Muhuni akopa milioni 50 CRDB awaachia pumba likidhaniwa ni duka la nafaka

Mbona huwa wanachimba kuta za nyumba, ilikuwaje washindwe kufungua gunia randomly?
 
Kwa ujinga wa nchi hii usishangae hata hilo wazo alipewa na watumishi wa benki waliompa mkopo ambao kwenye ukaguzi nao wamejifanya kushangaa pia. Kipindi hicho walishakula mgao wao kwenye hiyo M50 kitambo.

Hii ni sawa na polisi wanaoiba na kuua mtu halafu hao hao kujifanya wanachunguza kilichotokea.
 
Hv unaweza kopa pesa mingi hvyo Kwa dhamana ya Duka tuu, ?? Si wanahtaj kitu kisichohamishika .... Naamin kabisa wakat aankopa alijaza magunia ya nafaka , alipochukua hela ndo akabadrisha akaweka pumba , nafaka akatokomea nazo .... Ni mchezo ambao ameuchora mda mrefu na baadhi ya wafanyakaz wa bank , huyo afisa mkopo kazi anayo
 
Kuna uhalifu hapo.Waanze na maafisa mikopo wao hao CRDB.Nimetulia paleee navuta kiko yangu yenye tumbaku mbichi.
 
Kimeumana.

Mangi kamla mangi.

Hapo lazima TAPELI ni mangi kushirikiana na mangi mwingine Afisa Mikopo kapiga.

Hata huyo anayeongea hapo ni mangi kabisa
 
Huo ni
mchongo kutoka watu wa benki wala huto siyo mhuni.

Huwezi kupewa mkopi bila watu kukagua mzigo kama ndio ulikuwa dhamana. Usikute kwenye hiyo 50 kaondoka na 20 TU zingine kawaachia wenye mchongo wao
Sio mbaya!Kuliko kwenda kuua roho zisizo na hatia kuiba mil 4 kajiongeza.Wizi nyakati hizi unahitaji connection hili utoboe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…