Mume wa mwimbaji Injili adaiwa kumbaka shemejiye

Dar es Salaam. Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, (jina tunalihifadhi kwa sasa), anatuhumiwa kumbaka shemeji yake mdogo (17).

Taarifa za tukio hilo ziliripotiwa juzi saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule), zikimtuhumu mwanamume huyo kwamba alimbaka binti huyo mara tatu na kumsababishia maumivu makali.

Binti huyo alifika katika kituo hicho cha polisi akiwa na ndugu zake wawili ambao walilalamika kwamba kulikuwa na jitihada kubwa kutoka upande wa mtuhumiwa wa kuzima kesi hiyo.

Akizungumza na gazeti hili nje ya kituo hicho, binti huyo alisema shemejiye alimbaka mara ya kwanza, Ijumaa iliyopita na Jumapili alipombaka mara mbili ndani ya gari.

Alisema mara ya kwanza alikaa kimya baada ya mtuhumiwa kumtishia kwamba angemdhuru kama angetoa taarifa ya tukio hilo alilofanyiwa wakiwa sebuleni nyumbani kwako Tabata Kimanga, lakini aliamua kutoa taarifa kwa ndugu zake baada ya kubakwa mara ya pili.

Polisi katika kituo hicho walithibitisha kupokea taarifa za tukio hilo lakini walishindwa kwenda kumkamata mtuhumiwa kwa maelezo kwamba hawakuwa na askari wa kutosha na kuahidi kwamba angekamatwa jana. Hata hivyo, hadi jana mtuhumiwa huyo alikuwa hajakamatwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi kutwa nzima ya jana hakupatikana kuzungumzia tukio hilo na kila simu yake ilipopigwa (kati ya saa nane mchana na saa mbili usiku), ilipokewa na msaidizi wake akisema bosi wake ana kazi nyingine.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema hakuwa amepokea taarifa yoyote ya aina hiyo.

Mwimbaji anena

Alipoulizwa jana, mwimbaji huyo alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia kwa undani tuhuma zinazomkabili mumewe na kwamba alikuwa anajisikia vibaya kutokana na tukio hilo kuhusisha watu wake wa karibu.

“Of course (bila shaka), hili sio tukio zuri. Kwa sasa sina uwezo wa kuzungumza kwa sababu hili suala lipo Polisi. I am confused (nimechanganyikiwa), ukizingatia kwamba linasemekana kutokea wakati sikuwepo nyumbani, naomba tuzungumze baada ya akili kutulia,” alisema.

Kadhalika, jana saa 6:20 mchana, gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mtuhumiwa ambaye baada ya kupewa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili alisema: “Samahani sana ujue sikusikii kabisa,” kisha alikata simu.

Gazeti hili lilimpigia tena simu lakini ilikatwa na baada ya hapo kila alipopigiwa haikupokewa. Baadaye saa 6:35 mchana, mtu aliyejitambulisha kuwa ni mdogo wa mtuhumiwa alipiga simu chumba cha habari akitaka kuonana na mhariri wa gazeti hili, kwa maelezo kwamba alipewa namba husika na kaka yake.

“Samahani, mimi (anataja ina) niko hapa nje Ofisi za Mwananchi, nilifika hapa kutaka kuonana na mhariri maana nasikia mwandishi wenu alikuwepo polisi tangu jana kwenye tatizo lililompata kaka yangu, sasa wakati nasubiri kuonana na mhariri kaka amenipigia simu akisema namba hii imempigia, kwa hiyo naomba tuonane ili tuzungumze tuone jinsi ya kumsaidia,” alisema.

Baada ya kuonana na mwandishi wa habari wa gazeti hili, alisema suala hilo lilikuwa likijadiliwa katika ngazi ya familia, hivyo wasingependa liandikwe kwenye vyombo vya habari.

Vipimo vya hospitali

Juzi, baada ya tukio hilo kuripotiwa, mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Amana ambako alifunguliwa faili la matibabu na kupewa namba ya usajili 667. Aliingia chumba cha matibabu namba 21 kumuona daktari kwa ajili ya vipimo zaidi.

Matokeo ya vipimo yalionyesha kuwa binti huyo alikuwa amefanya ngono kwa nguvu. Katika fomu hiyo ya uchunguzi, daktari aliandika ‘High vagina swab’.

Baada ya vipimo, familia ilirudi katika Kituo cha Polisi kupeleka matokeo ya vipimo vya daktari, hivyo kufungua faili la kesi lililopewa namba RB TBT/RB/319/2014 na namba TBT/IR/1865/2014. Jana binti huyo alikwenda tena Amana ambako alifanyiwa vipimo vilivyobaki vya VVU na mimba. Vipimo vya awali vya VVU vilionyesha kuwa hakuwa ameathirika na hakupata ujauzito.

Mtoto alipo

Habari ambazo zililifikia gazeti hili jana jioni, zilisema mtoto aliyebakwa alichukuliwa na familia ya Mchungaji Josephat Gwajima.

Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Mchungaji Gwajima bila mafanikio, lakini lilimpata mkewe, Grace ambaye hakuwa tayari kuthibitisha kuwapo au kutokuwapo kwa mtoto huyo nyumbani kwake.

“Naomba nisiwe msemaji katika jambo hilo, yupo msemaji mwenyewe ambaye naamini mnamfahamu naye ni Mchungaji Gwajima, kwa hiyo mtafuteni, yeye atasema kama mtoto yupo hapa au hayupo na kama yupo sababu zake ni zipi,” alisema Grace.

Alipoombwa atoe mawasiliano ya simu ya mchungaji huyo, Grace alisema: “Kwa kweli kama unaweza, kesho nenda pale Kanisani Kawe utapewa utaratibu wa kuonana naye.

Source: Mwananchi
BREAKING NEWS:"WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA SOKOINE-MOROGORO WAGOMA TENA"
 
MMmmmmmh Nosspass!! una uhakika lakini? Ila jamani hii dunia imebadilika sana, hivi huyo anayembaka shemejie haoni aibu? Angekuwa ni mdogo wake wa kike kafanyiwa hivyo angejisikiaje? Ila tusiangalie shilingi upande mmoja, labda shemeji mtu mavazi, mwonekano ulikuwa kimtegomtego, maana hawa mabinti wa sasa hivi ni full majanga. Labda vaa ya shemeji, zungumza na ukaribu na shemeji ulileta matamanio kiasi shemeji akashindwa kuhimili.........(afu ukute kashemeji karembooo kuliko dadamtu ! Walah mi mdogo wangu atakuja kwangu jmosi j2 haya mama kwenuuu!!! Vitoto vya sikuhizi majangaaaa!!
 
Mtoto wa Miaka ''17'' Abakwe si uongo huu !

Hao wamepeana tu
 
Huyo mdogo wake muongo.mi mwenyewe nimepiga sana leo anasema kabakwa?kapenda huyo
 
Munkar punguza wivu, hapaswi kuzidisha wivu ktk mapenzi
 
Dar es Salaam. Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, (jina tunalihifadhi kwa sasa), anatuhumiwa kumbaka shemeji yake mdogo (17).

Taarifa za tukio hilo ziliripotiwa juzi saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule), zikimtuhumu mwanamume huyo kwamba alimbaka binti huyo mara tatu na kumsababishia maumivu makali.

Binti huyo alifika katika kituo hicho cha polisi akiwa na ndugu zake wawili ambao walilalamika kwamba kulikuwa na jitihada kubwa kutoka upande wa mtuhumiwa wa kuzima kesi hiyo.

Akizungumza na gazeti hili nje ya kituo hicho, binti huyo alisema shemejiye alimbaka mara ya kwanza, Ijumaa iliyopita na Jumapili alipombaka mara mbili ndani ya gari.

Alisema mara ya kwanza alikaa kimya baada ya mtuhumiwa kumtishia kwamba angemdhuru kama angetoa taarifa ya tukio hilo alilofanyiwa wakiwa sebuleni nyumbani kwako Tabata Kimanga, lakini aliamua kutoa taarifa kwa ndugu zake baada ya kubakwa mara ya pili.

Polisi katika kituo hicho walithibitisha kupokea taarifa za tukio hilo lakini walishindwa kwenda kumkamata mtuhumiwa kwa maelezo kwamba hawakuwa na askari wa kutosha na kuahidi kwamba angekamatwa jana. Hata hivyo, hadi jana mtuhumiwa huyo alikuwa hajakamatwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi kutwa nzima ya jana hakupatikana kuzungumzia tukio hilo na kila simu yake ilipopigwa (kati ya saa nane mchana na saa mbili usiku), ilipokewa na msaidizi wake akisema bosi wake ana kazi nyingine.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema hakuwa amepokea taarifa yoyote ya aina hiyo.

Mwimbaji anena

Alipoulizwa jana, mwimbaji huyo alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia kwa undani tuhuma zinazomkabili mumewe na kwamba alikuwa anajisikia vibaya kutokana na tukio hilo kuhusisha watu wake wa karibu.

“Of course (bila shaka), hili sio tukio zuri. Kwa sasa sina uwezo wa kuzungumza kwa sababu hili suala lipo Polisi. I am confused (nimechanganyikiwa), ukizingatia kwamba linasemekana kutokea wakati sikuwepo nyumbani, naomba tuzungumze baada ya akili kutulia,” alisema.

Kadhalika, jana saa 6:20 mchana, gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mtuhumiwa ambaye baada ya kupewa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili alisema: “Samahani sana ujue sikusikii kabisa,” kisha alikata simu.

Gazeti hili lilimpigia tena simu lakini ilikatwa na baada ya hapo kila alipopigiwa haikupokewa. Baadaye saa 6:35 mchana, mtu aliyejitambulisha kuwa ni mdogo wa mtuhumiwa alipiga simu chumba cha habari akitaka kuonana na mhariri wa gazeti hili, kwa maelezo kwamba alipewa namba husika na kaka yake.

“Samahani, mimi (anataja ina) niko hapa nje Ofisi za Mwananchi, nilifika hapa kutaka kuonana na mhariri maana nasikia mwandishi wenu alikuwepo polisi tangu jana kwenye tatizo lililompata kaka yangu, sasa wakati nasubiri kuonana na mhariri kaka amenipigia simu akisema namba hii imempigia, kwa hiyo naomba tuonane ili tuzungumze tuone jinsi ya kumsaidia,” alisema.

Baada ya kuonana na mwandishi wa habari wa gazeti hili, alisema suala hilo lilikuwa likijadiliwa katika ngazi ya familia, hivyo wasingependa liandikwe kwenye vyombo vya habari.

Vipimo vya hospitali

Juzi, baada ya tukio hilo kuripotiwa, mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Amana ambako alifunguliwa faili la matibabu na kupewa namba ya usajili 667. Aliingia chumba cha matibabu namba 21 kumuona daktari kwa ajili ya vipimo zaidi.

Matokeo ya vipimo yalionyesha kuwa binti huyo alikuwa amefanya ngono kwa nguvu. Katika fomu hiyo ya uchunguzi, daktari aliandika ‘High vagina swab’.

Baada ya vipimo, familia ilirudi katika Kituo cha Polisi kupeleka matokeo ya vipimo vya daktari, hivyo kufungua faili la kesi lililopewa namba RB TBT/RB/319/2014 na namba TBT/IR/1865/2014. Jana binti huyo alikwenda tena Amana ambako alifanyiwa vipimo vilivyobaki vya VVU na mimba. Vipimo vya awali vya VVU vilionyesha kuwa hakuwa ameathirika na hakupata ujauzito.

Mtoto alipo

Habari ambazo zililifikia gazeti hili jana jioni, zilisema mtoto aliyebakwa alichukuliwa na familia ya Mchungaji Josephat Gwajima.

Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Mchungaji Gwajima bila mafanikio, lakini lilimpata mkewe, Grace ambaye hakuwa tayari kuthibitisha kuwapo au kutokuwapo kwa mtoto huyo nyumbani kwake.

“Naomba nisiwe msemaji katika jambo hilo, yupo msemaji mwenyewe ambaye naamini mnamfahamu naye ni Mchungaji Gwajima, kwa hiyo mtafuteni, yeye atasema kama mtoto yupo hapa au hayupo na kama yupo sababu zake ni zipi,” alisema Grace.

Alipoombwa atoe mawasiliano ya simu ya mchungaji huyo, Grace alisema: “Kwa kweli kama unaweza, kesho nenda pale Kanisani Kawe utapewa utaratibu wa kuonana naye.

Source: Mwananchi

kama jina lipo na mnalo kwa nini mulihifadhi? Vinginevyo mnachochea uhalifu kwa kuogopa kutaja majina. ssipendi hii tabia na huwa siendeleikusoma taarifa kama hizi za kuhifadhiana.
 
kula mama mkwe,kula hauzgel,kula shemeji,jirani,rafiki wa mke wake,sister,vijanafunzi vya primary,sekretari wake khaaa!! Ntajaza seva!!

sasa unafikiri wiki nzima mkeo yupo anapiga tu shoo mikoani wewe upo hamu inakaba na kuna mtoto mbichi yupo tu anamaliza makochi na msosi wako kwann usikatafune
 
Hivi kwa nini watu wanapenda sana kumdhihaki mungu...kila siku majukwaani kuimba nyimbo za wokovu kumbe mioyoni mwao wamejaa uovu na tamaa:A S cry:
 
Vyovyote vile......sawa pengine dogo muongo alitaka mwenyewe......lakini upo uwezekano mkubwa wa tendo kufanyika.......kama tendo limefanyika kuna implication mbili kubwa za kibinadamu.......moja yule ni mdogo wa mke wake.......sisi wanaume tuna tamaa lakini ukifika hapo huna tofauti na mbwa.........pili ni under 18 ..........itazua kesi kubwa zaidi........si vizuri kuhukumu kabla ukweli halisi kufahamika lakini ni somo kwetu akina baba........tamaa zipo lakini lazima ubaki na behaviour za kibinadamu ili uwe tofauti na mbwa anayeweza kumpanda hata mtoto wake..........Pole sana Bi Mbasha....
 
kama jina lipo na mnalo kwa nini mulihifadhi? Vinginevyo mnachochea uhalifu kwa kuogopa kutaja majina. ssipendi hii tabia na huwa siendeleikusoma taarifa kama hizi za kuhifadhiana.

Hawa ni washenzi sana, ndo walewale wa kuku kanya bata kaharisha, wanabagua nani wa kumtaja (wasio na uwezo kifedha wanatajwa, nadhani kutokana na kuwa hawana fedha za kulishtaki gazeti wala kutoa rushwa) na nani wakumhifadhi (wenye uwezo kifedha wanahifadhiwa kwakuwa wanaweza kulifikisha gazeti mbele ya vyombo vya sheria na au wanatoa rushwa ili wasitajwe) hili gazeti limeanza kuchuja siku hizi
 
Naanza kukosa imani na waendeshaji wa hii tovuti. Hili ni jukwaa la siasa, sasa hii habari inahusika hapa kweli na kwanini iachwe badala yakupelekwa sehemu husika.
 
Huu ndio ubaya wa umaarufu. Flora angekua mtu baki mambo yasingefika huku. Vicky angekua kajamba nani asingepata presha na kulazwa. Umaarufu siutaki najilia vyangu tartiiib
 
kula mama mkwe,kula hauzgel,kula shemeji,jirani,rafiki wa mke wake,sister,vijanafunzi vya primary,sekretari wake khaaa!! Ntajaza seva!!

Ya huyu huyu haya au umeyaandika tu??
 
Hivi kwa nini watu wanapenda sana kumdhihaki mungu...kila siku majukwaani kuimba nyimbo za wokovu kumbe mioyoni mwao wamejaa uovu na tamaa:A S cry:
Siku zote nimekuwa siwaamini wanaojidai kuokoka au kujitakasa mbele ya jamii kwamba wao wanamjua Mungu kuliko mwingine, unafki mtupu.
 
Back
Top Bottom