Mume wa Maunda Zoro ni mfano wa Wanaume wa hovyo wa Dar es Salaam

Mume wa Maunda Zoro ni mfano wa Wanaume wa hovyo wa Dar es Salaam

MTOCHORO

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2016
Posts
5,107
Reaction score
6,535
Nimesikitishwa sana na Kifo cha Maunda Zoro, vibao vyake ni vya enzi zangu nilivipenda sana. Nakumbuka mchumba wangu wa enzi hizo akiniimbia Nataka niwe wako.

Ila nimesikitika zaidi kwa kuwa alikua akiishi na mtu wa hovyo sana. Ambaye mbali na kukaa nae miaka yote akimzalisha watoto watatu bila kufunga ndoa, pia hakuwahi kumjali.

Ukimsikiliza akihojiwa anasema alipigiwa simu mkewe kapata ajali, akaendelea kukaa Nyumbani huku akiwasiliana na watu. Anasema "MAMA akaniambia usitoke nikampigia RTO akasema ndio wanajaribu kumtoa, nampigia mdogo wangu aendee akafika baada ya kama dakika kumi akaniambia kafika ila bado wanahangaika kumtoa. Hatimaye wamemtoa kafariki."

Mwisho anasema kama angepatiwa huduma ya kwanza mapema angepona kwasababu kama kwa kuchelewa kupata Msaada. Wakati yeye alibaki Nyumbani akichat.
 
In the first place ndio alitakiwa awe wa kwanza kufika eneo la tukio.. Wanawake siku hizi wanabeba mzigo mkubwa rohoni kisa kulinda ndoa.. Wengi wanaishi kwa mateso ya kukosa mapenzi ya kweli lakini hawana jjnsi wanaogopa kuachika
 
Maunda alitoka msibani..

Lakini baadae akapitia sehemu, umeiona ile video ya alivyovaa huko alipopitia.? Kavaa kigauni kifupi kapiga make up huku kakumbatiana na mwanaume anaimba na anaonekana alilewa..

Ukiiona hiyo video utapata majibu mengi sana..

Maana yake alibadilisha nguo alibadilishia wapi.? Alipakia make up wapi.?

Unaniacha nyumbani na watoto unaaga unaenda msibani, unapitia sehemu kulewa ukiwa na mwanaume, unarudi saa 4 ..

Wanaume tunapitia mengi sana..
 
In the first place ndio alitakiwa awe wa kwanza kufika eneo la tukio.. Wanawake siku hizi wanabeba mzigo mkubwa rohoni kisa kulinda ndoa.. Wengi wanaishi kwa mateso ya kukosa mapenzi ya kweli lakini hawana jjnsi wanaogopa kuachika
Exactly my thoughts.
IMG_20220415_110153.jpg
 
Back
Top Bottom