MUHIMU: Tuma maoni yako ya Rasimu ya Katiba Mpya, Mabaraza ya CHADEMA

MUHIMU: Tuma maoni yako ya Rasimu ya Katiba Mpya, Mabaraza ya CHADEMA

Napendekeza serikari moja tu yaani zenji pawe mikoa tu au Kama itashindikana utawala wa majimbo yaani Zenji atawale Gavana au waziri mkuu na Tz bara atawale Gavana aishi pale magogoni na Rais awe mmoja tu ahamie Dodoma kwa makazi ya kudumu yaani mfumo wa Muungano uwe Digtal kama miungano ya kule USA na UK na Kama itashindikana hii Nina Imani kero za muungano hazitakwisha kamwe
 
Asante sana MAN OF LETTERS, ngoja niainishe hoja zangu vizuri.
Kamanda Mjuni Lwambo

Naona una munkari kweli kweli kushiriki Mabaraza ya Katiba Mpya ya CHADEMA. Utaratibu wa hapa utawekwa. Wananchi walioko hapa watawekewa utaratibu wao maalum.

Kwa sasa, kwa kutumia emails na namba ya simu, ni kama ilivyoelezwa hapo juu...

Karibu.
 
Aksante sana mkuu Makene,maoni yangu ni machache na ni kama ifuatavyo:

A) Napendekeza serekal 3 tanganyika,zanzibar na ile ya muungano,ikishndkana basi serekal moja tu kila mtu akae kwake
B) Mfumo wa serekali uwe wa majimbo
C) Rasilimal asili zitumike kwa maendeleo ya jimbo husika huku serekal kuu ikipata parcent flan kwa maendeleo ya majimbo mengne yasiyokua na rasilimal hzo kama madin mbuga na mengneyo
D) Mawaziri wasiteuliwe bali waombe kazi kutokana na taaluma na wizara husika pia pawepo tume maalumu tena huru ya kuwadahili
E) Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya waondoke pawepo maseneta
F) Wananchi wawe na mamlaka ya kumwajibsha mbunge wao kama hatawatetea na kuwaletea maendeleo watu wake
G) Rais apunguziwe mamlaka kiutendaji hasa ktk teuzi zake
H) Wananchi wawe na nguvu ya kumshtak Rais hasa atakapokutwa na kashfa za ufisadi, wizi pia kinga ya Rais iondolewe pindi anapomaliza muda wake.

Nitarud tena badae.
 
At least for once after half a century that Tanzanians are up in arms about wanting a new constitution, I am just wondering if they(common wananchi) know what exactly they want written down.

I think it would be prudent to know what was in the old one first and identify the issues that caused it to fail, and then decide what amendments to make otherwise Tanzanians might be duped by some know-it-all politicians who labour for their stomachs day in and day out and are only interested in rilying to Muungano(Tanganyika na Zanzibar) to push for amendments that would empower them even more and enable them to rob Tanzania blind!


My people are destroyed for lack of knowledge - Hosea 4:6
 
Tume huru ya uchaguzi ni muhimu sana na iwe angalau kama ile ya kenya. Wajumbe wa tume waombe hiyo kazi na wafanyiwe interview ya wazi kwenye meadia hasa television ya taifa na majaji watoke kati yao nje ya Tanzania. Pia maoni ya wananchi yatumike kupima uadilifu wao kwenye mchujo wa awali
 
maoni yangu....
vyama vyote vyenye mfumo wa kidini(iwe dhahiri au kificho) vifutwe
vyama vyote vyenye kuendesha siasa za kigaidi na kuua wanachama wake kwa ajili ya kujipatia umaarufu, vifutwe
 
Ahsante kwa kupata nafasi hii ya kutoa maoni juu ya katiba tunayoitaka. Napendekeza yafuatayo yaingizwe kwenye katiba:- (1) Kuwepo serikali tatu kama ilivyo kwenye rasimu ya katiba (2) Kuwepo wagombea binafsi (3) Mikataba yote ambayo nchi inaingia na wawekezaji wa ndani na wa nje lazima ijadiliwe na kupitishwa na bunge kabla ya kusainiwa.
 
Napendekeza mambo yafuatayo" 1. Kuwe na presidential debate kwa wagombea urais angalau mitatu katika mikoa kadhaa,pia kuwe na vice presidential debate vilevile, mgombea au chama kisichoshiriki kiondolewe mara moja kwenye nafasi ya kugombea! 2. Mbunge ama diwani akifukuzwa na chama chake aendelee kuwa mbunge au diwani, bali akijiondoa kwenye chama apote pia ubunge au udiwani! Bila kusahau urais pia! 3. Kuandikisha kuwa mpiga kura iwe ni lazima kwa kila mtanzania aliyetimiza umri wa kupiga kura! Pia spika asiwe mbunge au mwanachama wa chama chochote cha siasa!
 
7. Mawaziri wote wateuliwe na wasiwe wabunge. na neno chama cha mapinduzi lisisike kwenye maneno yao wawakilishapo report au budget au popote kwa lengo la kusifu au nn!!

kamanda usihofu,hawatakuwepo hawa, wametumaliza vya kutosha
 
Naunga mkono 100% mapendekezo ya CHADEMA, na napendekeza kwamba SAFARI zote za rais zihojiwe moja kwa moja na BUNGE katika maeneo ya
1. Sababu ya safari
2. Anapoelekea wap?
3. Gharama zake
4. Faida ya safar hiyo
kwa nchi. nk

*Dharura zitazamwe..
Pia itungwe sheria ya kusimamia hilo.
 
Walimu,mawaziri na wabunge nao watoto wao wasome shule ya serikali
 
nakubaliana kwa kiasi kikubwa na mapendekezo ya chadema ila uraia ubaki wa nchi moja,nafasi ya mke wa rais katiba ieleze kuwa atabaki na mambo ya kijamii lakini sio kama sasa eti na yeye anakuwa kama rais,rasilimali muhimu kama madini,mafuta,gesi,upepo,joto ardhi,wanyama,mbunga,lazima mikataba iwe wazi kwa umma wote,bunge lazima lijadili na kupitia.serikali lazima imiriki angalau 30%ya hisa zote ktk kila mradi ktk sekta hizo ambazo ni za bure kwa vile mali ni zetu.RAIS ASHITAKIWE .
 
Naomba cheo cha wakuu wa wilaya na Mikoa kifutwe au isiwe viongozi wa kisiasa bali wa umma kwa taaluma zao
 
mshahara wa rais na viongozi wote ijulikane posho zao kiasi gani,wanalipa kodi kiasi gani?(2)misamaha ya kodi isiwepo kama itakuwepo kidogo sana tena bunge lijadili na kuidhinisha(3)shule za kata zisiwepo kabisa zirudishwe shule za kitaifa(4)makao makuu yawe dodoma(6)viti maalum visiwepo(7)idadi ya wizara lazima zijulikane kikatiba 12 zinatosha sana(8)uchaguzi wa rais lazima ashinde kwa zaidi 50% na ruhusa kuhojiwa mahakamani(8)barozi zipungue(9)rais asiteue kila sehemu mfano vyuo vikuu wanataaluma ndo wamchague mkuu wa chuo,majaji ndo wamchague jaji mkuu
 
mshahara wa rais na viongozi wote ijulikane posho zao kiasi gani,wanalipa kodi kiasi gani?(2)misamaha ya kodi isiwepo kama itakuwepo kidogo sana tena bunge lijadili na kuidhinisha(3)shule za kata zisiwepo kabisa zirudishwe shule za kitaifa(4)makao makuu yawe dodoma(6)viti maalum visiwepo(7)idadi ya wizara lazima zijulikane kikatiba 12 zinatosha sana(8)uchaguzi wa rais lazima ashinde kwa zaidi 50% na ruhusa kuhojiwa mahakamani(8)barozi zipungue(9)rais asiteue kila sehemu mfano vyuo vikuu wanataaluma ndo wamchague mkuu wa chuo,majaji ndo wamchague jaji mkuu

taifa lazima liwe na ukomo wa kukopa na mikopo yenyewe lazima ipate ruhusa ya bunge
 
(10)Taifa lazima liwe na ukomo wa kukopa na kukopa kuwe kwa ajili ya miradi ya maendele kwa ruhusa ya bunge kujadili na kuridhia
 
Serikali ya majimbo ni muhimu,tume huru ya uchaguzi,wakuu wa mikoa wafutiliwe mbali.
 
Napendekeza chaguzi zote zifanyike siku za kazi. Imekuwa ni kawaida tangu muda mrefu chaguzi mbalimbali za viongozi wa kisiasa zinafanyika siku ya Jumapili. NACHUKIA SANA KASUMBA HII. Tujifunze kwenye Nchi za wenzetu. Kwa mujibu wa dini zetu na madhehebu yetu hapa nchini, asilimia 99 ya wafuasi wa dini mbalimbali wanaabudu siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Hivyo basi ni vema uchaguzi ukafanyika siku yoyote kati ya hizi:- Jumatatu - Alhamisi. Nasema hivi kwa sababu kuna watu wengi huwa wanshindwa kujitokeza kupiga kura kutokana na kubanwa na ratiba za Ibada.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom