Muhuni akopa milioni 50 CRDB awaachia pumba likidhaniwa ni duka la nafaka

Muhuni akopa milioni 50 CRDB awaachia pumba likidhaniwa ni duka la nafaka

Kwa ujinga wa nchi hii usishangae hata hilo wazo alipewa na watumishi wa benki waliompa mkopo ambao kwenye ukaguzi nao wamejifanya kushangaa pia. Kipindi hicho walishakula mgao wao kwenye hiyo M50 kitambo.

Hii ni sawa na polisi wanaoiba na kuua mtu halafu hao hao kujifanya wanachunguza kilichotokea.
Kuna movie moja nimesahau title,jamaa waliiba bank "milioni mia moja" halafu meneja wa bank hiyo akaiba "milioni mia nne" na kuwaambia vyombo vya upelelezi kuwa wameibiwa milioni mia tano.

Ngoma ikabaki kwa wezi kuanza kufikiria wajitokeze na kusema kuwa wao wameiba milioni mia moja au wanyuti.
 
Hii video inawafedhehesha na kuwadiscredit CRDB wenyewe. Yaani how come wanaweza kulizwa kipumbavu namna hiyo na mteja kwa kiasi kikubwa hivy?
 
Waafrika tuna safari ndefu wahindi,waarabu na wapemba hukopeshana bila maandishi na mikopo hulipwa

Mswahili kumkopesha shida ,makaratasi kibao ,dhamana kibao na mkopo halipi anatoroka na kutokomea gizani

Ndio maana wahibdi,waarabu na wapemba hupata mikopo upesi na kirahisi kuliko waswahili ujanja janja mwingi wa kijinga kama wa huyo aliyechukua milioni 50 mjinga mkubwa
 
Hii video inawafedhehesha na kuwadiscredit CRDB wenyewe. Yaani how come wanaweza kulizwa kipumbavu namna hiyo na mteja kwa kiasi kikubwa hivy?
Wala inamdhalilisha mkopaji

Ulitaka benki waanze kumwaga chini kila gunia ku cheki kilichomo?

Alichofanya ni utoto na ujinga

Sasa milioni 50 itampeleka wapi kimaisha? Atabaki tu kuishi maisha ya kujificha ficha hawezi kaa sehemu ya public ,kusafiri nk anaishi kwa woga na inawezekana hiyo pesa kwa sasa ilishaisha
 
Wafanyakazi wa CRDB wamechukua hela kupitia huyo muhuni na walivyo matura hizo hela siku hizo hizo za kupokea mkopo nao wanapewa chao kupitia akaunti zao za crdb hiyo hiyo jamaa kabla hajawekewa hela anatakiwa atoe hela ya rushwa kubwa kabla hajawekewa mzigo ili asiwakimbie na wao...
Wahuni ndio wanakopa hela za riba kubwa mtaani kwanza kuwapa hao wezi wenzie ili asiwakimbie..
 
Back
Top Bottom