Mume wangu hapendi kula nyumbani

Mume wangu hapendi kula nyumbani

Ila sijui ni dada sijui mdogo wangu miss chuga ndoa yako ina tatizo kubwa...hebu kama ni mwombaji mzuri omba san utafunuliwa...kuna jambo zito si dogo mm nina miaka kadhaa si haba kwny ndoa ila sijaexperience changamoto kama unazopitia ww...yani ni za kawaida kuhandle ila ww naona ni nzito acha hili la kula lile la kunyimwa unyumba n.k n.k....
 
Kwani mwanamke kutojua kupika ndiyo licence ya mume kula nje? Ukiona mwanaume anafanya hivi basi ujue ni mshamba fulani. Dunia ya sasa wakati mwingine unakaa na mkeo jikoni mnapika wote. Yale mambo ya mume kutoingia jikoni yamepitwa na wakati.
Hayo ni masiha ya kwenye sinema , a typical african men hawezi kuwa na muda wa kukaa jikoni kupika pika na mkewe, ipo hivo.
Huwezi kupika nitakula wanakojua kupika
 
Habari zenu wapendwa?

Naombeni msaada Mume wangu amekuwa pasua kichwa hapendi kula nyumbani, najua kupika nampikia vyakula vizuri lakini akija anakula tu kidogo anaacha wakati mwingine hali kabisa ukimuliza hana sababu.

Mwanzo nilijua labda napika vibaya lakini siyo maana watu wengine wakila hata wageni wanakifurahia sana chakula mpaka wananisifia najua kupika Ila mme wangu ndo tatizo anaweza akala hata vijiko 5 akasema ameshiba.

Hii hali kwakweli inaniumiza sana akili na uzuri ana mwili nahisi labda atakuwa anakula uko nje akija anakuwa labda ameshiba maana ka jinsi anavyokula hapa ndani alitakiwa awe hana hata afya yani kwa kifupi ni Kama tu hali Ila anagusagusa Kuna wakati hadi nawaza sijui kalogwa.
Wanaume huwa tunapiga Sana supu mtaani

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hayo ni masiha ya kwenye sinema , a typical african men hawezi kuwa na muda wa kukaa jikoni kupika pika na mkewe, ipo hivo.
Huwezi kupika nitakula wanakojua kupika
And who are ''typical african men?''. Ndugu yangu unaishi karne mbili nyuma.
 
Imebidi nipitie nyuzi zake
Sina uhakika kama alifosi ndoa lakini ndoa yake ilikuwa inaonekana itakuwa chungu kabla hata haijafungwa

Nimeisoma itakua kuna tabia mbaya alizionyesha baada ya yy kutolewa mahari labda dharau...thats why mama mkwe akawa hataki tena...na kaka amefosi kuoa naona labda sasa na yy ndo anayaona...itakua huyu bi dada hana heshima ana mdomo mchafu...
 
Shida sio kula je unapika anachokipenda?
Umemaliza agiza Pepsi nitalipia

Mfano mimi binafsi napenga ugali na majani ya maboga ya karanga (mama huwa anajua na nikipita kwake lzm anipikie hivyo)

Kwa mchepuko wangu nikienda huwa ananipikia chipsi [emoji848][emoji848]
 
Anashiba small house.
Ila Dada inaonyesha kama hukua chaguo la huyo mumeo hivi🤔
 
And who are ''typical african men?''. Ndugu yangu unaishi karne mbili nyuma.
A typical africani men ni mimi ambaye nikitoka asubuhi nyumbani ninakuwa nimebeba majukumu matatu by default
1 nitimize mahitaji ya familia yangu
2 nitimize mahitaji ya wazazi wangu na wazazi wa mke wangu kama wapo
3 nisaidie ndugu kwa kile ambacho ninakiweza ,
Kuna mliobahatika !! , kila kitu kipo kwenye pipeline haya ninayokueleza huwezi kuelewa na ndo maana hata muda wa kupikapika na mkeo unapata.
 
Unajua kupika ? Inawezekana unamchemshia mchuzi , ilhali mwenzio keshakutana na madikodiko kwa mama k!
Mf binafsi wife anajua sana kupika na kaniteka kwa hilo , ila kuna siku nilikula chapati Tabata kiwango cha sgr , mara kadhaa nikikumbuka huwa nachochora kwenda huko kwa chai.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Na hataki kuachika
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] maana ana visanga Miss Chuga sijapata kuona
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kuachika sio rahisi jaman.
Tumuombeee.
 
Vile mmeo anachungulia huu uzi kwa mbali hapa JF baada ya kushiba msosi mzuri kutoka kwa nyumba ndogo😁😁😁
downloadfile-6.jpg
 
anaweza akala hata vijiko 5 akasema ameshiba.
Ni chakula gani hicho ambacho mumeo hula kwa kijiko?

Nadhani wewe unajua kupika, lakini hujui ni aina gani ya chakula upike. So unapika chakula ambacho mumeo hali! Lazima ale kidogo ashibe.

Ukweli ni kuwa wanaume wengi tunakula huko mtaani kama nyumbani hakipikwi kitu ambacho tunapenda. Tena ukute mumeo ni mtu wa asili ya kutosema kwa haraka kama kitu hakipendi, yaani hawezi kukwambia moja kwa moja kuwa hapendi kitu flani, anaona atakuudhi kukwambia moja kwa moja. Hivyo wewe ndio tumia maarifa.

Cha kufanya, nenda out na mumeo (wewe ndo umtoe na ikiwezekana mlale huko huko), mwache aagize yeye kwanza chakula, chunguza ataagiza nini! Chunguza pia kama ni breakfast ataagiza nini. Baada ya hapo utajua unapaswa kupika vyakula gani kwa mumeo.
 
Back
Top Bottom