Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Wakuu story ni kwamba huyu jamaa kwenye picha amemuua huyo mkewe usiku wa kuamkia leo huko Mwanza ikidaiwa ni baada ya kumkataza mkewe asiende kwenye show ya Mondi.

Baada ya kumwambia asiende kwenye hiyo show ya Nasib Abdul, mke akakaidi akaenda.

Jamaa amempiga risasi saba za kichwa na inasemekana na yeye kajiua japo maiti yake haijaonekana.

Ila na nyie Wanawake mpunguze visirani. Inaonesha jinsi huyu Marehemu alikuwa mkaidi na hamsikilizi Mme wake.

Mme kakuambia sitaki uende pahala fulani then wewe unakaidi ni nini kama sio dharau na kiburi?

By the way anything else Happen for a reason.

RIP Binti Mzuri



==================================

Mama mzazi wa marehemu, Bi Tiba Mohamed anasimulia kilichotokea kuhusu ndoa ya mwanaye na mumewe ambao wamedumu katika ndoa kwa muda wa miezi mitano, kwani walifunga pingu za maisha Desemba 30, 2021.

Anasimulia: “Watoto wangu waliitwa na baba yao hapa nyumbani (Mei 28, 2022), walipofika baba yao akapata dharura hivyo hakuzungumza nao nikabaki nao tukawa tunataniana tu.

“Alikuwa akinitania kwa kufurahi kuwafunga Simba akawa anishawishi na mimi nihamie Yanga (Yanga iliifunga Simba bao 1-0 siku hiyo kwenye CCM Kirumba Mei 28, 2022).

“Baadaye baba yake akapiga simu na kusema mume wa Swalha amepiga simu kumjulisha kuwa amefika na hivyo Swalha aende akampokee Igombe.

“Swalha akasema gari yake haina mafuta, hivyo wakakubaliana wakutane nyumbani na mwanaume akasisitiza kuwa ana njaa sana, akamtaka mke wake aende akampikie.

“Nikawasindikiza hadi barabarani mida ya saa moja usiku, muda huohuo mume wake akapiga simu akiwa anafoka, nikamtaka awe na subira mkewe anakuja yupo njiani.

CHANZO CHA UGOMVI
“Kuhusu ugomvi kati yao labda ni kuhusu simu, Jumatano iliyopita alipata tenda ya kwenda kumpodoa bibi harusi Shinyanga. Alipofika huko wakati akiwa kwenye kazi mume akawa anapigapiga simu, Swalha akawa anamwambia asimpigie kwa kuwa yupo kwenye kazi.

“Ijumaa jioni akawa anamtafuta hivyohivyo na kumsisitiza arudi nyumbani, Ijumaa hiyohiyo jioni akarudi akafika nyumbani usiku, mume akawa anapiga simu, Swalha akapokea na kumwambia anaomba apumzike kwa kuwa amepodoa watu wengi na amesimama muda mrefu hivyo amechoka.

“Mwanaume akawa anaendelea kupiga simu usiku huohuo, Swalha akalala, alikuja kushtuka saa tisa usiku akakuta miss call 42. Akampigia alivyopokea wakaanza kukwaruzana tena, mwanaume akawa analalamika na kumfokea alikuwa wapi na anafanya nini mpaka hapokei simu.

“Swalha alivyoona wanazidi kugombana akaamua kuweka simu pembeni ili ugomvi usiwe mkubwa.

“Asubuhi yake mume wake akanipigia simu na kusema kuwa mke wake amemjibu vibaya. Kwa hiyo ndio akapanga kurudi Mwanza.

“Baba yake alivyomuita hapa nyumbani nadhani alitaka wazungumze kuhusu hilo, lakini ikatokea wamepishana na mume alivyofika nadhani ugomvi utakuwa uliendelea.

KUHUSU KUPIGWA RISASI
“Taarifa ni za kweli, pale ndani (wanapoishi Swalha na mumewe) kulikuwa na watoto watatu wametuambia risasi zilipigwa.

“Wanasema huyo baba alikuwa na kawaida ya kuijaribu silaha yake, mara nyingine anapiga hewani, hivyo walivyosikia mlio wa risasi wakawandelea kulala.

“Ni hadi waliposikia Swalha amepiga kelele mara moja tu lakini risasi zikawa zinaendelea kupigwa. Mtoto mmoja akaenda kusikiliza mlangoni kwa Swalha kisha akatoka mbio kwenda kwa kuwataarifu majirani.

“Wakaenda Polisi, kumbe yule mtoto alivyotoka tu yule baba naye (mume wa Swalha) akaondoka. Polisi walivyofika wakauchukua mwili wa Swalha.

“Taarifa za tukio sisi tulianza kuzipata kutoka Kisiwani huko anapofanyia kazi (mume wa Swalha), ndipo majirani wa Swalha na askari wakaja kutoa taarifa wakisema mwanangu ana hali mbaya ameshambuliwa kwa risasi.

“Baba Swalha akaondoka na ndugu zangu kwenda huko maana nilibaki nyumbani, niliishiwa nguvu baada ya taarifa hizo, nikashindwa kwenda, saa tisa usiku wakarejea na ndipo nikajulishwa kuwa Swalha ameshafariki dunia.

“Marehemu hakuwa na mtoto na sijajua nini kinaendelea mpaka sasa.

“Kuhusu huyo mume wake haijulikani yuko wapi, kwani Polisi mara ya mwisho walisema wameangalia simu yake ikaonekana yupo maeneo ya Tunza.”

JESHI LA POLISI LINAMSAKA MTUHUMIWA
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi ni kuwa ni kweli tukio hilo limetokea kutokana na mgogoro wa ndani wa kifamilia na mtuhumiwa ametoroka, anaendelea kusakwa kwa kuwa alitoroka baada ya tukio.

Kuhusu madai kuwa mtuhumiwa ni mtu wa usalama kama inavyodaiwa na baadhi ya watu amesema sio kweli, ni mvuvi na anamiliki silaha yake kihalali. Jina lake halijatajwa kutokana na sababu maalum.

Ahadi yake ishafika mbeleyake nyuma yetu
 
Sasa we mtu mumeo anapiga simu mara 42 hupokei uko nje ya mji eti unadai umechoka!! yaani kuchukua simu hata basi kuiweka loud au headphone inakuwa shida !!? huyo alikuwa ananyanduliwa
Na wewe mwanaume unajielewa kabisa unapiga simu mara 42 unataka nini.?

Call her once, send an sms ya unachotaka kumwambia then mute..asipojibu mda akija home atatoa maelezo hadi ya ziada.
 
Hili suala wala halieleweki, mara alizima cm, mara calls 42, [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Tabu tupu woiiiiiih
 
Mmmmmhhhhhhh mjadala inaonekana wanaume mnavutia upande wenu....


Hakuna JUSTIFICATION WHATEVER ya kukufanya utoe uhai wa mwenzako...


Mrudishe ulikomtoa mtoto wa watu maana uliupende Uzuri wake hukuangalia TABIA wala majibu yake na ulikubaliana Naye wakati wa uchumba LEO kaingia kwenye NDOA UNALETA WIVU NA KUMWEKEA MIPAKA!!!!! Utakuwa na akili sawasawa????

Ukimkuta binti wa watu anapenda kwenda NIGHT CLUBS na ukamwoa katika mazingira hayo hayo BASI JUA UKIINGIA KWENYE NDOA NA UKATAKA ABADILIKE BASI NI MKATABA MWINGINE NA MNATAKIWA KUKAA MEZANI......


Yaani kuna watu wakati wanatafuta wachumba wanaongozwa na tamaa na hasa kile kitu katikati ya mapaja yao, wakishaoa ndiyo wanaanza kuweka masharti......

Kwakweli kama atanusurika ANYONGWE HADI KUFA na kutuulia mdada mwenzetu...
.kwahyo na sisi mkitukuta tunaupenda tigo then nyie hamtoi,, ni ruhusa kuja na pisi ndani niile mzigo then iondoke c ndio?
 
Diamond fahidi maisha na umaarufu kadri unavyoweza maisha hayana second chance kula bata kaka lahiti ningekuwa na umaarufu hata wa kingwendu tu mngenikoma
Angefanya nini kwa mfano if you were Kingwendu?
 
Hata mke anitukane matusi yote hakuna tusi jipya sio kumuua mtu,sasa unampiga mke risasi kwa vile huna nguvu za kumpiga vibao...ukiona mke hamuwezani achane nae uongeze siku za kuishi
jamaa ni jinga fulani ivi alidhani bastola ni toi
 
Na iyo potential cruelty.sijui of low quality.
Yaani bana ke akikuzidi hadhi yaani nakuambia unaweza ukamsalimia akaenda kuogea dawa kuwa ni mkosi.
Kuna demu alikuwa anasoma udbs akatokewa na jamaa aliyekuwa anasoma Soed aka ualimu. Nakuambia demu alichomjibu ni kuwa hujawaona walinu wenzako wote huko mpaka umekuja kwangu???
Yaani demu aliona Kama amepatwa na mkosi kutongozwa na mwalimu na huku haoni walimu ndio viongozi wa nchi.
Yaani mwalimu inabidi adanganye kozi yake ili amle demu.
Mshkaji wa hgl inabidi aende na kitabu Cha pure maths shule ya mademu.
Mie mwenyewe Kuna demu alikuwa anagonga masters ni ticha kitaluuma Sasa bana si akajua kuwa namie niko postgraduate Sasa alikuja kucheki Kaunta na kozi zimeandikwa code ya second year. Yaani nakuambia demu alitaka akaombewe kwa upako.
Mwanzoni alilegea nikamshika mapaja ,tukaongea maisha anavyosomesha wadogo zake.
Alikuwa na paja laini Ile mbaya Sasa alivyojua nakuambia hata salamu nikawa sipewi.
Yaani mie nimeoa wakati Sina hata mia.
Kuna mwingine nilimdanganya nimedisco second year to third akanipiga chini.
Yaani ke wa kuoa inabidi umuonyeshe magumu ama Tabia ngumu na mbaya uone Kama atakuvumilia ama atakuwa anakushauri Cha kufanya
 
Ww hujapewa sharti lolote huko uliko olewa!
ama unaongea tu bla bla!
Naona hamtaki kuelewa baadhi yenu!!!

Mweleze mtu UHALISIA AJUE RED and GREEN kabla haujaingia NAYE kwenye ndoa!!!! Wanaume wengi huficha standards zao hizo wakati wa UCHUMBA kwa kuhofia kuwa wataachwa!!!! Matokeo yake binti wa watu atajivalia zake vimini kama alivyoamua na kuamini ataendelea hivyo kwenye ndoa!!!

Jamani WANAWAKE NAO WATU NA WANA MITAZAMO YA VILE WANATAKA MAISHA YAO YA MBELENI YAWE!!!!

Kuna mwingine anatamani kuvaa vimini, kwenda clubs, kuhudhuria show za miziki, viti virefu, kusafiri kidogo kupumzika kama ana vijisenti vyake... SASA UTAKUTA MWANAUME ANAJUA KABISA AINA YA MWANAMKE ANAYEMTONGOZA ANA SIFA ZIPI lakini kwa kuwa wanaongozwa vilivyo kati ya mapaja yao na binti wa watu aliyeko mbele yake ana umbo ambalo kila akipita anachanganya wakware BASI MWANAUME HUYU ATAMRIDHIA HIVYO HIVYO ALIVYO...

Akishaingia tu kwenye ndoa na kumbebesha MIMBA BASI MASHARTI KIBAO... mara nguo hizi hapana, group flani za WhatsApp hapana, clubs hapana, yaani masharti KAMA YOTE YAANI..

Utakuta binti wa watu anajihisi KUSUFFOCATE kwenye ndoa, anakosa raha ya kuenjoy maisha na kuwa na stress!!!!

USHAURI WA BURE: TAFUTA UNAYEENDANA NAYE!!!! UKIKUTA KALELEWA NA ANAISHI TOFAUTI NA UNAVYOTAMANI AU FAMILIA UNAYOOTA KUIJENGA BASI either umwambie mkubaliane kabla ya ndoa au utafute mwingine!!!!

Hakuna JUSTIFICATION ya kumdhalilisha, kumuua, au kumfanyia uovu mwingine wowote!!!! MWANAMKE AKIAMUA KULIPIZA UTAJUTA!!!!!!

Ndiyo maana Wengine wanalea watoto si wao, wengine wanatangulia kabla ya wakati wao, na wengine wanatoa uroda hata kwa BODABODA!!!!!

Jifunzeni kuheshimu wenza wenu, wale siyo watumwa wenu jamani.....

HII NI KWA WALE WANAOJIFANYA WAO WAZUNGU HAWANA SHIDA NA WAKIINGIA KWENYE NDOA BASI WANAJIFANYA KUSHUKIWA NA MALAIKA NA KUWEKA MASHARTI KAMA YOTE!!! JINGA KABISA!!!

JENGENI MAHUSIANO YENU KATIKA MISINGI YA UKWELI NA UWAZI NA USIMLAZIMISHE MTU IKIWA HAMUENDANI
 
Hata mke anitukane matusi yote hakuna tusi jipya sio kumuua mtu,sasa unampiga mke risasi kwa vile huna nguvu za kumpiga vibao...ukiona mke hamuwezani achane nae uongeze siku za kuishi
Sio kila mtu ana uwezo wa kuchanganua mambo kama wewe mkuu!

Sio kila mtu anaweza kutawala hisia na hasira zake kama wewe.

Kila kiumbe kina uniqueness yake tofauti na kingine.
 
si umrudishe kwao kama kakushinda?
Ata jamaa kama yupo hai saiz anawaza ivyo ivyo kama unavyosema ww, tatzo binadam ana vtu ving kichwan hasira kinyongo na kujisahau na mengine kuna mambo unayafanya kwa maamuz ya asira yanakugharim baadae ,ndio maana din zote zinafundsha upendo aman na kuchunga ndim zetu yanatakiwa ayo ili kudhibit hasira au kinyongo cha binadam maana kuna muda kaur yako kwa mwanzako au matendo yako yako kwa mwenzako ndio chanzo cha mtu kutumia asira au maamuz ya araka kwann tufke uko ndo maana mung akasema binadam tuheshimiane bila kuangalia cheo umr walaa wala nafas maana hatujui la mbele , sasa kama unatakiwa heshima na ustaarabu kwa kila binadam vp kwa mumeo au mkeo ,yote kwa yote tukubali ndio ubinadam na mapungufu yake
 
Back
Top Bottom