Mume wangu hapendi ndugu zangu

Mume wangu hapendi ndugu zangu

Duh kwa hilo pole sana mkuu.

Kiukweli hiyo ni ngumu sana kumbadilisha huyo mtaalam hapo, sijui kama inawezekana kuibadili tabia ya mtu sina uhakika.
Kupenda na kuchukia ni vitu viwili vipo katika same line but different pole.

Labda kama kuna njia ipo ya kumfanya mtu kupenda kitu anacho kichukia tena anakichukia kitu unconditionally narudia ni ngumu sana.

Mkuu, najua feelings ulizonazo kwa mdogo wako( nina mdogo wangu pia huyu dogo sipendi ataseke kabisa hata nkiambiwa kafanya nini huwa najitahidi kumrekebisha kwa upole sana tofauti na wengine mpaka home wanajua). Lakini kama njia utakazopewa na members zikigoma njia nzuri ni kutowaweka pamoja.

Kutokukaa pamoja itakusaidia wewe zaidi kutokupata stress ndogondogo kama hizo.
Unaweza kubadilisha tabia yoyote mkuu. Kumbuka hakuna anaye zaliwa na hasira,chuki wala hofu..vyote unajifunza kulingana na mazingira ama malezi unayo pitia..mwisho inakuwa tabia ambayo inaku control kutoka kwenye subconscious mind..maana huko ndo store ya matabia yote uliyo jifunza..mwisho pia unaweza ku empty hizo takataka zote ukiamua..kuna procedure zake (Meditation)
 
Ikishindikana mtaftie hostels karibu na chuo as long as home wanamudu kulipia hizo huduma haina shida.

Mie nina shemeji yangu mmoja ndio ana michongo hio alijaribu kumtwist cousin sis wangu awe kama ananichukia ila niliposanuka nikahama home kwao. Ilikuwa wakati wa chuo hivyo hivyo nikaenda kupanga kwangu nashukuru na mke nilimpata huko huko.
Kjmbe kukaa home kunatukoseshwa wake
 
Una maneno mengi huwezi kushaurika zaidi kuna vitu unataka usapotiwe uhalalishe mawazo yako.

Mara nyingine jizoeshe kusikiliza usiyopenda kuyasijia yatakusaidia.

Kwa maelezo yako nimejua kuwa mmeo sio mbaya kiasi unachotuaminisha isipokuwa una mambo yako unayataka yatokee kwa lazima.
Hee makubwa🤣 ubaya wa mume wangu nliouweka ni upi? Wewe nikuulize ungekua una ndugu wa kuja kuishi kwako ungekataa ili umfurahishe mwenzi wako? Jamani mbona mume wangu nimemsifia sana huko juu. Yani kila post nasema kabisa ana upendo. Na wala simuhukumu. Mimi nimekuja kuomba ushauri hii situation naiwekaje sawa. Sio kwamba mume wangu aadhibiwe. Au sijaeleweka mkuu?

Sasa sitaki kushaurika na nini? Wengi wameniambia nimfukuze mdogo wangu napo nawauliza wanishauri nasemaje kumtoa. Sasa mtu nakataa kushaurika kivipi tena?
 
Shida imeanzia pale, kutokuwa na mahusiano mazuri sana na baba yenu. Kisaikolojia wote mmevaa vazi la victim wewe na wadogo zako, hvyo hakuna mwanaume yeyote mtamwona ni mzuri kwenu kwa sasa include mmeo. Zaidi kila kitu atakachoongea mme wako utaona ni manyanyaso tu mnanyanyaswa, sometimes labda anaongea kikawaida tu, ila litakuzwa hilo jambo katika sura ya manyanyaso.... nazifahamu hz mambo,.. Anza wewe kuitoa hyo conflict kwanz ndan yako dhidi ya Baba Mzazi.. Utanishkuru

Mkuu wewe umemaliza...huyu dada asome hii post kwa kurudia atajifunza zaidi.
Nasisitiza tena...shida iko kwake zaidi
 
Sasa mtu kudai mashuka ambayo nimempa mdogo wangu alalie anasema abaki na pair moja nayo ni kujiona victim. Hata mimi nilidhani hivyo lakini kuna matukio naona kabisa ni changamoto na wala sii u victim.

Haaah! kama hali imefikia uko, ipo shida mahali, jaribu kuifahamu na kuitatua, maana mambo cjui ya mashuka najuaga ni ya wanawake, aikitakiwa yeye kufanya hvyo, kaa nae tu chini pindi akiwa sawa, tena kuwa mpole, uwe msikilizaji zaidi utajifunza kitu kwake, jione nawe ni mkosaji tu ata kama akuna ulichokosea(Najua ni gharama).. Ipo hali ya mashindano kati yenu wazazi, baadae italeta shida kubwa kama hamtotumia hekima..
 
Yes na mimi hii ndo mbinu yangu. Namwambiaga nisamehe mimi ila namwambia naomba anielekeze nifanyeje ili mambo yaende sawa. Hasemi kitu. Ukinyamaza anasema unamdharau. Ukijibu yanaibuka mengine. Yani niko tu dilemma
 
Hee makubwa🤣 ubaya wa mume wangu nliouweka ni upi? Wewe nikuulize ungekua una ndugu wa kuja kuishi kwako ungekataa ili umfurahishe mwenzi wako? Jamani mbona mume wangu nimemsifia sana huko juu. Yani kila post nasema kabisa ana upendo.

Sasa sitaki kushaurika na nini? Wengi wameniambia nimfukuze mdogo wangu napo nawauliza wanishauri nasemaje kumtoa. Sasa mtu nakataa kushaurika kivipi tena?

Kumbe ulizoandika ni sifa njema?
Sasa unataka ushauriwe nini?.

Kaa pembeni uvue huo ujuaji then urudi jukwaani upokee ushauri labda utaelewa.

Mmeo atakuwa yuko sahihi lakini nina hisi kuna kitu hakiko sawa kwako.
Sio lazima unjibu...naishia hapa
 
Kumbe ulizoabdika ni sifa njema?
Sasa unataka ushauriwe nini?.

Kaa pembeni uvue huo ujuaji then urudi jukwaani upokee ushauri labda utaelewa.

Mmeo atakuwa yuko sahihi lakini nina hisi kuna kitu hakiko sawa kwako.
Sio lazima unjibu...naishia hapa
Sawa mkuu asante
 
Mumeo ni mchoyo pia anapenda uhuru nyumban kwake kuna muda anataman akushike tako afu sebuleni kumejaa watu.

Hz inshu za wababa kukariri pakukaa sebuleni inatakiwa lizingatiwe maana akikaa tofauti na alipopazoea hawez enjoy,siti ya baba iheshimiwe

Suruhisho ni kumtoa mdogo wako hapo nyumbani akapange tu

Sisi familia yetu ipo mwanza,huko dar tuna ndugu kibao tu lakini kuna wadogo zangu wawili wamesomea huko lakini tulikuwa tumewapangishia vyumba,hii ni baada ya kuona mdogo wetu wa kwanza alivyonyanyasika mpaka kukosa uhuru wa kujisomea na hao ndugu wenyewe kuna watoto wao huwa wanakuja huku mwanza na tunawapokea vizur tu lakin wao walishindwa kabisa kuwakirimu wadogo zetu
 
Mume atakuwa ameomba mzigo nini?
Aise wanawake mnavumilia upuuzi mwingi kisa kuitwa mke🤣🤣🤣
Yaani mtu ana wabagua ndugu zako wee bado umekaa tuu. Hiyo tayari ni strait kuachana. Ndugu kwanza de libolo can go.
Yani ndo maana naomba ushauri. Naona wengine wanasema nimuondoe mdogo wangu. Ndo nauliza sababu nisemeje? Kwamba sasa rudi nyumbani? Na wengine wananishutumu kuwa mimi mjuaji🤣 ndo naelewa kweli binadamu tumeumbwa tofauti.
 
Mrs Fulani...
Tofautisha kati ya upendo na kujali, unaweza kumjali mtu na haumpendi ndio maana huko njiani tunawajali wasiojiweza lakini haina maana kwamba tunawapenda.

Waswahili waliposema ukipenda boga na ua lake walikuwa na maana pana na ndio hii ninayoimaanisha hapa.

Mtu mwenye roho ya kimasikini huwa ana vitabia lukuki kama uchoyo, ubinafsi, kisirani n.k, uusikute anamchukia mdogo wako sababu haoni pia mkiwasaidia nduguze.
Asante nimekuelewa sana yaani
 
Ndoa bado changa ila watapatikana tu
Daah wewe dada una dhambi.
Ndoa bado changa unaanza kuleta ndg?

Mmeo anataka mjiachie kwanza.
Waisrael wana tabia kuwa watu wakioana wapewe zaidi ya mwaka wafurahie hata vitani mme hatakiwi kwenda.
Mapema mno kwa ninyi nyote kuanza kuleta ndg zaidi ya kusalimia na kuondoka.

Muendako utaiharibu ndoa yenu.
Kama mna uwezo kubalianeni mumpangishie huyo binti then baadae mnaweza kuanza kuishi na ndg daah
 
Pole sana nenda naye tu taratibu wala usiumize moyo wako kwa tabia yake hiyo.
 
Yani ndo maana naomba ushauri. Naona wengine wanasema nimuondoe mdogo wangu. Ndo nauliza sababu nisemeje? Kwamba sasa rudi nyumbani? Na wengine wananishutumu kuwa mimi mjuaji🤣 ndo naelewa kweli binadamu tumeumbwa tofauti.
Yes weww mjuaji tena sana😂
 
Kama dogo ni pisi kali na bado ana muda mrefu wa kuendelea na chuo ni best ukamtoa hapo home akapange tuu. Wanaume sie genye knows no boundaries 🤣🤣🤣🤣.
 
Kama kwenu kupo vizuri kama ulivyosema ungemrudisha tu mdogo wako kwenu. Japo hujaweka wazi unaonekana ni mtu wa kukaribisha karibisha sana watu hapo kwenu.

Ni muhimu ukajua kuwa umeolewa wewe kama wewe na not as a package
Mume wangu ana ndugu wengi kuliko mimi. Tatizo langu mimi ni mtu nnaependa sana wageni niwapikie tufurahi. Hata wa mume nawajali hivo hivo na wanakujaga zaidi ya wa kwangu and i really enjoy. Anaeishi hapa ni mdogo wangu mmoja tu na sio kwamba tunamuhudumia kifedha. Ni anahudumiwa na mzazi bado ila hapa anakua karibu na chuo tu, nilichokuelewa ni kwamba nilitakiwa nikae mimi kama mimi. Mungu anipe busara sasa ya kusema ndugu wasije kwangu
 
Hee makubwa🤣 ubaya wa mume wangu nliouweka ni upi? Wewe nikuulize ungekua una ndugu wa kuja kuishi kwako ungekataa ili umfurahishe mwenzi wako? Jamani mbona mume wangu nimemsifia sana huko juu. Yani kila post nasema kabisa ana upendo. Na wala simuhukumu. Mimi nimekuja kuomba ushauri hii situation naiwekaje sawa. Sio kwamba mume wangu aadhibiwe. Au sijaeleweka mkuu?

Sasa sitaki kushaurika na nini? Wengi wameniambia nimfukuze mdogo wangu napo nawauliza wanishauri nasemaje kumtoa. Sasa mtu nakataa kushaurika kivipi tena?
Kwa nini asiishi hostel?
 
Nikushauri dada, kwa mazingira hayo mpeleke mdogo wako kwa ndugu wengine, maana hapo ni shida mumeo hampendi
 
Yes weww mjuaji tena sana😂

Si ulishaaga mkuu🤣 au umerudi ili unipime kama naweza kubishana. Ili u prove point? Sawa mimi mjuaji. Sawa mimi nna mapungufu mengi. Sawa mimi ndo mwenye shida. Si nilishaelewa upande wa ushauri wako ndo maana nikasema asante🤝 narudia tena kusema asante🤝 ushauri wenu ntautazama na kuufanyia kazi. Shukrani kwa mara nyingine🤝
 
Back
Top Bottom