Mume wangu hapendi ndugu zangu

Mkuu kwaiyo huyu ni mke wa yule mwamba amejibu mapigo
 
Huyo wa shemeji kumjibu mume wala haihusiki kwanza mume wangu hata jamii forum account hana. Angekua ana jeuri ningeshamcharaza mwenyewe na anamuogopa mume wangu kweli.

Na kwa bahati nzuri mdogo wangu hadi leo anaamini mimi ndo mkorofi nna mcontrol kuliko shemeji yake😃 nimeona bora nibebe mimi ubaya. Ye anaaamini shemeji yake ni mkimya hana shida. Na mimi naendeleza imani hiyo so hiyo story yako hapa wala haiingii
 
Mimi huwa na support mahitaji ya nyumbani, vitu vingi tunavyotumia na mume wangu nimetoka navyo kwenye hustle zangu kabla ya ndoa so sijaja hapa kizembe mkuu, kuanzia mali hadi usafiri na hilo wala sijawahi kulitaja wala sihesabii so ukisema niko hapa kitegemezi sio kweli. Siwezi kuelezea career yangu na sitaki kujionesha kwa mume kwamba nnataka kutake over majukumu ya familia I tried that once tuligombana sana, ukinunua gesi anaona unatamba, ukienda kujifanyia shopping anaona unamdharau sijui kama unaelewa. So saizi nafanya biashara zangu online sio kwamba niko apeche alolo ila uwezo niliokua nao sio wa mimi kuja kumtambia mume.


Na kwa kusema hivyo watu watasema kwanini nisimpangie dogo hostel, hivi mnajua gharama za mtoto kukaa hostel kuanzia malazi, chakula na huduma zingine.? Saizi napambana kujiwekea akiba ya mipango yangu ya baadae. Na kingine kumtoa huyu mtoto ni kumpeleka home tu maana hizo cost ni sawa na yeye kutoka kwetu kwenda chuo
 
Thubutu kumfukuza ndugu yako kwa kuwa mwanaume ni baba yako hatokuja kuku cheat wala kukuacha. Hao wanaokushauri ni wapumbavu eti mfukuze dogo. Wa kwao wamewafukuza? Miroho mibaya tu.

Ndo nyie mkiumwa mnaenda kusumbua marafiki wawachangie hamna hata wa kukusogezea kopo la kutemea mate. Na ukute mume kaenda kuoa mke wa pili au mke kaenda kufanya yake hukooo we umebaki huna hata kumsumbua.

Dada mtoa mada nilichoona unataka ushauri jinsi ya kumfanya mume aelewe kuishi na watu ila watu wameacha kushauri wana attack.

Usifukuze ndugu. Huyo mume aache roho mbaya siku atakufanyia kibaya hutoamini
 
pamoja na yote dada yangu inaonekana unalazimisha Sana hio ndoa lakn utabaki kuwa ukweli tu huyo mwanaume ni WA ajabu huwezi kusema mtu anakupenda alafu hampendi ndugu Yako wa damu hapo una mume Bali unaishi jitu la hovyo hakupendi na ndio maana haogopi kumchukia ndugu Yako Huku akikuonyesha. mkatae haraka
 
Ifike mahala tuache tabia ya kuishi na ndugu, ww umeoa au umeolewa hakuna sababu ya kuishi na ndugu kama hakuna ulazima, hicho ndo chanzo cha matatizo mengi.
 
Shida ni kwamba huyo mdogo wako hana faida naye halafu na wewe pengine unamjibu hovyo mme wako na hamkujadiliana wakati wa kumleta
 
Ndo umeona uje kunielezea huku mtandaoni????
Huu ni ushahidi [emoji35][emoji35][emoji35]

Sasa ikifika tarehe 1 mwezi wa 12 sitaki kumwona huyu mdogo wako vinginevyo ntawafukuza wote.

Na unajua kabisa kuwa huwa sitaki ujinga wa kutangazwa kwenye mitandao.
 
Hahah

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
mimi was reverse. mama mdogo alianza kuniapproach nilipomgiga chini alinichukia. wife akanijia juu kuwa namchukia mama yake mdogo. baada ya miaka zaidi ya mitano ndipo nikamwambia siwezi kuoa mtu na mama yake.....alichoka, hajarudia kuniuliza tena
Hukutakiwa kusema hii Mzee,hizi tunakufa nazo

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana kwa changamoto za maisha mama, kwa jinsi ninavyoona hapo uyo mumeo kwa vyovyote inawezekana kwa asilimia kubwa kamtongoza mdogo wako ndio mana kamuwekea gumu fulani hivi, afu kingiine yawezekana aujazaa nae mumeo bado hamjapata mtoto bado ndio mana itakuwa inampa shida aje ndugu yako badala ya kumpatia mtoto ili na yeye apate raha ya kuwa na mtoto, ayo ni mawazo yangu suala la kisirani sidhani mama ila Kaa kwa kutulia ukweli utaujua tu.
 
Unavypmuamini sana mdogo ako lol. Tunza akiba ya imani kidogo

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…