Mume wangu hapendi ndugu zangu

Watu wapole, unaoona wametulia ni noma sana.

Tuombe tu asije akakupiga sapraizi ukabaki mdomo wazi...
Sitoshangaa ndugu yangu. Kikubwa ntamshukuru Mungu kwa yote. Ila sitoishi na guilt kwamba nilimtendea mtu ubaya
 
Kuuwa kunaanzia hapo hapo
Mungu awaepushe na balaa ila huyo ni zaidi ya mchawi
 
Watu wapole, unaoona wametulia ni noma sana.

Tuombe tu asije akakupiga sapraizi ukabaki mdomo wazi...
Sitoshangaa ndugu yangu. Kikubwa ntamshukuru Mungu kwa yote. Ila sitoishi na guilt kwamba nilimtendea mtu ubaya
 
Watu humu ndani mna ubinafsi, mnasema amfukuze mdogo wake, we wako ungefukuza? Siku akipata shida na mume akimkimbia ndugu hawatomsaidia hata kidogo mimi nna uzoefu na hilo tukio nna binamu yangu hadi leo anagalagala kwa marafiki. Mume alimwambia sitaki kuona ndugu zako hapa na yeye akatii ndoa, mume kamzalia nje na kahamia kwa hawara, wanae hawana hata ada na ndugu wote wanamuangalia tu. Na uwezo wa kumsaidia wanao.

Huyu mtoa mada namuelewa sana tu ila nyie mnaosema afanye maamuzi ndo mnafeli
 
Moyo wa mtu ni kichaka.
Usiamini unamjua.

Hawezi akaanza tu kumchukia mdogo wako bila sababu zilizojificha ndani ya uvungu wa moyo wake.
 
Kwa binadamu wa kawaida ni ngumu labda akufanyie unafki. Atawapenda ukiwepo lakini moyoni ataumia
 
Nikuulize kitu, mfano mkeo akijifungua utaweza kumhudumia uzazi peke yako? Bila msaada wa ndugu zake?
 
Dada yako amefanyaje sasa. Mi ndo nachotaka kujua.
 
Kumbe mna tabia ya kujazana kwa ndugu
 
Nashukuru sana. Mtoto akija anafanya vishughuli vidogo vya nyumbani then anaingia kulala. Kukaa sebleni ni hadi mimi ni lazimishe
 
Kumbe mna tabia ya kujazana kwa ndugu
Kujazana wapi? Mdogo mmoja ndo amejazana? Hivi nyie wenzangu mnaishi Afrika au marekani? Hivi afrika hapa utakaa nyumbani peke yako. Ukizaa mtoto unamuacha na nani na hawa mahousegirl wanaotoroka kutwa. Mume anashinda ofisini, unarudi nyumbani unakuta housegirl ametoroka kaacha mtoto ndani kafunga na mlango. Hivi situation kama hiyo napo utamwita nani aje kwako akusaidie? Mume atakubali mlee mtoto pamoja?

Ushauri nnaoomba ni maneno ya kumwambia huyu mtoto arudi kwao ili mume awe na amani anayotaka
 
Huu mjadala unathibitisha wanaosema wanawake huwa hawaongei kutafuta solution wanaogea kutoa nyongo tu basi (though mimi nakuwa outlier kwenye hili swala), mtu unapewa solution unatumia muda kuelezea nadharia, mara nampenda, ananipenda, sijui sisi waafrika, hukutaka solution ulitaka tu kuelezea hisia zako otherwise majibu yako yangejikita zaidi kwenye nini ufanye na ufanyeje, practical solutions, wewe umejikita zaidi kwenye hisia zako juu ya tatizo zima na mumeo na mdogo wako.

Samahani me sina suluhisho nilikuwa nasoma tu comments.

Pia I can't relate to your problem maana mimi nyumba yangu ni kama kituo cha mabasi yaendayo kasi ile sas 12 jioni, tukipika mchana utadhani msiba kumbe hata mgeni hamna siku hiyo, sitting room utafikiri kibanda cha kuonyeshea mechi, na vyumbani ndo usiseme utafikiri kambi ya wakimbizi hadi tumeamua kuongeza kitanda kingine chumbani kwetu mashemeji wapate pa kulala, juzi nikasikia wanatuteta eti hii mimba ya nane wameipataje mbona kila siku tunalala wote?
 
Asante🤝
 
daah, pole sana

hapo imebaki hatua mbaya zaidi, endeleeni kuomba na ikiwezekana mdogo ako ahame hapo alipo

allivyoweka chumvi huoni ni Mungu tu angeweza kuweka sumu? maisha haya jamaniiiii
 
pole kwa kituo cha mabasi. Mimi anaishi mtu mmoja tu anaeshinda jioni tu akitoka chuo, weekend anashinda nyumbani kwa wazazi. Mda mwengine hata usiku hali chakula nyumbani anakula anapotoka.
 
Na
ndo ushauri nliokua naomba kwamba mtoto namwambiaje sasa nenda nyumbani hapa basi. Naona watu wananihukumu. Hakuna anasema mwambie dogo sasa ondoka yani hilo neno la busara ndo nnalolitafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…