Mume anataka kumuacha mke kisa kumpeleka mtoto shule na ex wake

wadau huyu Dada tumshauri nn?
Mume wangu anataka kuniacha kwa kumpeleka Mtoto shule Mimi na X ambaye tulizaa kabla ya ndoa!

Mimi ni mama wa watoto 3. Mtoto wangu wa kwanza nilizaa na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa kwenye mahusiano lakini alikuja kuoa mwanamke mwingine. Mwanzo mimi na yeye hatukuwa tunaongea kabisa kwani aliniacha vibaya, baadaye nilikutana na huyu mume wangu wa sasa. Katika mahusiano alikuwa ni mwanaume mzuri mpaka nikasahau kama nilishawahi kuumizwa.

Mpaka tunafunga ndoa, nilikuwa sifikirii kabisa kuhusu baba wa mtoto wangu, kwani huyu mume wangu alikuwa ananihudumia mimi na mwanangu kwa kila kitu. Kuna kipindi baba wa mtoto alirudi na kuomba msamaha, akasema anataka kuwa sehemu ya maisha ya mtoto na kulipa ada na mambo mengine.

Nilimkubalia na kwa kuwa ni mtoto wangu sikuona haja ya kuomba ruhusa kutoka kwa mume wangu, hivyo akaanza kulipa ada. Baadaye nililazimika kumwambia mume wangu kuwa ada inalipwa na baba yake mtoto, kwani kuna kipindi walilipa ada mara mbili shuleni.

Mume wangu alilipa ada ya mtoto bila kuniambia, wakati huo baba yake alikuwa tayari ameshalipa. Alikasirika kwa nini sikumwambia, lakini nilimwambia ni mwanangu na yule ni baba yake, hivyo ana haki zote. Tuliongea, yakasahaulika kwani watu waliniambia hata kama yeye si baba wa mtoto, kwa heshima nilitakiwa kumwambia kwani alibeba majukumu wakati baba wa mtoto kanitelekeza. Niliomba msamaha, yakamalizika, tukarudi kwenye hali nzuri.

Mtoto wangu amemaliza darasa la saba mwaka huu, na kuna shule mimi na baba yake tulipanga kumpeleka ili afanye usaili, ambayo ipo mkoani. Nilipoongea na mume wangu kumwambia kuwa tunataka kumpeleka mtoto, aliniambia hapendi hicho kitu, kwamba kama ni kumpeleka, nimpeleke mimi mwenyewe au baba yake ampeleke mwenyewe lakini si kuongozana kwenye gari moja mpaka mkoani, alikataa kabisa.

Nilijaribu kumuelewesha kuwa yule tumeshatengana naye, ni mzazi mwenza wangu tu, lakini hata hakujali. Aliniambia, "kama vipi nitakupeleka mimi, ila siwezi kukuruhusu kupanda gari moja na X wako." Nilimwambia hapana, yule ni baba yake mtoto na ana haki hivyo huwezi kunipangia. Aliniambia, "kama ukienda, ukirudi rudi huko huko." Mimi namjua mume wangu, ni mtu wa kunitishia-tishia kwani anahisi hajiamini, kwa kuwa huyo baba wa mtoto ana pesa zaidi, anaona kama ana hofu. Hivyo nilimwambia hapana.

Tulipanga na baba wa mtoto tukampeleka mtoto huko mkoani, nilimuaga lakini hakunijibu chochote. Nilienda na sikufanya chochote, hata usiku nilimpigia video call ili aone kuwa sipo chumba kimoja na huyo mwanaume, lakini hakupokea. Baada ya interview, nilirudi nyumbani ila kufika niliambiwa kuwa baba ameondoka. Nilimpigia simu kumtafuta, akaniambia "nimekuachia nyumba utakaa na watoto, mimi sidhani kama naweza kuendelea kuwa mume wako tena."

Sikufanya chochote, nilikaa kimya nikijua kuwa hasira zikiisha atarudi, lakini juzi nimepewa wito wa kuitwa Baraza la usuluhishi kwani mume wangu amefungua madai ya talaka. Kaka, sijui nifanye nini. Ndoa yangu bado naipenda, sina mahusiano na baba wa mtoto; nilimpeleka tu mtoto, nashindwa kuelewa kama huyu mwanaume ananipenda kweli au la. Sikulala na X wangu na nimemwambia aongee naye, lakini hataki kabisa. Naomba ushauri wako, kaka, sijui nifanye nini?

HUPANGIWI JIPANGIE MWENYEWE SASA
Mshukuru Sana huyo MUMEO,binafsi Kwanza siwezi kuoa single mother lakini pia siwezi kulea Mtoto wa mwanaume mwingine tena akiwa hai. Zaidi sipendi kubishana na mwanamke kwenye mambo hatarishi. Hilo balaa lake ungekutana nalo siku unatoa Wazo la kusafiri na X- wako yaani ningekuhukumu vikali kwa kuleta Wazo la kipumbavu ... Wewe ni mwanamke mpuuzi
 
Kwa hakika wengi tunazikufuru NEEMA ZA MUUMBA kwa ujinga wetu, umepata mwanaume amekusitiri wewe na mwanao wakati ambao huyo aliekupa mimba amekukimbia na kwenda kuoa mwengine na bado akakubali kukuhudumia na mwao ambaye siyo damu yake wewe unaona ni jambo la kawaida????

Mpaka Ada akakubali kumlipia wewe unadhani ni jambo rahisi???

Sawa amerudi aliyekuzalisha akakukimbia, unaruhusu vipi awe sababu ya kukuharibia ndoa na mtu ambaye alikuhifadhi wakati yeye amekukimbia?

Binafsi naona una shida kichwani au unampenda sana huyu x wako ndiyo maana alivyokuambia mmpeleke mtoto pamoja mkoani na mumeo akakukataza, ukaamua kumtii yeye na kumuasi mumeo!!!

Kwa nini usikubali ushauri wa mumeo ukampeleka wewe au huyo X wake ukang'ang'ania lazima muende wote!!!

Jamani akina dada wenzangu mbona tunakujidhalilisha hivyo!!!! Huyo mumeo ana haki ya kukuacha na kuacha kumhudumia huyo mtoto!! Na hata ikitokea mmesuluhishwa usishangae akakuwekea masharti mapya kuhusu huyo mtoto ikiwemo aende kwa baba yake!!!

Pambana na hali yako, vingine vya kujitakia!! Uwe single mother tena huenda ndiyo nyota yako.......
 
Kiukwel kabisa uyo dada alikosea sio kidogo ila acha alione joto la jiwe kiherehere Cha nyengez kimemponza
 
Mshukuru Sana huyo MUMEO,binafsi Kwanza siwezi kuoa single mother lakini pia siwezi kulea Mtoto wa mwanaume mwingine tena akiwa hai. Zaidi sipendi kubishana na mwanamke kwenye mambo hatarishi. Hilo balaa lake ungekutana nalo siku unatoa Wazo la kusafiri na X- wako yaani ningekuhukumu vikali kwa kuleta Wazo la kipumbavu ... Wewe ni mwanamke mpuuzi
Itaoa tu🤸
 
Back
Top Bottom