Mume wangu hapendi ndugu zangu

Hili nalo ne o yaani ndoa changa alafu unaleta mdogo wako kwa kweli mume ana haki ya kununa. Mtu alikuwa na expectations za kugegeduana garden sebuleni kitchen shower leo unaleta ndugu naakosa uhuru. Aise amefanya vibaya sana.
 
Kabisa...muishi mume na mke basi. Ndugu saidia kwa njia nyingine wakiwa huko mbali. Shauri yako mtashare de libolo wewe na mdogo wako 🤣🤣🤣🤣
 
Nikushauri dada, kwa mazingira hayo mpeleke mdogo wako kwa ndugu wengine, maana hapo ni shida mumeo hampendi
🤝 mdogo wangu ata opt kurudi nyumbani maana hata wenyewe wanasemaga mimi ndo nawaelewa kuliko mtu mwengine so akitoka hapa ni atarudi nyumbani tu. Bora awe ameamua yeye. Nikiamua mimi ni kama kumfukuza. Yaani acha tu ndugu yangu Mungu anipe busara haswa
 
Maandiko yanasema ."mwanamke ataachana na wazazi wake,na ndugu zake,ataambatana na mume wake na wao watakua mwili mmoja.ukitafakari maneno haya vizuri wote ntakua na makosa,kwanza Kama sasa mmekua ni mwili mmoja kwa nini mume wako afanye hivyo?la pili kiuhalisia hautakiwi kuishi na ndugu zako swala linakuja familia zetu za kiafrica umaskini bado ni tatizo kubwa.hauwezi kuishi bila kusaidia ndugu,kwani sio wote wanakua wamepiga hatua,ni jinsi gani ya kuangalia namna gani unamsaidia
 
Hili nalo ne o yaani ndoa changa alafu unaleta mdogo wako kwa kweli mume ana haki ya kununa. Mtu alikuwa na expectations za kugegeduana garden sebuleni kitchen shower leo unaleta ndugu naakosa uhuru. Aise amefanya vibaya sana.


Mkuu wanawaje wa kiafrika ndio wachawi wa mahusiano yao.
Huyu dada sisi ambao tunakoment tofauti na anavyotaka kusikia yeye anatuona wachawi na kututukana kimoyomoyi lkn ipo siku atakumbuka hizi koments.

Nakuhakikishia hilo lijamaa ipo siku litakula wadogo zake ajutie hili analolileta, atamchukia mune na atawachukia hao ndg zake anaowatetea hadi kijasho kinamshuka.

Wengine tumeona mengi.
Unaowapenda zaidi ndio watakuumiza zaidi...fanya mambo kwa kiasi na tahadhari
 
Akae hostel za ndani ya chuo haitakuwa changamoto sana
Sasa wewe ni mwanaume. Kumtupa mtoto huko si ntakua katili na kikubwa ntampa tu stress bi mkubwa maana stress za wanae zote huwa ananimwagia mimi nizisort so hawa ni wangu
 
Uishi Maisha marefu madam

Nakazia hapo
 
😂😂😂😂
Mtani wangu ninatamani sana nikushauri kitu ambacho kamwe huwezi kukikwepa lkn ndio hivyo.

Najua hutaipenda post yangu lkn hutaiepuka kukupata siku za usoni.

1. Huwezi kumpenda mdogo wako akiwa
nje ya kwako na ahisi unampenda?

2. Unajua pia huwezi kupata vyote unavyovitaka viwe? Yaani kuwa na mdogo wako home kwako na furaha ya ndoa kwa pamoja?

3. Yes unaweza kufanikisha mdogo wako akae nawe lkn furaha ya mume hutaipata kwani sio utashi wake.

4. Jifunze kuchagua cha kwanza kwanza...kumbuka sheria ya ndoa ni kutengwa na ndg na jamaa zako? usijidanganye...ndg watakuja kusalimia na kuondoka tu na sio kukaa.

5. Msikilize mmeo anachotaka eidha awe na roho mbaya au hata hujamwelewa kwanini afanya hivyo...nenda naye taratibu. Ukilazimisha utalia kwani anaweza kufanya maamuzi magumu yakakuumiza milele, mimi ni mwanaume na nina huruma kuliko unavyofikiri lkn ukienda kinyume na sheria yangu utalia.

6. Unaweza kuwapenda ndg sanaa lkn kuna siku watakusapraiz na utawachukia milele...ipo siku utamkuta kitandani kwako na mmeo na hutaamini macho yako na upendo unao wapa.

Katika hili nilikuwaga na gf wangu mrembo sana wadogo zake mapacha visu hatari.
Aliwapenda sana, kiasi kwamba tulikuwa tukisafiri pamoja nao na aliwaamini sana.
Huwezi amini walimgeuka na kuanza kutaka kutembea na shemeji yao na akagundua hilo...nisingekuwa na msimamo ningewachanganya....nahisi unalitaka hili hasa siku ukiona mmeo anampenda huyo binti ujue tayari.

Kuwa na kiasi katika kupenda ndg
 
Unatakiwa tu utafute njia ya hekima ya kuongea na ndugu yako ili asije akamchukia shemejie au akakufikiria vibaya wewe,
Mdanganye either kipato cha shemeji kimeshuka sasa kutulisha itakua ishu so nenda kwanza tuweke mambo sawa!
Maji ndo ushayavulia nguo mama na huwezi kuachana na mumeo kwa hiyo sababu so tumia akili zaidi kuliko moyo kutafuta suluhu!
 
Nikipata nafasi nitakagua simu ya mama Yoyoo kama yupo JF... maana na yeye ana hii mambo kaniletea mdogo wake half brother nimlee.... hiyo kitu sikuielewa.
 
Sio bure kuna sababu inayosababisha hayo. Nachokushauri mtoe huyu binti akakae hosteli ili kupunguza hiyo migogoro.
Hayo mambo ya ndugu yanategemea mtu anachukuliaje na inabidi uende nae taratibu Malezi ya familia yako na mumeo ni tofauti na the way mnavyo handle ndugu inatofautiana pia

Muombe MUNGU mambo yakae sawa hapo baadae ni muda tu
 
Itoshe kusema kuwa unajielewa sana na u mke bora
 
Aiseee ila tupunguze ishi na watu, tujitahidi kuishi kila mtu kivyake
 
Mimi nimeona watu wameshauri vitu Vingi lakin tayari una majibu yako kichwani ukitaka ushauri kubali kishauriwa japo wakat mwingine ushauri unaopewa unaweza kuwa mgumu kwako
 
Huyo kamtongoza mdogo wako kachomoa!

Amini nakwambia, ndo maana kisirani

Kongole kwa mdogo wako ana tabia njema sana[emoji122][emoji122]
 
Kama uwezo wa kupangisha chumba mahali unao, Basi mpangishie chumba.

Amani ni nzuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…