Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Wakuu story ni kwamba huyu jamaa kwenye picha amemuua huyo mkewe usiku wa kuamkia leo huko Mwanza ikidaiwa ni baada ya kumkataza mkewe asiende kwenye show ya Mondi.

Baada ya kumwambia asiende kwenye hiyo show ya Nasib Abdul, mke akakaidi akaenda.

Jamaa amempiga risasi saba za kichwa na inasemekana na yeye kajiua japo maiti yake haijaonekana.

Ila na nyie Wanawake mpunguze visirani. Inaonesha jinsi huyu Marehemu alikuwa mkaidi na hamsikilizi Mme wake.

Mme kakuambia sitaki uende pahala fulani then wewe unakaidi ni nini kama sio dharau na kiburi?

By the way anything else Happen for a reason.

RIP Binti Mzuri


==================================

Baada ya kifo cha Swalha Salum kilichotokea Mei 28, 2022 maeneo ya Busweli Jijini Mwanza, Mama mzazi wa marehemu, Bi Tiba Mohamed anasimulia kilichotokea kuhusu ndoa ya mwanaye na mumewe, Said Oswayo ambapo wahusika hao wamedumu katika ndoa kwa muda wa miezi mitano, kwani walifunga pingu za maisha Desemba 30, 2021.

Anasimulia: “Watoto wangu waliitwa na baba yao hapa nyumbani (Mei 28, 2022), walipofika baba yao akapata dharura hivyo hakuzungumza nao nikabaki nao tukawa tunataniana tu.

“Alikuwa akinitania kwa kufurahi kuwafunga Simba akawa anishawishi na mimi nihamie Yanga (Yanga iliifunga Simba bao 1-0 siku hiyo kwenye CCM Kirumba Mei 28, 2022).

“Baadaye baba yake akapiga simu na kusema mume wa Swalha amepiga simu kumjulisha kuwa amefika na hivyo Swalha aende akampokee Igombe.

“Swalha akasema gari yake haina mafuta, hivyo wakakubaliana wakutane nyumbani na mwanaume akasisitiza kuwa ana njaa sana, akamtaka mke wake aende akampikie.

“Nikawasindikiza hadi barabarani mida ya saa moja usiku, muda huohuo mume wake akapiga simu akiwa anafoka, nikamtaka awe na subira mkewe anakuja yupo njiani.

CHANZO CHA UGOMVI
“Kuhusu ugomvi kati yao labda ni kuhusu simu, Jumatano iliyopita alipata tenda ya kwenda kumpodoa bibi harusi Shinyanga. Alipofika huko wakati akiwa kwenye kazi mume akawa anapigapiga simu, Swalha akawa anamwambia asimpigie kwa kuwa yupo kwenye kazi.

“Ijumaa jioni akawa anamtafuta hivyohivyo na kumsisitiza arudi nyumbani, Ijumaa hiyohiyo jioni akarudi akafika nyumbani usiku, mume akawa anapiga simu, Swalha akapokea na kumwambia anaomba apumzike kwa kuwa amepodoa watu wengi na amesimama muda mrefu hivyo amechoka.

“Mwanaume akawa anaendelea kupiga simu usiku huohuo, Swalha akalala, alikuja kushtuka saa tisa usiku akakuta miss call 42. Akampigia alivyopokea wakaanza kukwaruzana tena, mwanaume akawa analalamika na kumfokea alikuwa wapi na anafanya nini mpaka hapokei simu.

“Swalha alivyoona wanazidi kugombana akaamua kuweka simu pembeni ili ugomvi usiwe mkubwa.

“Asubuhi yake mume wake akanipigia simu na kusema kuwa mke wake amemjibu vibaya. Kwa hiyo ndio akapanga kurudi Mwanza.

“Baba yake alivyomuita hapa nyumbani nadhani alitaka wazungumze kuhusu hilo, lakini ikatokea wamepishana na mume alivyofika nadhani ugomvi utakuwa uliendelea.

KUHUSU KUPIGWA RISASI
“Taarifa ni za kweli, pale ndani (wanapoishi Swalha na mumewe) kulikuwa na watoto watatu wametuambia risasi zilipigwa.

“Wanasema huyo baba alikuwa na kawaida ya kuijaribu silaha yake, mara nyingine anapiga hewani, hivyo walivyosikia mlio wa risasi wakawandelea kulala.

“Ni hadi waliposikia Swalha amepiga kelele mara moja tu lakini risasi zikawa zinaendelea kupigwa. Mtoto mmoja akaenda kusikiliza mlangoni kwa Swalha kisha akatoka mbio kwenda kwa kuwataarifu majirani.

“Wakaenda Polisi, kumbe yule mtoto alivyotoka tu yule baba naye (mume wa Swalha) akaondoka. Polisi walivyofika wakauchukua mwili wa Swalha.

“Taarifa za tukio sisi tulianza kuzipata kutoka Kisiwani huko anapofanyia kazi (mume wa Swalha), ndipo majirani wa Swalha na askari wakaja kutoa taarifa wakisema mwanangu ana hali mbaya ameshambuliwa kwa risasi.

“Baba Swalha akaondoka na ndugu zangu kwenda huko maana nilibaki nyumbani, niliishiwa nguvu baada ya taarifa hizo, nikashindwa kwenda, saa tisa usiku wakarejea na ndipo nikajulishwa kuwa Swalha ameshafariki dunia.

“Marehemu hakuwa na mtoto na sijajua nini kinaendelea mpaka sasa.

“Kuhusu huyo mume wake haijulikani yuko wapi, kwani Polisi mara ya mwisho walisema wameangalia simu yake ikaonekana yupo maeneo ya Tunza.”

JESHI LA POLISI LINAMSAKA MTUHUMIWA
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi ni kuwa ni kweli tukio hilo limetokea kutokana na mgogoro wa ndani wa kifamilia na mtuhumiwa ametoroka, anaendelea kusakwa kwa kuwa alitoroka baada ya tukio.

Kuhusu madai kuwa mtuhumiwa ni mtu wa usalama kama inavyodaiwa na baadhi ya watu amesema sio kweli, ni mvuvi na anamiliki silaha yake kihalali. Jina lake halijatajwa kutokana na sababu maalum.


MUME NAYE AKUTWA AKIWA AMEFARIKI
Said Oswayo anayedaiwa kuhusika na mauaji ya mkewe, Swalha Salum ikidaiwa alimuua kwa kumfyatulia risasi kadhaa amekutwa amefariki na mwili wake kuokotwa kando ya Ziwa Victoria katika Ufukwe wa Rock Jijini Mwanza, leo Mei 30, 2022

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Mairi Makori amesema: "Mwili umekutwa kandokando ya ziwa na umetambuliwa na mmoja wa ndugu zake. Umekutwa na tundu kichwani."

"Inavyoonekana hajafika hapa, aliletwa na maji, inasadikika amejiua kwa risasi lakini uchunguzi unafanyika na tutatoa ripoti kamili."


Ndio shida ya kutokuwa na Mchepuko.angekuwa na michepuko yasingempata hayo majanga .
 
Achana na maneno ya motivation speaker. Hata wa kujinyonga huwa anafika Point of no return
Nenda kamuokote huko si nasikia na yeye kajipiga kageuka mbwa wewe mwanamme unajipiga risasi? stupid, angekuwa mwanammke kweli angesimama mbele za watu ya nini kujipiga risasi mbwa mwitu huyo akaozee huko kama atapata hata wa kumzika. shenzi type.
 
Kuna demu wa kuthaminiwa na kuna demu mwenye tamaa tamaa. Hebu kamthamini Irene Uwoya ili tukuone ulivyo bingwa wa kupiga simu😄 kama mtatoboa hata mwezi mmoja.
Hivi sisi wanaume tumerogwa? hatujui hata mwanamke wa kuowa na mwanamke wa kupita tu? wako wanawake kama unawataka jitahidi uwapitie wanawake sio kila mwanamke wa kuowa na wala sio kila mwanamme wa kuowa ila kama ukiingia kichwa unataka kuowa kama huyo uliyomtaja basi ujuwe utegemee nini usifanye hasira. Jamani fanya makosa yote usifanye kosa kuchagua mke bora huyo sio mke tu atakuwa Mama ya watoto wako. Ndio maana huyo Irene kuna mtu anamchezea tu hakuna harusi hapo.
 
Jamaa kazingua, ingawa hatuwezi kumuona ni mmbaya kwa hilo tukio maana kila mtu ana background yake. Mungu awatie nguvu waliopotelewa na wapendwa wao bwana Swalla na Osway... Mie nakula pepo tu ya hapa duniani na mama yangu Nuzulati .. karibu nyumbani
Shukrani. Mungu awatunze
 
Pisi yamoto mno sema inasemekana mwamba alichukua kipindi ana jiwe la maana wakawa wanaenda sawa mtoto full option yani kila atakacho muhuni anapangua mwamba akaoa kabisa na kazi alimuachisha akawa anaenda nae sawa ila kilichotokea mwamba aliyumba kipesa so akapoteza control.

Kama mjuavyo watoto wakali ni chakula ya team fisi wote wenye visu vikali so kwenye mpunga lazma ang'oke tu. Jamaa yake akaanza kuingiza wivu sasa maana kusikilizwa ikawa hamna demu akitaka kutoka hata ukimpiga ban hasikilizi anaforce tu.

Kilichofata baada ya hasira na uchungu.
Iwe fundisho kwa wanaodhani pesa inanunua penzi
 
Mwanaume Umerudi nyumbani mwanamke hayupo na ulimwambia Una njaa ukirudi ukute Amepikaaa... Unafikaa unapiga simu usiku mzima hapokeiiii missed call 42! Baadae mama ake anasema alikuwa amelala anarudi nyumbani unamuuliza anakujibu Shit.. Nasemaa kama wewe huyo ni mkeoo bhasi labda iwe ndo mara ya kwanza kafanya hivyo ila ukute ndio tabiaa yakee bhasi Hasiraa zake sio za kawaidaa.. Kuna jamaa alijua mke wake anachepuka na akapata Uhakikaa alirudi nyumbani akamshikia bastola nusuu amlipuee ila akaishia kupiga mbwa wakee risasi.. sio jambo dogoo hasa kwa mwanamke uliemjali na kumpa kila kitu
 
Hapana alitaka kuondoka ila baba mtu akamzuia asiondoke kwa vile alishawahi kuachika ila siyo hivyo huyo Saidi alimteka akili baba mkwe wake kwa mapene ndo sababu kubwa baba mtu kulazimisha mtoto wake asiondoke, ila huyo dada na marafiki zake nao wajua ni watu wa kujiachia Sasa sijui huyo Said alitaka kuprove nini kwa kumuoa na kuwa naye muda wote bila kwenda kwa mke mkubwa kama matarajio ya muolewaji.
....Yote hayo yanafanyika katika Miezi Mitano TU ya Ndoa! Kwa Nini Walioana??
 
Hua sipigi simu zaidi ya mara mbili kama hatuna appointment.

Napiga mara moja. Nakaa saa mbili napiga tena.

No response? Naacha text "Hope you are fine. Please call me back"

Unapiga simu 42 times? How?

Ladies if a nigga beats you mteme. Over time that fool will see the beating ain't enough.
 
Wakataeni wanaume msiowapenda na sio kula hela zao mtitarajia watawaacha tu kirahisi baada ya kuwa mmewafanyia ujinga, wewe humependi mwanaume unaingia nae kwenye ndoa ili iweje???
Hapo ndo wanakosea wadada wa mjini ukishaolewa ht km humpendi mwanaume tulia ishi kiafrica zaidi kua mume ndo kiongozi,Kuna maisha ukiwa na mwenza wako unapaswa uyaache haswaa ya kujirusha Tena ukiwa mke ndo kabisaa,shida wadada wa mjini hawataki kubadilika wanaishi kwa kukariri tu ndo maana inawagharimu mnooo..ndoa kiafrica ni utii kwa mume,baasi ukiweza Hilo hutagombana na mmeo
 
Muhimu ni kujitambua,ndoa ni sacrifice haiwezekani uingie ndoani na uishi kama single lazima mtashindwana tu...

Lakini ni muhimu kabla ya ndoa uhakikishe umemaliza bata zote na unaingia ndoani kutulia.
Una focus project za familia nk huwezi kupata muda wa kwenda show za diamond nk
Ndoa inahitaji ukomavu wa pande zote mbili
Uko sahihi Sana,yaani Kuna vitu vingine as wanawake tunajiuiza tunakosa majibu sisi pia!ndoa ni lazima Mmoja awe chini ya mwingine!
 
Back
Top Bottom