Muhuni akopa milioni 50 CRDB awaachia pumba likidhaniwa ni duka la nafaka

Muhuni akopa milioni 50 CRDB awaachia pumba likidhaniwa ni duka la nafaka

Muhuni akili mingi inadaiwa kama inavyoonekana kwenye video kuwa amekopa milioni 50 CRDB kwa kuwa alijua lazima wakague biashara yake, aliweka magunia mengi yakionekana yana nafaka kumbe ni uchafu tu, na yeye ametokomea yaani ameyeya.
View attachment 2522488
Waliopitisha mkopo wanahusika pia, iweje gunia la mchele toka Moro lifanane kwa nje kwa ushonaji wa mkono na gunia la mchele toka Mbeya! Duka unalikopesha mil.50 halina bidhaa za mil.10! Yaani kagunia kamoja ka maharage na kamoja mchele unaouzwa! Mimi ningeanza na afisa mikopo aliyelikagua duka na ningejifanya sijawahi kumuona tangu nizaliwe.
 
Dhamana ya 50m iko wap hapo?... Wafanyakazi ndio mmeiba hyo pesa...
50m nyie CRDB huwa mnakagua mpk kwake.. statement za mwaka mzma... Wadhamini..
 
Kwa ujinga wa nchi hii usishangae hata hilo wazo alipewa na watumishi wa benki waliompa mkopo ambao kwenye ukaguzi nao wamejifanya kushangaa pia. Kipindi hicho walishakula mgao wao kwenye hiyo M50 kitambo.

Hii ni sawa na polisi wanaoiba na kuua mtu halafu hao hao kujifanya wanachunguza kilichotokea.
Kweli kabisa
 
IMG_0771.jpg

Niwaambie tu huyu ndiye anasababisha tunaomba mkopo wa vikundi wa laki 5 tunaambiwa tuwe na TIN number yenye biashara mapato laki 8 kwa mwezi.
 
Hv unaweza kopa pesa mingi hvyo Kwa dhamana ya Duka tuu, ?? Si wanahtaj kitu kisichohamishika .... Naamin kabisa wakat aankopa alijaza magunia ya nafaka , alipochukua hela ndo akabadrisha akaweka pumba , nafaka akatokomea nazo .... Ni mchezo ambao ameuchora mda mrefu na baadhi ya wafanyakaz wa bank , huyo afisa mkopo kazi anayo
Nadhani dhamana ya vitu kama nyumba au viwanja lazima iwepo kwani ukiwa na biashara hizi za mtaani tu siyo rahisi kupewa. Mimi nilivyoelewa, japo huenda siko sahihi: Nadhani jamaa ndiyo alikuwa ametuma maombi ya mkopo na hapo walienda kuakagua biashara yake kwanza kabla hawajampa mkopo.
 
Unaongea au una uzoefu wa hiyo biashara?

Au unatumia duka lako kama standard ya maduka yote ya nafaka tanzania?

Kuna maduka ya nafaka yana mzigo zaidi hata ya 800M.

Mkuu duka si ndio hilo ktk video,au kuna store underground hatujaiona[emoji3063][emoji3063]
 
Hiyo hela yote ina maana hakuweka dhamana kitu kisichohamishika? Mimi kwa uelewa wangu uwepo wa biashara ni justification kwamba unafanya biashara hivyo una qualify kupata mkopo wa biashara. Maofisa wa bank walitakiwa kuangalia umiliki na cash flow ya hiyo biashara na sio vinginevyo. Otherwise wamepigwa kishamba sana.
Kuna mikopo ambayo dhamana inakuwa biashara yenyewe.
 
Tukiomba sisi mikopo hamtupi mnaenda wapa watu wenu,nasemajeeeeeeeeee SAFI sanaaaa Nasemajeeeee Safi sana Milioni 50 Pumba nyingiiiiiiii (nisaidieni kupga ule mluzi wa dj AllyB)
 
Aisee inawezekana sasa hapo sijui itakuaje?
Hasara hiyo kwa bank, huenda jamaa alichemka marejesho, hata lengo la bank huenda ilikuwa ikamate mzigo ila wamekuta hayo madude.. ila haya mambo yanaongeza ugumu sana wenye nia njema kupewa mkopo. Bank kama CRDB haiwezi ingia mkenge wa kufungua kesi hiyo .. funika kombe mwana haramu apite ndio kitachotokea
 
Kuna uhalifu hapo.Waanze na maafisa mikopo wao hao CRDB.Nimetulia paleee navuta kiko yangu yenye tumbaku mbichi.
Huo mkopo umekaa kimchongo. Kirahisi tu watoe milioni 50 bila hata ya dhamna ya mali isiyo hamishika? Huu utaratibu wameanza lini?

Na mpaka mfanyabiashara afikie hatua ya kukopa milioni 50, ni lazima atakuwa ameshakopa hela pungufu ya hizo, na kulipa marejesho kwa ukamilifu.

Lakini bado huqezi kukopa mkop wa biashara bila ya kuwa na tax clearance, utambulisho, kupiga picha nje na ndani ya eneo la biashara yako, nk. So kama vigezo vyote hivyo vilifuatwa, mhusika atakamatwa kirahisi sana.

Na kama havikufuatwa, basi Maafisa mikopo wana mkono wao kwenye huo mkopo.
 
Back
Top Bottom