Natamani ningepata muda wa kutoa ushauri uso kwa uso na hawa wapendwa. Shetani hubambikwa vitu vingi sana - kama hili. Hakuna aliyelogwa au kupagawa - Hawa na Adamu hawajushikiwa kisu na shetani kumuasi MUNGU, walishawishika na kwa hiari zao wakakaidi agizo tskayifu. Flora jiulize haya; Una mchango gani katika mumeo kukukasirikia hadi kutaka kukuua? Amepata wazimu - sitaki kuamini hivi. Ever reaction is a response to an action! Tatizo la unyumba litamalizwa na wanandoa wenyewe, siyo Gwajima au propaganda kwenye vyombo vya habari. Kwa taarifa yako "smear campaign" inaweza kukuchafua mwenyewe. Tulia, jihoji - umechangi kiasi gani kumfanya kumfanya mwenzio atende kosa? Kidole kimoja huonesha mwenzio kakosa, lakini vidole vitatu vinakusonda wewe kuwa umsababishia kukosa mara 3 na kidole kimoja kinaelekea mbinguni kuwa MUNGU ni shahidi. Soma hapa "Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu; ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. (RUM. 15:5, 6 SUV)
Sent from my iPhone using JamiiForums