Mume wangu hapendi ndugu zangu

Nimesitikitika.
Isije kuwa mumeo alimkuta mdogo wako ktk mazingira tatanishi na mwanaume au ashamsikia anaongea na simu na mwanaume so jamaa anaona yeye analea halafu kuna fala anakula kama kaoa.

Pia, inawezekana jamaa tu hataki anataka kulea watoto wake kwa amani.

Au anafantasi flan hivi akiwa home ajiachie na kiboksa tu sa ahapo huyo dogo anambana.

Yote kwa yote fanya hivi uwe unafanya maombi kila siku usiku kuhusu hilo suala atabadilika. Au anaweza kusikiankuwa umelfanya ktkaombi so anaweza kubadilika au kuongea shida iko wapi
 
Asante kwa ushauri wa maombi. 🙏
 
Asante sana🤝🙌🙏
 
Inaonekana wewe ulitaka dogo aje kuishi hapo kwenu bila kujadili na mumeo na kujiridhisha kuwa ameridhia. Wanawake mnamajaribu sana muda mwingine na kutaka watu waonekane wanaroho mbaya.


Kuna rafiki yangu anapitia hii changamoto. Yaani mkewe anaweza ongea na mama yake jambo wakapanga sijui kuna ndugu anakuja mkoani kuja kufanya labda interview au kuja kwa swala lolote lile bila ya kumshirikisha mwanaume wake. Halafu anakuja mwambia mgeni yupo njiani anakuja na basi ameshakaribia kuwa kuna mtu anakuja.


Jamaa ameshamkanya mara kadhaa na kumuelekeza kuwa maisha hayaendi hivyo mwanamke haelewi.

Kuna siku kulikuwa na harusi ya upande wa mwanamke kuna wageni wakaja mjini mwanamke anakuja mshirikisha mwanaume wageni wapo sebuleni, sasa unamshirikisha nini hapo na maamuzi tayari keshafanya.

Jamaa akatazama ile tupsi akaona haina shida. Kimya kimya akabeba nguo zake chache akaenda zake kulala guest akawa anaamkia huko kwenda kwenye shughuli zake na kurudia huko. Mwanamke akashtuka jamaa harudi home.

Kumpigia simu jamaa akamwambia unajiskiaje mimi kufanya maamuzi bila kukwambia lolote?!

Basi nimekupisha ukae na wageni mimi naona hatusikilizani na unafanya mambo bila kunishirikisha. Nitatafuta sehemu yangu nyingine ya kuishi nitakaa huko, wewe kama utataka kuonana na mimi utakuja na kunitembelea ila huko mimi siji tena. Nimekupisha ukae na kwa uhuru ukaribishe unayejiskia bila kuhangaika kunambia. Mwanamke akaomba msamaha na kutaka yaishe. Jamaa akakaa siku kadhaa mwanamke akalalamika balaa kwa familia ya jamaa.

Kukakaliwa kikao jamaa akafunguka yote. Tokea siku ile mwanamke akaacha hayo mambo.
 
Umeongea vyema sana kaka angu. Ntatafuta tena neno lenye busara nimwambie kwamba huyu ni mtoto. Amlee tu kama mwanae
Unaonekana unampenda sana mdogo wako. Ila kuwa na mipaka na hisia zako. Kuna wanaume wanapenda sana mama na baba zao kiasi kwamba akioa anataka waje waishi nyumba moja, sidhani kama utafurahia akifanya hivyo.
 
Ni mchoyo mmeo
Kwan mumeo anashinda nyumbani muda mwingi wanakutana wapi??mdogo wako anaenda chuo mmeo kwenye mihangaiko yake wanakutana wapi muda mwingi
 

Muhamishie hostel
 
Mpangishie mdogo wako chumba acha kuishi na mke mwenzio atakapokuchukulia mume hii umefungiliwa na Mungu mdogo wako anamsumbua mumeo ndio maana hataki akae hapo ndugu sio vizuri kuishi Kwa wanandoa
 
Unaonekana unampenda sana mdogo wako. Ila kuwa na mipaka na hisia zako. Kuna wanaume wanapenda sana mama na baba zao kiasi kwamba akioa anataka waje waishi nyumba moja, sidhani kama utafurahia akifanya hivyo.
Kwangu mimi sioni shida akileta mama yake. Mama namjua ni mtu mwenye upendo sana ikitokea hivyo sitaona shida. Basi naona tuko tofauti
 
Sasa kwanini mke alete ndugu wa kijijini anaekuja kwenye interview bila mawasiliano na mume.

Hadi nalalamika ni kwamba miaka mitatu kabla ya kuoana mume wangu alilijua hili swala. Na wala haikua kuchukua ndugu zangu wote. Ni huyu mmoja tu awe karibu na shule.

Sasa kama mtu anakubali then anakuja kugeuka baadae basi hapo ni changamoto
 
Mi nimekuelewa unampenda mdogo wako na unaipenda sana ndoa yako vizuri sana, unashindwa kumrudisha dogo home kwamba unaanza kuwaambiaje mama sio.! Pia kwa hali hiyo labda ungetamani Kufata ushauri wa wadao hapo kumhamishia mdogo wako hostel ila bahati mbaya bado uchumi wako sio safi saf,i sasa unafanya nini? Umejinasibu mme wako ni mtu safi sana na anajali saana si ndio? Sasa fanya ngea nae kwa faragha KUU muombe huyo dogo amalizie siku zake za masomo hapo kwenu then apite hivi, Mme wako anataka muwe nyie tu mfurahie life yenu ya mwanzomwanzo ya ndoa msikilize, Uafrika unaousema wewe utakuja tu na ataelewa vizuri
 
Mungu ni mwema: nimepokea mgeni kutoka kijijini kwa mume wangu kaingia mchana huu kiukweli nimefurahi na mengi. Mume wangu atajifunza Kupitia hili kwamba ukishakua mkubwa kuna mambo hayaepukiki. Picha linaanza mapokezi niliyompa haamini. Na tutakua nae hapa kwa mwezi. Labda maneno yatapungua. Ushauri wenu wa kumtoa mdogo wangu nimeupokea Mungu anipe busara ya maneno ya kumuondoa ila hadi aondoke na huyu ndugu yake aondoke atatoka na funzo kubwa sana.

Asanteni
 
Kwa uzoefu:-
  • Unayempigania sasa hivi, baada ya kupata kazi au mji wake anaweza kuwa changamoto kwako, na asikumbuke namna unavyoweka ndoa yako rehani kwa sasa.​
  • Kwa sababu yuko chuo, akae hosteli au nyumbani kwa wazazi wake wewe uwe unamsapoti pale panapohitajika.​
  • Kuendelea kumtetea yeye, ni kuweka ndoa yako rehani kwa kitu ambacho huna uhakika uko mbeleni kama mtakuwa bega kwa bega.​
  • Uwe upande wa mumeo na usimpande kichwani, tokeni 'out' mkiwa wawili na akupe sababu kwa nini kuna hizo changamoto, na nini kifanyike​
  • Kwa wale waliopitia mafunzo; maisha ya ndoa ni mke na mme tu ndio wanaofanya maamuzi, sio ndugu wala wazazi.​
  • Punguza msongamano hapo nyumbani, ili uweze kumpa mapenzi vizuri, iwe; jikoni, bafuni, kolidoni n.k​
  • Mzalie watoto wa kutosha; na pambania watoto, na usipambanie ndugu kwa sababu na wao watakuwa na wake/waume zao na hawatamkumbuka mumeo, ingawa kwa sasa wanatumia hela zake.​
 
Yaani umekaza kichwa kama hamnazo.
Sasa mnataka niseme na mama mkwe Simpendi tena? Au ndo wanadamu hawana jema. Watu wameshauri nifukuze mdogo wangu. Hakuna hata mmoja aliekuja kuniambia wangu nilimfukuza na imekua hivi hivi. Yani hakuna jema
 
Hiyo sababu ya kwanza umeongea point kubwa sana. Najua kabisa mdogo wangu akipata kwake hata ye anaweza asiwe na moyo nliokua nao maana wanadamu tunabadilika sana. Hili nimelielewa sana tu. I’m sure huyu mtoto akiondoka mume wangu atakua na amani
 
Hakuna mwanaume anafundishwa na mwanamke king'ang'anizi kama wewe.Mimi nakuambia zingatia msingi mkuu wa ndoa ambao ni watu wa wili tu.Hao wengine wote wabaki kuwa ndugu wasalimiaji tu.Vinginevyo utavunja Ndoa kwa sababu ya hao ndugu.
 
Pambania ndoa yako; kuna ule wimbo-' kila mtu, atauchukua mzigo wake mwenyewe'
 
Sasa mnataka niseme na mama mkwe Simpendi tena? Au ndo wanadamu hawana jema. Watu wameshauri nifukuze mdogo wangu. Hakuna hata mmoja aliekuja kuniambia wangu nilimfukuza na imekua hivi hivi. Yani hakuna jema
Ndugu,tafuta muda ujifunze kwa watu waliokuzunguka juu ya kuharibu ndoa.Ndoa nyingi zimechangiwa na upande mmoja kuruhusu nduku kuingilia maisha ya wanandoa.Hili mahitaji maneno mengi dadangu.Sisi wanaume tunaojua maana ya uhuru ndani ya Ndoa,ndiyo tunakupa ukweli.
 
Kwanza huyo Jamaa anapata wapi muda wa kuonana na watu wa nyumbani,mie huwa nikiondoka nyumbani SAA 12:30 kurudi ni SAA 3-6 usiku hadi watoto huwa wananimisi.
Ndugu akija nyumbani anaweza akamaliza wiki nzima ndio akaniona has a Jumapili.
Jamaa anashinda nyumbani, huwa ana hesabu nyanya na vitunguu 😂😂, ulinzi madhubuti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…