somji
Senior Member
- Jan 11, 2015
- 114
- 67
Nchck 0752886798Habari zenu natafuta ton 25 za choroko
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nchck 0752886798Habari zenu natafuta ton 25 za choroko
Choroko ni moja ya mazao ya jamii ya mikunde hustawi eneo lenye mwanga wa kutosha pamoja na udongo wa tifutifu.pia masoko yake ni mazuri mfano kwa masasi 1300-1500@kg
Hakihitaji mvua nyingi na hakuna magonjwa yanayoathiri isipokuwa wadudu wanashambulia majani pamoja na choroko wakati za kuzaa hivyo suluhisho ni kupulizia dawa za kuu wadudu kama NINJA,KARATE,DUDU ALL e.t.c kila baaea ya siku 14 kuanzia wakati zinatoa maua
Huchukua siku 60 hadi kuvuna japo hazizai kwa mkupuo yaani kadri unyevu ulivyo ndivyo nazo huzidi kutoa maua na kuzaa.pia waweza mwagilia kama unavyolima kunde.
Katika kupanda tofauti ya shina na shina ni sm 35 na tofauti ya mstari na mstari sm 55.pia kila shina moja unatia punje 2-3 za choroko,halihitaji mbolea ila unahitaji kupulizia dawa ya kuuwa wadudu hasa wakati zinazaa walau mara 21 .h
ivyo vijana tujishughulishe tupige kazi
TumainiKunde aina gani ndio zina soko zuri?
Hey guys, mimi ni mgeni lkn ni mwenyeji Sana kwa kupita humu ndani nimekuwa nafuatilia michango ya akina Malila na wenzie Muda mrefu, Sasa safari hii nimelima mihogo na choroko Tanga maeneo ya Marungu natarajia kuvuna mwezi wa 6 mwishoni mkae mkao wa kula Insha Allah
Mkuu hiyo ni bei ya jumla au reja reja?Dar es salaam bei ni 2500 @1kg
Bei 1600 mpaka 3000 kwA wanunuzi wa exportNaomba kwa anaye jua bei ya choroko na kunde kwa jumla inauzwaje anijuze tafadhali..
Nilitaka nilime mvua za vuli zikianza mwezi wa kumi kama heka 5 hivi, so sinto pata soko?Bei 1600 mpaka 3000 kwA wanunuzi wa export
Lakini kwA sahvi msimu wa choroko ushapita ni mpaka messi wa tatuu mwakani...mkuu