Mume wangu hapendi ndugu zangu

daah, pole sana

hapo imebaki hatua mbaya zaidi, endeleeni kuomba na ikiwezekana mdogo ako ahame hapo alipo

allivyoweka chumvi huoni ni Mungu tu angeweza kuweka sumu? maisha haya jamaniiiii
Ahsante sana .
Yani dada angu ana mtihani Sana.
Mdogo wetu kuondoka hawezi maana anamsaidia Dada kwenye uzazi maana kipindi Cha mwisho Cha ujauzito alikua na changamoto.
 
Ubaya wa watu wazuri kama wewe dada huwa wanaweza kumuamini mtu kwa asilimia zote kirahisi maana wanahisi kila mtu ana moyo mzuri kama wao

Dunia hii kila mtu ana dark side ambayo wewe huijui, KAMWE usiusesemee moyo wa mtu, iwe mdogo au mume wako

Uaminifu uliokithiri huzaa uadui na chuki iliyokithiri. Kuwa makini isikukute
 
Namrudishaje nyumbani mtoto sasa nawaambiaje? Wakati mimi ndo nilishadadia aje akae huku karibu na chuo. Leo nasema arudi kwasababu gani.
Kama ni mwanafunzi wa chuo, mtafutie chumba ajitegemee mtaani, hapo kwako anaweza kuja weekends.
 
Hiyo tabia ni ya muda mrefu ni vile watu huficha makucha kipindi Cha mahusiano na kujidhihirisha ndani ya ndoa. Hata mwanamke mbinafsi huonekana mapema pia all in all hii tabia sio kabisa Mimi najuaga wanaume watu wenye mioyo safi wasio na hekaheka kama hizi kulinganisha na wanawake
 
Story ya upande mmoja hii, hatujajua mapungufu ya mleta mada na mdogo wake. Nnavyowajua wanawake (hasa hawa waliolelewa na mzazi mmoja) huwa wana matatizo sana kwenye mahusiano so tutunze maneno yetu.
 
Na

ndo ushauri nliokua naomba kwamba mtoto namwambiaje sasa nenda nyumbani hapa basi. Naona watu wananihukumu. Hakuna anasema mwambie dogo sasa ondoka yani hilo neno la busara ndo nnalolitafuta.
Siku hizi sipendi kutoa ushauri lakini ngoja nijaribu.

Mwambie mdogo wako una tatizo la uzazi so unaomba arudi nyumbani kwa muda mbaki wenyewe , kuna kitu mlishauriwa. Hopefully anakuheshimu kama mkubwa wake so hatouliza maswali mengi. Kama mna utani sana iweke kirafiki I such a way asijifikirie yeye akufikirie wewe na tatizo lako
 
Ahsante sana .
Yani dada angu ana mtihani Sana.
Mdogo wetu kuondoka hawezi maana anamsaidia Dada kwenye uzazi maana kipindi Cha mwisho Cha ujauzito alikua na changamoto.
Mungu atamvusha, maombi yenu kwake Mwenyezi Mungu atayasikia
bora ameondoka

hivi jamani kwa nini watu tunakuwa wabinafsi kama tunajua sekunde ijayo ya maisha yetu? Mungu atuongoze
 
Mungu aniepushie hili🙏
 
Nani kakwambia nimelelewa na single mom? Mama angu kavumilia hadi leo anavumilia vituko vya mmewe eh ya huko sitaki kuyaingilia hayanihusu. Yangu yenyewe napambana nayo. Mapungufu yangu ndo yakamfanye mtu amchukie mtu mwengine? How
Story ya upande mmoja hii, hatujajua mapungufu ya mleta mada na mdogo wake. Nnavyowajua wanawake (hasa hawa waliolelewa na mzazi mmoja) huwa wana matatizo sana kwenye mahusiano so tutunze maneno yetu.
 
Anajua sina tatizo la uzazi ila asante kwa ushauri. Ni wazo zuri sana naanza kupata mwanga wa design ya vitu vya kushauri
 
Hakuna wetu wenye lawama kama ndugu!! Ndugu hutumika kuvunja ndoa ! Kwani wakati unamleta ndugu yako ulimshirikisha mumeo? Kama uliamua mwenyewe kumleta bila kumshirikisha mume wako hapo Kuna shida! Kwa maelezo yako unapenda sana kuleta ndugu nyumbani kwako ukishaolewa unahitaji nafasi ya kuishi na kujitawala namume. Ndugu wakishajaa kwenye nyumba Kuna freedom kubwa hupotea kwa wanandoa mfano itakuwa ngumu kumhag mume akiwa anatoka kazini wakati ndugu wamejazana sebuleni hata mapenzi mtaanza kuvizia usiku tu wakati ndugu wamelala nk
Kuna watu by nature hawapendi wageni pengine mume wako yupo katika hilo group kumbadili itakuwa ngumu itabidi umvumilie tu maana hakuna namna ! Nimeandika mengi lakini ndugu Wana changamoto sana sio wa upande wa mke Wala wa mume! Mke anaweza kuwa anatumia muda mwingi na ndugu zake kuongea mambo tu ya kwao akasahau kabisa kuwa kaolewa
 
 
Umeolewa ww au mdogo wako?.

Peleka dogo nyumbani huyo acheni maswala ya kiswahili, ww usingeolewa angeishi wapi?.

Kiukweli hili swala la ndugu kujazana kwa wana ndoa ni kero kubwa na ndio sababu mojawapo ya ndoa nying kuyumba na mwishowe kuvunjika.
 
Kumbe ulizoandika ni sifa njema?
Sasa unataka ushauriwe nini?.

Kaa pembeni uvue huo ujuaji then urudi jukwaani upokee ushauri labda utaelewa.

Mmeo atakuwa yuko sahihi lakini nina hisi kuna kitu hakiko sawa kwako.
Sio lazima unjibu...naishia hapa
Na kweli nimjuaji ,na ana maneno mengi hashauriki,walomshauri ampangie ndugu yake wametisha sana,hiyo ndo solution.. anaonekana anapenda misifa anataka mamaake amuone *HERO*kwamba anamsaidia majukumu huku kwny reality analeta mvurugano na mmewe anaependa privacy,ndoa bado changa "km alivyo sema mtoa post"mme anataka privacy a-enjoy na mkewe , awe huru na mji wake ,sema mkewe ndo much know wa viwango
 
Na wala sijawahi kuwa na mawazo labda anamtaka, ndiyo maana anafanya hivi visirani vyote. Mazingira niliyomlea mdogo wangu namjua na ana tabia njema sana.
ring... ring... ring... kengele hiyo inatakiwa ikuamshe kimawazo.

Rudisha huyo mdogo wako nyumbani haraka sana, inawezekana japo hakuambii kiukamilifu lakini kuna kitu kimejificha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…