ya matumizi mapya mwenye ardhi nikiwa na hiza 50%. Na hili liishie kwenye Halmashauri. Kodi kwa serikali kuu iwepo lakini kwa makubaliano na Halmashauri husika.

2. Naunga mkono muundo wa serikali 3

3.Hizi ndizo ziwe na vingozi wa Kanda zitakazoundwa na kukubaliwa na wana Kanda. Vingozi wa hizi Kanda wachaguliwe na kuondolewa na mabaraza ya Halmashauri. Gharama za viongozi na uendeshaji wa hizi kanda zitokane na Kanda. Siungi mkono kuwepo kwa wakuu wa mikoa au wilaya wanaotokana na Serikali kuu.

4. Serikali ya muungano iundwe upya kwa makubaliano mapya ya serikali ya Tanganyika na Zanzibar. Hii itafanyika baada ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika

5. Mali asili ni mali ya mahali ilipo na serikali itakubaliana na au tozo kwa kitakachopatikana pale au itangia ubia na aliyepo kwenye eneo hilo katika makubaliano ya asili mia 50% kama amana ya awali. Mwekazaji ikiwepo serikali itahusu asimia 50 iliyobaki wakishirikiana na Halmashauri. Na kama Halmashauri imewekeza thamani yake itaingia kwenye asili mia ya mwenye eneo.

6. Halmashauri itashiriki kuelimisha mwenye eneo kuhusu mwendelezo wo wote wa eneo.

7. Napendekeza usimamizi (uwaziri) uwe kama ifutavyo

a. Huduma za Jamii (Afya, Elimu, Majeshi, utawala(serikali kuu na Bunge), Biashara na masoko)

b. Mali asili (Misitu, Madini, Maji na Nishati)

c. Hazina (Mapato, Matumizi)

d. Meendeleo (Miundo Mbinu, Science na Teknologia)

e. Uchumi na Mipango (Kilimo, Viwanda, Uchukuzi)

f. Mahusiano ya Kimataifa

g. Wizara ya Sheria na Katiba

Wizara zisidi saba yenye muundo unaunganisha na miundo kwenye halmashauri. Kwenye mabano ni Idara za kitaalamu. Mawaziri watapendekezwa baada ya kutuma maombi kwa chama kitakachochaguliwa kuwa madarakani kwa vigezo au sifa wazi za waizara husika. Wote watapitishwa na Bunge na kula kiapo cha utii kwa rais/waziri mkuu.

Faida.

1. Kupeleka usimamizi wa shughuli za maendeleo kwa wananchi

2. Kupunguza majukumu ya serikali kuu na matumizi husika.

3
----nitaendelea
 
Back
Top Bottom