Muliro awakana Makada wa CHADEMA wanaodai kuteswa, kutupwa porini

Muliro awakana Makada wa CHADEMA wanaodai kuteswa, kutupwa porini

Sasa kama anakana polisi hawakuwakamata, kuwapiga na kuwatesa, si Jeshi la Polisi lingewakamata na kuwashtaki viongozi/wanachama wa Chadema kwa kusema/kuchapisha habari za uwongo, halafu wapelekwe mahakamani, na huko ndiko ukweli ujulikane?
kuna vyombo vingine vya ukamataji sio lazima polisi, inawezekana walikamatwa na askari wa wanyama pori,
 
Kamanda Murilo na Wewe ipo siku utakufa tutakuzika kwenye Jeneza, usisahau hilo
 
View attachment 3318629
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amekanusha jeshi hilo kuwakamata makada wa Chadema waliokuwa wakihudhuria kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 24, 2025.

Awali Kamanda Muliro aliwaonya viongozi na wanachama wa Chadema kutofika mahakamani hapo kufuatilia kesi hiyo, kwa madai kuwa wanataka kushinikiza Lissu aachiliwe huru, jambo ambalo lilipingwa na viongozi wa chama hicho waliowataka wanachama wao kufika kufuatilia kesi hiyo.

Kesi hiyo iliyosikilizwa kwa njia ya mtandao, ilitawaliwa na vurugu, baada ya polisi wa kutuliza ghasia kuwatawanya wafuasi wa Chadema na wengine wakikamatwa.

Msikilize Amani Golugwa: Golugwa adai makada 21 waliteswa

Aprili 25, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), Amani Golugwa alitaja wanachama 21 aliodai kuwa walikamatwa na polisi wakiwa njiani kuelekea Mahakama ya Kisutu na kisha kuteswa kabla ya kutupwa maporini ndani na nje ya Dar es Salaam.

Waliotajwa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Said Mzee anayedaiwa kupigwa mwili mzima, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Ally Juma ambaye naye amedaiwa kupigwa marungu kwenye uti wa mgongo na kuvunjwa mguu wa kulia na mkono wa kushoto.

Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Fedha wa chama hicho, Tito Kitalika anayedaiw akuwa na hali mbaya kutokana na kipigo alichopata na Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto aliyevunjwa mguu na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, John Pambalu ambaye pia anadaiwa kuvunjwa mguu.

Wengine ni Peter Alex, Emmanuel Severine, Bwire G Bwire, Elizabeth Mangosho, Taliflo Mussa Mussa, Emmanuel Modest Mwihawa, Nasra Said (mwandishi wa habari), Ramadhan Kilengo, Pendo Jonas Kileo, Twaha Mwaipaya, Raphael Makalla mzee wa miaka 70, aliyeteguka mguu.

Wengine ni Shaaban Kirita aliyeokotwa kutoka Coco Beach baada ya kuokolewa na wasamaria wema na Erick Zakaria Bulega.

Angalia maelezo: Waeleza walivyoteswa

Muliro akana kukamata makada Chadema

Akizungumza na Jamii Forums leo Aprili 28, Kamanda Muliro amesema waliokamatwa Aprili 24 ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche na Katibu Mkuu, John Mnyika na walirudi wakiwa salama.

“Sisi tuliwakamata Heche na Mnyika, waliulize kama wana majeraha. Hao wengine tuwakamate tuwapeleke wapi? Waulizeni walikamatwa wapi?” amehoji.

Heche aeleza alivyokamatwa: Heche adai kutekwa na polisi

Licha ya picha za video kuonyesha watu mbalimbali wakimakamatwa na kuwekwa kwenye magari ya polisi, Kamanda Muliro amekana.

“Hebu muwahoji hao, kwa hiyo kila aliyepigwa na kujeruhiwa siku hiyo alikamatwa na polisi? Ukienda pale MOI (Muhimbili Orthopedic Institute), kila aliyejeruhiwa alikamatwa na polisi?”

Ametetea sababu ya kuwafukuza wanachama wa Chadema eneo la Mahakama akisema wangesababisha shughuli za mahakama hiyuo zisimame.

Alipoulizwa kama kuna sharia inayowazuia watu kwenda kusikiliza kesi zao mahakamani, amesema:

“Sisi tuliweka mazingira mazuri kwa mahakama kufanya kazi. Kwani hao Chadema peke yao ndio wenye kesi? Pale Kisutu kuna mahakakimu wangapi? Kama Mahakimu wapo 20, kesi moja ya Lissu ndio isimamishe kesi nyingine 19? Hao wanyonge wengine wasisikilize kesi zao?

“Iweje watu kama 3,000 waje pale mahakamani wapige kelele dunia yote ijue?” amehoji.

Kamanda Muliro pia amesema kauli ya viongozi wa Chadema ya kutaka Lissu aachiliwe ndio imewaponza Chadema.

“Walisema tunataka Mahakama imwachilie Lissu la sivyo tutachukua hatua” amedai Muliro.

Ameendelea, “kwa hiyo ulitaka tusubiri hiyo hatua?Ulitaka tusubiri ushahidi? Sisi kazi yetu ni kuzuia uhalifu usifanyike.

“Hili ni jiji la biashara, ukiangalia upande huu kuna vituo vya mafuta, ukiangalia upande huu kuna maduka, ukiangalia upande huu kuna Maktaba ya Taifa. Ni pesa tupu,” amesema.

Alipoulizwa kama polisi wataendelea kuzuia watu kuhudhuria kesi za Lissu, Muliro amesema, “Sisi tunaangalia mtu mwenye nia ya kufanya uovu, tukimbaini tutamkamata. Kazi ya polisi ni kuzuia uovu sio kusubiri utokee.”

Mnyika aeleza alivyokamatwa: Mnyika alivyokamatwa


Kuvunjwa mkutano Kariakoo
View attachment 3318643
Akizungumia tukio la polisi kuzuia mkutano wa hadhara uliotakiwa kufanywa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche Aprili 22, Muliro amesema walivunja baada ya kuona kuna hatari.

Awali Chadema walisema kuwa walishatioa taarifa kwa Jeshi la Polisi siku sita kabla ya kufanya mkutano huo, lakini siku hiyo ndipo polisi waliwajibu na kuvunja mkutano huo, hali iliyosababisha vurugu na kisha Heche kikamatwa na polisi.

“Sawa walitoa taarifa wiki moja kabla, lakini kama kukitokea shida muda mfupi tusizuie? Kuna watu pale wanafanya biashara na wasingependa kufanyiwa mkutano. Kuna watu sio wana Chadema pale unafikiri wote watakubali?” amehoji Muliro.

Alipoulizwa sababu ya kuvutana na Chadema ilihali mikutano mingine ikiwamo ya CCM hufanyikia Kariakoo, Muliro amesema hawana upendeleo kwa chama chochote.

“CCM huwa tukiwashauri huwa wanakubali, hawapigi kelele na ushahidi ninao. Mbona wao tukiwashauri huwa wanakubali tu?

“Mbona Chadema wamefanya mikutano maeneo mbalimbali na tumewapa ulinzi? Wamefanya mikutano Manzese, Buza Mwanagati, Buza Kwa Mama Kibonge, Tegeta, Temeke na maeneo mengine. Wamefanya mikutano na wamewasema polisi, mbona hatukuzia?”
JE MULIRO NI KADA WA CHAMA?
 
Hata Augusto Pinochet alijibu kwa dharau sana kipindi hiko.

Leo kiko wpi?
Hivi unafikiri kwa akili za huyo afande anaweza kuwa anamfahamu hata Pinochet au Pol Pot? Hao ma form four failures wamepewa vyeo vilivyowazidi maarifa. Polisi liachane na hawa wazee wasiojitambua waweke wasomi kwenye hizo nafasi.
 
Nae atalipwa Sawa Sawa na matendo yake ,unachopanda leo ndicho utakachovuna kesho
 
kuna vyombo vingine vya ukamataji sio lazima polisi, inawezekana walikamatwa na askari wa wanyama pori,
Hii hoja unaweza kuithibitishaje in relation to kilichotokea Kisutu mahakamani siku hiyo? Kulikuwa na vyombo vingapi vya ukamataji, wakati Muliro mwenyewe akisema Jeshi la Polisi lilikuwa limeimarisha ulinzi? Mbona yeye hakuvitaja?
 
Kuacha Damu ya mtu ipotee kama vile gogo ni mbaya hata kwa wale waliokaa kimya .

Yaani mtu apige mtu asiye na hatia na kumuua hadharani au hata kwa siri halafu eti jamii ikae kimya na kusamehe eti inamwachia Mungu !! Sio sawa labda kama wenzake wanamtoa kafara ! Na yeye anajitoa kafara kama YESU lakini kama ni kupigania haki basi mapambano hayaishi hapo yanatakiwa ya waguse Wauaji kwa namna ya kuwafanya wajue.

Hivi kwa mfano LimuLilo hata kwa kuliangalia linahofu ya kumwaga damu ya mtu ,au hata kumwogopa Mungu . Kwanza ukiliambia habari ya Mungu linakudharau na kukuona unaliletea masihara . Na unaposema unamwachia Mungu ni lazima uwe na imani ya kimungu kweli sio mchezo mchezo maana ukisema sisi tumesamehe basi ujue Mungu naye anasamehe maana umewaombea msamaha . Unasubiri kuingia peponi .

Watawala Katili walitumia Ukatili kuitawala Dunia na kuwaumiza watu kwa karne nyingi sana huku wakifurahia misamaha ya ukatili wao lakini pia walifanikiwa kufuta matambiko ya haki ya asili kwa kuungana na waliokua wanayapinga ili jamii ibaki gizani na kutawaliwa kama wanyama.

Enzi za Babu zetu katika mila za makabila mengi mtu akikutwa ameuawa ,Ndugu zake wanatangaza hadharani kuwa wanatoa muda kwa aliyemuua ndugu yao ajitokeze hadharani Ili wamhukumu kwa kumpiga faini ya kulipa fidia lakini akisipotoka kwa muda uliotajwa basi watarudi kwenye matambiko .
Tambiko lilifanyika na Yule mtu alikua anazika ndugu zake kila mwaka kwa Tarehe ile ile kila mwaka mpaka ukoo unaisha kabisa na yeye anakua wa mwisho ili apate majuto makubwa . Baada ya hapo watu wanafanya tambiko la kupooza hasira ya mizimu.

Palikua hakuna kucheka na wauaji wasiojulikana ?
Leo hii watu wanaangalia ndugu au rafiki yao au baba yao au mtoto wao anauawa na watu wasiojulikana na sio kwamba ameliwa na Simba au chui au mamba ,wanakaa kimya kama vile kuku amekufa kwa kideri . Hii ni dhambi kuliko ushirikina.

Leo mtu akiibiwa hata Mbuzi wake anahangaika kujua nani ameiba au ameingia kwenye zizi na kuua wanyama wake .
Hata Mkulima au mfugaji hawezi kukaa kimya ngombe wake akauawa au mazao yake Yakaliwa.
Akikaa kimya mazao yake Yakaliwa basi mwakani wataingiza tena mifugo . Lakini mifugo wamekula mahindi ya mtu . Kesho ukatia sumu kwenye shamba wakafa ng'ombe mia . Mwakani hathubutu kuingiza ng'ombe labda awe mgeni .
Aliyesema jino kwa jino ni yeye kwa sababu alijua kuwa kisasi ni Tiba ndiyo maana mahakama zipo kwa ajili ya kulipa visasi badala ya waliokosewa lakini kama mahakama zinasimama kuwalinda waonevu basi kisasi kinarudi mikononi mwa watu katika asili yao iliyoonekana . Asili ipo kwa ajili ya kulinda wanyonge wasionewe na wenye nguvu .

Kila aliyeumizwa au kuuawa atafute haki yake katika asili ili watu waogope kumwaga damu za watu wanyonge wasio na nguvu wala hatia.

Anapigwa kitu kila akisimama mbele za watu anableed damu kama maji hata avae pampus zinatoka kwama mto Rufiji .
Kama ni mwanaume pigwa kitu anakua kichaa na kutoa mboohh hadharani .

Lakini eti tumesamehe tutamwachia Mungu . Mungu atasamehe pia maana mmeridhika . Ndio maana watu waliuzwa kama wanyama na Mungu alikaa kimya kwa sababu waliridhika wakati aliwapa nguvu za kuwaadhibu waovu kwa adhabu kali badala yake wakaungana na Watekaji kwa tamaa ya kupewa rushwa za Kaniki na shanga . Ndugu zao wakachukuliwa kwenda kuwa watumwa .

Tukapoteza nguvu za Mungu za asili na uhuru wetu katika jamii yetu na ardhi yetu.

Leo Bomu lenye pilipili linawaogopesha watu wenye uwezo wa kumfanya mtu avimbe tumbo na kumpiga kifafa akiwa nyumbani kwake kabla hata hajampiga mtu risasi 😆😆😆
Maana ni pilipili tu hakuna sumu .

Watawala wao wanafanyiwa matambiko ya kula aina kuwatisha na kuwakalia watu. Wanachoshindwa kujua ni kwamba matambiko siku zote yanazingatia sana Haki . Yaani kudhulumu mtu huyoboi hata kwa mganga gani !1 Eti Mbunge anashinda kwa dhulma na ameua watu halafu anakwenda Bungeni kabisa kwa raha kabisa kama Musukuma na Mawazo . Yeye anajizatiti kwa waganga halafu waliopoteza ndugu zao wanakwenda kuomba Mungu amsamehe muuaji .Mungu atasamehe maana ameombwa .😆😆😆😆.
Damu inasubiri kulipizwa .
Ilikua ni wote kwa mtaalamu ili mizimu na asili iamua nani mwenye haki .Leo Msukuma angekua anaokota Makopo na kulala makaburini
MKuu Mahakama zetu hazitoi haki tena. tugeukie Mahakama za kimila ili tupate haki
 
MKuu Mahakama zetu hazitoi haki tena. tugeukie Mahakama za kimila ili tupate haki


Kweli kabisa kisasi ni tiba .
Ndio maana mtoto mdogo akipigwa akipigwa kwa kuonewa na mwenzake analia sana .
Lakini alitokea mtu akampga au aka mkaripia vikali yule aliyempiga mwenzake basi yule mtoto ananyamaza na kupata afya kuwa ametendewa haki na wanaendelea kucheza pamoja.
Lakini kila mtoto anapopigwa kwa kuonewa wazazi au watu wazima wanamcheka na kumwambia shauri yako ,ukome basi ipo siku atachukua jiwe na kumbonda yule anayemuonea kwa hasira au hata kumngata kwa meno .
Na pia anakua na chuki isiyoisha na mara nyingi hawezi kucheza naye kwa furaha . Mtoto anayekosoa mtu wa kumtetea anapoonewa anakua na kinyongo na kuishi kwa huzuni. Hata kazi za nyumbani anaona kuzifanya ni kama adhabu.
Mzazi akipendelea mtoto mmoja kwa kila kitu,yaani anamnunulia nguo nzuri mtoto mmoja, anampa pesa mtoto mmoja, anampa urithi mtoto mmoja, anacheza naye na kufurahi na kunywa na kula na mtoto mmoja . Lakini wengine anakua mkali na kuwanyanyasa kwa ukali huku akiwa anawapa masharti magumu hata ya kupata chakula kama vile ukichelewa muda wa kula hatutakuwekea chakula lakini yule mmoja akichelewa anawekewa . Hapo hakuna mzazi anachofanya zaidi ya kujenga chuki kwake na kumjengea yule mtoto chuki kwa ndugu zake na mwisho wanaweza wakauana .

Samia hakupata urais kwa kuchaguliwa na hata pangetokea fursa ya kugombea baada ya Magufuli asingepata kura ndani na nje ya Chama chake . Lakini sio hivyo tu hata kwao Zanzibari hawezi kupata kura kwa sababu hajawahi kuwa na historia na maono ya kuwa mkuu Amiri Jeshi mkuu kwenye nchi kwa sababu tangu utoto wake anafundisha katika dini yake anayoiamini na kuwa tayari kuifia kwamba Mwanamke ni hakupewa ruhusa na Allah kuwa juu ya Watu katika maamuzi.

Hivyo kwa imani aliyonayo Samia hakuwahi kudhani kuwa atakua juu ya Nchi kama amiri jeshi mkuu. Hivyo hakuna ndoto iliyowahi kuingia ndani yake na hivyo hana maono yoyote juu ya Taifa hili . Na kama kuna mtu anamini kuwa Samia atalipekeka mbele Taifa hili anajidanganya sana. Samia analipeleka Taifa hili kwenye Mazingira ya Kongo yaani patakuwa na Matajiri wakubwa sana ambao kwao haki haina umuhimu wowote maana watatumia pesa zao na madaraka yao kushinda jambo lolote mbele ya sheria .
Samia anajenga taifa la kishetani lisilo na habari na wanyonge zaidi ya kuwapa pesa za rushwa na kuwapa vyakula kwenye mikutano na futari na kuwapeleka hija Maka na wengine Israel kama zawadi . Atajenga viwanja vya michezo , misikiti ,makanisa hata nchi nzima maana ndiyo maono ya binadamu wa akili ya chini kabisa ili kufurahisha nafsi yake na watu kupata furaha ya muda huku matatizo yao yakiwa mengi sana . Ndio maana baadhi ya vijana wasomi wanageuka kuwa Machawa bila tija yoyote kwa taifa . Yaani Kijana ana masters ya Kilimo anaishi mbezi beach kama Chawa badala ya kwenda Mvomero kulima na kuanzisha kampuni na kiwanda cha kusindika mazao.

Watu wanasema Samia ndiye Rais aliyechaguliwa na Mungu . Ni sawa .
Kuna wakati Mungu anaacha jambo lifikie anapotaka yeye kutokana na makosa ya binadamu . Tanzania kuna rushwa kila mahali kutokana na kuwa na makabila na hulka tofauti kila mmoja anataka kupelekea watu wake na familia yake . Tanzania umaskini wa kifamilia ni mkubwa sana . Lakini watazania Kwa ujumla wao wanakaa bila kubaguana na wameingiliana sana kijamii.
Sasa kwa hulka ya rushwa na ubinafsi mkubwa jambo ambalo Linamchukiza Mungu . Hivyo Tanzania ni lazima pawe na Rais asiyependa rushwa kabisa na asiyependa kuona wanyonge wanatwishwa mzigo mkubwa wa kodi wakati wa juu wanakula na kipa jalalani .
Samia ni zao la rushwa na kutaka manufaa binafsi sio taifa katika Chaguzi. Samia hakushindanishwa na yeyote katika kumpata tangu 2015 .
Magufuli katika maono makubwa aliyokua nayo alisema wazi kuwa Chaguo lake hakuwa Samia bali Huseni Mwinyi. Wote ni mashahidi Mwinyi ni Rais anayefanya vizuri zaidi.

Samia alipenya ili Tanzania ipate mabadliko ya kimifumo na kuondokana na mifumo ya kiCCM ya kutuletea Viongozi wasio na maono ambao Mungu hawezi kuwatumia kuleta maendeleo ya kudumu . Yaani mifumo itakayowapa watu waliozaliwa na vipaji kujitokeza au kuombwa na jamii Wagombee uongozi kwa uhuru na kushindana kwa haki na kwa hoja atakayegusa shida za wananchi atachaguliwa .

Ndio maana Samia alipoapishwa kwa bahati njema toka kwa Mungu watu viongozi wa dini ya Kikristo walipata furaha kuu na wote walioonewa kwa dhulma na mifumo walifurahi .
Wakristo wana kitu kinaitwa Roho Mtakatifu tofauti na Waislam . Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwajulisha binadamu mambo yatakayokuja mbeleni bila kutumia usomaji wa nyota au unajimu .
Kwa hiyo Wakristo wengi walikua wameshaonyeshwa kuwa Magufuli ataondoka . Hata wanajimu kama Shehe yahaya pia alitabiri hivyo.
Kifo cha JPM kilikua ni ishara ya Kuelekea mwisho wa Mif'umo kandamizi ya CCM pamoja na kwamba alikua ni mzalendo .Kwa hiyo Mama Samia alikua ameanza vizuri sana Kuelekea kwenye Tanzania mpya yenye haki na usawa na uongozi unaopatikana kwa haki maana yeye alipewa nafasi yake kwa haki bila kupindisha katiba iliyomtaka ashike urais baada ya Rais kufa.

Samia kazi yake kuu ilikua ni kubadili mifumo ya dhulma kuwa ya haki kwa sababu haki ndiyo iliyombeba sio dhulma .
Rushwa itamfanya aanguke maana mifumo ya Rushwa inamchukiza Mungu sana .

Upande wa Waislam ni wazi kuwa hawakumtaka Mwanzoni kabisa tofauti na Wakristo . Hao mashekhe wanaoudanganya umma miongoni mwao ndio waliotumwa na kundi fulani kwenda kumshauri ajiuzulu wakati ule hali ya Magufuli ilipokua mbaya ili rais asiwe Mwanamke kinyume na matakwa ya dini. Leo wanamkubali sana kwa sababu ya Rushwa na misaada . Lakini ni wazi bila haki nchi itaporomoka kabisa.

Unafika Tanga kuna magofu ya viwanda vijana hawana ajira halafu unatoa mabilioni ya kujenga Nyumba za ibada badala ya viwanda. Vijana wakiwa na ajira na pesa watajenga nyumba za ibada wenyewe kwa pesa zao .
Matokeo yake vijana na watoto wanashinda kwenye nyumba za ibada na kusubiri misaada toka Oman ,mwishowe wanatumika kwenye ugaidi huko Somalia na Msumbiji.

Jenga viwanda vijana wapate ajira watachanga wenyewe na kujenga nyumba zao za ibada .
 
Ni swala la muda tu.......iko siku yote yatakuwa hadharani
 
Akili, mbinu na vifaa vya kisasa inatakiwa kutumika kukabiliana na hawa watu
wao wana silaha na wananguvu nyingi lakini hata Goliathi alikufa kwa namna Daudi alivyofanya
Hawa kudili nao ni kwa kutumia soft weaponry, wala hamna haja ya kukimbizana nao sana. Revenge zinapigwa kimya kimya tu wanadondoka mmoja baada ya mwengine.
 
WanaCHADEMA waliofariki nao walikuwa madikteta?
Kichwa cha Panzi!!!Tofautisha kati ya Kaini kumuua Habili na Mungu kumwua Kaini! Wana CHADEMA wamefariki kwa kuuawa na Mapolisi/CCM a.k.a Wasiojulikana!!!
Mwendazake kauawa kwa kudra za Mwenye enzi Mungu!
Upo?
 
Hawa kudili nao ni kwa kutumia soft weaponry, wala hamna haja ya kukimbizana nao sana. Revenge zinapigwa kimya kimya tu wanadondoka mmoja baada ya mwengine.
Kifo cha Mwendazake ni mfano hai kabisa. Huwezi ukapingana na Mungu ukabaki salama!
 
Back
Top Bottom