Mume wangu hapendi ndugu zangu

[emoji23][emoji23][emoji23]...Aisee mwamba anaulizia hadi vi shuka anavotumia mdogo ako?Asee hii ni Abnormality yani dume zima kabisa na midevu linahangaikia na vitu vidogo vya kijinga namna hii?
 
Watu wa jamiiforum msiwe wepesi kuhukumu. Mbona nimesema kabisa sina uwezo wa kumpangia. Sasa mnaposema nataka kuwa hero kwa mzazi wangu, hivi mzazi hakai dar, amekuachia mtoto umlee kwasababu akiwa mwenyewe mzazi anaamini hana usimamizi. Na mimi sina uwezo wa kumpangia na mzazi atauliza unampangia si umrudishe nyumbani. Nnachotaka ni sababu ya kumtoa hapa nyumbani. Huo ndo ushauri nnaotaka na sio mnanihukumu. Yani nnachoelezea ni hiyo wananiambia mtoe dogo mpangie sina ela hiyo na kumtoa ni kumpeleka home, nahitaji tu maneno ya busara ya kumwambia. Sasa mnakaza kunihukumu hamna kingine. Wenye busara maneno wanaweza kunipa ndo nayasubiri.

So far asante kwa hukumu ila ungejua maisha au sapoti ambayo mama yangu anahitaji sio kipesa ila ile ya kuona ana msaada tu wa kumuangalizia watoto huku dar ndo ungeelewa . Ila siwalaumu mna haki ya kunihukumu kwasababu hamjui mengine
 
Simple tu, umeolewa na mtu asiyekupenda na mwenye roho ya kimasikini
Very simple ukweli mchungu mtu anaekupenda hawezi kuchukia ndugu zako hata kidogo dada hapo cha kufanya mpeleke mdogo wako hostel basi kuepusha kero zisizo na kichwa wala miguu...mimi pia naishi na mdogo wangu na mume wangu anamchukulia kama mdogo wake
 
"naomba nikute siti ya kukaa" ,,[emoji1787][emoji1787][emoji1787] huyo kaka yetu ana roho mbaya.
 
Nnavotamani hizi comment niwe natoa mimi🙌🏼 ila watu wanakazana kunihukumu. Nyie kufukuza ndugu ni jambo rahisi hivi?
 
Watu kama hawa katika familia wapo sana, wanapenda sifa na kuonekana wema bila kujali anaumiza upande wa mume.
Mimi binafsi napenda privacy sana.
Kwangu hawezi kukaa ndugu yangu wala upande wa pili.
Nitasaidia wakiwa mbali.
Kama kuja kwetu wasalimie na kukaa siku kadhaa wasepe.
Kukaa na ndg ni mzigo, watakufanya uishi maisha wayatakayo wao, watataka special treatment na mimi huo ujinga sinaga kabisa.
Nikiwa kwangu mimi ndiye mfalme sitakagi mbambamba za ndg.

Kwa misimamo yangu nitawaudhi kwani sitaki kuuishi uongo uongo
 
Kwa maelezo haya huyu mwanaume ni mbinafsi na hapendi watu wa upande wako, anapenda ndugu zake tu. Kwa kuwa umesema ana upendo kwako, jipange kuzungumza naye kwa Upendo kabisa. Tafuta sehemu nyingine tofauti na nyumbani, muulize nini shida. Wengine Wana mitazamo mibaya juu ya ndugu wa mke wake.
Ikishindikana tafuta utaratibu mwingine wa kumsaidia mdogo wako, usipoteze ndoa kwa sababu ya Hilo. Maana sio lazima kuishi na ndugu zako humo, wadogo Wana kwao.
 
Tabia nikama ngozi haiwezi kubadilika ila pia inawezekana labda mumeo ni mbinafsi ndo maana hapendi ndugu zako hivyo ili asije akaleta madhara kwa ndugu zako jaribu kuwa makini nae ikiwezekana huyo mdogo wako mrudishe tu nyumbani ili kuepusha matatizo
 
Hayajakukuta, au kwenu uko peke yako, subiri siku uumwe af mkeo awe mbali af ita ndugu uliowakataza kuja kwako uone kama utapata msaada. Sio kazi ya kuhukumu. Usijione kama huna shida ya watu. Ipo siku utawahitaji na hutowaona. Mungu atusaidie sote🤝
 
Sikiliza dada.
Jambo la msingi ni kudumisha upendo lkn sio kuishi pamoja.
Hivyo watakuja wanakaa siku kadhaa na kuondoka.
Lkn huwezi kuweka ndg standby kusubiria uumwe akusaidie.

Au mngekuwa yatima ni haki kumkaa na mdogo wako hadi ufike muda wa kujitegemea
 
Ni kweli huyo jamaa anaoneka hapeni kuishi na watu zaidi ya mke na watoto au mfanyakazi jamaa atakuwa ana tabia za kizungu kupenda uhuru bila buguza ndani ya nyumba, Huyo dada itabidi alete mfanyakazi wa ndani ili aone huyo mfanyakazi atachukuwa na mumewe.
 
Mkuu huyu mwanaume ni mbinafsi yeye kama yeye siyo tu kwa upande wa ndugu wa mke ata kwa upande wa ndugu zake, ndiyo maana ndugu zake wanaenda kwake kwa kupita na kuondoka na siyo kwa kuishi inamaana ndugu zake wanamjua ndugu yao ni mtu wa kupenda kuishi maisha ya peke yake bila mapishano kwenye nyumba.
 
ondoa mdogo wako Mambo anayosema kwenu kuhusu MUMEO yahovyo Sana kibaya mdogo wako hajui anaowambia hayo maneno wanamrudishia MUMEO Kama yalivyo. hauishi morogoro wewe na baba ako kipindi ulimwambia aje bila kumtaarifu mumeo
 
Mumeo kakuoa wewe sio mdogo wako acha kumpa mwamba mzigo usiomhusu mrudishe Mdogo wako nyumbani kwao.
 

 
Sasa yatima unakaa nae wakati mume hamtaki?
Si ndo yale yale.

Mume kama hataki ndugu ni hataki tu. Kikubwa tupo Afrika. Kama mtu umeamua kufukuza ndugu fukuza tu. Ila siku ukiwahitaji naongea kwa experience hutowaona.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…