Mume kumsaidia mke kazi nyumbani siku ambayo haendi kazini ni wajibu au hiari?

SteveJr99

Senior Member
Joined
May 13, 2019
Posts
137
Reaction score
291
Tunajua wanaume ni viongozi na vichwa katika familia zetu na majukumu ya mwanamume na mwanamke huwa yanafahamika vizuri tu ndani ya nyumba.

Sasa ni kwanini siku ambayo mwanamume akipumzika nyumbani yaani haendi kazini mwanamke analazimisha kwamba umsaidie kazi na usipofanya ananuna hii ikanifanya niulize swali hili

Je, mwanaume kumsaidia mwanamke kazi nyumbani ni wajibu au hiari?
 
Tunajua wanaume ni viongozi na vichwa katika familia zetu na majukumu ya mwanamke na mwanamke huwa yanafahamika vizuri tu ndani ya nyumba.

Sasa ni kwanini siku ambayo mwanamume akipumzika nyumbani yaani haendi kazini mwanamke analazimisha kwamba umsaidie kazi na usipofanya ananuna hii ikanifanya niulize swali hili je mwanaume kumsaidia mwanamke kazi nyumbani ni wajibu au hiari?
Iwe kwa hiari na kwa maamuzi ya mwanaume mwenyewe. Hii habari ya kuona ni lazima nitoe msaada huo haipo..!!
 
Tunajua wanaume ni viongozi na vichwa katika familia zetu na majukumu ya mwanamume na mwanamke huwa yanafahamika vizuri tu ndani ya nyumba.

Sasa ni kwanini siku ambayo mwanamume akipumzika nyumbani yaani haendi kazini mwanamke analazimisha kwamba umsaidie kazi na usipofanya ananuna hii ikanifanya niulize swali hili je mwanaume kumsaidia mwanamke kazi nyumbani ni wajibu au hiari?
Fanya kazi za kiume Tu ,mfano kunavitu ambavyo vimearibika sio mpaka umwite fundi we mwenyew tu unaeza fix,
 
Ni wajibu wako kufanya hivyo na sio hiari,65%ya familia za sasa ni single mothers na ndio wanalea watoto pekee yao,wanaume wengi ni sperms donors
 
Tunajua wanaume ni viongozi na vichwa katika familia zetu na majukumu ya mwanamume na mwanamke huwa yanafahamika vizuri tu ndani ya nyumba.

Sasa ni kwanini siku ambayo mwanamume akipumzika nyumbani yaani haendi kazini mwanamke analazimisha kwamba umsaidie kazi na usipofanya ananuna hii ikanifanya niulize swali hili je mwanaume kumsaidia mwanamke kazi nyumbani ni wajibu au hiari?
Hao vilaza wa aina hiyo huwa mnawatoa wapi na hadi mnawaoa?
 
Wik end baada ya kitoka tizi, unafanya usafi wote room, badae unatoka madogo kwenda sokoni, siku hiyo nasimamia show jikoni natoa sotojo la kibishi / mchemsho au chama choma ya kibabe, ukiwa na madogo jikoni ni mwendo wa vicheko na kufurahi....
 
Tunajua wanaume ni viongozi na vichwa katika familia zetu na majukumu ya mwanamume na mwanamke huwa yanafahamika vizuri tu ndani ya nyumba.

Sasa ni kwanini siku ambayo mwanamume akipumzika nyumbani yaani haendi kazini mwanamke analazimisha kwamba umsaidie kazi na usipofanya ananuna hii ikanifanya niulize swali hili

Je, mwanaume kumsaidia mwanamke kazi nyumbani ni wajibu au hiari?
Kama wewe ndio unafanyiwa hivyo, ebu usitu jumuishe kwenye mambo ya kijinga kabisa...☹️
Na ole wako unijibu, nitakutandika khelbu sasa hivi...😕
 
Nikioa tamsaidia baadhi ya kazi isipokua kutosha vyombo na kufua
 
Kwangu ni hiari na nina tafsiri kama upendo, sio masuala ya kulazimishana.

Kibaya sana mie mvivu mnoo na hivi vikazi vya nyumbani. So nikijisikia nafanya.
 
Kuoa sio kuwa mlemavu kwamba Kila kitu ni kuagiza tu.....lete kile, peleka hiki, toa pale, weka hapo wakati huo umekaa tu tangu asubuhi huna kazi yyt zaidi ya kuikumbatia rimoti. Tufanye kazi

Uvivu haufai
 
Ni Surprise, Huwa haitolewi kila siku au kwa mazoea na haina ratiba tena inatakiwa kua mara chache chache sana kwa kushtuliza ili kuithaminisha.
 
Tusaidiane endapo wote tunafanya kazi
Wote tunarudi tumechoka
Nikiwa naandaa dinner wewe unanisaidia kunyoosha nguo n.k
Sio lazima ila ni upendo tu wote tunachoka
 
Ukijaribu kufanya huo ujinga mwisho wa siku inakuwa mazoea, mwanaume kazi yako kutafuta hela! Sasa umeoa ili iweje kama bado unahangaika na kazi za nyumbani?
 
Back
Top Bottom