Muige panya katika harakati za utafutaji, utatoboa

Muige panya katika harakati za utafutaji, utatoboa

Inamaana hata kama nyumba ina paka huyo panya atakaa wapi?
Oyaa rudisha hii avatar picha
bill-duke-predator.jpg
 
Nadhani wote tunamjua mnyama panya, sasa bwana panya anajua kabisa akisema amkimbie binadamu kwa kuogopa kifo na kuhamia porini, atakufa njaa. Tena kabla ya njaa huenda akauliwa na wanyama wakali zaidi.

Anachofanya panya ni kusoma ratiba ya binadamu ndani ya nyumba, saa ngapi anaenda kazini anafunga mlango, saa ngapi analala anazima taa. Jiko liko usawa upi akajipimie misosi na stoo au dari ni wapi akaandae bed room yake na familia.

Pia anawafunza wanae kutambua chakula kilichodondoka ndio chao, wakiona kisafi, kimenona, juu ya gazeti, huo mtego, wasile! Kwa mtindo huo,panya hunenepa na kuzaliana kizazi hadi kizazi.

Sasa wewe, bosi kakufokea ushawaza kukimbia kazi, mteja kakujibu jeuri, sijui kakopa hajalipa, unataka kufunga biashara. Utakufa NJAA wewee!
Niache us*nge na mimi,

Nipamabane
 
very wise words, be blessed
 
Watanzania wengi tunaishi kama panya aisee muda wote kukimbizana na changamoto za maisha.

Viongozi wetu wao wametulia wanakula vinono na familia zao ingawa tunaishi nao nchi moja.

Ukikosea tu ukaibukia sebuleni uninvited your in for it.

Inequalities is real in Tanzania.
 
Maisha mkuu, mwalimu tosha
Ni kweli mkuu, shukrani kwa mtazamo huu, unaweza kufunza wengine katika namna ya kupambana na maisha.

Inaonyesha ni jinsi gani unavyoweza kukabiliana na Maisha kupitia changamoto mbalimbali.
 
Ni kweli mkuu, shukrani kwa mtazamo huu, unaweza kufunza wengine katika namna ya kupambana na maisha.

Inaonyesha ni jinsi gani unavyoweza kukabiliana na Maisha kupitia changamoto mbalimbali.
Kama unasumbuliwa na panya nyumbani kwako fuga nyoka tu, panya wote wanakimbia
kufuga nyoka mkuu, si bora panya
 
Nafurahia utafutaji wa simba akili nyingi
Anatumia
Hakurupuki
Anapata changamoto lakini hakati tamaa
Simba hali mizoga
Yupo imara
Anajali familia
Kinachomsaidia simba ni mwili mkubwa na kapewa nguvu nyingi. Lakini pia hakuna mnyama juu ya simba anayekula nyama. Changamoto ya simba ni poachers tu ambayo si sana.

Panya katolewa mfano sababu ni kiumbe mdogo. Hakuna mahali ataishi huru atabaki salama. Binadamu anamuwinda, ndege wanamuwinda na nyoka wanamuwinda.

Anaishi kwa binadamu ila kwa timing na hiyo inawasaidia pia waendelee kuzaliana.

We ukikutana na mwanadamu siku mbili tu mmeshazoeana na kuaminiana na wakati mwingine mnazuliana. Ila panya anakaa hata mwaka kwa binadamu ila hataki mazoea.

Jamaa kawaza sana.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom