Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kinaanza rasmi kuendesha Mabaraza ya Katiba, ambapo wananchi wote watashirikishwa kujadili na kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba Mpya, kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo;
====================
[TABLE="width: 942"]
[TR]
[TD]S/N
[/TD]
[TD]IBARA
[/TD]
[TD]MAPENDEKEZO YA CHAMA (CHADEMA)
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1.[/TD]
[TD]2 Eneo la Jamhuri ya. Muungano[/TD]
[TD]Neno Tanzania Bara liondolewe na kuandika Tanganyika kila palipo na neno Tanzania Bara.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]4(1) Lugha ya Taifa[/TD]
[TD]Lugha ya Taifa itakuwa Kiswahili na miswada/sheria zote zitaandikwa kwayo pamoja na lugha zingine[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3.[/TD]
[TD]5 Tunu za Taifa[/TD]
[TD]Viongozwe vipengele hivi demokrasia ya vyama vingi, utawala wa sheria,uwazi na haki za binadamu.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]4.[/TD]
[TD]6(2) Daftari la wapiga kura[/TD]
[TD]Liwe mahali ambapo kila raia akifikisha miaka 18 ana andikishwa wakati wowote.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]5.[/TD]
[TD]17&85 watumishi wa umma.[/TD]
[TD]Mishahara ya watumishi wote wa umma pamoja Rais ijulikane.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]6.[/TD]
[TD]32 (2) haki ya kuandamana[/TD]
[TD]Kila mtu ana haki kwa amani na bila kubeba siraha kukusanyika/kuandamana kuzuia njia na kuwasilisha malalamiko.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]7.[/TD]
[TD]35(e) kugoma[/TD]
[TD]Kugoma au kusitisha nguvu kazi yake mahali pa kazi.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]8.[/TD]
[TD]47 Haki ya kumiliki rasilimali[/TD]
[TD]Iongezwe ibara mpya ya 48 haki ya kumiliki rasilimali za asili zote Ardhi, Madini, mafuta na gesi, maji na misitu na wanyama pori.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]9.[/TD]
[TD]60 (7)nyongeza[/TD]
[TD]Kiongozwe kifungu cha 7 Maadili na miiko ya uongozi na utumishi wa umma, Haki za binadamu na wajibu wa raia. Tume huru ya Taifa ya uchaguzi.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]10.[/TD]
[TD]Serikali tatu (3)[/TD]
[TD]Kuwepo serikali ya Muungano, serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanganyika.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]11.[/TD]
[TD]75(d) Uchaguzi wa rais.[/TD]
[TD]Umri wa mgombea urais uwe miaka kumi na nane[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]12.[/TD]
[TD]83(i) kinga dhidi ya mashtaka ya Rais.[/TD]
[TD]Wakati wowote Rais akiwa madarakani na baada ya kuacha kushika madaraka aweze kushtakiwa.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]13.[/TD]
[TD]105 (2) (b) wabunge wa kuteuliwa[/TD]
[TD]Kipengele hiki kifutwe na badala yake iwe wabunge 20 watakaochaguliwa kutokana na uwiano wa kura zilizopigwa kwa vyama vya siasa.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]14.[/TD]
[TD]117(i) (a) Mgombea Ubunge[/TD]
[TD]Umri wa mgombea ubunge uwe miaka 18 na si 25 kama inavyopendekezwa.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]15.[/TD]
[TD]123(2) uwajibikaji wa mbunge.[/TD]
[TD]Hii ifutwe na kuongeza :mbunge aliyependekezwa na chama cha siasa atapoteza ubunge wake ikiwa atafukuzwa au kuvuliwa uanachama wa chama chake cha siasa.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]16.[/TD]
[TD]123(3) mbunge kuhama/kujiunga na chama cha siasa.[/TD]
[TD]Kuongeza ibara ndogo :endapo mbunge kwa ridhaa yake atajiondoa au kujivua uanachama wa chama cha siasa au kujiunga na chama kama alikuwa mgombea huru basi atapoteza sifa ya kuwa mbunge.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]17.[/TD]
[TD]124 adhabu kwa mbunge[/TD]
[TD]Kuondoa kabisa ibara hiyo na badala yake iseme wananchi wa jimbo au kata watakuwa na haki ya kuwaondoa madarakani kwa sababu na kwa kufuata utaratibu na sheria.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]18.[/TD]
[TD]182 Tume Huru ya uchaguzi.[/TD]
[TD]Kuongeza wajumbe wa vyama vya Mawakili na vyama vya siasa.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]19.[/TD]
[TD]184 Tume Huru ya Uchaguzi[/TD]
[TD]Watumishi wote wa Tume Huru ya uchaguzi wasiwe watumishi wa serikali.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]20.[/TD]
[TD]234 Mkurugenzi wa usalama wa Taifa.[/TD]
[TD]Ateuliwe baada ya kuthibitishwa na Bunge[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]21.[/TD]
[TD]Nyongeza[/TD]
[TD]Kuanzishwa kwa mchakato wa katiba ya Tanganyika, kuundwa TUME ya Katiba ya Tanganyika.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Maoni yangu kwa baadhi ya Mapendekezo ya CDM;
Maoni.32 (2) haki ya kuandamana
Kila mtu ana haki kwa amani na bila kubeba siraha kukusanyika/kuandamana kuzuia njia na kuwasilisha malalamiko.
Badala yake Ibara ya 9 ya Maoni yangu napendekeza kuongeza na itaisomeka;
9.-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia mamlaka ya nchi (Serikali, Bunge na Mahakama) isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.
(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya Ibara ndogo ya (1) ni batili na ni kitendo cha uhaini isipokuwa Maandamano yoyote ya Amani ya Umma ya kudai haki au kuondoka madarakani kwa maamlaka ya Nchi hayatachukuliwa kuwa ni Uhaini.
(3) Wakati wote wote wa maandamano ya Amani ya Wananchi, Mamlaka ya Nchi haitachukua wala kutumia Nguvu ya dola kuyazima au kuvuruga maandamano isipokuwa inaweza kuyapinga Maandamano kwa kufungua shauri Mahakamani ya juu au kuitisha Kikao cha dharua cha Bunge ilikupata Uamuzi wa hatua itakayochukuliwa.
(4) Kwa vyovyote vile na wakati wote wote ule wa Maandamano ya Amani ya Wananchi itakuwa ni marufuku kwa washiriki au mshiriki kuwa na silaha ya aina yoyote.
35(e) kugoma
Kugoma au kusitisha nguvu kazi yake mahali pa kazi.
Maoni ; Hapana kwa mapendekezo haya; Ukiangalia 35(4) inatosha kulinda haki hiyo na hapa waheshimiwa wanatakiwa wawe na dhamira safi.
(4) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu haki za wafanyakazi na utaratibu utakaowezesha wafanyakazi kutumia haki zao.
60 (7)nyongeza
Kiongozwe kifungu cha 7 Maadili na miiko ya uongozi na utumishi wa umma, Haki za binadamu na wajibu wa raia. Tume huru ya Taifa ya uchaguzi.
Hapa nadhani kuna makosa ya kiuandishi maana Nyongeza inayorejewa tayari ina mambo saba; NYONGEZA [Imetajwa katika Ibara ya 60]
Mambo ya Muungano
________________
1. Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
3. Uraia na Uhamiaji;
4. Sarafu na Benki Kuu;
5. Mambo ya Nje;
6. Usajili wa Vyama vya Siasa; na
7. Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na mambo ya Muungano.
ambayo inaweka masharti mapya katika sheria nyingine.
8. Maadili na miiko ya uongozi na utumishi wa umma, Haki za binadamu na wajibu wa raia naTume huru ya Taifa ya uchaguzi.