Choroko ni moja ya mazao ya jamii ya mikunde hustawi eneo lenye mwanga wa kutosha pamoja na udongo wa tifutifu.pia masoko yake ni mazuri mfano kwa masasi 1300-1500@kg
Hakihitaji mvua nyingi na hakuna magonjwa yanayoathiri isipokuwa wadudu wanashambulia majani pamoja na choroko wakati za kuzaa hivyo suluhisho ni kupulizia dawa za kuu wadudu kama NINJA,KARATE,DUDU ALL e.t.c kila baaea ya siku 14 kuanzia wakati zinatoa maua
Huchukua siku 60 hadi kuvuna japo hazizai kwa mkupuo yaani kadri unyevu ulivyo ndivyo nazo huzidi kutoa maua na kuzaa.pia waweza mwagilia kama unavyolima kunde.
Katika kupanda tofauti ya shina na shina ni sm 35 na tofauti ya mstari na mstari sm 55.pia kila shina moja unatia punje 2-3 za choroko,halihitaji mbolea ila unahitaji kupulizia dawa ya kuuwa wadudu hasa wakati zinazaa walau mara 21 .h
ivyo vijana tujishughulishe tupige kazi