Mulugo: Mwaka Kesho Serikali itashindwa kuwapeleka watoto Sekondari

Wakati wanasema elimu bure hawakuona matokea ya hilo miaka 6 ijayo...
 
Rais yeye hajui hilo. Yeye kichwani kwake anawaza tu kujenga shule za wasichana na Academy za michezo kila mkoa.

..hoja yako ni nzuri sana.

..lakini maandalizi yalitakiwa yaanze miaka 6 iliyopita, tangu mpango wa "elimu bure" ulipoanza.

..lingine linalopaswa kujadiliwa ni VIWANGO VYA UELEWA vya watoto waliosoma ktk program ya " elimu bure. "
 
Amekuwa muwazi kwamba anamiliki shule inaitwa "Southern High land"

Pia issue ya capacity ya miundombinu ya kubeba form one in the comming years ni ndogo sana. Sijui kama itawezekana. Halafu tatitizo litakuwa endelevu hata kwenda A-level pia vyuo.
Wakubali kushusha ada watapata wateja. Kwa ada zao si rahisi PPP kuwa applicable.
 
MULUGO anashule yake mwenyewe maeneo ya kabwe ukiwa unaelekea teofilo kisanji university..nacheka sana
 
Narudia tena kwa usafiri wa kuunga na gundi ni mateso makubwa kwa watoto. Najua ninachozungumza baada ya kuzungumza na Wannafunzi kuhusu walivyokuwa wakiteseka na usafiri na kusababisha mara nyingi kufika majumbani kwao saa tatu usiku au hata zaidi na wengi kusababisha kuchukia shule.
Serikali huwa inakurupuka na kuja na taratibu za hovyo ambazo hazifanyiwi TATHMINI yoyote ili ili kuona kama ina ufanisi au la.
ilishawahi kufanyika miaka ya nyuma ila itabidi wawekeze kwa walimu
 
Hilo jinga halijui lolote utahangaika bure kazi yao kupiga mapambio hata kwenye mambo ya msingi
 
Hivi unajua mpaka sasa hivi kuna wanafunzi hawajaanza form one kwa kukosa madarasa ?
 
Watanzania wanawasikiliza sana viongozi wao wakiambiwa msivae barakoa nakubali,wakiambiwa chanjo za korona ni batili wanakubali,wakiambiwa katiba mpya sio lazima wanakubali,wakiambiwa zaaneni kwa bidii watoto wasasomeshwa wanakubali yaani ni watiifu sana.Kuongoza hii nchi ni rahisi kuliko kuchunga ng'ombe malishoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…