Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa onyo kali kwa kundi la watu wanaodaiwa kufanya vurugu mara baada ya ibada katika maeneo ya Kibo, Ubungo, likisema halitavumilia vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani vinavyofanyika chini ya mwavuli wa dini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Julai 5, 2025, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, kundi hilo linaelezwa kuwa limekuwa likijitokeza kila Jumapili kwa wiki mbili mfululizo mwezi Juni, baada ya ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), na kuanza kupiga kelele na kujaribu kuingia barabarani kwa nguvu kwa lengo la kuchochea vurugu.
“Kuna kundi la watu ambao wamekuwa wakitokea kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM) na mabango baada ya ibada, wakati wenzao wakitawanyika kwa amani kuendelelea na kazi zingine wao huanza kupiga kelele na kutaka kuingia. barabarani kwa nguvu kwa lengo la kufanya vurugu”, imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Jeshi hilo limeweka bayana kuwa halipingi watu kuabudu kwenye maeneo yaliyo rasmi kisheria, lakini pia lina wajibu wa kulinda haki na usalama wa watu wengine kwenye maeneo hayo.
“Jeshi la Polisi linawatahadharisha watu hao na kutoa onyo kali kuwa halitaruhusu kundi hilo kuendelea na mipango ya vurugu na uvunjifu wa amani kama ambavyo wamekuwa wakijaribu kufanya. Wakijaribu tena watajikuta kwenye msuguano mkali wa usimamizi wa sharia”, ameeleza Muliro.
Kamanda wa Polisi amesema kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria katika kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuimarika jijini Dar es Salaam, na kuwahimiza waumini wote kuendelea na ibada zao kwa amani bila kukiuka sheria.