Mume wa mwimbaji Injili adaiwa kumbaka shemejiye

JIGWAMA ujana ule mwenyewe uzee uulete kwenye ndoa ya watu

Gwajima sio mzee Masai, ni kijana tu! Lakini tusipende kuhukumu, kwani hizi ni habari za kwenye media tu, hata mimi na wewe tunaweza tunga!

Ni vema tukaacha yeye aliyemwita amhukumu mwenyewe kama kweli amefanya hayo.
 
The truth will live forever
Go fight for ur right mbasha
 
Watu hawajui kuwa hii topic chanzo ni hapa Jf kwa sababu jana Thread ilifichwa kule Celebrity forum halafu usiku waliifunga Mods nadhani kwa usalama wa mkuu The bold.Jana alikuwa anatishiwa na mpaka sahizi hatujui nini kinaendelea.

The Bold katekwa tayari
 

Nabii yupi huyo mkuu? Kwenye Biblia au kwenye media! JF raha sana
 

Mungu ndio kajibu sasa, baada ya kilio cha muda mrefu, au majibu kwako ni yepi?
 

Kuna nini mpaka hii saga ihame toka kwa mr mbasha ihamie kwa mzee wa hammer, hapa kuna maswali mengi sana ya kujiuliza, na huyu alieanzisha hipropaganda ni nani na kwa maslahi ya nani!

Tupate vithibitisho kuwa huyo mzee wa hammer alikuwa anagegeda hiyo kitu hata msg tu ambazo mbasha anaweza kuwa ameshawahi kuona, vinginevyo huu ni upepo tu, kuruhusu skendo ya king'asti Kamata isahaulike.
 

Uthibitisho uliopo ni mzee wa hammer kumpeleka frola kusoma uk pasipo ridhaa ya mbasha....kuzunguka na flora nchin kwenye mikutano ....kumpangia chumba hotelin frola . ......mkuu huon Pana kitu kinaleta utata hapa??????

Mwisho jiulize yule binti alivyobakwa Mara ya mwisho kwanin alikimbilia kutoa taarifa kwa walinzi wa MZEE wa hammer kwan hana ndugu wa karibu????
Mengine naogopa yasije kunipata kama ya the bold Jana usiku
 

We ni nani mpaka u hide identy yako? Umetumwa na nani? Aisee kama hii issue sio kweli basi wewe fundi sana wa majungu, hutofautiani na kamati ya fitna ya JK 2005
 

Dar es Salaam. Emmanuel Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amejitokeza hadharani na kusema kwamba atakwenda polisi mwenyewe kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17.

Faili la tuhuma dhidi ya Mbasha lilifunguliwa Jumatatu iliyopita katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule) wakati shemejiye huyo (jina tunalihifadhi), alipotaarifu kuwa Mbasha alimbaka mara tatu kwa siku mbili tofauti. Kesi hiyo ilipewa namba TBT/RB/3191/2014 na TBT/IR/1865/2014.

Tangu siku hiyo, polisi imekuwa ikieleza kuwa inamsaka Mbasha bila ya mafanikio lakini mwishoni mwa wiki mtuhumiwa huyo aliongea na gazeti hili na kuelezea upande wake wa tukio hilo na kwamba yuko tayari kujisalimisha ili ukweli ubainike.

“Tuhuma dhidi yangu ni za kutengeneza,” alisema Mbasha na kufafanua kuwa yote hayo yanatokana na mgogoro wa kifamilia baina yake na Flora na familia yake ambao alisema umedumu kwa siku kadhaa.

“Mimi sijabaka na sijawahi kubaka; sijatenda dhambi yoyote; sijafanya kitu chochote na kibaya haya mambo yote ni ya kusingiziwa tu. Mungu wangu ni shahidi. Na kwa kuwa sijafanya hiyo dhambi kama wanavyodai, basi Mungu wangu atanitetea,” alisema Mbasha ambaye anaonekana zaidi kwenye video ya wimbo wa Maisha ya Ndoa alioshirikiana na mkewe Flora.

“Si wamesema wananitafuta, nitakwenda mwenyewe polisi. Nitawasikiliza na nitatoa maelezo yangu. Kama wakinipeleka mahakamani basi ukweli utajulikana... ipo siku kila kitu kitakuwa wazi.”

Kabla ya kufunguliwa kwa faili la tuhuma hizo, msichana huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala (Amana) ambako alifunguliwa faili la matibabu namba 667. Matokeo ya vipimo ambavyo vilifanywa na daktari kung’amua kama binti huyo aliingiliwa vinaonyesha kuwa kulikuwa na mbegu utokaji wa mbegu usio wa kawaida (HVD).

Kadhalika binti huyo alifanyiwa vipimo kuona kama ameambukizwa virusi vya Ukimwi (VVU), pia kupata ujauzito, lakini matokeo ya awali yalionyesha kuwa yupo salama.

Akiwa nje ya kituo cha polisi Jumatatu usiku, binti huyo aliliambia gazeti hili kwamba mara ya kwanza alibakwa mchana Mei 23 na kwamba mtuhumiwa alirudia kitendo hicho Jumapili Mei 25 usiku ndani ya gari katika eneo la Tabata, ambako anadai alifanyiwa kitendo hicho mara mbili.

Hata hivyo, Mbasha alihoji: “Hivi kweli hata kama mimi ni mbakaji, kweli nimbake mtoto wa kumlea mwenyewe mara tatu, yaani Ijumaa halafu nirudie tena Jumapili? Hata kama ni kusingiziwa basi tuhuma hizi zimezidi.”

“Huyu binti nimekaa naye miaka mingi na sijawahi kumfanyia hivyo. Hapo nyumbani kwangu wamekaa mabinti wengi, wakiwamo shemeji zangu wadogo zake na Flora na sikuwahi hata kuwagusa, leo hii kwa nini wananifanyia hivi?”

Mgogoro wa familia

Source, Mwananchi
 

Hivi KKKT siku hizi hakuna sakaka? Zaka? Malimbuko? Changizo? Minada tena hii hatari sana, kama vyote hivyo hakuna basi na mm nakuja huko!! Au hivi vikifanyika kwenye makanisa ya kina Gwajima, Kakobe ndio uwizi peke yake, ila KKKT na RC ni sawa!

Nawaza tu
 
Kwa maneno aliyosema Frola inaonekana kabisa hii issue kama imepikwa

" Mimi nishamsamehe lakini hii kesi iko chini ya familia sio mimi alafu kesi imeshafika polisi na kijinai anajificha nini si aende polisi"

Huyu ndo mke mwema atokaye kwa bwana.

Jamani hata ningekuwa mimi Frola ningeongea hivo! Isitoshe hawana mawasiliano kama ilivoandikwa kwenye Mwananchi.

Mimi namuelewa Frola maana hajamsikia asalu wake wa moyo utetezi wake, anachokisikia ni kama haya tunayosikia wengine! Sasa mnafikiri kwanini asiseme hivyo?
 
Duh!.yamemkuta tena Gwajima. Aliwahi pigwa vibao na jamaa mmoja kwenye saloon moja hivi .kisa Gwajima alimla mwanamke wa huyo jamaa , Kuweni makini na Gwajima ni mchafu sana.

Tupia picha mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…