Mume wangu hapendi kula nyumbani

Anza kumpikia vyakula vinavyopikwa bar kama mchemsho, kongoro, supu ya mkia, ulimi, mishkaki, mbuzi choma uone kama atachomoa!



Nimecheka Kwa sauti [emoji23][emoji28]

Jamani imeshakuwa ni mtihani sasa.

Aanze kupajua machinjioni na minadani [emoji14][emoji14]
 
Kuna wanaume wanajua kula vizuri sana usipime [emoji108][emoji108]

Anajua cha nazi , mafuta n.k.

Anajua mchuzi leo haujatiwa ndimu [emoji108]

Anajua tui Leo halikupigwa ,

Anajua tui la nazi Leo halikuchemka na kuiva,

Anajua chukuchuku,

Anajua ugali ulosongwa ukasongeka [emoji108]

Baba yangu yupo hivyo pia.
 
Wanaume wengine wanapenda kula wali wa kupikia mkaa Au kuni ili upaliwe [emoji108]

Umwekee na ukoko ule wa chini na juu pembeni wengine huita mahaba!

Hata binafsi napenda hivyo sana!
 
Au weye ni miongoni mwa wale wanaopika kwa mwendokasi?

Wali kwa Rice cooker?

Nasikia siku hizi hizo rice cooker mnapikia kila kitu ?!

Eti dakika chache chakula kimeeiva [emoji848]
Halafu utarajie utamu halisi kweli?

Bongo sio America wala Ulaya ,

Mambo sio magumu kiivyo bana!

Tupike kiasili chetu, Tuienzi asili bila kujali mabadiliko ya kiteknolojia,

Kuna mambo hayapaswi kubadilika mfano kwenda chooni, kula, kupumua n.k
 
Umesha pandishwa cheo, bi mkubwa kaa kwa password.
Lol [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mtamuua mwenzenu kwa presha🤣🤣🤣🤣msimfanye aanze kupekua simu ya mumewe aambulie kipigo
 
Aisee[emoji23]Bina[emoji23]
Ushauri wako huu utawaingiza watu mkenge.
 
Ukweli ni kwamba Kuna mahali anakula anashiba ...akija kwako anatimiza wajibu tu.
Tufanyeje awe anakula home hyo ni topic nyingine
 
KUNA THREAD ULISHASEMA MUME WAKO ANATUMIA DAWA YA KUPUNGUZA UNENE WEWE BADALA YA KUMSAPOTI UNAMJAZIA MAVYAKULA, JUA TATIZO LA MMEO NA USMAPOTI, YAANI WE NI MBINAFSI HATARI
 
Namuomba mumeo ...niazime japo kwa mwezi mmoja🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…