Mume kumgeuza rafiki ndio kila kitu kwake

Sio ushauri ni maoni 🤺
 
Na wewe umetoa bonge la ushauri!🤣🤣 "utafute rafiki wa kiume mshauriane kiume zaidi"...hata mambo ya faragha we umshirikishe rafiki, hata ya kiuchumi we mwambie tu kila kitu.

We jamaa bwana!!
Eroni kunywa maziwa. Fresh kwa mangi Sina siji kulipa
 
Duh, ndugu hiki kisa hakipaswi kuwa comment. Hii ilitakiwa iwe katika uzi unaojitegemea. Kuna somo kubwa mno hapa.
 
Huu ni uandishi wa kijana ambaye bado yupo chuo au amemaliza hivi karibuni bado hajaanza kusota na vibahasha,
Kuna mada zingine zinakua kubwa unaachana nazo tu.
Kuna mada kama uwezo wa kuchangia huna bora utulie usome comments utajifunza kitu.
hivi hii ni hali ya kawaida au kuna kurogwa?
 
Jamani nyumba niijenge Mimi halafu niwaachie, labda nisiwe Mimi. Ni mwanaume gani mjinga anaweza kukubali kuishi kwenye nyumba ambayo haikuitolea jasho asee nitaenda niichome moto na wote waliomo.
 
Hawa watu huwa wanapenda watuchagulie marafiki wa kuwa na nao

Ukimuoa tu anahakikisha marafiki zako wote anawaondoa

Nakumbuka kuna rafiki yetu alipooa siku za wkend tulikuwa tukienda kwake mke ananuna au anafagia ili mradi awatimulie vumbi tu,mwisho wa siku ilibid tuache kwenda kwa jamaa
 
Huo urafiki, urafiki gani ? Dunia ya leo hii iliyojaa mapicha-picha. Kuna kinachompa jeuri huyo rafiki, simama imara huihitaji hata kwenda popote isipokuwa "Sala yashinda hofu" na Mungu atashughulika naye. Wala usipoteze muda wako kwa kumfaatilia mume wako au kumchunguza.
 
Kuna mada kama uwezo wa kuchangia huna bora utulie usome comments utajifunza kitu.

hivi hii ni hali ya kawaida au kuna kurogwa?
Siamini sana kwenye uchawi ila naamini kuna watu wamejaaliwa kipaji cha kulaghai watu, ana manipulate mind yako na hisia zaki unakua kama robot anakuendesha atakavyo, wapo watu wa hivyo wake kwa waume, wana maneno mazuri, yenye ushawishi wa hali ya juu na kama amekutarget huchomoki labda na wewe uwe na nguvu dhidi yake.
 
Hawezi kuwa sawa tena. Ila huyo rafiki nae ana moyo. Kisa nyumba akakubali kushare mkewe akijua live anakung'utwa.

Maisha yana mambo mengi mno.
Kha! Hujawahi sikia watu wanatoa wake zao wakaolewe na maboss baada ya muda huyo boss anafilisiwa au anauliwa, wazee wanachukua chao wanahamia kwa mwingine,

Maisha yana mambo si haba
 
Sema watu wengi wanao hamia dar wakapata marafiki uku dar wanabadlika sana sijui ulimbukeni nishawai pata kesi kama yako

Yaani mwanaume anatumia muda mwingi na rafiki kuliko mkewe ambaye akiumwa ndio atamuogesha

Be patient mpotezee acha kumfwatilia fanya mambo yako usionyeshe kukelekwa na tabia zake
 
Jamani nyumba niijenge Mimi halafu niwaachie, labda nisiwe Mimi.ni mwanaume gani mjinga anaweza kukubali kuishi kwenye nyumba amabyo haikuitolea jasho+a see nitaenda niichome moto na wote waliomo.
Inauma ila ukifikiria jela unapiga moyo konde kua hivyo vitu vinatafutwa,
Kosa lake ni kuweka majina ya mwanamke hivyo alikua hana chake na hata ukienda mahakamani inahesabika ulimpa zawadi ukizingatia hamkuoana.
 
Acha ujinga mume huwa hachunguzwi utajiumiza kichwa bure.

Mume huwa haulizwi umetoka wapi,utarudi saa ngapi? au ulikuwa wapi na ilikuwa na nani?

Mume hachaguliwi marafiki!

Mume anahitaji nafasi (space) muache afanye mambo yake as long as anakutimizia mahitaji yako na wanao ( chakula,mavazi,malazi na tendo la ndoa)

Mume hafatiliwi/kuulizwa/kuchunguzwa mipango yake ya utafutaji.!!

Weka hili akilini.

Unachotakiwa kumpatia mumeo ni Heshima, uskivu na utii ,Space (nafasi) na tendo la ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…