Muhtasari wa kilimo cha baadhi ya mazao jamii ya kunde

Muhtasari wa kilimo cha baadhi ya mazao jamii ya kunde

Mkuu hizo ni stori za watu tu ukweli halisi haupo hivyo, hebu soma hapa labda mimi naona vibaya, pitia hii link uone halihalisi

CHANGAMOTO YA KUKOSA SOKO LA UHAKIKA KWA WAKULIMA CHANZO CHA UMASIKINI

WAKULIMA wa zao la dengu katika kijiji cha Amani kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa soko la uhakika kwenye zao hilo ikiwemo miundombinu ya barabara kuwa mibovu hali ambayo inawafanya kushindwa kusafirisha mazao yao.

Wakiongea na mwandishi wa habari aliyetembelea wakulima wa kijiji hicho walisema kuwa zao hilo limekuwa mkombozi katika kunyanyua pato la familia lakini kubadilika kwa bei ikiwa wengine wanauza shilingi 45,000 mpaka 55,000 kwa gunia moja na kukosa soko la uhakika imekuwa ni tatizo, ikiwemo wadudu wahalibifu pamoja na panya.
 
Habari wadau,

Kampuni ya Kilimo Business and Associates www.facebook.com/KILIMOBIZNET kwa kushirikiana na Chama Cha wakulima wahitimu Tanzania (Tanzania Graduate Farmers Association-TGFA) www.facebook.com/TanzaniaGFA inapenda kuwataarifu wajasiriamali na wadau wengine wa kilimo kwamba tunaendelea kupokea order za mbegu za mikunde kama dengu, mbaazi, choroko, kunde n.k.

open
open
open
open
open
open

Mbegu hizi tunazinunua kwa makubaliano maalum kutoka kwa wanunuzi wa mazao hayo (baadae atakuja kununua kama watakubaliana bei na mzalishaji) pia vituo vya utafiti pamoja na agents wa mbegu hizo zenye ubora na viwango.

Tunashauri wale wakulima ambao wangependa kuwa na hakika ya biashara yao na hata kununua mbegu zenye ubora wakubali kutumia huduma zetu kwa kuuliza na hata kutoa order mapema kabla mzimu haujaanza.

BONYEZA HAPA Ili kuweza kuwekwa kwenye list ya wadau muhimu pamoja na kutoa order yako ya mbegu ama kutafutiwa soko la hakika tafadhali BONYEZA HAPA.
Kumbuka mbegu zote tunazosambaza zimefanyiwa tafiti na zimethibitishwa na TOSCI..... Pia mkumbuke mbegu ikishakaa zaidi ya miez 7 lazima irudishwe ikapimwe.

Kwa mawasiliano zaidi piga namba 0718664645 ama 0789856246 ama 0763954635 email kilimobiznet@gmail.com

open
open
open
 
TUnashukuru kwa wale ambao wanaendelea kutupigia simu na hata kutuandikia email... Usichukie ukikuta simu yako haipokelewi. Tutakupigia ama kukujibu sms utakayotuma
 
Choroko ni moja ya mazao ya jamii ya mikunde hustawi eneo lenye mwanga wa kutosha pamoja na udongo wa tifutifu.pia masoko yake ni mazuri mfano kwa masasi 1300-1500@kg
Hakihitaji mvua nyingi na hakuna magonjwa yanayoathiri isipokuwa wadudu wanashambulia majani pamoja na choroko wakati za kuzaa hivyo suluhisho ni kupulizia dawa za kuu wadudu kama NINJA,KARATE,DUDU ALL e.t.c kila baaea ya siku 14 kuanzia wakati zinatoa maua
Huchukua siku 60 hadi kuvuna japo hazizai kwa mkupuo yaani kadri unyevu ulivyo ndivyo nazo huzidi kutoa maua na kuzaa.pia waweza mwagilia kama unavyolima kunde.

Katika kupanda tofauti ya shina na shina ni sm 35 na tofauti ya mstari na mstari sm 55.pia kila shina moja unatia punje 2-3 za choroko,halihitaji mbolea ila unahitaji kupulizia dawa ya kuuwa wadudu hasa wakati zinazaa walau mara 21 .h

ivyo vijana tujishughulishe tupige kazi

Mkuu waweza nipa ushari mzuri wa zao hili?tafadhali tuwasiliane kupitia medardaristides@yahoo.com
 
Mm niliwachek mkaniambia hamna mbegu za kunde kwa sasa..
Nashsuri mkajipange kwanza then mtakuja upya.
 
Hey guys, mimi ni mgeni lkn ni mwenyeji Sana kwa kupita humu ndani nimekuwa nafuatilia michango ya akina Malila na wenzie Muda mrefu, Sasa safari hii nimelima mihogo na choroko Tanga maeneo ya Marungu natarajia kuvuna mwezi wa 6 mwishoni mkae mkao wa kula Insha Allah

Mkuu tupe mrejesho wa muhogo ilikuwaje kwenye mavuno katika hekali ulizolima ulipata tani ngapi kwa kila hekali, na ulitumia mbegu gani, na sokoni bei ilikuwaje wakati wa kuuza mzigo wako??
 
Habari wataalam wa kilimo na ufugaji,
Naomba kwa mwenye ufahamu na zao la kunde,
1. Hekari moja inaweza kutoa gunia ngapi za kunde(mavuno)
2. Ni mbegu gani inayo zaa sana ya muda mfupi na inayo pendwa sokoni?
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.
 
Samahani wakuu nilipotea kwa muda, kuhusu mihogo baadhi ilipata ugonjwa ikaaribika iliyobakia niliuza kwa sh, 150000/= tu, nikaona nibadilishe zao nimepanda miembe ya kisasa aina ya Ngowe heka moja mwaka jana, na mihogo pia ninayo heka 1 yakutoka mwezi wa 9 na mengine heka 2 itatoka mwakani kwenye mwezi wa 2-3. Kweli kilimo kinachanga moto wakuu kinahitaji uvumilivu sana
 
Naomba kwa anaye jua bei ya choroko na kunde kwa jumla inauzwaje anijuze tafadhali..
 
Naomba kwa anaye jua bei ya choroko na kunde kwa jumla inauzwaje anijuze tafadhali..
Bei 1600 mpaka 3000 kwA wanunuzi wa export
Lakini kwA sahvi msimu wa choroko ushapita ni mpaka messi wa tatuu mwakani...mkuu
 
Bei 1600 mpaka 3000 kwA wanunuzi wa export
Lakini kwA sahvi msimu wa choroko ushapita ni mpaka messi wa tatuu mwakani...mkuu
Nilitaka nilime mvua za vuli zikianza mwezi wa kumi kama heka 5 hivi, so sinto pata soko?
 
Back
Top Bottom