MUHIMU: Tuma maoni yako ya Rasimu ya Katiba Mpya, Mabaraza ya CHADEMA

Sijaelewa huu uzi umewekwa Sticky kwa ajili ya Chadema tu.

Nadhani katiba hii siyo ya Chadema ni ya Tanzania nzima.

Sisi ambayo siyo wafuasi wa Chadema hatuna nafasi kwenye huu uzi.

Kila la heri kwenye maoni yenu ya katiba.

Mkuu siamini kama vyama vingine vililetewa mapendekezo halafu vikashindwa kupewa haki hapa JF.

Asante kwa kutupisha mkuu.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kinaanza rasmi kuendesha Mabaraza ya Katiba, ambapo wananchi wote watashirikishwa kujadili na kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba Mpya, kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo;

1. Mikutano ya hadhara, itakayoanza leo katika maeneo mbalimbali ya nchi, ikiongozwa na timu mbili za viongozi wakuu,
Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibroad Slaa.

Mikutano hiyo itafanyika nchi nzima. Ratiba ya mikutano yote, itaendelea kutolewa kwa umma, kupitia vyombo vya habari (mainstream & social media).

2. Kutuma ujumbe mfupi kwa simu. Mwananchi anaweza kutuma maoni yake ya Katiba Mpya kupitia simu ya mkononi, kwenye NAMBA HII YA SIMU; 0789 24 82 24.

3. Email; chademamaoni@gmail.com

4. Kwa kupitia JamiiForums, toa maoni yako kwenye hii thread, ukishatoa maoni; jaza fomu ifuatayo;

Fomu ya maoni juu ya Rasimu Katiba Mpya (CHADEMA) - 2013

ili kukubaliana au kutokubaliana na vipengele vilivyoonyeshwa kwenye Jedwali.

Mfumo huu utatumika kwa facebooks, twitter, group emails, k.m mabadiliko, wanabidii n.k,

====================

[TABLE="width: 942"]
[TR]
[TD]S/N

[/TD]
[TD]IBARA

[/TD]
[TD]MAPENDEKEZO YA CHAMA (CHADEMA)

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1.
[/TD]
[TD]2 Eneo la Jamhuri ya. Muungano
[/TD]
[TD]Neno Tanzania Bara liondolewe na kuandika Tanganyika kila palipo na neno Tanzania Bara.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.
[/TD]
[TD]4(1) Lugha ya Taifa
[/TD]
[TD]Lugha ya Taifa itakuwa Kiswahili na miswada/sheria zote zitaandikwa kwayo pamoja na lugha zingine
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3.
[/TD]
[TD]5 Tunu za Taifa
[/TD]
[TD]Viongozwe vipengele hivi demokrasia ya vyama vingi, utawala wa sheria,uwazi na haki za binadamu.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]4.
[/TD]
[TD]6(2) Daftari la wapiga kura
[/TD]
[TD]Liwe mahali ambapo kila raia akifikisha miaka 18 ana andikishwa wakati wowote.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]5.
[/TD]
[TD]17&85 watumishi wa umma.
[/TD]
[TD]Mishahara ya watumishi wote wa umma pamoja Rais ijulikane.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]6.
[/TD]
[TD]32 (2) haki ya kuandamana
[/TD]
[TD]Kila mtu ana haki kwa amani na bila kubeba siraha kukusanyika/kuandamana kuzuia njia na kuwasilisha malalamiko.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]7.
[/TD]
[TD]35(e) kugoma
[/TD]
[TD]Kugoma au kusitisha nguvu kazi yake mahali pa kazi.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]8.
[/TD]
[TD]47 Haki ya kumiliki rasilimali
[/TD]
[TD]Iongezwe ibara mpya ya 48 haki ya kumiliki rasilimali za asili zote Ardhi, Madini, mafuta na gesi, maji na misitu na wanyama pori.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]9.
[/TD]
[TD]60 (7)nyongeza
[/TD]
[TD]Kiongozwe kifungu cha 7 Maadili na miiko ya uongozi na utumishi wa umma, Haki za binadamu na wajibu wa raia. Tume huru ya Taifa ya uchaguzi.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]10.
[/TD]
[TD]Serikali tatu (3)
[/TD]
[TD]Kuwepo serikali ya Muungano, serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanganyika.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]11.
[/TD]
[TD]75(d) Uchaguzi wa rais.
[/TD]
[TD]Umri wa mgombea urais uwe miaka kumi na nane
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]12.
[/TD]
[TD]83(i) kinga dhidi ya mashtaka ya Rais.
[/TD]
[TD]Wakati wowote Rais akiwa madarakani na baada ya kuacha kushika madaraka aweze kushtakiwa.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]13.
[/TD]
[TD]105 (2) (b) wabunge wa kuteuliwa
[/TD]
[TD]Kipengele hiki kifutwe na badala yake iwe wabunge 20 watakaochaguliwa kutokana na uwiano wa kura zilizopigwa kwa vyama vya siasa.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]14.
[/TD]
[TD]117(i) (a) Mgombea Ubunge
[/TD]
[TD]Umri wa mgombea ubunge uwe miaka 18 na si 25 kama inavyopendekezwa.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]15.
[/TD]
[TD]123(2) uwajibikaji wa mbunge.
[/TD]
[TD]Hii ifutwe na kuongeza :mbunge aliyependekezwa na chama cha siasa atapoteza ubunge wake ikiwa atafukuzwa au kuvuliwa uanachama wa chama chake cha siasa.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]16.
[/TD]
[TD]123(3) mbunge kuhama/kujiunga na chama cha siasa.
[/TD]
[TD]Kuongeza ibara ndogo :endapo mbunge kwa ridhaa yake atajiondoa au kujivua uanachama wa chama cha siasa au kujiunga na chama kama alikuwa mgombea huru basi atapoteza sifa ya kuwa mbunge.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]17.
[/TD]
[TD]124 adhabu kwa mbunge
[/TD]
[TD]Kuondoa kabisa ibara hiyo na badala yake iseme wananchi wa jimbo au kata watakuwa na haki ya kuwaondoa madarakani kwa sababu na kwa kufuata utaratibu na sheria.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]18.
[/TD]
[TD]182 Tume Huru ya uchaguzi.
[/TD]
[TD]Kuongeza wajumbe wa vyama vya Mawakili na vyama vya siasa.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]19.
[/TD]
[TD]184 Tume Huru ya Uchaguzi
[/TD]
[TD]Watumishi wote wa Tume Huru ya uchaguzi wasiwe watumishi wa serikali.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]20.
[/TD]
[TD]234 Mkurugenzi wa usalama wa Taifa.
[/TD]
[TD]Ateuliwe baada ya kuthibitishwa na Bunge
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]21.
[/TD]
[TD]Nyongeza
[/TD]
[TD]Kuanzishwa kwa mchakato wa katiba ya Tanganyika, kuundwa TUME ya Katiba ya Tanganyika.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Ongeza na hili:katiba itamke kwamba ni kosa la jinai kwa raia aliye na umri wa kupiga kura asipopiga kura,hii itawawia vigumu magamba kununua shahada za kupigia kura
 
Rais katika jambo lolote la kitaifa linalohusu kazi zake kama rais hatafanya uamuzi kinyume au nje ya ushauri wa vyombo vilivyoundwa kisheria kwa ajili ya kumshauri,aweza kushtakiwa na kupoteza uhalali wa kuongoza pindi bunge likithibitisha kuwa uamuzi alioufanya kinyume na ushauri umeleta athari kiuchumi,kijamii n.k
 
Naomba katiba ijayo pamoja na kuweka haki za binadamu kama za kutembea,kazi na nyingine zote haki ya kuishi itambulike tangu mtoto akiwa tumboni . Sababu wasichana wamekua wakitoa mimba hovyo na vichanga kuwekwa majalalani sheria hazichukuliwi.

Pamoja na hayo ndani ya hosptali maalum za kutoa vichanga vilivyoaribikia tumboni zilindwe ( MARIA STOPERS HOSPTALS) hawa wamekua majangili ya kutoa vichanga tumboni kwa wanafunzi ili kuwatunzia heshima waheshimiwa waliowapatia mimba hizo.
 
Wananchi, maelfu kwa maelfu wanazidi kujitokeza kwenye Mabaraza Huru ya Katiba Mpya, kutoa maoni yao kwenye rasimu.

Wale ambao hawajafikiwa na mikutano ya hadhara, wanaweza kuendelea hapa;

Ujumbe mfupi wa simu; 0789248224 na

Email; chademamaoni@gmail.com
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1376904401.944708.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1376904401.944708.jpg
    131.6 KB · Views: 32
  • ImageUploadedByJamiiForums1376904493.095501.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1376904493.095501.jpg
    128.4 KB · Views: 35
Watanzania wengi wanaendelea kujitokeza kushiriki Mabaraza Huru ya Rasimu ya Katiba Mpya, yanayoendeshwa na CHADEMA;
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1376923639.454270.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1376923639.454270.jpg
    65.3 KB · Views: 29
Mkuu Tumaini Makene na Kurugenzi ya Habari

Haya hapa chini ni maoni yangu ambayo bado naendelea kudadafua kadri muda utakavyo ni ruhusu ila michango ya Wadau inahitajika maana Rasimu ya Katiba kwa jinsi ilivyo ina maeneo mengi yenye kuhitaji dhamira safi kuwa kuiweka sawa na kutuwezesha kuitumia kwa kati ya miaka 25-50 bila kuwekaweka viraka.

2. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari.

2. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanganyika ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari.

9.-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia mamlaka ya nchi isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.
(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya Ibara ndogo ya (1) ni batili na ni kitendo cha uhaini kama itakavyoelezwa katika sheria za nchi.

9.-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia mamlaka ya nchi (Serikali, Bunge na Mahakama) isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.

(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya Ibara ndogo ya (1) ni batili na ni kitendo cha uhaini isipokuwa Maandamano yoyote ya Amani ya Umma ya kudai haki au kuondoka madarakani kwa maamlaka ya Nchi hayatachukuliwa kuwa ni Uhaini.

(3) Wakati wote wote wa maandamano ya Amani ya Wananchi, Mamlaka ya Nchi haitachukua wala kutumia Nguvu ya dola kuyazima au kuvuruga maandamano isipokuwa inaweza kuyapinga Maandamano kwa kufungua shauri Mahakama ya juu au kuitisha Kikao cha dharua cha Bunge ilikupata Uamuzi wa hatua itakayochukuliwa ili kulinda Amani na kuepusha Taifa na Madhara kwa kuzingatia Ibara za Katiba hili.

(4) Kwa vyovyote vile na wakati wote wote ule wa Maandamano ya Amani ya Wananchi itakuwa ni marufuku kwa washiriki au mshiriki kuwa na silaha ya aina yoyote.

10.-(1) Malengo ya Taifa yaliyoainishwa ndani ya Katiba hii yatakuwa ni mwongozo kwa Serikali, Bunge, Mahakama, vyama vya siasa, taasisi, asasi na mamlaka nyingine na kwa kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine yoyote na katika utekelezaji wa uamuzi wa kisera kwa madhumuni ya kujenga jamii huru, makini na iliyo bora.
(2) Serikali itatoa taarifa Bungeni si chini ya mara moja katika kila mwaka, kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya nchi ili kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya Taifa yaliyoainishwa katika Katiba hii.

Maoni;
10.-(1) Malengo ya Taifa yaliyoainishwa ndani ya Katiba hii yatakuwa ni mwongozo kwa Serikali, Bunge, Mahakama, vyama vya siasa, taasisi, asasi na mamlaka nyingine na kwa kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine
yoyote na katika utekelezaji wa uamuzi wa kisera kwa madhumuni ya kujenga jamii huru, makini na iliyo bora.
(2) Serikali itatoa taarifa Bungeni si chini ya mara moja katika kila mwaka, kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya nchi ili kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya Taifa yaliyoainishwa katika Katiba hii na Bunge litapewa nafasi ya kuijadili na kupiga kura ya kuikubali au kuikataa taarifa husika kwa kutumia Kanuni ya Bunge katika kufikia maamuzi.

11.-(1) Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha udugu, amani, umoja na utengamanowa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora na kujitegemea.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), lengo hilo kuu litaendelezwa na kuimarishwa katika nyanja zote kuu,ikijumuisha nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na
kimazingira.
(3) Katika kutekeleza malengo ya Taifa ya:

(c) kiuchumi, Serikali inachukua hatua zinazofaa ili:
(i) kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuondoa umaskini;
(ii) kuhakikisha kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha
kuwa utajiri wa Taifa unaendelezwa,unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya
wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;
(iii) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima,wafugaji na wavuvi;
(iv) kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na kukuza fursa za uwekezaji;
(v) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kukuza kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuhakikisha kuwa
wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli
zao;
(vi) kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa mazao kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, utafutaji na uendelezaji wa masoko ya mazao yao;
(vii) kuweka utaratibu mzuri wa upangaji na usimamiaji wa mizania ya bei za mazao na
pembejeo;
(viii) kuimarisha na kuendeleza uwekezaji wa ndani,upatikanaji wa pembejeo za kilimo, maeneo ya ufugaji na vifaa vya uvuvi;
(ix) kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa fursa na nafasi za wazi kwa watu wote na kuanzisha shughuli za kiuchumi na kukuza mazingira yaliyobora kwa ajili ya kuhamasisha sekta binafsi katika uchumi;
(x) kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anapata fursa ya kufanya kazi, kwa maana ya kufanya shughuli yoyote halali inayompatia kipato;
(xi) kuweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kujipatia
elimu na kuwa huru kupata fursa sawa ya kutafuta elimu katika fani anayoipenda hadi
kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake;

Maoni;
11.-(1) Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha udugu, amani, umoja na utengamano wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora na kujitegemea.

kuwa utajiri wa Taifa unaendelezwa,unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;

(iii) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa vikundi vya shughuli za Kiuchumi na kuwashirikisha katika hatua za kuandaa sera na Kanuni za shughuli husika.

(v) Kupitia Serikali za Washirika wa Muungano Serikali itaweka mazingira bora kwa ajili ya kukuza kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuhakikisha kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao;

(vii) kuweka utaratibu mzuri wa upangaji na usimamiaji wa mizania ya bei za mazao zitokanazo na shughuli za uchumi hasa kilimo,Ufugaji na Uvuvi .

(viii) kuimarisha na kuendeleza uwekezaji wa ndani kwa kuhakikisha ,upatikanaji wa Mitaji kwa ajili ya pembejeo za kilimo, madawa na majasho ya Mifugo na vifaa vya uvuvi;

(ix) kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa fursa na nafasi za wazi kwa kila mmoja kuanzisha shughuli za kiuchumi kwa kukuza mazingira yaliyo bora kwa ajili ya kuhamasisha sekta binafsi katika uchumi;

(xii) Serikali itahakikisha mkataba wowote utakaoingiwa na Serikali au taasisi zake na Serikali zingine au Makampuni binafsi unakuwa wa wazi kwa kuweka nakala ya mkataba husika kwenye magazeti na Tovuti ya Wizara/taasisi husika isipokuwa mikataba ya Ulinzi ambao Kamati ya Bunge ya Ulinzi ndiyo itakayo kuwa na Mamlaka ya kukagua kabla Mkataba wenyewe hauja sainiwa kuona kama masilahi ya Taifa yamezingatiwa au lah na kama Mkataba haukuzingatia masilahi ya Taifa Kamati itatoa mapendekezo ya kuzingatiwa na Wizara husika na Nakala kupewa Spika wa Bunge.

16.-(1) Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza, ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi,mali na thamani zake na madeni yake katika Tume ya
Maadili na Uwajibikaji.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza mali zake na madeni:
(a) yake binafsi;
(b) ya mwenza wake wa ndoa; na
(c) watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane,mara moja kila mwaka, au kadri itakavyoamuliwa na sheria.

Maoni;
16.-(1) Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza, ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi,mali na thamani zake na madeni yake katika Tume ya Maadili na Uwajibikaji.

(d) Utangazaji wa Mali za kiongozi kupitia kifungu cha 16(2); a na b ya Katiba hii utafanywa chini ya Kiapo na itakuwa Kosa la jinai kusema uongo.
(e) Bunge litatunga sheria itakayo simamia na kuwezesha Umma kuweza kuhakiki ukweli wa mali zilizotangazwa na Kiongozi wa Umma.

19. Masharti yaliyoainishwa katika Ibara za 13 mpaka 18 yatatumika pia kwa watumishi wa umma baada ya kufanyiwa marekebisho stahiki.

Maoni
;
19. Masharti yaliyoainishwa katika Ibara za 13, 18 na 20 ya Katiba hii yatatumika pia kwa watumishi wa umma na Bunge litatunga Sheria ya Tume ya Maadili ya Uongozi wa Umma itakuwa na Kanuni itakayosimamia Masharti ya Katiba hii.

Hii imewekwa hapa kwa ajili ya mrejeo wa maoni ya Ibara ya 19

20
.-(1) Bila ya kuathiri masharti yoyote ya Katiba hii, kiongozi yeyote wa Umma atapaswa kuheshimu na kutii maadili ya viongozi wa umma, ikiwemo Miiko ya Uongozi.
(2) Miiko ya Uongozi inayorejewa katika Ibara ndogo (1),itakuwa kama ifuatavyo:
(a) Kiongozi wa umma hatopaswa:
(i) kuvunja au kukiuka masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano;
(ii) kutoa au kupokea rushwa;
(iii) kujilimbikizia mali kinyume cha sheria;
(iv) kusema uongo au kutoa taarifa zisizo za ukweli;
(v) kutoa siri za Serikali kinyume na sheria isipokuwa zilizokinyume na Masilahi ya Umma kadri katiba hii ilivyoelekeza;
(vi) kutumia wadhifa, nafasi au cheo chake kwa manufaa yake binafsi, familia yake, ndugu, jamaa au marafiki zake au mtu yeyote aliye na uhusiano naye wa karibu;
(vii) kufanya vitendo vya uzembe, uvivu, ubaguzi,kiburi, dharau au unyanyasaji wa kijinsia.
(b) Kiongozi wa umma atapaswa:
(i) kuheshimu na kuendeleza dhana ya uwajibikaji wa pamoja, kwa viongozi wanaohusika; na
(ii) kuheshimu na kuendeleza maadili ya viongozi wa umma, ikijumuisha:
(aa) kuwa na tabia na mienendo inayokubalika katika jamii;
(bb) kuheshimu, kutunza na kulinda mali za umma; na
(cc) kutambua, kuheshimu na kuzingatia Kanuni za Maadili na Mienendo ya Watumishi wa Umma, Kanuni za Kudumu za Watumishi wa Umma, nyaraka za umma na miongozo mbalimbali ya Serikali kuhusu viongozi na watumishi wa umma.
(iii) kutenganisha shughuli za biashara na masuala yanayohusiana na uongozi.
(3) Kiongozi yeyote wa umma ambaye anatuhumiwa na kuthibitika kwa makosa ya:
(a) kimaadili;
(b) udhalilishaji wa mtu au wa kijinsia; na
(c) wizi au ubadhirifu wa mali za umma,atasimamishwa kazi mpaka suala lake litakapoamuliwa kwa mujibu wa sheria au taratibu nyingine zinazowahusu viongozi wa umma.

21.-(1) Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia katika ajira nyingine yoyote yenye malipo ya mshahara.
(2) Mtumishi wa umma haruhusiwi kuchaguliwa au kuteuliwa kushika madaraka katika chama cha siasa.
(3) Mtumishi wa umma aliyestaafu na anayepokea malipo ya pensheni kutokana na fedha za umma haruhusiwi kuwa mwenyekiti,mkurugenzi au mtumishi zaidi ya vipindi viwili katika:
(a) shirika au kampuni inayomilikiwa au kuendeshwa kwa fedha za umma; au
(b) chombo chochote cha umma

(2) Mtumishi wa umma haruhusiwi kuchaguliwa au kuteuliwa kushika madaraka katika chama cha siasa .
(3) Mtumishi wa umma aliyestaafu na anayepokea malipo ya pensheni kutokana na fedha za umma anaruhusiwa tu kuwa Mwenyekiti na si kwa zaidi ya vipindi viwili vya jumla ya miaka kumi katika;

(b) chombo chochote cha umma.
(4) Mtumishi wa Umma aliyewahi kuwa Mwenyekiti kwa mujibu wa Ibara hii baada ya kumaliza vipindi vyake vya kuwa Mwenyekiti hatabadilishiwa aina ya Pensheni badala yake atabaki na kuendelea kupokea Pensheni yake ya utumishi wa awali.

24.- (7) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa na unaozingatia misingi kwamba -

(a) wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote vinapohitajika kufanyiwa uamuzi na mahakama au mamlaka nyingine inayohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia atakuwa na haki ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria
kutokana na uamuzi wa mahakama au mamlaka nyingine inayohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu aliyehukumiwa kwa kutenda kosa hilo hadi itakapothibitika mahakamani kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chochote ambacho wakati alipotenda kitendo hicho hakikuwa ni kosa chini ya sheria;
(d) ni marufuku kwa mtu kupewa adhabu ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendeka;
(e) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu,heshima ya mtu na faragha itahifadhiwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi wa tuhuma na uendeshaji wa masharti ya jinai na katika shughuli nyingine ambazo mtu anakuwa katika kizuizi cha mamlaka ya nchi au katika
kuhakikisha utekelezaji wa adhabu; na
(f) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazotweza au kudhalilisha.

(d) ni marufuku kwa mtu kupewa adhabu ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo kisheria wakati kosa linalohusika lilipotendeka;
(e) haki ya usawa wa binadamu,heshima ya mtu na faragha itahifadhiwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi wa tuhuma na uendeshaji wa masharti ya jinai na katika shughuli nyingine ambazo mtu anakuwa katika kizuizi cha mamlaka ya nchi au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu; na

29.-(1) Kila mtu:
(a) anao uhuru wa-
(i) kuwa na maoni na kueleza fikra zake;
(ii) kufanya mawasiliano na vile vile anayo haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake;
(iii) ubunifu na sanaa;
(iv) kitaaluma na tafiti za kisayansi; na
(b) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu:
(i) matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi; na
(ii) utekelezaji wa mamlaka ya nchi kuhusu sera za kitaifa na shughuli ya maendeleo ya jamii; na
(iii) masuala mengine muhimu kwa jamii.
(2) Utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika Ibara ndogo ya (1), utajumuisha wajibu muhimu kwa mwananchi na wajibu huo unaweza kupunguza haki hizo kutokana na:
(a) vita au machafuko ya kisiasa; au
(b) propaganda kuhusu vita, ushawishi wa chuki kwa misingi ya rangi, ukabila, ubaguzi wa kijinsia, dini au masuala yoyote yanayoweza kuleta madhara kwa Taifa.

(b) propaganda kuhusu vita, ushawishi wa chuki kwa misingi ya rangi, ukabila, ubaguzi wa kijinsia, dini ,propaganda kuhusu shughuli za Uchumi yenye mlengo wa ubaguzi au masuala yoyote yanayoelekea kuleta madhara kwa Taifa.
(c) kabla au baada ya mamlaka husika kuchukua hatua kupunguza/kusitisha uhuru wa mtu kwa mujibu wa Ibara 29;2(b) ya katiba hii basi mamlaka husika italiarifu Bunge katika kikao kijacho baada ya tukio husika kuhusu sababu na hatua za kisheria ambazo zimechukuliwa/ inatarajia kuchukuliwa ilikuliepusha Taifa na madhara.

30.-(1) Kila mtu anao uhuru wa-
(a) kutafuta, kupata na kutumia habari na taarifa na kusambaza taarifa hizo; na
(b) kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za upashanaji wa habari bila kujali mipaka ya nchi.
(2) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vile vile vitakuwa na:
(a) haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa wanazopata;
(b) wajibu wa:
(i) kusambaza habari na taarifa kwa wananchi; na
(ii) kuheshimu na kulinda utu, heshima, uhuru na staha ya wananchi dhidi ya habari na taarifa
wanazozitumia, wanazozitayarisha na kuzisambaza.
(3) Serikali na taasisi zake, asasi za kiraia na watu binafsi watakuwa na wajibu wa kutoa habari kwa umma juu ya shughuli na utekelezaji wa shughuli zao.
(4) Masharti ya Ibara hii yatalazimika kuzingatia masharti ya sheria ya nchi itakayotungwa kwa ajili hiyo na kwa madhumuni ya kulinda usalama wa Taifa, amani, maadili ya umma, haki, staha na uhuru wa watu wengine.

(4) Bunge litatunga sheria ya Habari yenye kulinda Usalama wa Taifa, Amani, Maadili ya Umma, haki, staha na uhuru wa watu wengine bila kuathiri masharti yoyote ya ibara ya Katiba hii.

32.Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi,kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kujumuika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Maoni;
32.(1)Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi,kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kujumuika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
(2)Katika kutumia uhuru binafsi kwa mujibu wa ibara ndogo ya 32(1) itakuwa marufuku kwa Mtumishi wa Umma kutumia cheo au nafasi yake kwenye utumishi wa Umma kuinufaisha Jumuiya/taasisi ya Imani kwa namna ambayo italeta taswira ya upendeleo au ubaguzi kwa kuwa naye ni mshirika wa Jumuiya hiyo au lah! lakini ananufaika/atanufaika yeye binafsi au taasisi anayoitumikia kupitia Jumuiya hiyo ya Kiimani kwa namna yoyote ile .

36.-(1) Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengine bila malipo yanayolingana na thamani halisi ya mali hiyo na yatakayotolewa mapema.
(3) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, haki ya umiliki na hifadhi ya mali haitahusu mali iliyothibitishwa kwamba haikupatikana kwa njia halali.

(3)Madhumuni ya kutaifisha mali ya Mtu, Familia, Kampuni au kikundi lazima yawe ni kwa manufaa ya Umma na mwathirika anaweza kupinga Mahakamani utaifishaji kwa madhumuni tajwa.
(4) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, haki ya umiliki na hifadhi ya mali haitahusu mali iliyothibitishwa kwamba haikupatikana kwa njia halali.

37. Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wake na kwa madhumuni haya, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha wananchi kupata hati ya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia wake bila ya upendeleo na ubaguzi wa aina yoyote, na pale inapohitajika, nyaraka za kumwezesha kusafiri.

Maoni;
37.(1) Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wake na kwa madhumuni haya, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha wananchi kupata hati ya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia wake bila ya upendeleo na ubaguzi wa aina yoyote, na pale inapohitajika,nyaraka za kumwezesha kusafiri.
(2) Gharama zitakazotozwa kwa Raia kujipatia hati hizi lazima zizingatie hali ya uchumi wa Nchi na wa mwananchi mmoja mmoja na kwa vyovyote vile gharama ya upatikanaji wa hati ya kusafiria isizidi asilimia Ishirini na tano (20%) ya Kima cha chini cha Kisheria cha Mshahara kwa wakati huo.

38.-(1) Mtu aliyekamatwa au aliyewekwa kizuizini anayo haki ya:
(a) kuelezwa kwa lugha anayoifahamu -
(i) sababu ya kukamatwa;
(ii) haki ya kutokutoa maelezo yoyote; na
(iii) matokeo ya kutoa maelezo;
(b) kutoa maelezo;
(c) kuwasiliana na wakili na mtu mwingine ambaye msaada wake ni muhimu kwa mtuhumiwa;
(d) kutolazimishwa kutoa maelezo ya kukiri kosa ambayo yatatumika kama ushahidi dhidi yake; na
(e) kupelekwa mahakamani mapema iwezekanavyo.
(2) Mamlaka za nchi zitaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha:
(a) mtuhumiwa kupata nakala ya mashtaka yanayomkabili na kumbukumbu ya mwenendo wa mashtaka;
(b) mtuhumiwa au mfungwa kupata nakala ya mwenendo wa mashtaka baada ya shauri kukamilika mahakamani;
(c) mtuhumiwa au mfungwa kufikishwa mahakamani ili kuthibitisha uwepo wake.

(d) Utaratibu utakaowekwa na Mamlaka ya Nchi kwa mujibu wa kifungu cha 2;a na b cha ibara hii lazima uzingatie hali ya Uchumi wa Nchi hasa suala la gharama na usiwe utaratibu wenye taswira ya ubaguzi au upendeleo

39.-(1) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ataendelea kuwa na haki zote za msingi zilizoainishwa katika Katiba hii kwa kiwango anachostahiki katika mazingira ya kuwekwa kizuizini au katika ulinzi.
(2) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ana haki ya kuiomba mahakama ili mamlaka ya nchi inayomuhifadhi kueleza sababu za yeye kuwekwa au kuendelea kuwa katika kizuizi au ulinzi.
(3) Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katikanchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake.

(3 Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake na anaweza kufungua Shauri kupinga Mahakamani hatua yoyote dhidi yake isipokuwa kama hatua hiyo imetokana na Uamuzi wa Mahakama.

42.-
(1) Kila mtoto ana haki ya-
(a) kupewa jina na uraia;
(b) kutoa mawazo, kusikilizwa na kulindwa dhidi ya uonevu,ukatili na udhalilishaji;
(c) kucheza na kupata elimu;
(d) kuhifadhiwa katika mazingira mazuri, kwa walio katika ukinzani na sheria;
(e) kupata lishe bora, makazi na huduma ya afya; na
(f) kushiriki katika shughuli zinazolingana na umri alionao; na
(g) kupata malezi na ulinzi wa wazazi, walezi au mamlaka ya nchi,bila ya ubaguzi wa rangi, utaifa, lugha, mtazamo wa kisiasa, jamii anayotokea, mali, uzazi, kabila, dini, jinsi au aina nyingine za hadhi.
(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoa kipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtoto.

Maoni;

42.-(1) Kila mtoto ana haki ya-

(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoa kipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtoto na jamii kwa ujumla.

43. Kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali za Washirika wa Muungano na jamii zitahakikisha kuwa vijana anawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.

Maoni;
43.- (1)Kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali za Washirika wa Muungano na jamii zitahakikisha kuwa vijana
wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.
(2)Kijana kwa mujibu wa Ibara ya Katiba hii atakuwa mtu wa Umri wa miaka kati ya 15-30

46
.-(1) Kila mwanamke ana haki ya:
(a) kuheshimiwa utu wake;
(b) kuwa salama dhidi ya unyonyaji na ukatili;
(c) kushiriki bila ya ubaguzi katika chaguzi na ngazi zote za maamuzi;
(d) kupata ujira sawa na mwanaume katika kazi;
(e) kulindwa dhidi ya ubaguzi, uonevu na mila zenye madhara;
(f) kulindwa kwa ajira yake wakati wa ujauzito na pale anapojifungua; na
(g) kupata huduma ya juu ya afya inayopatikana.
(2) Mamlaka husika za nchi zitaweka utaratibu wa kisheria utakaosimamia masuala yanayohusu utekelezaji wa masharti ya Ibara hii ikiwa ni pamoja na kukuza utu, usalama na fursa za wanawake wakiwemo wajane.

Maoni;

46.-(1) Kila mwanamke ana haki ya:

(g) kupata huduma ya afya inayopatikana.

49.-(1) Kila raia anao wajibu wa kulinda maliasili ya Taifa, mali ya mamlaka ya nchi na mali yoyote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.
(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha
rasilimali za nchi na maliasili za Taifa.
(3) Kila mtu anao wajibu wa kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na mali inayomilikiwa kwa pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa Taifa kwa makini kwa kuzingatia mipango endelevu na haki ya vizazi vijavyo.

(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha rasilimali za nchi na maliasili za Taifa.

(4) Ni marufuku kwa Mtu yoyote kutumia rasilimali au mali ya Umma kwa manufaa binafsi, familia yake au marafiki zake kinyume na taratibu/kanuni zilizopo za kisheria ambazo Mamlaka ya nchi itahakikisha wananchi wengi wanazijua /kuzifahamu ilikuweza kusimamia sawia ibara ya 49(1) ya katiba hii.
55.-(1) Kila mtu anayezaliwa Tanzania Bara au Zanzibar atakuwa raia wa Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa tarehe ya kuzaliwa, mama au baba yake ni au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania
atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa
kwake ikiwa wazazi wake au mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa Jamhuri ya
Muungano.
(3) Endapo mmoja kati ya wazazi alifariki kabla ya mtu huyo kuzaliwa,uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo chake unatumika, kwa madhumuni ya kutambua uraia wa mtu huyo aliyezaliwa baada ya mzazi aliyefariki kama kwamba mzazi huyo alikuwa anaishi hadi kuzaliwa kwa mtu huyo.
(4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muunganokatika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani, atahesabika kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.
(5) Mtoto aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane ambaye wazazi wake sio raia wa Tanzania, akiasiliwa na raia wa Jamhuri ya Muungano, kwa kuasiliwa kwake huko, kutawezesha mtoto huyo kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kujiandikisha.

Maoni
55.-(1) Kila mtu anayezaliwa Tanganyika au Zanzibar atakuwa raia wa Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa tarehe ya kuzaliwa, mama au baba yake ni au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa kwake ikiwa wazazi wake au mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa Jamhuri ya Muungano.
(3) Endapo mmoja kati ya wazazi alifariki kabla ya mtu huyo kuzaliwa, uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo chake unatumika, kwa madhumuni ya kutambua uraia wa mtu huyo aliyezaliwa baada ya mzazi aliyefariki kana kwamba mzazi huyo alikuwa anaishi hadi kuzaliwa kwa mtu huyo.
(4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano katika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani,atahesabika kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.

56.-(1) Mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, mtu ambaye amekuwa mkazi wa Tanzania Bara au Zanzibar kwa muda uliowekwa na sheria inayotumika Tanzania Bara au Zanzibar, na ambaye ametimiza masharti yote ya sheria ya Bunge la Tanzania Bara au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, anaweza kuomba kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Mtu aliyefunga ndoa na raia wa Jamhuri ya Muunganoanaweza kutuma maombi ya kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(3)Endapo ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2) itavunjika, kama mtu huyo hakuukana uraia wake, ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2), ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa kama ataukana uraia huo au ataomba na kupata uraia wa nchi nyingine.

Maoni;
56.-(1) Mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, mtu ambaye amekuwa mkazi wa Tanzania Bara au Zanzibar kwa muda uliowekwa na sheria inayotumika Tanganyika au Zanzibar, na ambaye ametimiza masharti yote ya sheria ya Bunge la Tanganyika au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, anaweza kuomba kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Mtu aliyefunga ndoa na raia wa Jamhuri ya Muungano anaweza kutuma maombi ya kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano na mara baada ya kukubaliwa kuwa Raia wa kuandikishwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mtu huyo atawasilisha hati ya kuukana Urai wa Nchi yake ya Awali.

(4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2),ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa kama ataukana uraia huo au ataomba na kupata uraia wa nchi nyingine
(5) Kwa vyovyote vile nimarufuku kuwa na Uraia wa Nchi mbili ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

57.-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye
serikali tatu ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
(c) Serikali ya Tanzania Bara.
(2) Shughuli za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa
na:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(b) Bunge la Jamhuri ya Muungano; na
(c) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyo
Serikali yaTanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yataainishwa katika Katiba za Washirika wa Muungano.

Maoni;
57.-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni:

(c) Serikali ya Tanganyika.

(3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyo Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yataainishwa katika Katiba za Washirika wa Muungano.

4;a. Washirika wa Muungano kupitia mabunge zao wanaweza kujadili na kupitisha hoja ya kuandaliwa kwa upiga wa Kura ya Maoni ya wananchi wote wa kila pande ya washirika kadri watakavyoona inafaa kuamua aina nyingine ya Muundo wa Muungano au kuvunjwa kwa Muungano.
(b) Kwa vyovyote vile idadi ya ushindi wa wapiga kura itakayo halalisha uamuzi wowote kwa mujibu wa Ibara ya Katiba ni lazima kuwa zaidi ya Theluthi mbili ya wapiga kura wote walioandikishwa kwa upande ulioamua kupiga kura hiyo ya maoni kuwezesha mabadiliko yoyote .

(c) Hoja yoyote kupitia Bunge la washirika au bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu uamuzi wa suala la Muundo wa Muungano lazima ni kwa kupiga kura ya siri na idadi ya zaidi ya theluthi mbili ya wabunge wote ndiyo itakayoamua hatima ya hoja husika.

(5) Itakuwa marufuku kwa Mtumishi wa Umma wa Jamhuri ya Muungano au wa Serikali za washirika kushabikia ,kushawishi watu,mtu au taasisi yoyote kuchagiza mabadiliko au kuvunjwa kwa Muundo uliopo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(6) Masharti ya kufuatwa kuwezesha mabadiliko au kuvunja Muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lazima yazingatie;
(a).kwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania kupeleka mswada binafsi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania akieleza nia,sababu,faida,madhara yatokanayo na hatua anayopendekeza na Bunge litajadili na kupitisha Uamuzi kwa kutumia kanuni za shughuli za Bunge
(b). kwa Mbunge wa Bunge la Mshirika kupeleka mswada binafsi ndani ya Bunge la Nchi yake akieleza nia,sababu,faida,madhara yatokanayo na hatua anayopendekeza na Bunge litajadili na kupitisha Uamuzi kwa kutumia kanuni za shughuli za Bunge husika

(c).kwa kikundi cha watu Raia halali wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuzaliwa au wa kuandikishwa waliokaa zaidi ya miaka Saba kuandaa madai yao ,kukusanya majina,.anuani ,sahihi zao na kuziwazilisha kwa Jaji wa Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Mawakili au Wakili.

(d) Uamuzi wowote wa Mahakama kama ni wakukubaliana na madai ya wafungua shauri basi Mahakama itaamuru Serikali ya Jamhuri au Serikali ya upande husika ya Mshirika wa Muungano kuitisha kura ya Maoni.

(e) Kwa vyovyote vile uamuzi wowote utokanao na Bunge la Jamhuri ya Tanzania , mmoja wa Mshirika wa Muungano au Uamuzi wa Mahakama kukubali ombi la wafungua shauri mahakamani kwa mujibu wa ibara 57.(6c) ya Katiba hii kuhusu kutengua Muundo wa Muungano au uwepo wake lazima kura ya maoni ipigwe kwa upande ulioleta hoja husika na kama hoja imeletwa kupitia Bunge au mahakama ya Muungano basi upigaji kura ya maoni utakuwa wa pande zote za Washirika wa Muungano na idadi yenye kuhalilisha maamuzi yoyote ni kwa mujibu wa Ibara 57;(4b) ya Katiba hii.

(7) Bunge litatunga Sheria itakayosimamia ugawanaji wa Mali zitakazokuwa zikisimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa niaba ya Washirika wa Muungano kama itatokea Muungano kuvunjika kwa mujibu wa Katiba hii.

Copy ; Zitto Invisible Mzee Mwanakijiji Mnyika
Itaendelea;
 
Mkuu Tumaini Makene na Kurugenzi ya Habari

Haya hapa chini ni maoni yangu ambayo bado naendelea kudadafua kadri muda utakavyo ni ruhusu ila michango ya Wadau inahitajika maana Rasimu ya Katiba kwa jinsi ilivyo ina maeneo mengi yenye kuhitaji dhamira safi kuwa kuiweka sawa na kutuwezesha kuitumia kwa kati ya miaka 25-50 bila kuwekaweka viraka.

2. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari.

2. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanganyika ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari.

9.-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia mamlaka ya nchi isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.
(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya Ibara ndogo ya (1) ni batili na ni kitendo cha uhaini kama itakavyoelezwa katika sheria za nchi.

Maoni
9.-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia mamlaka ya nchi (Serikali, Bunge na Mahakama) isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.
(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya Ibara ndogo ya (1) ni batili na ni kitendo cha uhaini isipokuwa Maandamano yoyote ya Amani ya Umma ya kudai haki au kuondoka madarakani kwa maamlaka ya Nchi hayatachukuliwa kuwa ni Uhaini.

10.-(1) Malengo ya Taifa yaliyoainishwa ndani ya Katiba hii yatakuwa ni mwongozo kwa Serikali, Bunge, Mahakama, vyama vya siasa, taasisi, asasi na mamlaka nyingine na kwa kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine yoyote na katika utekelezaji wa uamuzi wa kisera kwa madhumuni ya kujenga jamii huru, makini na iliyo bora.
(2) Serikali itatoa taarifa Bungeni si chini ya mara moja katika kila mwaka, kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya nchi ili kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya Taifa yaliyoainishwa katika Katiba hii.

Maoni;
10.-(1) Malengo ya Taifa yaliyoainishwa ndani ya Katiba hii yatakuwa ni mwongozo kwa Serikali, Bunge, Mahakama, vyama vya siasa, taasisi, asasi na mamlaka nyingine na kwa kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine
yoyote na katika utekelezaji wa uamuzi wa kisera kwa madhumuni ya kujenga jamii huru, makini na iliyo bora.
(2) Serikali itatoa taarifa Bungeni si chini ya mara moja katika kila mwaka, kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya nchi ili kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya Taifa yaliyoainishwa katika Katiba hii na Bunge litapewa nafasi ya kuijadili na kupiga kura ya kuikubali au kuikataa taarifa husika kwa kutumia Kanuni ya Bunge katika kufikia maamuzi.

11.-(1) Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha udugu, amani, umoja na utengamanowa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora na kujitegemea.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), lengo hilo kuu litaendelezwa na kuimarishwa katika nyanja zote kuu,ikijumuisha nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na
kimazingira.
(3) Katika kutekeleza malengo ya Taifa ya:

(c) kiuchumi, Serikali inachukua hatua zinazofaa ili:
(i) kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuondoa umaskini;
(ii) kuhakikisha kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha
kuwa utajiri wa Taifa unaendelezwa,unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya
wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;
(iii) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima,wafugaji na wavuvi;
(iv) kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na kukuza fursa za uwekezaji;
(v) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kukuza kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuhakikisha kuwa
wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli
zao;
(vi) kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa mazao kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, utafutaji na uendelezaji wa masoko ya mazao yao;
(vii) kuweka utaratibu mzuri wa upangaji na usimamiaji wa mizania ya bei za mazao na
pembejeo;
(viii) kuimarisha na kuendeleza uwekezaji wa ndani,upatikanaji wa pembejeo za kilimo, maeneo ya ufugaji na vifaa vya uvuvi;
(ix) kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa fursa na nafasi za wazi kwa watu wote na kuanzisha shughuli za kiuchumi na kukuza mazingira yaliyobora kwa ajili ya kuhamasisha sekta binafsi katika uchumi;
(x) kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anapata fursa ya kufanya kazi, kwa maana ya kufanya shughuli yoyote halali inayompatia kipato;
(xi) kuweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kujipatia
elimu na kuwa huru kupata fursa sawa ya kutafuta elimu katika fani anayoipenda hadi
kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake;

Maoni;
11.-(1) Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha udugu, amani, umoja na utengamano wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora na kujitegemea.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), lengo hilo kuu litaendelezwa na kuimarishwa katika nyanja zote kuu,ikijumuisha nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na
kimazingira.

(3) Katika kutekeleza malengo ya Taifa ya:

(c) kiuchumi, Serikali inachukua hatua zinazofaa ili:
(i) kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuondoa umaskini;
(ii) kuhakikisha kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha
kuwa utajiri wa Taifa unaendelezwa,unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;
(iii) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa vikundi vya shughuli za Kiuchumi na kuwashirikisha katika hatua za kuandaa sera na Kanuni za shughuli husika.
(iv) kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na kukuza fursa za uwekezaji;
(v) Kupitia Serikali za Washirika wa Muungano Serikali itaweka mazingira bora kwa ajili ya kukuza kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuhakikisha kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao;
(vi) kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa mazao kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, utafutaji na uendelezaji wa masoko ya mazao yao;
(vii) kuweka utaratibu mzuri wa upangaji na usimamiaji wa mizania ya bei za mazao zitokanazo na shughuli za uchumi hasa kilimo,Ufugaji na Uvuvi .
(viii) kuimarisha na kuendeleza uwekezaji wa ndani kwa kuhakikisha ,upatikanaji wa Mitaji kwa ajili ya pembejeo za kilimo, madawa na majasho ya Mifugo na vifaa vya uvuvi;
(ix) kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa fursa na nafasi za wazi kwa kila mmoja kuanzisha shughuli za kiuchumi kwa kukuza mazingira yaliyo bora kwa ajili ya kuhamasisha sekta binafsi katika uchumi;
(x) kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anapata fursa ya kufanya kazi, kwa maana ya kufanya shughuli yoyote halali inayompatia kipato;
(xi) kuweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kujipatia
elimu na kuwa huru kupata fursa sawa ya kutafuta elimu katika fani anayoipenda hadi
kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake;
(xii) Serikali itahakikisha mkataba wowote utakaoingiwa na Serikali au taasisi zake na Serikali zingine au Makampuni binafsi unakuwa wa wazi kwa kuweka nakala ya mkataba husika kwenye magazeti na Tovuti ya Wizara/taasisi husika isipokuwa mikataba ya Ulinzi ambao Kamati ya Bunge ya Ulinzi ndiyo itakayo kuwa na Mamlaka ya kukagua kabla Mkataba wenyewe hauja sainiwa kuona kama masilahi ya Taifa yamezingatiwa au lah na kama Mkataba haukuzingatia masilahi ya Taifa Kamati itatoa mapendekezo ya kuzingatiwa na Wizara husika na Nakala kupewa Spika wa Bunge.

16.-(1) Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza, ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi,mali na thamani zake na madeni yake katika Tume ya
Maadili na Uwajibikaji.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza mali zake na madeni:
(a) yake binafsi;
(b) ya mwenza wake wa ndoa; na
(c) watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane,mara moja kila mwaka, au kadri itakavyoamuliwa na sheria.

Maoni;
16.-(1) Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza, ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi,mali na thamani zake na madeni yake katika Tume ya Maadili na Uwajibikaji.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza mali zake na madeni:
(a) yake binafsi;
(b) ya mwenza wake wa ndoa; na
(c) watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane,mara moja kila mwaka, au kadri itakavyoamuliwa na sheria.
(d) Utangazaji wa Mali za kiongozi kupitia kifungu cha 16(2); a na b ya Katiba hii utafanywa chini ya Kiapo na itakuwa Kosa la jinai kusema uongo.
(e) Bunge litatunga sheria itakayo simamia na kuwezesha Umma kuweza kuhakiki ukweli wa mali zilizotangazwa na Kiongozi wa Umma.

19. Masharti yaliyoainishwa katika Ibara za 13 mpaka 18 yatatumika pia kwa watumishi wa umma baada ya kufanyiwa marekebisho stahiki.

Maoni
;
19. Masharti yaliyoainishwa katika Ibara za 13, 18 na 20 ya Katiba hii yatatumika pia kwa watumishi wa umma na Bunge litatunga Sheria ya Tume ya Maadili ya Uongozi wa Umma itakuwa na Kanuni itakayosimamia Masharti ya Katiba hii.

20.-(1) Bila ya kuathiri masharti yoyote ya Katiba hii, kiongozi yeyote wa Umma atapaswa kuheshimu na kutii maadili ya viongozi wa umma, ikiwemo Miiko ya Uongozi.
(2) Miiko ya Uongozi inayorejewa katika Ibara ndogo (1),itakuwa kama ifuatavyo:
(a) Kiongozi wa umma hatopaswa:
(i) kuvunja au kukiuka masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano;
(ii) kutoa au kupokea rushwa;
(iii) kujilimbikizia mali kinyume cha sheria;
(iv) kusema uongo au kutoa taarifa zisizo za ukweli;
(v) kutoa siri za Serikali kinyume na sheria isipokuwa zilizokinyume na Masilahi ya Umma kadri katiba hii ilivyoelekeza;
(vi) kutumia wadhifa, nafasi au cheo chake kwa manufaa yake binafsi, familia yake, ndugu, jamaa au marafiki zake au mtu yeyote aliye na uhusiano naye wa karibu;
(vii) kufanya vitendo vya uzembe, uvivu, ubaguzi,kiburi, dharau au unyanyasaji wa kijinsia.
(b) Kiongozi wa umma atapaswa:
(i) kuheshimu na kuendeleza dhana ya uwajibikaji wa pamoja, kwa viongozi wanaohusika; na
(ii) kuheshimu na kuendeleza maadili ya viongozi wa umma, ikijumuisha:
(aa) kuwa na tabia na mienendo inayokubalika katika jamii;
(bb) kuheshimu, kutunza na kulinda mali za umma; na
(cc) kutambua, kuheshimu na kuzingatia Kanuni za Maadili na Mienendo ya Watumishi wa Umma, Kanuni za Kudumu za Watumishi wa Umma, nyaraka za umma na miongozo mbalimbali ya Serikali kuhusu viongozi na watumishi wa umma.
(iii) kutenganisha shughuli za biashara na masuala yanayohusiana na uongozi.
(3) Kiongozi yeyote wa umma ambaye anatuhumiwa na kuthibitika kwa makosa ya:
(a) kimaadili;
(b) udhalilishaji wa mtu au wa kijinsia; na
(c) wizi au ubadhirifu wa mali za umma,atasimamishwa kazi mpaka suala lake litakapoamuliwa kwa mujibu wa sheria au taratibu nyingine zinazowahusu viongozi wa umma.

21.-(1) Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia katika ajira nyingine yoyote yenye malipo ya mshahara.
(2) Mtumishi wa umma haruhusiwi kuchaguliwa au kuteuliwa kushika madaraka katika chama cha siasa.
(3) Mtumishi wa umma aliyestaafu na anayepokea malipo ya pensheni kutokana na fedha za umma haruhusiwi kuwa mwenyekiti,mkurugenzi au mtumishi zaidi ya vipindi viwili katika:
(a) shirika au kampuni inayomilikiwa au kuendeshwa kwa fedha za umma; au
(b) chombo chochote cha umma

Maoni;

21.-(1) Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia katika ajira nyingine yoyote yenye malipo ya mshahara.
(2) Mtumishi wa umma haruhusiwi kuchaguliwa au kuteuliwa kushika madaraka katika chama cha siasa .
(3) Mtumishi wa umma aliyestaafu na anayepokea malipo ya pensheni kutokana na fedha za umma anaruhusiwa tu kuwa Mwenyekiti na si kwa zaidi ya vipindi viwili vya jumla ya miaka kumi katika;
(a) shirika au kampuni inayomilikiwa au kuendeshwa kwa fedha za umma; au
(b) chombo chochote cha umma.
(4) Mtumishi wa Umma aliyewahi kuwa Mwenyekiti kwa mujibu wa Ibara hii baada ya kumaliza vipindi vyake vya kuwa Mwenyekiti hatabadilishiwa aina ya Pensheni badala yake atabaki na kuendelea kupokea Pensheni yake ya utumishi wa awali.

24.- (7) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa na unaozingatia misingi kwamba -

(a) wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote vinapohitajika kufanyiwa uamuzi na mahakama au mamlaka nyingine inayohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia atakuwa na haki ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria
kutokana na uamuzi wa mahakama au mamlaka nyingine inayohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu aliyehukumiwa kwa kutenda kosa hilo hadi itakapothibitika mahakamani kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chochote ambacho wakati alipotenda kitendo hicho hakikuwa ni kosa chini ya sheria;
(d) ni marufuku kwa mtu kupewa adhabu ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendeka;
(e) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu,heshima ya mtu na faragha itahifadhiwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi wa tuhuma na uendeshaji wa masharti ya jinai na katika shughuli nyingine ambazo mtu anakuwa katika kizuizi cha mamlaka ya nchi au katika
kuhakikisha utekelezaji wa adhabu; na
(f) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazotweza au kudhalilisha.

Maoni;
24.- (7) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa na unaozingatia misingi kwamba -
(a) wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote vinapohitajika kufanyiwa uamuzi na mahakama au mamlaka nyingine inayohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia atakuwa na haki ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria
kutokana na uamuzi wa mahakama au mamlaka nyingine inayohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu aliyehukumiwa kwa kutenda kosa hilo hadi itakapothibitika mahakamani kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chochote ambacho wakati alipotenda kitendo hicho hakikuwa ni kosa chini ya sheria;
(d) ni marufuku kwa mtu kupewa adhabu ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo kisheria wakati kosa linalohusika lilipotendeka;
(e) haki ya usawa wa binadamu,heshima ya mtu na faragha itahifadhiwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi wa tuhuma na uendeshaji wa masharti ya jinai na katika shughuli nyingine ambazo mtu anakuwa katika kizuizi cha mamlaka ya nchi au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu; na
(f) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazotweza au kudhalilisha.

29.-(1) Kila mtu:
(a) anao uhuru wa-
(i) kuwa na maoni na kueleza fikra zake;
(ii) kufanya mawasiliano na vile vile anayo haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake;
(iii) ubunifu na sanaa;
(iv) kitaaluma na tafiti za kisayansi; na
(b) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu:
(i) matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi; na
(ii) utekelezaji wa mamlaka ya nchi kuhusu sera za kitaifa na shughuli ya maendeleo ya jamii; na
(iii) masuala mengine muhimu kwa jamii.
(2) Utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika Ibara ndogo ya (1), utajumuisha wajibu muhimu kwa mwananchi na wajibu huo unaweza kupunguza haki hizo kutokana na:
(a) vita au machafuko ya kisiasa; au
(b) propaganda kuhusu vita, ushawishi wa chuki kwa misingi ya rangi, ukabila, ubaguzi wa kijinsia, dini au masuala yoyote yanayoweza kuleta madhara kwa Taifa.

Maoni;
29.-(1) Kila mtu:
(a) anao uhuru wa-
(i) kuwa na maoni na kueleza fikra zake;
(ii) kufanya mawasiliano na vile vile anayo haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake;
(iii) ubunifu na sanaa;
(iv) kitaaluma na tafiti za kisayansi; na
(b) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu:
(i) matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi; na
(ii) utekelezaji wa mamlaka ya nchi kuhusu sera za kitaifa na shughuli ya maendeleo ya jamii; na
(iii) masuala mengine muhimu kwa jamii.
(2) Utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika Ibara ndogo ya (1), utajumuisha wajibu muhimu kwa mwananchi na wajibu huo unaweza kupunguza haki hizo kutokana na:
(a) vita au machafuko ya kisiasa; au
(b) propaganda kuhusu vita, ushawishi wa chuki kwa misingi ya rangi, ukabila, ubaguzi wa kijinsia, dini ,propaganda kuhusu shughuli za Uchumi yenye mlengo wa ubaguzi au masuala yoyote yanayoelekea kuleta madhara kwa Taifa.
(c) kabla au baada ya mamlaka husika kuchukua hatua kupunguza/kusitisha uhuru wa mtu kwa mujibu wa Ibara 29;2(b) ya katiba hii basi mamlaka husika italiarifu Bunge katika kikao kijacho baada ya tukio husika kuhusu sababu na hatua za kisheria ambazo zimechukuliwa/ inatarajia kuchukuliwa ilikuliepusha Taifa na madhara.

30.-(1) Kila mtu anao uhuru wa-
(a) kutafuta, kupata na kutumia habari na taarifa na kusambaza taarifa hizo; na
(b) kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za upashanaji wa habari bila kujali mipaka ya nchi.
(2) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vile vile vitakuwa na:
(a) haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa wanazopata;
(b) wajibu wa:
(i) kusambaza habari na taarifa kwa wananchi; na
(ii) kuheshimu na kulinda utu, heshima, uhuru na staha ya wananchi dhidi ya habari na taarifa
wanazozitumia, wanazozitayarisha na kuzisambaza.
(3) Serikali na taasisi zake, asasi za kiraia na watu binafsi watakuwa na wajibu wa kutoa habari kwa umma juu ya shughuli na utekelezaji wa shughuli zao.
(4) Masharti ya Ibara hii yatalazimika kuzingatia masharti ya sheria ya nchi itakayotungwa kwa ajili hiyo na kwa madhumuni ya kulinda usalama wa Taifa, amani, maadili ya umma, haki, staha na uhuru wa watu wengine.

Maoni;
30.-(1) Kila mtu anao uhuru wa-
(a) kutafuta, kupata na kutumia habari na taarifa na kusambaza taarifa hizo; na
(b) kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za upashanaji wa habari bila kujali mipaka ya nchi.
(2) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vile vile vitakuwa na:
(a) haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa wanazopata;
(b) wajibu wa:
(i) kusambaza habari na taarifa kwa wananchi; na
(ii) kuheshimu na kulinda utu, heshima, uhuru na staha ya wananchi dhidi ya habari na taarifa
wanazozitumia, wanazozitayarisha na kuzisambaza.
(3) Serikali na taasisi zake, asasi za kiraia na watu binafsi watakuwa na wajibu wa kutoa habari kwa umma juu ya shughuli na utekelezaji wa shughuli zao.
(4) Bunge litatunga sheria ya Habari yenye kulinda Usalama wa Taifa, Amani, Maadili ya Umma, haki, staha na uhuru wa watu wengine bila kuathiri masharti yoyote ya ibara ya Katiba hii.

32.Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi,kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kujumuika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Maoni;
32.(1)Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi,kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kujumuika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
(2)Katika kutumia uhuru binafsi kwa mujibu wa ibara ndogo ya 32(1) itakuwa marufuku kwa Mtumishi wa Umma kutumia cheo au nafasi yake kwenye utumishi wa Umma kuinufaisha Jumuiya/taasisi ya Imani kwa namna ambayo italeta taswira ya upendeleo au ubaguzi kwa kuwa naye ni mshirika wa Jumuiya hiyo au lah! lakini ananufaika/atanufaika yeye binafsi au taasisi anayoitumikia kupitia Jumuiya hiyo ya Kiimani kwa namna yoyote ile .

36.-(1) Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengine bila malipo yanayolingana na thamani halisi ya mali hiyo na yatakayotolewa mapema.
(3) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, haki ya umiliki na hifadhi ya mali haitahusu mali iliyothibitishwa kwamba haikupatikana kwa njia halali.

Maoni;

36.-(1) Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengine bila malipo yanayolingana na thamani halisi ya mali hiyo na yatakayotolewa mapema.
(3)Madhumuni ya kutaifisha mali ya Mtu, Familia, Kampuni au kikundi lazima yawe ni kwa manufaa ya Umma na mwathirika anaweza kupinga Mahakamani utaifishaji kwa madhumuni tajwa.
(4) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, haki ya umiliki na hifadhi ya mali haitahusu mali iliyothibitishwa kwamba haikupatikana kwa njia halali.

37. Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wake na kwa madhumuni haya, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha wananchi kupata hati ya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia wake bila ya upendeleo na ubaguzi wa aina yoyote, na pale inapohitajika, nyaraka za kumwezesha kusafiri.

Maoni;
37.(1) Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wake na kwa madhumuni haya, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha wananchi kupata hati ya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia wake bila ya upendeleo na ubaguzi wa aina yoyote, na pale inapohitajika,nyaraka za kumwezesha kusafiri.
(2) Gharama zitakazotozwa kwa Raia kujipatia hati hizi lazima zizingatie hali ya uchumi wa Nchi na wa mwananchi mmoja mmoja na kwa vyovyote vile gharama ya upatikanaji wa hati ya kusafiria isizidi asilimia Ishirini na tano (20%) ya Kima cha chini cha Kisheria cha Mshahara kwa wakati huo.

38.-(1) Mtu aliyekamatwa au aliyewekwa kizuizini anayo haki ya:
(a) kuelezwa kwa lugha anayoifahamu -
(i) sababu ya kukamatwa;
(ii) haki ya kutokutoa maelezo yoyote; na
(iii) matokeo ya kutoa maelezo;
(b) kutoa maelezo;
(c) kuwasiliana na wakili na mtu mwingine ambaye msaada wake ni muhimu kwa mtuhumiwa;
(d) kutolazimishwa kutoa maelezo ya kukiri kosa ambayo yatatumika kama ushahidi dhidi yake; na
(e) kupelekwa mahakamani mapema iwezekanavyo.
(2) Mamlaka za nchi zitaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha:
(a) mtuhumiwa kupata nakala ya mashtaka yanayomkabili na kumbukumbu ya mwenendo wa mashtaka;
(b) mtuhumiwa au mfungwa kupata nakala ya mwenendo wa mashtaka baada ya shauri kukamilika mahakamani;
(c) mtuhumiwa au mfungwa kufikishwa mahakamani ili kuthibitisha uwepo wake.

Maoni
38.-(1) Mtu aliyekamatwa au aliyewekwa kizuizini anayo haki ya:
(a) kuelezwa kwa lugha anayoifahamu -
(i) sababu ya kukamatwa;
(ii) haki ya kutokutoa maelezo yoyote; na
(iii) matokeo ya kutoa maelezo;
(b) kutoa maelezo;
(c) kuwasiliana na wakili na mtu mwingine ambaye msaada wake ni muhimu kwa mtuhumiwa;
(d) kutolazimishwa kutoa maelezo ya kukiri kosa ambayo yatatumika kama ushahidi dhidi yake; na
(e) kupelekwa mahakamani mapema iwezekanavyo.
(2) Mamlaka za nchi zitaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha:
(a) mtuhumiwa kupata nakala ya mashtaka yanayomkabili na kumbukumbu ya mwenendo wa mashtaka;
(b) mtuhumiwa au mfungwa kupata nakala ya mwenendo wa mashtaka baada ya shauri kukamilika mahakamani;
(c) mtuhumiwa au mfungwa kufikishwa mahakamani ili kuthibitisha uwepo wake.
(d) Utaratibu utakaowekwa na Mamlaka ya Nchi kwa mujibu wa kifungu cha 2;a na b cha ibara hii lazima uzingatie hali ya Uchumi wa Nchi hasa suala la gharama na usiwe utaratibu wenye taswira ya ubaguzi au upendeleo

39.-(1) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ataendelea kuwa na haki zote za msingi zilizoainishwa katika Katiba hii kwa kiwango anachostahiki katika mazingira ya kuwekwa kizuizini au katika ulinzi.
(2) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ana haki ya kuiomba mahakama ili mamlaka ya nchi inayomuhifadhi kueleza sababu za yeye kuwekwa au kuendelea kuwa katika kizuizi au ulinzi.
(3) Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katikanchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake.

Maoni;
39.-(1) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ataendelea kuwa na haki zote za msingi zilizoainishwa katika Katiba hii kwa kiwango anachostahiki katika mazingira ya kuwekwa kizuizini au katika ulinzi.
(2) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ana haki ya kuiomba mahakama ili mamlaka ya nchi inayomuhifadhi kueleza sababu za yeye kuwekwa au kuendelea kuwa katika kizuizi au ulinzi.
(3 Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake na anaweza kufungua Shauri kupinga Mahakamani hatua yoyote dhidi yake isipokuwa kama hatua hiyo imetokana na Uamuzi wa Mahakama.

42.-(1) Kila mtoto ana haki ya-
(a) kupewa jina na uraia;
(b) kutoa mawazo, kusikilizwa na kulindwa dhidi ya uonevu,ukatili na udhalilishaji;
(c) kucheza na kupata elimu;
(d) kuhifadhiwa katika mazingira mazuri, kwa walio katika ukinzani na sheria;
(e) kupata lishe bora, makazi na huduma ya afya; na
(f) kushiriki katika shughuli zinazolingana na umri alionao; na
(g) kupata malezi na ulinzi wa wazazi, walezi au mamlaka ya nchi,bila ya ubaguzi wa rangi, utaifa, lugha, mtazamo wa kisiasa, jamii anayotokea, mali, uzazi, kabila, dini, jinsi au aina nyingine za hadhi.
(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoa kipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtoto.

Maoni;
42.-(1) Kila mtoto ana haki ya-
(a) kupewa jina na uraia;
(b) kutoa mawazo, kusikilizwa na kulindwa dhidi ya uonevu,ukatili na udhalilishaji;
(c) kucheza na kupata elimu;
(d) kuhifadhiwa katika mazingira mazuri, kwa walio katika ukinzani na sheria;
(e) kupata lishe bora, makazi na huduma ya afya; na
(f) kushiriki katika shughuli zinazolingana na umri alionao; na
(g) kupata malezi na ulinzi wa wazazi, walezi au mamlaka ya nchi,bila ya ubaguzi wa rangi, utaifa, lugha, mtazamo wa kisiasa, jamii anayotokea, mali, uzazi, kabila, dini, jinsi au aina nyingine za hadhi.
(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoa kipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtoto na jamii kwa ujumla.

43. Kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali za Washirika wa Muungano na jamii zitahakikisha kuwa vijana anawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.

Maoni;
43.- (1)Kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali za Washirika wa Muungano na jamii zitahakikisha kuwa vijana
wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.
(2)Kijana kwa mujibu wa Ibara ya Katiba hii atakuwa mtu wa Umri wa miaka kati ya 15-30
46.-(1) Kila mwanamke ana haki ya:
(a) kuheshimiwa utu wake;
(b) kuwa salama dhidi ya unyonyaji na ukatili;
(c) kushiriki bila ya ubaguzi katika chaguzi na ngazi zote za maamuzi;
(d) kupata ujira sawa na mwanaume katika kazi;
(e) kulindwa dhidi ya ubaguzi, uonevu na mila zenye madhara;
(f) kulindwa kwa ajira yake wakati wa ujauzito na pale anapojifungua; na
(g) kupata huduma ya juu ya afya inayopatikana.
(2) Mamlaka husika za nchi zitaweka utaratibu wa kisheria utakaosimamia masuala yanayohusu utekelezaji wa masharti ya Ibara hii ikiwa ni pamoja na kukuza utu, usalama na fursa za wanawake wakiwemo wajane.

Maoni;
46.-(1) Kila mwanamke ana haki ya:
(a) kuheshimiwa utu wake;
(b) kuwa salama dhidi ya unyonyaji na ukatili;
(c) kushiriki bila ya ubaguzi katika chaguzi na ngazi zote za maamuzi;
(d) kupata ujira sawa na mwanaume katika kazi;
(e) kulindwa dhidi ya ubaguzi, uonevu na mila zenye madhara;
(f) kulindwa kwa ajira yake wakati wa ujauzito na pale anapojifungua; na
(g) kupata huduma ya afya inayopatikana.
(2) Mamlaka husika za nchi zitaweka utaratibu wa kisheria utakaosimamia masuala yanayohusu utekelezaji wa masharti ya Ibara hii ikiwa ni pamoja na kukuza utu, usalama na fursa za wanawake wakiwemo wajane.

49.-(1) Kila raia anao wajibu wa kulinda maliasili ya Taifa, mali ya mamlaka ya nchi na mali yoyote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.
(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha
rasilimali za nchi na maliasili za Taifa.
(3) Kila mtu anao wajibu wa kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na mali inayomilikiwa kwa pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa Taifa kwa makini kwa kuzingatia mipango endelevu na haki ya vizazi vijavyo.

Maoni;
49.-(1) Kila raia anao wajibu wa kulinda maliasili ya Taifa, mali ya mamlaka ya nchi na mali yoyote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.
(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha rasilimali za nchi na maliasili za Taifa.
(3) Kila mtu anao wajibu wa kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na mali inayomilikiwa kwa pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa Taifa kwa makini kwa kuzingatia mipango endelevu na haki ya vizazi vijavyo.
(4) Ni marufuku kwa Mtu yoyote kutumia rasilimali au mali ya Umma kwa manufaa binafsi, familia yake au marafiki zake kinyume na taratibu/kanuni zilizopo za kisheria ambazo Mamlaka ya nchi itahakikisha wananchi wengi wanazijua /kuzifahamu ilikuweza kusimamia sawia ibara ya 49(1) ya katiba hii.

55.-(1) Kila mtu anayezaliwa Tanzania Bara au Zanzibar atakuwa raia wa Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa tarehe ya kuzaliwa, mama au baba yake ni au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania
atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa
kwake ikiwa wazazi wake au mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa Jamhuri ya
Muungano.
(3) Endapo mmoja kati ya wazazi alifariki kabla ya mtu huyo kuzaliwa,uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo chake unatumika, kwa madhumuni ya kutambua uraia wa mtu huyo aliyezaliwa baada ya mzazi aliyefariki kama kwamba mzazi huyo alikuwa anaishi hadi kuzaliwa kwa mtu huyo.
(4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muunganokatika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani, atahesabika kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.
(5) Mtoto aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane ambaye wazazi wake sio raia wa Tanzania, akiasiliwa na raia wa Jamhuri ya Muungano, kwa kuasiliwa kwake huko, kutawezesha mtoto huyo kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kujiandikisha.

Maoni
55.-(1) Kila mtu anayezaliwa Tanganyika au Zanzibar atakuwa raia wa Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa tarehe ya kuzaliwa, mama au baba yake ni au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa kwake ikiwa wazazi wake au mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa Jamhuri ya Muungano.
(3) Endapo mmoja kati ya wazazi alifariki kabla ya mtu huyo kuzaliwa, uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo chake unatumika, kwa madhumuni ya kutambua uraia wa mtu huyo aliyezaliwa baada ya mzazi aliyefariki kana kwamba mzazi huyo alikuwa anaishi hadi kuzaliwa kwa mtu huyo.
(4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano katika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani,atahesabika kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.
(5) Mtoto aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane ambaye wazazi wake sio raia wa Tanzania, akiasiliwa na raia wa Jamhuri ya Muungano, kwa kuasiliwa kwake huko, kutawezesha mtoto huyo kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kujiandikisha.

56.-(1) Mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, mtu ambaye amekuwa mkazi wa Tanzania Bara au Zanzibar kwa muda uliowekwa na sheria inayotumika Tanzania Bara au Zanzibar, na ambaye ametimiza masharti yote ya sheria ya Bunge la Tanzania Bara au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, anaweza kuomba kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Mtu aliyefunga ndoa na raia wa Jamhuri ya Muunganoanaweza kutuma maombi ya kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(3)Endapo ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2) itavunjika, kama mtu huyo hakuukana uraia wake, ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2), ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa kama ataukana uraia huo au ataomba na kupata uraia wa nchi nyingine.

Maoni;
56.-(1) Mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, mtu ambaye amekuwa mkazi wa Tanzania Bara au Zanzibar kwa muda uliowekwa na sheria inayotumika Tanganyika au Zanzibar, na ambaye ametimiza masharti yote ya sheria ya Bunge la Tanganyika au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, anaweza kuomba kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Mtu aliyefunga ndoa na raia wa Jamhuri ya Muungano anaweza kutuma maombi ya kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano na mara baada ya kukubaliwa kuwa Raia wa kuandikishwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mtu huyo atawasilisha hati ya kuukana Urai wa Nchi yake ya Awali.
(3)Endapo ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2) itavunjika, kama mtu huyo hakuukana uraia wake, ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2),ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa kama ataukana uraia huo au ataomba na kupata uraia wa nchi nyingine
(5) Kwa vyovyote vile nimarufuku kuwa na Uraia wa Nchi mbili ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

57.-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye
serikali tatu ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
(c) Serikali ya Tanzania Bara.
(2) Shughuli za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa
na:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(b) Bunge la Jamhuri ya Muungano; na
(c) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyo
Serikali yaTanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yataainishwa katika Katiba za Washirika wa Muungano.

Maoni;
57.-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
(c) Serikali ya Tanganyika.
(2) Shughuli za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa
na:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(b) Bunge la Jamhuri ya Muungano; na
(c) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyo Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yataainishwa katika Katiba za Washirika wa Muungano.

4;aWashirika wa Muungano kupitia mabunge zao wanaweza kujadili na kupitisha hoja ya kuandaliwa kwa upiga wa Kura ya Maoni ya wananchi wote wa kila pande ya washirika kadri watakavyoona inafaa kuamua aina nyingine ya Muundo wa Muungano au kuvunjwa kwa Muungano.
(b)Kwa vyovyote vile idadi ya ushindi wa wapiga kura itakayo halalisha uamuzi wowote kwa mujibu wa Ibara ya Katiba ni lazima kuwa zaidi ya Theluthi mbili ya wapiga kura wote walioandikishwa kwa upande ulioamua kupiga kura hiyo ya maoni kuwezesha mabadiliko yoyote .

(c)Hoja yoyote kupitia Bunge la washirika au bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu uamuzi wa suala la Muundo wa Muungano lazima ni kwa kupiga kura ya siri na idadi ya zaidi ya theluthi mbili ya wabunge wote ndiyo itakayoamua hatima ya hoja husika.

(5) Itakuwa marufuku kwa Mtumishi wa Umma wa Jamhuri ya Muungano au wa Serikali za washirika kushabikia ,kushawishi watu,mtu au taasisi yoyote kuchagiza mabadiliko au kuvunjwa kwa Muundo uliopo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(6) Masharti ya kufuatwa kuwezesha mabadiliko au kuvunja Muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lazima yazingatie;
a.kwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania kupeleka mswada binafsi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania akieleza nia,sababu,faida,madhara yatokanayo na hatua anayopendekeza na Bunge litajadili na kupitisha Uamuzi kwa kutumia kanuni za shughuli za Bunge
(b). kwa Mbunge wa Bunge la Mshirika kupeleka mswada binafsi ndani ya Bunge la Nchi yake akieleza nia,sababu,faida,madhara yatokanayo na hatua anayopendekeza na Bunge litajadili na kupitisha Uamuzi kwa kutumia kanuni za shughuli za Bunge husika

(c).kw kikundi cha watu Raia halali wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuzaliwa au wa kuandikishwa waliokaa zaidi ya miaka Saba kuandaa madai yao ,kukusanya majina .anuani ,sahihi zao na kuziwazilisha kwa Jaji wa Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Mawakili au Wakili.
(d) Uamuzi wowote wa Mahakama kama ni wakukubaliana na madai ya wafungua shauri basi Mahakama itaamuru Serikali ya Jamhuri au Serikali ya upande husika ya Mshirika wa Muungano kuitisha kura ya Maoni.

(e)Kwa vyovyote vile uamuzi wowote utokanao na Bunge la Jamhuri ya Tanzania , mmoja wa Mshirika wa Muungano au Uamuzi wa Mahakama kukubali ombi la wafungua shauri mahakamani kwa mujibu wa ibara 57.(6c) ya Katiba hii kuhusu kutengua Muundo wa Muungano au uwepo wake lazima kura ya maoni ipigwe kwa upande ulileta hoja husika na kama hoja imeletwa kupitia Bunge au mahakama ya Muungano basi upigaji kura ya maoni utakuwa wa pande zote za Washirika wa Muungano na idadi yenye kuhalilisha maamuzi yoyote ni kwa mujibu wa Ibara 57;(4b) ya Katiba hii.

(7) Bunge litatunga Sheria itakayosimamia ugawanaji wa Mali zitakazokuwa zikisimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa niaba ya Washirika wa Muungano kama itatokea Muungano kuvunjika kwa mujibu wa Katiba hii.

Itaendelea;

Mp Kalix

This is great kaka. Asante sana na karibu kwa mwendelezo wako kamanda.
 
Last edited by a moderator:
Watanzania wanasonga mbele...Dodoma mjiini leo
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1376939787.639134.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1376939787.639134.jpg
    100.5 KB · Views: 33
  • ImageUploadedByJamiiForums1376939907.891385.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1376939907.891385.jpg
    98.9 KB · Views: 27
Asanteni Dodoma kwa kutoa maoni yenu mbele ya Baraza Huru la Rasimu ya Katiba Mpya...
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1376940309.053092.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1376940309.053092.jpg
    111.9 KB · Views: 24
  • ImageUploadedByJamiiForums1376940395.171534.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1376940395.171534.jpg
    136.1 KB · Views: 28
Asateni Kasulu, Igunga, Zenga, Urambo, Tabora...
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1376940942.831748.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1376940942.831748.jpg
    114.3 KB · Views: 35
  • ImageUploadedByJamiiForums1376941167.921378.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1376941167.921378.jpg
    110.1 KB · Views: 38
  • ImageUploadedByJamiiForums1376941245.930667.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1376941245.930667.jpg
    114.3 KB · Views: 36
JINA: Nimetuma- chademamaoni@gmail.com
P.O BOX…….
Kinampanda, Singida

[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 706"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]S/N
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]IBARA
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]MAPENDEKEZO YA CHAMA (CHADEMA)
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]1.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]2 Eneo la Jamhuri ya. Muungano
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Neno Tanzania Bara liondolewe na kuandika Tanganyika kila palipo na neno Tanzania Bara-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]2.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]4(1) Lugha ya Taifa
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Lugha ya Taifa itakuwa Kiswahili na miswada/sheria zote zitaandikwa kwayo pamoja na lugha zinginE-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]3.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]5 Tunu za Taifa
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Viongozwe vipengele hivi demokrasia ya vyama vingi, utawala wa sheria,uwazi na haki za binadamu-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]4.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]6(2) Daftari la wapiga kura
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Liwe mahali ambapo kila raia akifikisha miaka 18 ana andikishwa wakati wowote-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]5.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]17&85 watumishi wa umma.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Mishahara ya watumishi wote wa umma pamoja Rais ijulikane-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]6.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]32 (2) haki ya kuandamana
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Kila mtu ana haki kwa amani na bila kubeba siraha kukusanyika/kuandamana kuzuia njia na kuwasilisha malalamiko-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]7.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]35(e) kugoma
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Kugoma au kusitisha nguvu kazi yake mahali pa kazi-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]8.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]47 Haki ya kumiliki rasilimali
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Iongezwe ibara mpya ya 48 haki ya kumiliki rasilimali za asili zote Ardhi, Madini, mafuta na gesi, maji na misitu na wanyama pori-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]9.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]60 (7)nyongeza
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Kiongozwe kifungu cha 7 Maadili na miiko ya uongozi na utumishi wa umma, Haki za binadamu na wajibu wa raia. Tume huru ya Taifa ya uchaguzi-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]10.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Serikali tatu (3)
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Kuwepo serikali ya Muungano, serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanganyika-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]11.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]75(d) Uchaguzi wa rais.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Umri wa mgombea urais uwe miaka kumi na nane-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]12.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]83(i) kinga dhidi ya mashtaka ya Rais.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Wakati wowote Rais akiwa madarakani na baada ya kuacha kushika madaraka aweze kushtakiwa-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]13.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]105 (2) (b) wabunge wa kuteuliwa
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Kipengele hiki kifutwe na badala yake iwe wabunge 20 watakaochaguliwa kutokana na uwiano wa kura zilizopigwa kwa vyama vya siasa-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]14.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]117(i) (a) Mgombea Ubunge
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Umri wa mgombea ubunge uwe miaka 18 na si 25 kama inavyopendekezwa-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]15.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]123(2) uwajibikaji wa mbunge.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Hii ifutwe na kuongeza :mbunge aliyependekezwa na chama cha siasa atapoteza ubunge wake ikiwa atafukuzwa au kuvuliwa uanachama wa chama chake cha siasa-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]16.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]123(3) mbunge kuhama/kujiunga na chama cha siasa.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Kuongeza ibara ndogo :endapo mbunge kwa ridhaa yake atajiondoa au kujivua uanachama wa chama cha siasa au kujiunga na chama kama alikuwa mgombea huru basi atapoteza sifa ya kuwa mbunge-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]17.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]124 adhabu kwa mbunge
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Kuondoa kabisa ibara hiyo na badala yake iseme wananchi wa jimbo au kata watakuwa na haki ya kuwaondoa madarakani kwa sababu na kwa kufuata utaratibu na sheria-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]18.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]182 Tume Huru ya uchaguzi.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Kuongeza wajumbe wa vyama vya Mawakili na vyama vya siasa-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]19.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]184 Tume Huru ya Uchaguzi
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Watumishi wote wa Tume Huru ya uchaguzi wasiwe watumishi wa serikali-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]20.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]234 Mkurugenzi wa usalama wa Taifa.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Ateuliwe baada ya kuthibitishwa na Bunge-NDIO
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]21.
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Nyongeza
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Kuanzishwa kwa mchakato wa katiba ya Tanganyika, kuundwa TUME ya Katiba ya Tanganyika-NDIO
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

MAONI YANGU:
1. Kuwepo na serikali tatu-ikiwamo serikali ya TANGANYIKA. Hii itasaidia kuondosha kero za muungano.
2. Wakuu wa wilaya na mikoa waondolewe.Napendekeza kuwepo na mameya kama wakuu wa halmashuri watakaohusika na maendeleo ya halmashauri zao pamoja na mambo ya utawala ikiwemo kusimamia usalama. Hii ni kwa sababu wao hawajateuliwa na mtu bali wametokana na kura za wananchi. Nafasi ya mkurugenzi wa wilaya/mkoa/jiji au mji iendelee kuwepo au ibadilishwe Jinan a kuwa Governors. Hawa ndio wahusike na burget za majiji/wilaya/mikoa na kupanga maendeleo.
3. Katiba iweke wazi IDADI na MAJINA ya wizara katika serikali ya MUUNGANO na hatimaye ya TANGANYIKA pale itakapoundwa.Zanzibar nao watasema katiba yao iweje katika hili.Hii itapunguza au kukomesha uwezekano wa rais kuteua hovyo na kujaza wizara nyingi ambazo zinakuwa gharama kwa wananchi. Uwepo wa wizara kama zile zisizo maalumu utakoma kwa kufanya hivi maana rais atalazimika kuteua mawaziri kulinga na idadi na majina ya wizara zilizoainishwa katika katiba.
4. 4. Katiba iweke wazi kuwa Tanzania ambayo Ni itatokana na muungano mpya Kati ya TANGANYIKA na ZANZIBAR serikali yake haina Dini bali wananchi wake mmoja mmoja ndio wana dili na imani tofauti tofauti. Hivyo hakuna mtu atakaye ingilia uhuru wa kuabudu wa mtu mwingine wla kukashfu dini ya mtu mwingine.
5. Rais apunguziwe madaraka. Kwa hali ilivyo sasa rais ana madaraka makubwa mno yanayoweza kutishia uhai wa nchi yetu. Ni Rahisi kwa rais hivi sasa kuteua rafiki, Jamaa, ndugu, watoto, wajomba na mashangazi kuingia katika madaraka kitu ambacho kinatishia utendaji wa serikali yake pia. Napendekeza uteuzi wa rais uishie kwa mawaziri na manaibu mawaziri,Mkuu wa majeshi,IGP na Mkuu wa usalama wa taifa ambao nao watahitaji kuthibitishwa na bunge. Nafasi kama za wakurugenzi wa Idara mbali mbali, zitangazwe na watu wenye qualifications stahiki waombe na wasailiwe na tume ya ajira. Pia rais atazamwe kuhusu ZIARA nje ya nchi maana ziara zilizopita kiasi ni gharama kwa nchi. Kuwepo na control ya ziara za Rais toka kwa wananchi na gharama na faida/hasara ya ziara hizo ziwekwe wazi.
6. Katiba ya Tanzania iweke wazi kuwa Elimu ya msingi na secondary ni haki ya kila mtoto wa Tanzania na itatolewa Bure.
7. Spika na naibu spika wa Bunge la TANZANIA wasiwe miongoni mwa wabunge na wasitokane na chama chochote cha siasa.Napendekeza wateuliwe miongoni mwa majaji wa mahakama ya Rufaa ambao wana record nzuri ya uadilifu na utendaji uliotukuka, usio tiliwa mashaka na wathibitishwe na BUNGE.
8. Katiba iweke wazi kuwa rais wa Tanzania ataapishwa siku angalau sitini (60) baada ya matokeo kutangazwa, Kumekuwa na haraka ya watu kukimbilia kujitangaza huku wakiacha maswali kuhusu uhalali wa ushindi wao.Katika kipindi cha kusubiri kuapishwa, kuwe kuna kuhoji matokeo. Pia napendekeza matokeo ya Uchaguzi kuanzia udiwani hadi urais yawe yanatangazwa moja kwa moja toka vituoni badala ya kusubiri hadi yafike ngazi ya taifa.
9. Kuwepo na sheria ya kuwabana maofisa wa TUME YA UCHAGUZI wanaoenda kinyume na maadili ya kazi yao pindi ikionekana wazi kuwa walighushi nyaraka za matokeo ili kumpa ushindi mgombea wa chama wanachopendelea wao.
10. Katiba iipe uwezo serikali kutaifisha mali zilizopatikana kwa njia zisizo halali kama ufisadi, wizi wa mali za umma,uuzaji wa madawa ya kulevya na kuwafungulia mashitaka wahusika mara moja na hapa kila anayeingia katika utumishi wa umma afanyiwe audit ya mali zake kwanza.
11. Katika izungumze kuhusu fedha-Control ya pesa ya Tanzania haiko vizuri na watu wanatumia sana pesa za kigeni hapa nchini bila kuhojiwa wala kulipia kodi. Control hafifu ya uingizwaji wa pesa za kigeni unashusha thamani ya Shilingi yetu.
12. Katiba ikataze wananchi kuchangishwa fedha kwa ajili ya maendeleo maana wanalipa KODI. Kodi mbali mbali zinazokusanywa na serikali ndio zifanye maendeleo na uchngiaji wa maeendeleo kwa watu binafsi uwe wa hiari.
13. Wabunge mwanamke na mwanaume haijakaa sawa.
Mwisho wa maoni
 
Ok, kazi nzuri, hata sisi wengine tutajaza online
 
Usibaki nyuma.

Toa maoni yako hapa JF, kwenye fomu iliyoko kwenye hii thread, au tume ujumbe mfupi kwenye namba 0789248224 au email; chademaoni@gmail.com.

Wenzako hapa wanashiriki moja kwa moja, kwenye Mabaraza Huru ya Katiba Mpya, yanayoendeshwa na CHADEMA nchi nzima.
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1377014884.207716.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1377014884.207716.jpg
    96.3 KB · Views: 33
  • ImageUploadedByJamiiForums1377014897.897130.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1377014897.897130.jpg
    143.8 KB · Views: 34
  • ImageUploadedByJamiiForums1377014910.921879.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1377014910.921879.jpg
    114.9 KB · Views: 34
Songa pamoja na wenzako katika kushiriki kutoa maoni ya Rasimu ya Katiba Mpya, kwenye Mabaraza Huru ya CHADEMA.
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1377015121.207360.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1377015121.207360.jpg
    119 KB · Views: 33
  • ImageUploadedByJamiiForums1377015138.755788.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1377015138.755788.jpg
    84.8 KB · Views: 33
  • ImageUploadedByJamiiForums1377015174.582559.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1377015174.582559.jpg
    133.3 KB · Views: 29
Maoni huru, si yale ya kujifungia vyumbani...
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1377016310.191273.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1377016310.191273.jpg
    77.3 KB · Views: 25
Maoni kwenye Rasimu ya Katiba Mpya, Mabaraza Huru ya CHADEMA. Wananchi wa Manyara asanteni.
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1377016758.125514.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1377016758.125514.jpg
    122.8 KB · Views: 24
  • ImageUploadedByJamiiForums1377016821.530218.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1377016821.530218.jpg
    130.6 KB · Views: 29
Inafahamika vyema kuwa siku ya jumapili ni siku ya ibada ya wakristo lkn mara zote ndo imekuwa ikitumika kama siku rasmi ya kupiga kura hapa kwetu TZ, hii imekuwa ikiathiri sana watu wengi kujitokeza kwenda kupiga kura, maana kuna watu/madhehebu mengi sana ktk dini hiyo huitumia siku ya jumapili muda mwingi kuwa ibadani mengine kuanzia asubuhi mpaka jioni.Kwa experiece yangu wengi wakifika vituoni wakikuta foleni ndefu kidogo basi hurudi nyumbani kujiandaa kwenda kusali na hapo suala la kupiga kura ndo halipo tena.

NAPENDEKEZA KATIBA MPYA IANISHE siku ya kupiga kura kwa chaguzi zetu iwe ni siku ya kazi ya kiserikali na siku hiyo ikafanywa kuwa public holiday kwa watu kwenda kupiga kura tu.
Wenzetu kenya wameianisha kabisa katika katiba yao ni JUMANNE.
 
Mkuu Tumaini Makene

More updates;

59.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka ya utekelezaji kwa mambo yote yaliyoorodheshwa kuwa Mambo ya Muungano, na wakati inapotekeleza majukumu yake, itazingatia mamlaka yake iliyopewa chini ya Katiba hii.

(2)Utekelezaji wa majukumu ya Serikali utafanywa kwa namna na kwa misingi iliyowekwa na Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge.
(3) Bila ya kuathiri aukukiuka masharti ya Ibara hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kwa makubaliano na masharti maalum baina yake na Serikali ya Zanzibar au Serikali ya Tanzania Bara, inaweza kutekeleza jambo lolote lililo chini ya mamlaka ya Serikali ya Zanzibar au Serikali ya Tanzania Bara kwa mujibu wa masharti ya makubaliano hayo.

Maoni;

59.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka ya utekelezaji kwa mambo yote yaliyoorodheshwa kuwa Mambo ya Muungano, na wakati inapotekeleza majukumu yake, itazingatia mamlaka yake iliyopewa chini ya Katiba hii.

(2)Utekelezaji wa majukumu ya Serikali utafanywa kwa namna na kwa misingi iliyowekwa na Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge.

(3) Bila ya kuathiri au kukiuka masharti ya Ibara hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kwa makubaliano na masharti maalum baina yake na Serikali ya Zanzibar au Serikali ya Tanganyika, inaweza kutekeleza jambo lolote lililo chini ya mamlaka ya Serikali ya Zanzibar au Serikali ya Tanganyika kwa mujibu wa masharti ya makubaliano hayo.
(4) Kwa ajili ya utekelezaji na kuondoa mgogoro au taswira ya upendeleo au ubaguzi makubaliano yoyote kwa mujibu wa Ibara ya 59;(3) kama yatahitaji mali au pesa toka hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ni lazima yawe makubaliano yatakayokuwa na manufaa sawa kwa pande zote za Washirika wa Muungano.

61.-(1) Kwa mujibu wa Katiba hii, Washirika wa Muungano ni Tanzania Bara na Zanzibar.

(2) Serikali ya Tanzania Bara itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Tanzania Bara.
(3) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.
(4) Washirika wa Muungano watatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na Katiba zao.
(5) Washirika wa Muungano watakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano na watatekeleza majukumu yao kwa masuala yote yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Washirika wa Muungano kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na Katiba za Washirika wa Muungano.

Maoni;

61.-(1) Kwa mujibu wa Katiba hii, Washirika wa Muungano ni Tanganyika na Zanzibar.
(2) Serikali ya Tanganyika itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Tanganyika
(3) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.
(4) Washirika wa Muungano watatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na Katiba zao.
(5) Washirika wa Muungano watakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano na watatekeleza majukumu yao kwa masuala yote yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Washirika yasiyo ya Muungano kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na Katiba za Nchi zao(Tanganyika /Zanzibar) kwa Mambo yote yasiyokuwa ya Muungano.

Mamlaka ya Washirika wa Muungano

62.-(1) Kila Mshirika wa Muungano atakuwa na mamlaka na haki zote juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano, na katika utekelezaji wa mamlaka hayo, kila Mshirika wa Muungano atazingatia misingi ya ushirikiano na mshirika mwingine kwa kuzingatia haki na usawakwa ajili ya ustawi ulio bora kwa wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano.
(2) Bila ya kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii, kila Mshirika wa Muungano atakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha mahusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mambo yaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Mshirika wa
Muungano.
(3) Mshirika wa Muungano anaweza, wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Ibara ndogo ya (2), kuomba mashirikiano kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kufanikisha mahusiano na jumuiya au taasisi ya kimataifa au kikanda, na Serikali ya Jamhuri Muungano inaweza kutoa ushirikiano kwa mshirika huyo kwa namna itakavyohitajika.

Maoni;

Uhusianao wa Washirika wa Muungano na Nchi au Mashirika ya Nje.

62 (1) Bila ya kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii, kila Mshirika wa Muungano atakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha mahusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mambo yaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Mshirika wa Muungano.
(2) Mshirika wa Muungano anaweza, wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Ibara ndogo ya (1), kuomba mashirikiano kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kufanikisha mahusiano na jumuiya au taasisi ya kimataifa au kikanda, na Serikali ya Jamhuri Muungano inaweza kutoa ushirikiano kwa mshirika huyo kwa namna itakavyohitajika.
(3) Kwa ajili ya utekeleza mzuri wa Ibara ya 62;(1 na 2) ya Katiba hii Bunge litatunga Sheria na Kanuni itakayosimamia mipaka ya Mahusiano Kati ya Washirika wa Muungano na Nchi zingine

Maoni;

Mahusiano kati ya Washirika wa Muungano.

63.-(1) Kila Mshirika wa Muungano anaweza, katika kutekeleza majukumu yake katika maeneo mbalimbali, kutekeleza majukumu hayo kwa misingi ya kushirikiana na kushauriana na Mshirika wa Muungano mwingine au baina ya Mshirika wa Muungano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kukuza na kulinda maslahi ya Taifa na maendeleo ya wananchi.
(2) Washirika wa Muungano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wanaweza kushauriana na kushirikiana katika mambo ya uongozi, utawala,vyombo vya uwakilishi na kimahakama.
(3) Utendaji wa Serikali za Washirika wa Muungano au wa chombo chochote kati ya vyombo vya serikali hizo na uendeshaji wa shughuli, utatekelezwa kwa kuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano na nia na umuhimu wa haja ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya
Taifa.

(4) Katika kufanikisha na kurahisisha shughuli za utendaji na Mawasilaiano kwa pande zote Washirika wa Muungano kupitia Katiba zao watatakiwa kuunda Wizara ambayo pamoja mambo wengine, itasimamia na kutekeleza Majukumu yaliyotajwa kati Ibara ya 62 na 63 ya Katiba hii.

Mawaziri Wakaazi

64.-(1) Kila Mshirika wa Muungano atateua Waziri Mkaazi atakayeratibu na kusimamia mahusiano baina ya Serikali za Washirika na kati ya Serikali ya Mshirika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2)Mawaziri Wakaazi watakuwa na ofisi zao na watafanya kazi wakiwa Makao Makuu ya Serikali ya Muungano.
(3) Pamoja na majukumu mengine watakayopangiwa na Serikali za Washirika wa Muungano, Mawaziri Wakaazi watakuwa na majukumu yafuatayo:

(a) kushughulikia mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu ushirikiano au mahusiano ya kimataifa; na
(b) kuwa kiungo baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Washirika wa Muungano na baina ya Serikali za Washirika wa Muungano.

Maoni;

Ibara hii ni ya Kufutwa kabisa na badala yake maudhui yake yahamie 63(4)

65.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itapata mamlaka yake kutoka kwa wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na kusimamiwa na chombo kitakachopewa mamlaka na Katiba hii, na vilevile, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

zitapata mamlaka kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na kusimamiwa na vyombo vitakavyopewa mamlaka chini ya Katiba zao.
(2) Serikali za Washirika wa Muungano, katika kutekeleza mamlaka zao, zitawajibika kustawisha mamlaka ya wananchi kwa kugatua madaraka kwa serikali za mitaa zitakazoanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania Bara au Katiba ya Zanzibar, kama itakavyokuwa.
Maoni;

65.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itapata mamlaka yake kutoka kwa wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na kusimamiwa na chombo huru kitakachopewa mamlaka na Katiba hii, na vilevile, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitapata mamlaka kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na kusimamiwa na vyombo huru vitakavyopewa mamlaka chini ya Katiba zao.
(2) Serikali za Washirika wa Muungano, katika kutekeleza mamlaka zao, zitawajibika kustawisha mamlaka ya wananchi kwa kug'atua madaraka kwa serikali za mitaa zitakazoanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika au Katiba ya Zanzibar, kama itakavyokuwa.

66.-(1) Bila ya kuathiri wajibu wa kila raia kwa mujibu wa Katiba hii, viongozi wakuu wenye mamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano waliotajwa katika Ibara ndogo ya (3) watawajibika, kila mmoja wao katika kutekeleza madaraka waliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii au Katiba za Washirika wa Muungano kuhakikisha kuwa analinda, kuimarisha na kudumisha Muungano.

(2) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara ndogo ya (1), kila mmojawapo wa viongozi wakuu waliotajwa katika Ibara ndogo ya (3), kabla ya kushika madaraka yake ataapa kuutetea na kuudumisha Muungano kwa mujibu wa Katiba hii.
(3) Viongozi Wakuu wanaohusika na masharti ya Ibara hii ni:
(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(c) Rais wa Tanzania Bara; na
(d) Rais wa Zanzibar.

Maoni;

66.-(1) Bila ya kuathiri wajibu wa kila raia kwa mujibu wa Katiba hii, viongozi wakuu wenye mamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano waliotajwa katika Ibara ndogo ya (3) watawajibika, kila mmoja wao katika kutekeleza madaraka waliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii au Katiba za Washirika wa Muungano kuhakikisha kuwa analinda, kuimarisha na kudumisha Muungano.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara ndogo ya (1), kila mmojawapo wa viongozi wakuu waliotajwa katika Ibara ndogo ya (3),kabla ya kushika madaraka yake ataapa kuutetea na kuudumisha Muungano kwa mujibu wa Katiba hii.
(3) Viongozi Wakuu wanaohusika na masharti ya Ibara hii ni:
(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;

(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(c) Rais wa Tanganyika; na
(d) Rais wa Zanzibar.

68.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

(2) Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu na:
(a) atakuwa alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watu wake;
(b) atakuwa alama ya umoja na uhuru wa nchi na mamlaka yake;na
(c) atakuwa na dhamana ya kukuza na kuhifadhi umoja wa kitaifa.

Maoni;

(b) Rais
Rais wa Jamhuri ya Muungano
68.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu na:
(a) atakuwa alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watu wake;
(b) atakuwa alama ya umoja na uhuru wa nchi na mamlaka yake;na
(c) atakuwa na dhamana ya kukuza na kuhifadhi haki za binadamu pamoja na umoja wa
Kitaifa na;

(d)atakuwa na dhamana ya kukuza Uchumi kwa manufaa ya watanzania wote
(e) atakuwa na dhamana ya kulinda amani na Maendeleo ya Wananchi kwa ujumla wake.

69.-(1)Rais akiwa Mkuu wa Nchi, atakuwa na madaraka na majukumu yafuatayo:

(a) kuisimamia na kuilinda Katiba;
(b) kulinda utaifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(c) kuhutubia na kufungua rasmi Bunge Jipya na kulivunja Bunge baada ya kumaliza muda wake;
(d) kuhutubia na kufungua rasmi Kalenda ya Mwaka ya Mahakama;
(e) kuidhinisha uwasilishaji Bungeni makisio ya mapato na matumizi ya Serikali, Bunge na Mahakama katika mwaka wa fedha;
(f) kuweka saini katika Muswada wa Sheria uliyopitishwa na Bunge;
(g) kutunuku nishani za heshima kwa niaba ya Watu wa Jamhuri ya Muungano kwa ujumla;
(h) kuteua Mabalozi,Watu watakaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wawakilishi wa nchi katika taasisi mbalimbali za kimataifa;
(i) kupokea hati za utambulisho za Mabalozi wa nchi za nje nchini;
(j) kutoa msamaha kwa mtu yeyote anayetumikia adhabu iliyotolewa na Mahakama kwa mujibu wa sheria za nchi; na
(k) kuidhinisha utekelezaji wa adhabu ya kifo iliyotolewa kwa mujibu wa sheria za nchi.

(2) Rais akiwa Amiri Jeshi Mkuu, atakuwa na madaraka na majukumu yafuatayo:
(a) kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa;
(b) kuamuru Majeshi ya Ulinzi kwenda vitani au kusitisha vita;
(c) kutia saini makubaliano ya amani au kusitisha vita;
(d) kutangaza hali ya hatari au hali ya kuzingirwa eneo fulani;
(e) kuteua Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
(f) kuwapandisha vyeo maofisa wa vyombo vya ulinzi na
usalama katika ngazi mbalimbali na kutoa kamisheni kwa
maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

(3) Akiwa Kiongozi wa Serikali, Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa na madaraka na majukumu yafuatayo:
(a) kuongoza vikao vya Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano;
(b) kupanga, kuelekeza, kusimamia na kuratibu majukumu ya wizara na taasisi za serikali;
(c) kuwateua Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(d) kumteua Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu;
(e) kumteua Mwanasheria Mkuu na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na
(f) kuwateua makamishna wa Tume mbalimbali zilizoanzishwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

(4) Katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Ibara hii,Rais ataepuka kujinasibisha, kwa namna yoyote ile, na chama chochote cha siasa au kundi lolote kwa namna ambayo inaathiri umoja wa wananchi.

Maoni;

Madaraka na majukumu ya Rais

69.-(1)Rais akiwa Mkuu wa Nchi, atakuwa na madaraka na majukumu yafuatayo:

(a) kuisimamia, kuilinda na kuiheshimu Katiba hii wakati wote wa Uraisi wake na hata baada ya kustaafu na kuwa raia wa kawaida.

(b) kulinda utaifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

(c) kuhutubia na kufungua rasmi Bunge Jipya na kulivunja Bunge baada ya kumaliza muda wake kwa taratibu inayotambulika kwa mujibu Katiba hii.

(d) kuhutubia na kufungua rasmi Kalenda ya Mwaka ya Mahakama;

(e) kuidhinisha uwasilishaji Bungeni makisio ya mapato na matumizi ya Serikali, Bunge na Mahakama katika mwaka wa fedha;

(f) kuweka saini katika Muswada wa Sheria uliyopitishwa na Bunge;

(g) kutunuku nishani za heshima kwa niaba ya Watu wa Jamhuri ya Muungano kwa ujumla;

(h) kuteua Mabalozi,Watu watakaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wawakilishi wa nchi katika taasisi mbalimbali za kimataifa;

(i) kupokea hati za utambulisho za Mabalozi wa nchi za nje nchini;

(j) kutoa msamaha kwa mtu yeyote anayetumikia adhabu iliyotolewa na Mahakama kwa mujibu wa sheria za nchi isipokuwa waliohukumiwa Kifo Msamaha wao unaweza kuwa Kifungo cha maisha jela na katika kutoa Msamaha Raisi atazingatia na kufuata Ushauri wa Tume ya Magereza au tume yoyote yenye Mamlaka dhidi ya wafungwa.
(k) kuidhinisha utekelezaji wa adhabu ya kifo iliyotolewa kwa mujibu wa sheria za nchi.

(2) Rais akiwa Amiri Jeshi Mkuu, atakuwa na madaraka na majukumu yafuatayo:

(a) kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa;

(b) kuamuru Majeshi ya Ulinzi kwenda vitani au kusitisha vita baada ya Mashauriano na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa;

(c) kutia saini makubaliano ya amani au kusitisha vita baada ya Mashauriano na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa;
;

(d) kutangaza hali ya hatari au hali ya kuzingirwa eneo Fulani ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kutoa taarifa kadri iwezekanavyo kwa Raisi wa Eneo la Mshirika wa Muungano.

(e) kuteua Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama; na

(f) kuwapandisha vyeo maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama katika ngazi mbalimbali na kutoa kamisheni kwa maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

(g)Kwa vyovyote vile ibara ya 69.(2; b,c na d) ya Ibara hii haitamzuia Raisi kuchukua uamuzi wa dharua katika hali ya hatari kabla ya kufanya mashauriano na Baraza la Usalama wa Taifa kama ataona inafaa kufanya hivyo hata hivyo ataliarifu Baraza ndani ya Siku saba toka afanye Uamuzi huo

(3) Akiwa Kiongozi wa Serikali, Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa na madaraka na majukumu yafuatayo:

(a) kuongoza vikao vya Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano;

(b) kupanga, kuelekeza, kusimamia na kuratibu majukumu ya wizara na taasisi za serikali moja kwa moja au kupitia kwa Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara husika wa Serikali ya Muungano;

(c) kuwateua Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;

(d) kumteua Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu;

(e) kumteua Mwanasheria Mkuu na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na

(f) kuwateua makamishna wa Tume mbalimbali zilizoanzishwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

(g) Kusimamia na kutathimini utendaji wa Serikali ya Muungano kwa ujumla wake.

(h) Kusimamia utendaji na kuchukua hatua za haraka za kinidhamu dhidi ya wateule wote walio chini ya mamlaka yake ya Uteuzi watakaoenenda kinyume na Ibara ya 13 na 14 ya Katiba hii.

(4) Katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Ibara hii, Raisi ataepuka kujinasibisha, kwa namna yoyote ile, na chama chochote cha siasa au kundi lolote kwa namna ambayo inaathiri umoja wa wananchi.

-------------------

Copy Mnyika ,Invisible Mzee Mwanakijiji Zitto.

Itaendelea;
 
Last edited by a moderator:
Hadi sasa, kutokana na mikutano ya hadhara leo, ambayo imefanyika, Bunda, Mugumu, Tarime na Musoma (timu ya Mwenyekiti) na Same, Mwanga, Rombo na Vunjo (timu ya Katibu Mkuu), maoni yakiendelea kumiminika, mambo yanakwenda vizuri kama ifuatavyo;

Ujumbe mfupi wa simu ya mkononi;

Kutoka Mwanga, hadi sasa sms 214

Kutoka Vunjo, ambako mkutano umemalizika hivi punde, hadi sasa sms 516

Kutoka Rombo, hadi sasa sms 423

Kutoka Bunda, hadi sasa ni 264

Kutoka Tarime, hadi sasa sms 1,226

Kutoka Mugumu, Serengeti, hadi sasa sms 312

Kutoka Musoma ambako mkutano bado unaendelea, hadi sasa ni sms 278

Kamanda, Ni up date kutoka Iramba na Singida kwa Ujumla.
 
Back
Top Bottom