Mume wangu hapendi kula nyumbani

Mume wangu hapendi kula nyumbani

Habari zenu wapendwa?

Naombeni msaada Mume wangu amekuwa pasua kichwa hapendi kula nyumbani, najua kupika nampikia vyakula vizuri lakini akija anakula tu kidogo anaacha wakati mwingine hali kabisa ukimuliza hana sababu.

Mwanzo nilijua labda napika vibaya lakini siyo maana watu wengine wakila hata wageni wanakifurahia sana chakula mpaka wananisifia najua kupika Ila mme wangu ndo tatizo anaweza akala hata vijiko 5 akasema ameshiba.

Hii hali kwakweli inaniumiza sana akili na uzuri ana mwili nahisi labda atakuwa anakula uko nje akija anakuwa labda ameshiba maana ka jinsi anavyokula hapa ndani alitakiwa awe hana hata afya yani kwa kifupi ni Kama tu hali Ila anagusagusa Kuna wakati hadi nawaza sijui kalogwa.
Samahani dada unazungumzia chakula gani kwanza?
Jee anajua kuhusu wanaokuja kula na kukusifia?
 
Habari zenu wapendwa?

Naombeni msaada Mume wangu amekuwa pasua kichwa hapendi kula nyumbani, najua kupika nampikia vyakula vizuri lakini akija anakula tu kidogo anaacha wakati mwingine hali kabisa ukimuliza hana sababu.

Mwanzo nilijua labda napika vibaya lakini siyo maana watu wengine wakila hata wageni wanakifurahia sana chakula mpaka wananisifia najua kupika Ila mme wangu ndo tatizo anaweza akala hata vijiko 5 akasema ameshiba.

Hii hali kwakweli inaniumiza sana akili na uzuri ana mwili nahisi labda atakuwa anakula uko nje akija anakuwa labda ameshiba maana ka jinsi anavyokula hapa ndani alitakiwa awe hana hata afya yani kwa kifupi ni Kama tu hali Ila anagusagusa Kuna wakati hadi nawaza sijui kalogwa.
Chakula cha mumeo unatoa mpaka kwa wageni?
Huyo atakuwa anagonga nje kwako kimoja tosha kabisa
 
Pika Koronya, Chuzi Shatashata Nazi Saba, Acha Kupwaza Kule Moshi Wanaita Manjiriri! Weka Mboga Saba, Wakati Mwingine Unaweza Kuona Unajua Kumbe Laa

VP Mwanzo Ilikuwaje
 
Wana muda gani?
Kutafuta formula katika ndoa huanza hasa baada ya kupata mtoto kama ni extrovert, ila introvert inaweza kuchukua hata miaka 5 au zaidi. Maana hapo uhalisia wa kila mtu ndipo huanzia
 
Hata mpishi atoke mbinguni kuna vyakula mtu alietoka kunywa pombe hawezi kula

Mi sijui nina nyongo gani, nikitoka kulewa nikiwa na njaa hata dona maharage nakula ila isiwe tu kabeji(Kabichi)

Nyakati fulani na masela wangu tukiwa "uboizini"tulikuwa tunaenda kulewa vijijini, ule ugali tulikuwa tunakinga saa 12 jioni na kuufungia kwenye matranka, hata nikirudi saa 6 usiku nilikuwa nakula tu, na asubuhi naamka fresh,hakuna cha hangover wala nini na paredi nawahi.
 
Back
Top Bottom