Mume na mke wa ndoa kuishi makazi tofauti ila hukutana kwa ajili ya sex

Mume na mke wa ndoa kuishi makazi tofauti ila hukutana kwa ajili ya sex

Kinachokusumbua dogo ni ubinafsi na uchoyo fulstop

Alafu baada ya hayo matendo mtakayokuwa mnafanya mkizaa watoto watakaa na nani?
Sio ubinafusi tu na ujinga pia unachangia anahisi ndoa is all about sex ajawaza kuhusu malezi ya watoto watakuweje kwa huo mfumo wao
 
Kama kichwa cha maada tajwa hapo juu je kwa mustakabali wa ndoa na familia je maisha hayo yanafaa au yana athari kwenye saikolojia na hisia?

Binafsi nimewaza Hilo Jambo nikavutiwa nalo natamani niwe na mke hata kama tunaishi naye tarafa moja ila kila mmoja akae kwake ila kila mkijiskia kukutana kwa ajili ya tendo. Mmoja anamfuata mwenzake na sababu ya mimi kutaka utengano huo wa ratiba za kimaisha, ni kwasababu najihisi nina tabia flani ya ubinafsi nikikaa na mtu nahisi nitamchoka tutakerana yaani means natamani niwe najipikia mwenyewe chakula changu naweza kufanya kazi zangu peke yangu niwe huru kiasi flani tu naishi kama kibachelor ndani mwangu ila upendo kwa mke wangu ubaki palepale

Kama Kuna shida kubwa ndo tunasaidiana ila hizihizi ndogo ndogo kila mtu anapambana kivyake.Mke ninayemuoa akitoka kazini anaenda chumbani kwake anakaa kwa kutulia na Mimi nikitoka mishe mishe naenda kwangu nafanya yangu najipikia zangu mabalance diet, nacheki movies, naperuzi JF sitaki bughudha chumbani kugombana gombana na mtu sitaki makelele.

Ina maana ukienda kumsalimia mwenzako unaenda kwa ajili ya mapenzi tu.Ndo maisha nayoyataka kuishi ila kumpata mtu wa hivyo najua Kuna ugumu Sana maana jamii itastaajabu hio style yenu ya maisha ila je kwa maoni yenu wadau mnaonaje huo mchongo si umekaa vizuri tu.

NB: Mtoa maada nina miaka 26, mfanyabiashara mdogo mdogo na mtumishi mtarajiwa na sijawahi kukaa na mwanamke nikaishi naye geto even for 2 weeks

KikulachoChako
Mshana Jr
The Boss
Sky Eclat
Sisi wengine tunaishi na wake zetu vyumba tofauti,joto likipanda tunapeana location. Aje huku au niende huko.

Wengine chumba kimoja vitanda tofauti.

Ila hakuna kitu kibaya kama kuishi na mkeo mbali hata mtaa mmoja ni hatari sana.
 
Unaweza ukaoa halafu mkaishi nyumba moja na Mkeo lakini kila mmoja wenu akawa na chumba chake cha kulala. Siku ukiwa na hamu ya "tunda" basi unamfuata chumbani kwake na baada ya hapo unarudi chumbani kwako kulala.

Utaratibu huo umekuwa ukitumiwa na watu wa jamii mbalimbali duniani, kwa sababu za "kiimani" au mila na desturi. Kwa jamii hizo huwa ni mwiko kwa Mke kulala kwenye kitanda cha Mume. Hata baadhi ya Wafalme hutumia sana utaratibu huo wakiamini kuwa Mke kulala kwenye kitanda cha Mume huleta "nuksi" na "mikosi".
 
Ndiyo maana ndoa za siku hizi hazidumu na wengi haeataki kuoa

Wajiaje wewe utakuwa mzima siku zote bila kuigua ,utawezaje kuwa na akili salama

Mke kukumbatiana tayari mnachangamana jasho ambalo Lina vitu vingi vya tofauti , kulea watoto mkiwa pamoja ni slogan njema

Fikiria tena

Hapo hakuna ndoa
 
Ndoa ni muunganiko wa watu wawili waliopendana hadi Kuamua kuishi pamoja kihalali kwa taratibu za imani za wahusika.........

Muunganiko huo unajengwa katika msingi mkuu wa UPENDO ambapo ndani ya upendo kuna mambo kama vile......1) Kuvumiliana
2) Kuheshimiana
3) kuthaminiana
4) Kusameheana
Katika muktadha huo wa muunganiko wa UPENDO ni vigumu nafsi kukubaliana kuishi mbali na umpendaye........kufanya mapenzi ni sehemu ndogo ya maisha ya wapendanao kunakohitimisha thamani ya penzi lao......

Kama kitu pekee kinachounganisha PENZI lenu ni ngono maana yake nyie sio wapendanao bali ni watu waliokubaliana kuwa Karibu kwa ajili ya kupunguziana matamanio ya kimwili........

Hivyo basi wanandoa waliounganishwa na maana halisi ya ndoa hawawezi kuishi maisha hayo......
SEEMS LEGIT
 
Hayo mawazo ni kwa ma bachelor ambao wapo katika wakati wao sahihi. Umri ukiongezeka na busara zikaanza kukujia utaona umuhimu wa kuoa na kufurahia ndoa na mkeo.
 
Ndoa ni muunganiko wa watu wawili waliopendana hadi Kuamua kuishi pamoja kihalali kwa taratibu za imani za wahusika.........

Muunganiko huo unajengwa katika msingi mkuu wa UPENDO ambapo ndani ya upendo kuna mambo kama vile......1) Kuvumiliana
2) Kuheshimiana
3) kuthaminiana
4) Kusameheana
Katika muktadha huo wa muunganiko wa UPENDO ni vigumu nafsi kukubaliana kuishi mbali na umpendaye........kufanya mapenzi ni sehemu ndogo ya maisha ya wapendanao kunakohitimisha thamani ya penzi lao......

Kama kitu pekee kinachounganisha PENZI lenu ni ngono maana yake nyie sio wapendanao bali ni watu waliokubaliana kuwa Karibu kwa ajili ya kupunguziana matamanio ya kimwili........

Hivyo basi wanandoa waliounganishwa na maana halisi ya ndoa hawawezi kuishi maisha hayo......
Maneno ya busara na hekima haya.
 
Wewe hauhitaji ndoa, unatakiwa utafute pesa ununue wale midoli wakike wameboreshwa siku hizi. Nafikiri watengenezaji walijua kuna watu kama wewe.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndoa ni muunganiko wa watu wawili waliopendana hadi Kuamua kuishi pamoja kihalali kwa taratibu za imani za wahusika.........

Muunganiko huo unajengwa katika msingi mkuu wa UPENDO ambapo ndani ya upendo kuna mambo kama vile......1) Kuvumiliana
2) Kuheshimiana
3) kuthaminiana
4) Kusameheana
Katika muktadha huo wa muunganiko wa UPENDO ni vigumu nafsi kukubaliana kuishi mbali na umpendaye........kufanya mapenzi ni sehemu ndogo ya maisha ya wapendanao kunakohitimisha thamani ya penzi lao......

Kama kitu pekee kinachounganisha PENZI lenu ni ngono maana yake nyie sio wapendanao bali ni watu waliokubaliana kuwa Karibu kwa ajili ya kupunguziana matamanio ya kimwili........

Hivyo basi wanandoa waliounganishwa na maana halisi ya ndoa hawawezi kuishi maisha hayo......
Sawa baba Padri
 
Back
Top Bottom