Mume anataka kumuacha mke kisa kumpeleka mtoto shule na ex wake

Mshukuru Sana huyo MUMEO,binafsi Kwanza siwezi kuoa single mother lakini pia siwezi kulea Mtoto wa mwanaume mwingine tena akiwa hai. Zaidi sipendi kubishana na mwanamke kwenye mambo hatarishi. Hilo balaa lake ungekutana nalo siku unatoa Wazo la kusafiri na X- wako yaani ningekuhukumu vikali kwa kuleta Wazo la kipumbavu ... Wewe ni mwanamke mpuuzi
 
Kwa hakika wengi tunazikufuru NEEMA ZA MUUMBA kwa ujinga wetu, umepata mwanaume amekusitiri wewe na mwanao wakati ambao huyo aliekupa mimba amekukimbia na kwenda kuoa mwengine na bado akakubali kukuhudumia na mwao ambaye siyo damu yake wewe unaona ni jambo la kawaida????


Mpaka Ada akakubali kumlipia wewe unadhani ni jambo rahisi???

Sawa amerudi aliyekuzalisha akakukimbia, unaruhusu vipi awe sababu ya kukuharibia ndoa na mtu ambaye alikuhifadhi wakati yeye amekukimbia?

Binafsi naona una shida kichwani au unampenda sana huyu x wako ndiyo maana alivyokuambia mmpeleke mtoto pamoja mkoani na mumeo akakukataza, ukaamua kumtii yeye na kumuasi mumeo!!!

Kwa nini usikubali ushauri wa mumeo ukampeleka wewe au huyo X wake ukang'ang'ania lazima muende wote!!!

Jamani akina dada wenzangu mbona tunakujidhalilisha hivyo!!!! Huyo mumeo ana haki ya kukuacha na kuacha kumhudumia huyo mtoto!! Na hata ikitokea mmesuluhishwa usishangae akakuwekea masharti mapya kuhusu huyo mtoto ikiwemo aende kwa baba yake!!!

Pambana na hali yako, vingine vya kujitakia!! Uwe single mother tena huenda ndiyo nyota yako.......
 
Kiukwel kabisa uyo dada alikosea sio kidogo ila acha alione joto la jiwe kiherehere Cha nyengez kimemponza
 
Itaoa tu🤸
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…