MUHIMU: Tuma maoni yako ya Rasimu ya Katiba Mpya, Mabaraza ya CHADEMA

MUHIMU: Tuma maoni yako ya Rasimu ya Katiba Mpya, Mabaraza ya CHADEMA

Rais asiwe na mamlaka ya kuteua Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, bali viongozi hao (ambao hawatatokana na Wabunge) wagombee nafasi hizo kwa njia ya demokrasia. Wananchi wawapime kwa uwezo wao. Zama za kuletewa mfamasia au mveterinari kuja kuongoza Wizara ya Ndani, n.k., au Mjumbe wa NEC kuja kuwa Mkuu wa Mkoa, ZIMEISHA!

Rais asiruhusiwe kugombea zaidi ya kipindi kimoja cha miaka tano! Kisingizio "sijamaliza kutekeleza ahadi zangu" ni hoja mfu. Pia, kama ilivyo Marekani, Baraza la Mawaziri liwe na uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais, lakini kumuondoa Rais madarakani kusiathiri uwepo wa Bunge au Baraza la Mawaziri. Uchaguzi wa Rais pekee ndio urudiwe.

Wananchi wawe na uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani kwa wabunge wao, uchaguzi urudiwe apatikane mbunge mwenye uwezo. Wananchi wawe na uwezo wa kubadili vigezo vya mbunge wamtakaye jimboni mwao, kila ufikapo uchaguzi mkuu au mdogo, ili apatikane mbunge stahiki.
 
Hadi sasa, kutokana na mikutano ya hadhara leo, ambayo imefanyika, Bunda, Mugumu, Tarime na Musoma (timu ya Mwenyekiti) na Same, Mwanga, Rombo na Vunjo (timu ya Katibu Mkuu), maoni yakiendelea kumiminika, mambo yanakwenda vizuri kama ifuatavyo;

Ujumbe mfupi wa simu ya mkononi;

Kutoka Mwanga, hadi sasa sms 214

Kutoka Vunjo, ambako mkutano umemalizika hivi punde, hadi sasa sms 516

Kutoka Rombo, hadi sasa sms 423

Kutoka Bunda, hadi sasa ni 264

Kutoka Tarime, hadi sasa sms 1,226

Kutoka Mugumu, Serengeti, hadi sasa sms 312

Kutoka Musoma ambako mkutano bado unaendelea, hadi sasa ni sms 278

Kweli CDM ni nguvu ya umma,

TAHADHARI: Maoni haya tunataka yafanyiwe kazi, maana leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mza chini ya uongozi wa Mwenyekiti tumesikia kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba keshaanza kusema hatazingatia maoni ya Helkopta. Tunatoa maoni yetu juu ya hii Rasimu then tunasubiri hiyo rasimu ya pili, kama maoni hayatazingatiwa hiyo Katiba tutaikataa kwa nguvu zote.
Nawapongeza CDM kwa kuja na mpango huu wa kuwafikia Watanzania wote ili watoe maoni yao.
 
Hili la Chenge kuuwa watu kwa kuwagonga na gari, halafu analipa faini Sh. Laki moja na nusu na kusamehewa, hii sheria itazamwe upya. Yaani roho za watu kima chake ni laki na nusu?
 
1. Reajea kipengele Namba 11 - 75(d) Uchaguzi wa Rais. Mapendekezo ya chama yanasema, Umri wa mgombea uwe miaka kumi na nane (18). Nadhani hapa kuna kosa la uchapaji. Nakuomba Usahihishe hapa.

2. Kuhusu Serikali tatu (3): Naunga mkono (100%)
Napendekeza Muundo wa uungano uwe kama ifuatavyo:-

a) Tanganyika (Iongozwe na Waziri Mkuu atakayechaguliwa na wananchi Wote Wa Tanganyika)
b) Zanzibar (Iongozwe na Waziri Mkuu atakayechaguliwa na wananchi Wote Wa Zanzibar (Pemba na Unguja))
c) Jamhuri ya muungano wa Tanzania (Iongozwe na Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania atakayechaguliwa na wananchi Wote Wa Tanganyika na Zanzibar)
d) Waziri mkuu wa Wa Tanganyika na Waziri Mkuu wa Zanzibar wote wawajibike kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye atakaekuwa MKUU Wa NCHI.
 
HAKI ZA WANAWAKE ziwekwe wazi ikiwemo KATIBA kutaja ''UKEKETAJI'' kama Kosa la JINAI na Kifungo chake kiwe ni Miaka THELATHINI au MAISHA.
 
Iwepo serikali moja ya Jamhuri ya muungano wa Watu wa Tanzania .Serikali ya Zanzibar ifutwe na kupotea kama ilivyopotea serikali ya Tanganyika...ila majina ya Zanzibar na Tanganyika yanaweza kuitwa baadhi ya Mbuga za wanyama ama kitu chochote cha kudumu kwa ajili ya ukumbusho tu. Katiba iseme kuwa huko mbeleni kusiwepo na uwezekano wa kuanzisha serikali zaid ya JMT. Kama nchi nyingine itataka kujiunga na JMT mfano kama Rwandwa hivi sharti ifute userikali wake na iwe moja ya sehemu ya JMT.

Kwa leo ni haya.

Hii nimeipenda sana, sema hata hivo sioni sababu ya kua na hayo majina hata kwenye hizo sehemu za kudumu kwa ukumbusho, history inatosha tu kwani mtu akiwa anasoma kuhusu Tanzania atajua kabisa neno lenyewe limetokana na kuunganisha Tanganyika na Zanzibar. Tukisema tuwe na serikali tatu, hiyo serikali ya Muungano itafika kipindi iwe na nguvu nyingi sana za kuweza kuvunja muungano kabisa na hilo swala laweza kutokea, swala ni kupata maoni kwa wananchi, watu wengi wanataka muungano uwepo sasa ifutwe swala la serikali mbili tutambue moja tu na rais awe moja regardless atatoka upande gani, system iwe moja, cha ajabu tuna vitu vingi tunatofautiana afu tunakaa kusema nchi moja nchi moja,
 
Watanzania wenzangu nami pia napenda kuwaunga mkono CHADEMA kwa kuviona vipengele muhimu kwa
maslahi ya taifa letu . pendekezo langu ni moja tu ktk mapendekezo yote ya baraza la katiba la chadema ambalo ni juu
ya umri wa mgombea ubunge uaanzie miaka 21 na si 18 km ilivopendekezwa na baraza za chadema. Aidha mengine yote ni sawa ambae atapinga ni mchawi mkubwa kwa kizazi kijacho. asante.
 
Watanzania wenzangu nami pia napenda kuwaunga mkono CHADEMA kwa kuviona vipengele muhimu kwa
maslahi ya taifa letu . pendekezo langu ni moja tu ktk mapendekezo yote ya baraza la katiba la chadema ambalo ni juu
ya umri wa mgombea ubunge uaanzie miaka 21 na si 18 km ilivopendekezwa na baraza za chadema. Aidha mengine yote ni sawa ambae atapinga ni mchawi mkubwa kwa kizazi kijacho. asante.

n.b: Raia yeyote mwenye UMRI wa Miaka 18 na timamu ana HAKI SAWA YA kuchaguliwa au Kuchagua. Kwanini Atengwe? Hii inasaidia AJUE wajibu wa KULINDA na KUWAJIBIKA ipasavyo kwa TAIFA LAKE.
 
Makene nimekupata ila natamani sana nafasi ya rais iheshimiwe, miaka cdm iliyopendekeza ya 18 ni chache sana at least 30 hapa mtu anaweza kufanya maamuzi bila mihemko. ntatuma maoni yangu mengine via cdm email adress
 
Katiba itaje mikataba yote ipitie kwa bunge na kuwe na uwazi, rais apingwe mahakaman, iwekwe kwenye katiba au sheria kukataa ushoga na maswala ya dini,kwan viongoz au watawala wamekuwa wakifanya dini ndo mtaji wake,kwamba kiongoz yeyete atakaezungumzia udini au kuna watu wadini akamatwe akatoe uthibitisho mahakaman
 
Tunashukuru kwa taarifa bwana Makene. Mie nitaanza ni lile la serikali tatu (nakubaliana na mapendekezo ya wananchi yaliyopitishwa na tume), mawaziri wasitokane na wabunge (kama ilivyo katika rasimu), mgombea binafsi (kama ilivyo katika rasimu) na pia napendekeza wakuu wote wa wilaya wasiwepo na tuwe na serikali za majimbo.

Maoni hayo nitayawasilisha kwa njia sanifu baada ya kutupatia muongozo zaidi.

Vitambulisho vya Taifa viharakishwe nchi nzima na ndo vitumike kupigia kura 2015 kwani serikali iliyopo madarakani inatumia mwanya huo kuwabana wapiga kura warudi walikojiandikisha.
 
Binafsi nina mapendekezo yafuatayo:
1. Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi aombe kazi Mahakama Kuu na achaguliwe na vyama vyote vya siasa vyenye angalau wabunge wa kuchaguliwa watatu kwa idadi ya uwakilishi ulio sawa. Yaani kila chama kitateua idadi itakayoamuliwa na bunge ya wawakilishi wa kupiga kura ya kumteua Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na Msajili. Kwa mfano CCM ikitoa Hamsini, CUFT, TLP CHADEMA na NCCR vitoe wawakilishi wa idadi hiyohiyo kumpigia kura mgombea nafasi hiyo mmoja kati ya watano watakuwa wamechujwa na jopo la majaji kumi watakaoteuliwa na Jaji Mkuu. Kwa njia hiyo tutaepuka kuwapata watu wa aina ya kina Tendwa waliolithibitishia taifa kweupee juu ya ukada wao wa chama fulani. Washindi wa nafasi hizo mbili (Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na Msajili wa vyama vya siasa) ataapishwa na Jaji Mkuu na si Rais.
Mtindo huu huu unaweza tumika kumpata Spika na Naibu wake wasio wanafiki na mashabiki wa chama fulani.
2. Kila raia wa Tanzania awe na haki ya kupiga kura popote atakapokuwa, iwe ndani au nje ya nchi. Na liwe kosa la uhaini kumfanyia mizengwe mtu ili kumnyima haki yake hiyo.
2. Adhabu ya kosa la kubadilisha matokeo yaani (kuiba, kughushi au kutumia hila na udanganyifu wenye lengo la kubadili matokeo ya maamuzi huru ya wananchi) iwe ni kosa la uhaini lenye adhabu ya kifungo cha maisha au kifungo kisichopungua miaka ishirini jela na kazi ngumu.
3. Nafasi za Wakuu wa Wilaya na mikoa zipatikane kwa kupigiwa kura kwenye uchaguzi mkuu; yaani kuwepo na majina ya wagombea wawili kila jimbo watakaopigiwa kura na mshindi ndiyo awe Mkuu wa Wilaya, na mengine mawili wa eneo la kimkoa kwa nafasi ya ukuu wa Mkoa husika ambapo mshindi atakuwa Mkuu wa Mkoa husika.
 
11; 75(d) UCHAGUZI WA RAIS.
Napendekeza umbri wa mgombea uraisi uanzie miaka 40 na kuendelea.

Pia napendekeza kura za kumchagua mbunge zisipigwe kwa kuzigatia jinsia (jimbo moja kusimamisha jinsia mbili ) hicho kitu sio kizuri kwani ni vzuri kumchagua kiongozi kwa kuzingatia uwezo na sio sura au jinsia.
 
asante kwa nafasi hii,
1. Kuhusu umri wa kugombea uraisi, napendekeza iwe miaka 40 na si 18
2. kuhusu Muungano, napendekeza mambo ya muungano yapungue kabisa na yabaki matatu
3. Mgombea binafsi ruksa
4. tume huru ya uchaguzi, kwa maana kwamba wananchi kupitia wawakilishi wao ndio waweze kuchagua wajumbe wa tume.
asanteni kwa kunisikiliza
 
asante mkuu kwa kutuhabarisha

pendekezo langu ni lile linaoloonesha umri kwa mtu anayetaka ubunge, kuanzia miaka 18 na sio 25
kwa upande wangu mm naona umri wa kuanzia miaka 18 mtu huyo anakuwa yuko shuleni je hatamudu
vipi masomo na uwabikaji katika jimbo atakalogombea na kushinda? je masomo na ubunge ni wapi na wapi jamani?

Mtazamo: Pendekezo langu ni kwamba ni muhimu mtu anayetaka kuwa mbunge angeazia miaka 25 na kuendelea na sio hiyo miaka 18 iliyopendekezwa kwenye rasimu.
 
Kweli CDM ni nguvu ya umma,

TAHADHARI: Maoni haya tunataka yafanyiwe kazi, maana leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mza chini ya uongozi wa Mwenyekiti tumesikia kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba keshaanza kusema hatazingatia maoni ya Helkopta. Tunatoa maoni yetu juu ya hii Rasimu then tunasubiri hiyo rasimu ya pili, kama maoni hayatazingatiwa hiyo Katiba tutaikataa kwa nguvu zote.
Nawapongeza CDM kwa kuja na mpango huu wa kuwafikia Watanzania wote ili watoe maoni yao.

hamna jipya .maoni kwamikutano ya hadhara
 
Nakubaliana na vipengele vyote kasoro

11 ... Umri wa kugombea urais usiwe chini ya miaka 40

13 ... Wabunge wa viti maalum wasiwepo kabisa, na kusiwe na hili pendekezo la wabunge wawili kila jimbo .... Kila mbunge awe ni wa kuchaguliwa na si upendeleo wa aina yeyote!

14 ... umri wa kugombea ubunge usiwe chini ya miaka 25, na iongezwe lazima wawe na kisomo cha at least degree moja toka vyuo vinavyotambulika kimataifa

15 ... mbunge akifukuzwa na chama asipoteze ubunge hii ni kuzuia uhuni wa kukomoana. vyama viwe makini wanapopendekeza wagombea wao. Ila mbunge akikiuka mambo mengine ya kisheria apoteze ubunge wake


nyongeza:
idadi ya wabunge iwe fixed na kutegemea ratio sawa ya wananchi wanaowaongoza ... itokana na census ya kila miaka 10

kuwe na check and balances zinazoheshimika kati ya excutive branch, judicial na bunge

idadi ya wizara iwe fixed na iwepo kikatiba, sio kila rais aamke na kujiundia wizara lukuki
 
Sijaelewa huu uzi umewekwa Sticky kwa ajili ya Chadema tu.

Nadhani katiba hii siyo ya Chadema ni ya Tanzania nzima.

Sisi ambayo siyo wafuasi wa Chadema hatuna nafasi kwenye huu uzi.

Kila la heri kwenye maoni yenu ya katiba.
 
Back
Top Bottom