Mume wangu hapendi ndugu zangu

Mume wangu hapendi ndugu zangu

Wanawake linapokuja swala la ndugunzenunakua too emotional kiasi kwamba issue ya kawaida ya kusikilizana mnaifanya tofaouti kabisa. Jaribu kuwa msikivu na ondoa emotional umsukilize na umuulize kwa utulivu utapata solution.
Pia labda ya mmogo wako kuja hapo ulimshirikisha au ulifanya maamuzi ya upande mmoja au ulimshinikiza?
Kama alitoa approval yake sidhani kama angelalamikika .
Anachokiona pengine anaona unaweza kuwa mwamzo WA kuleta ukoo wako wote hapo kama hukuweka clear kwamba anakuja kufanya kwa sababu ipi.
Pia mdogo wako anawajibika hapo nyumbani au amekuja tu kumwomgezea house girl majukum.
Dunia imebadilika dada wanoume hatokubali imaya yake inngiliwe kirahisi au pia yupo cost conscious maana anaingia extra cost kumhudumia ndugu yako na pengine kipato chake hakikidhi, au pia usikute wewe mwenyew unaegemea zaidi upande WA nduguyo badaya ya kuwa fair.
Ukishaolewa familia yako ya kwnza ni wewe na mwenzi wako na waneno, hao ndio wanakua sababu ya hustle zenu.
Wengine ni wengi sana kuwasidia wote mtaharibu ikiwa Kila mtu atabase alikotoka.
 
Moyo wa mtu ni kichaka.
Usiamini unamjua.

Hawezi akaanza tu kumchukia mdogo wako bila sababu zilizojificha ndani ya uvungu wa moyo wake.
Kama mmesoma vizuri, mleta maada amesema huwa Binti anafanya makosa ambayo kwa kiasi Fulani jamaa an react na dada mtu anamtwtea binti kuwa binadamu huwa wanakosea.
 
daah, pole sana

hapo imebaki hatua mbaya zaidi, endeleeni kuomba na ikiwezekana mdogo ako ahame hapo alipo

allivyoweka chumvi huoni ni Mungu tu angeweza kuweka sumu? maisha haya jamaniiiii
Umemwamini huyu jamaa kabisa>
 
Vipi kuhusu hao ndugu wengine wanaokuja hapo kusalimia na anawatosa? Mimi siamini kwamba binti kamkataa, hapo issue ni gubu la mwamba, hataki ndugu wa mke waishi hapo.
Mi naona tatizo linaweza lisiwe ndugu za mke kuishi hapo tatizo ni namna wanavyokuja je.
Taarifa inatakiwa iwepo na idhini itoke kwa mume, sio from no where ndugu huyu hapa.
 
"naomba nikute siti ya kukaa" ,,[emoji1787][emoji1787][emoji1787] huyo kaka yetu ana roho mbaya.
Mpaka alisema hivyo inaonekana watu wanajazana na akiingia hawashituki wala kumpisha kiti. Mwamba inabidi aende chumbani
 
Wanawake linapokuja swala la ndugunzenunakua too emotional kiasi kwamba issue ya kawaida ya kusikilizana mnaifanya tofaouti kabisa. Jaribu kuwa msikivu na ondoa emotional umsukilize na umuulize kwa utulivu utapata solution.
Pia labda ya mmogo wako kuja hapo ulimshirikisha au ulifanya maamuzi ya upande mmoja au ulimshinikiza?
Kama alitoa approval yake sidhani kama angelalamikika .
Anachokiona pengine anaona unaweza kuwa mwamzo WA kuleta ukoo wako wote hapo kama hukuweka clear kwamba anakuja kufanya kwa sababu ipi.
Pia mdogo wako anawajibika hapo nyumbani au amekuja tu kumwomgezea house girl majukum.
Dunia imebadilika dada wanoume hatokubali imaya yake inngiliwe kirahisi au pia yupo cost conscious maana anaingia extra cost kumhudumia ndugu yako na pengine kipato chake hakikidhi, au pia usikute wewe mwenyew unaegemea zaidi upande WA nduguyo badaya ya kuwa fair.
Ukishaolewa familia yako ya kwnza ni wewe na mwenzi wako na waneno, hao ndio wanakua sababu ya hustle zenu.
Wengine ni wengi sana kuwasidia wote mtaharibu ikiwa Kila mtu atabase alikotoka.
Nilishaelezea kuwa hamuhudumii kabisa
 
Mi naona tatizo linaweza lisiwe ndugu za mke kuishi hapo tatizo ni namna wanavyokuja je.
Taarifa inatakiwa iwepo na idhini itoke kwa mume, sio from no where ndugu huyu hapa.
Ni kweli, kuwe na mawasiliano nani anakuja, mume aridhie...sio mtu unashangaa tu nyumba imejaa wageni hukupewa taarifa wala kukubaliana
 
Habari wakuu, nahitaji ushauri,

Mimi ni binti nimeolewa naishi na familia, mume wangu pamoja na mdogo wangu wa kike. Tatizo ni kwamba mume wangu amekuwa na kisirani sana juu ya huyu mdogo wangu wa kike. Kila anachofanya lazima mwanaume alalamike.

Na wala sijawahi kuwa na mawazo labda anamtaka, ndiyo maana anafanya hivi visirani vyote. Mazingira niliyomlea mdogo wangu namjua na ana tabia njema sana.

Mume wangu pia siwezi kumuhukumu kwa uhuni, hajanipa sababu ya kufanya hivyo. Kwahiyo kinachonichanganya ni kwanini ananipa wakati mgumu wa kumfanya mdogo wangu aishi kama yuko kwa mtu baki wakati mimi ni dada yake wa kuzaliwa naye kabisa?

Kila kitu ni lazima aseme kana kwamba huyu mtoto anamkwaza. Kinachoniuma mimi ni kwamba kila siku namuuliza hivi kama angekuwa anaishi hapa ndugu yako halafu mimi namfanyia hivi
Ungejiskiaje? Si ningeonekana mimi ndiyo mbaya sipendi ndugu wa mume?

Na kinachonishangaza, kuna kijana tunaishi naye hapa siyo ndugu wa damu wa mume wangu lakini anatusaidia kazi za hapa nyumbani, ametokea kijijini kwao. Sasa huyu hata akosee vipi mume wangu ukimwambia huyu kakosea hiki na hiki wala hutomuona akijigusa kwenda kumfokea wala kumsema.

Sana sana atajibaraguza tu ili uone ame 'react' na hii siyo mara ya kwanza. Chochote kinachomuhusu mtu wa kwao hutomuona mume wangu amekasirika, lakini ikiwa ni swala la kuhusu ndugu yangu atafoka haswa.

Inafika hatua anamnyima hadi vitu vya kutumia ndani ambavyo hata yeye anavitumia. Hiyo siyo shida, naumia kwasababu mimi huyu mtoto namchukulia kama mwanangu wa kumzaa, nimelichukua hilo jukumu kwa mama yangu tangu mdogo na kwa sasa mama haishi Dar na hatujawa na mahusiano mazuri sana na baba yetu kwa sababu ya mambo ambayo amekuwa akifanya kwetu sisi kama familia.

Kwahiyo najitahidi sana mdogo wangu asijihisi mpweke wala asione kuna pengo la kuumizwa kimalezi na baba yetu.

Na kuna siku ilikuwa sikukuu, nilimwambia mume ndugu zangu wanakuja kwasababu wazazi wetu hawaishi hapa Dar naomba sisi hapa tuwafanyie kitu kama kuwaalika wale hata chakula cha kawaida tu, akasema yeye hana hela.

Wala sikukasirika, nikajikokota nikanunua vyakula nikapika nioneshe kama mume wangu ndiyo amewaalika na wao waone wana kaka hapa mjini. Mume wangu wala hakuonesha ule ushirikiano ambao mimi huwa nautoa wakija ndugu zake, maana huwa napika haswa hadi kwenye kuni.

Nahangaika, napanga, naandaa, nikijua ndugu wa mume wangu wanakuja ila siku wamekuja wadogo zangu sikupata ushirikiano huo. Nilisema acha tu nivumilie kwasababu namheshimisha mume wangu mwenyewe.

Mara nyingine aliniliza na nikamwambia mimi huwa silii lakini unanitenda kama vile sisi kwetu ni masikini, yaani wadogo zangu walipita kutusalimia wakawa sebuleni akaniita chumbani akaniambia nataka kuja kukaa sebleni, naomba nikute siti ya kukaa. Kanakwamba wadogo zangu wamejaa pale maana walikuja kusalimia.

Kinachoniuma ni kwamba, sisi katika kukua kwetu hatujawahi kulelewa na ndugu, kama wadogo zangu wanakaa nje ya kwa baba na mama basi kwangu ndiyo pa kwanza, kwahiyo nikiona wanatendewa hivi naona kama ni mimi ndiyo napitia, sitamani wajione watu baki.

Na kuna muda huwa nawaza, ningekuwa na uwezo ningejenga nyumba yangu niwaweke wadogo zangu hadi watakapokuja kuolewa. Atakae tawanyika sawa, ila kwakuwa mzazi wetu ana uwezo ataona nampokonya wanae. Ila natamani sana wadogo zangu waishi maisha niliyotamani kuishi.


Ushauri unaohitajika;

1. Ni kosa mimi kumtetea mdogo wangu? Kwasababu ninapo jaribu kuuliza kwani tatizo lipo wapi hadi ufoke juu ya jambo dogo hivi, naonekana mkorofi au nataka kumpanda mume kichwani?!

2. Kiubinadamu, huyu mdogo wangu amekosea kuja kuishi kwangu? Nimemlea na hana tabia mbovu kwahiyo namjua, na kila siku namwambia mdogo wangu ikitokea leo dada yako nimedondoka, watoto wangu hutowaacha naamini.

Nampenda sana huyu mtoto, Mungu pekee ndiyo anajua. Kuna muda namwambia mume wangu basi nisamehe mimi naomba vumilia kidogo huyu mtoto akipata kazi ataondoka.

Kwasababu siyo kwamba kwetu tuna shida ya kifedha na wala mume wangu hamgharamii chochote zaidi ya chakula ninachokula mimi ndiyo anachokula huyu mtoto. Ni anakaa kwangu kwasababu ni karibu na chuoni anaposoma yeye.

Kwa upande wa nauli na gharama za kujikimu anatoa mzazi na mimi nikipata huwa nampa kidogo, nashindwa hata kusema namuhudumia maana biashara niliyokuwanayo ilishavurugika baada ya kumuomba mume tusimamie wote ili asiwe na wivu na wateja (stori ndefu haihusiki na mada).

Kwahiyo sina uwezo wa kumgharamia mdogo wangu kwa asilimia mia ila nikipataga 20, 30 nampa ajisogeze. Na mdogo wangu najua ananijali sana, kuna vitu ananifanyiaga huwa nahisi kama nina binti wa kike kabisa.

Yaani kiufupi sipo tayari ndoa yangu iingie doa kwasababu ya mimi kumtetea mdogo wangu na sipo tayari kugombana na mdogo wangu kwasababu yoyote, sijui kama nimeeleweka hapa?

3. Nifanyeje ili mume wangu awe na amani, mdogo wangu pia awe na amani na asijue kwamba shemeji yake huwa analalamika? Kwasababu kila ambacho mume huwa analalama mimi huwa natafuta namna ya kumuelekeza mdogo wangu kama vile mimi ndiyo nataka iwe hivyo, namwelekeza ili asije akafanya tena mume asione tunamdharau.

Na kibaya ni kwamba kuna siku mdogo wangu alisikia nikilalamika sana kwamba hii hali ya yeye mume wangu kukosa amani inaninyima raha, nataka anisaidie mawazo nifanyeje ili awe na furaha na nimuelewe ili niwe namrekebisha mdogo wangu na mimi niwe na amani, hakunijibu! Kesho yake mdogo wangu alikosa raha na sikutaka tena kuibua hiyo mada.

Kiukweli ndoa yetu haina miaka mingi lakini naumia, nilitamani sana mume wangu amlee mdogo wangu kama ambavyo mimi ningelea wa kwake. Lakini inanipa wakati mgumu sana kwamba isije ukatokea mtafaruku kati yao. Nitakae kuwa kwenye wakati mgumu ni mimi.

Uadui huwa hauishi ikiwa mmoja akijua mwengine anamchukia. Na kuna muda huwa namwambia mume, natamani hata na wewe aje ndugu yako hapa akae nikuoneshe jinsi inavyokua kuishi na familia, kuna vitu unavichukulia kama ni mwanao kafanya. Na mume kwangu ana upendo, anajitahidi sana kwakweli, kama kuna makosa ni madogo ya kiubinadamu, ndiyo maana nafukia mengine yoote.

Ninachotamani ni ushauri tu wa kumfanya mume wangu amuone mdogo wangu kama mdogo wake. Niwe na amani pia.

Naombeni ushauri.
Pole sana pia hongera una mwandiko mzuri hii ina dhihirisha kuwa wew ni mzoefu .... lakini nlicho gundua ni kwamba hayo yote anayofanya mumeo ni tabia yake yaani yeye ndo yupo ivo ni aina ya watu ambao ni wabinafsi ... huyo ndogo wako ukikaa naye chini kwa siku zijazo atakwambia mengi ambayo kwa sasa siyo rahisi kukwambia sukuhisho lq haraka mtoe nduguyako hapo japo ni mamuzi magumu sana
 
Pole sana pia hongera una mwandiko mzuri hii ina dhihirisha kuwa wew ni mzoefu .... lakini nlicho gundua ni kwamba hayo yote anayofanya mumeo ni tabia yake yaani yeye ndo yupo ivo ni aina ya watu ambao ni wabinafsi ... huyo ndogo wako ukikaa naye chini kwa siku zijazo atakwambia mengi ambayo kwa sasa siyo rahisi kukwambia sukuhisho lq haraka mtoe nduguyako hapo japo ni mamuzi magumu sana
Nashukuru sana nimekuelewa🙏 Anaondoka soon
 
pole my dear lakini usiendeshwe sana na hisia,kama ungekuwa huwezi kukaa mbali na huyo mdogo wako basi ni vyema usingeolewa ili uendelee kukaa naye.Kitu kingine mmeo kukaa na mdogo wako ni optional sio guarantee provided that hakuoa watu wawili.
kwa jinsi ulivohadithia nilitegemea ufanye uchunguzi wa siri ungeweza kubaini chochote,ni muhimu kuwa na assumptions na kuzifanyia kazi(kuwa mtu wa kureason kuliko kuendeshwa na hisia)yaani haiwezekani amchukie from no where lazima kuna kitu ether mmeo anamtaka alafu anamtolea nje au mdogo wako anamtaka mme wako(hapa naona hutaki kushughulisha ubongo wako unasema mdogo wako ni well disciplined,don't trust anyone).
USHAURI,sio ushauri tu bali ndo utaratibu mzuri,ndugu yako msaidie akiwa mbali sio lazima kukarabisha matatizo yasiyo ya msingi ameshakuwa mdada anajitambua kwa nini usimsaidie akiwa huko,(sababu za huyo kuendelea kukaa hapo sio za msingi).Pia umeshamjua mmewako na imedai kwako hana tatizo kwa nini usiendane naye?
 
Naona umepewa ushauri mwingi mzuri.

Mulipoanza kuishi kuanzia siku ya kwanza mkiwa ni mke na mume huyo mdogo wako mlikua nae au alikuja baadae? Na kama alikuja baadae ulimshirikisha mume wako na aliafiki swala hilo.

Kuna sehemu umesema mumeo hataki kumlea mdogo wako, mlizungumza kabla kwamba atakua pia na wajibu wa kuwalea ndugu zako na aliafiki?

Kumbuka kabla hajakuoa jukumu la kuwasaidia ndugu zake lilikua ni lake ambalo anaweza kuendelea nalo ,na jukumu la kumlea mke ni lake na umesema analitimiza,ila kuwasaidia ndugu zako sio sharti la ndoa ila ni msaada na hapaswi kulaumiwa.

Cha kufanya hivi sasa kaa na mume wako na umueleze umuhimu wa ndugu yako kuwa hapo na athari anazoweza kuzipata akiwa nje ya hapo,na usimueleze kama unampa maelekezo ila muoneshe kwamba unahitaji ushauri wake.
 
Na siku wakianza kucheka utakuja na uzi mwingine tena mrefu zaidi ya huu wenye huzuni na majuto makubwa sana.

Maana mwisho wa chuki ni upendo ......na mwisho wa upendo ni chuki.

Na utakia umechelewa sana.
 
Mpuuze mumeo fanya juu chini mpuuze Wala usimkasirikie Kama ni showw binuka HV
IMG_20221117_002858.jpg
 
Jifanye kipofu huoni anayofanya, hiyo ndio hulka yake na huwez mbadilisha na ukijaribu mtaishia kugombana.
Ushamjua mumeo tembea na beat nduguzo wakija pambana nao mwenyewe na huyo mdogo wako ishi nae hivyo hivyo itafikia wakat ataondoka haya unayosimulia yatabakia story. Hao watu wapo kwenye jamii hawabadiliki ni Mungu pekee ndiye mwenye kuweza.
 
Back
Top Bottom