Mume wangu hapendi ndugu zangu

Mume wangu hapendi ndugu zangu

Umeongea vyema sana kaka angu. Ntatafuta tena neno lenye busara nimwambie kwamba huyu ni mtoto. Amlee tu kama mwanae
Sema huenda ni malezi aliyokulia hawakuwahi kuchangamana na kufanya sharing. Kila mtu ana kitu chake so hajazoea kutoa vya kwake.

Niliwahi kuwa na rafiki yangu chuo nae amezaliwa kwao mwenyewe baba yake ni tajiri sana halikadhalika mama yake nae yuko njema kiuchumi.

Mwana tulielewana sana ndio mtu alinifundisha kunywa pombe na starehe za mabar na ma club. Alikuwa damu yangu sana toka day 1 tuna shea same birthdate na star sign.

Shida akawa hataki vitu vyake utumie, eti sijui ushee nae yani yuko radhi akununulie chako kipya ila sio utumie chake. Ila after 3 years niliweza kumbadilisha kuwa maisha hayako hivyo mpaka tunaachana mwaka wa 7 akawa kashaelewa kuwa maisha yako tofauti sana ukiishi kwenye jamii ya changanyikeni.

Aliweza ku cope kabisa na wahuni akaachaga ubinafsi.
 
Lazima uelewe, binadamu tumeumbwa tofauti, hata kimtazamo pia. Unachopenda wewe siyo mwingine apende.
Kuna watu kuishi na ndugu, wanaona ni mzigo usiobebeka. Huenda ni wachoyo, hawajawahi ishi familia kubwa.
Hebu mpeleke hostel huyo mdogo wako, awe anapita kuwasalimu tu.
Umenena hapo kwamba kuna watu hawana experience kuishi na ndugu, sasa maisha yetu ya kiafrica haya kweli tuta avoid? Utaweza kuishi bila watu ndani? Kwamfano mmepata watoto ndani ya nyumba mnaenda kazini mnamuacha na mtu baki akimdhuru nani atatetea? Kidogo akiwa na ndugu anakua na uoga flani.

Hostel amekosa kabisa na kumwachia kupanga ni ngumu binti kumwacha akapange wakati nyumbani papo hata kwa wazazi tu si itakua ajabu
 
Sometimes maisha ni magumu so anatafuta namba ya kupunguza mzigo hapo home.....or Kuna namna mnaishi anakosa kuwa huru....or mume amemtongoza dogo Ila akakataa so lzm amtafutie Visa ili hata baadae akija sema Shem alikuwa ananitaka aseme si unaona ndio maana nilikuwa simtak maana ananiharibia ndoa nilishaona kitambo......suluhisho,Kwanza wacontroll nfugu zako kutokujakuja kwako inaonekana ndugu zako wanakuja sana kwako hata ukipinga huo Ni uhalisia,jua umeolewa wewe,........huyo dogo Kama unaona kbs itakuja haribu mahusiano yenu ya ndoa kwanini usimpangishie tu........maana kituo kinachofuata huyo mme atatafuta mwanamke anayemsikiliza hapo ndio utaita maji mma......mdogo wako,wewe na watoto wako wote mtakosa malezi ya baba

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Naomba unipe huyo mdogo wako nikae naye hapa zero distance na chuo chake.
Ipo siku huyo mumeo atambaka mdogo wako inaonekana ana uchu wa ngono pia ana roho ya kimasikini sana anaona mdogo wako anafaidi.
Ikikupendeza nikae na mdogo wako karibu inbox sisi wote ni dugu moja.
 
Mtoe hapo nyumbani, mpangie chumba au mlipie hostel !

Usikute unalalama hapa ukute mdogo wako Ni type zile za vitoto vya chuo vimekaa kivivu vivu tu,,,, mda wote simu/tv , hapa muda na Kaz ndg ndg za hm mfano usafi,,,

Au ukute vile vi-slay queen kila weend ana birthday kwa rfk zake,,,,

Jaribu kum-shape vzr !

Mume hawezi kulalama ovyo Kuna shida, au alishamtaka akamnyima, dogo anaogopa kukuambia ili asivunje ndoa !

Best option mtoe hapo
U slay queen siwezi kukataa sana ila akirudi toka chuo lazima afanye kazi kama kuna vyombo ataosha. Katika malezi ya mama yetu huyu mtoto amelelewa na anapiga kazi vizuri tu. Lakini angekuwepo ndugu yake anafanya hivyo alafu mimi nakuwa na gubu angekubali?
 
Kama mdogo wako kavuka umrivwa miaka 18 tafuta chumba umpangie awe anakaa uko ila kama yuko chini ya umri uwo mpeleke kwa rafiki au ndugu yako yeyote mana umesema kwenu baba mkorofi fanya hivyo..
 
Kama mna uwezo kwanini msiruhusu huyo mdogo wako akapange, aishi mwenyewe.

Sio rahisi mtu kumkataa ndgu wa mke/mume lakini kikubwa ni mmoja kati yenu ajiongeze kulingana na dalili zinavoonekana.

Na tatizo hilo nahisi hata mdogo wako analijua coz mtu kama hakupendi mbona unaona tu huyu mtu ananichukia.
Mdogo wako asije akafeli kwa stress za hapo kwako kisa kukazania uonekane mwema kwa ndgu zako.

Tafuta njia mdogo wako akapange ila awe anakuja kuwasalimia mara kwa mara.

Kuna dalili mumeo kakataliwa kama wadau wanavosema. Huko kukaza kichwa ukiwatetea as if wewe ni mungu unaona hadi mawazo yao, sawa endelea kukaza.
 
Umenena hapo kwamba kuna watu hawana experience kuishi na ndugu, sasa maisha yetu ya kiafrica haya kweli tuta avoid? Utaweza kuishi bila watu ndani? Kwamfano mmepata watoto ndani ya nyumba mnaenda kazini mnamuacha na mtu baki akimdhuru nani atatetea? Kidogo akiwa na ndugu anakua na uoga flani.

Hostel amekosa kabisa na kumwachia kupanga ni ngumu binti kumwacha akapange wakati nyumbani papo hata kwa wazazi tu si itakua ajabu
Sawa naomba kukuliza hili swali. Kabla ya kumleta binti, hapo nyumbani Je ulishauriana na mume wako? Alikubali? Ama ulifanya maamuzi mwenyewe ya kumleta bila kumshirikisha mumeo?
 
Pole sana dear,nimekuelewa
Unakumbuka ulipoolewa uliambiwa ndoa ni uvumilivu?Basi maana yake ni hiyo sasa,uliambiwa unaishi na binadamu na si malaika basi binadamu mwenyewe ndo huyo sasa!
Kwanza kubali kuwa umeolewa na mwanaume mchoyo na mbinafsi na ndo mana wakija ndugu zako anasema hana ela ila wakija ndugu anatoa,hizo ni tabia za ubinafsi!
Kama mwanamke nilie kwenye ndoa nakushauri umtoe huyo mdogo wako hapo as umesema kwenu una uwezo wa kumlipia hostel,usitake kuforce kukaa nae though umesema unampenda mana utaumia tena sana tu huko mbele kadri siku zinavyozidi kwenda na hata huo upendo unaosema unauona kwa mumeo hutauona tena!
Kumbuka kuna kuchoka as wewe pia ni binadamu,na maudhi na maumivu ndo husababisha ndoa nyingi leo kuwa ndoa jina au kusambaratika kabisa!
Mwache aende alafu wewe endelea kumuombea kwa Mungu aguse moyo wake mana uchoyo ni dhambi!
Kuna vitu unaweza kuvumilia kirahisi kwenye ndoa ila sio kuona mwenzio hataki ndugu zako,yani unajiona hata wewe huna thamani kwake ndo mana nakwambia mtoe kwanza huyo hapo ili usijitengenezee maumivu yasiyo ya lazima!
Once again pole sana,
 
Kama mdogo wako kavuka umrivwa miaka 18 tafuta chumba umpangie awe anakaa uko ila kama yuko chini ya umri uwo mpeleke kwa rafiki au ndugu yako yeyote mana umesema kwenu baba mkorofi fanya hivyo..
Umri amevuka, nyumbani pa kuishi papo ni wa kumwambia tu rudi nyumbani, sasa namwambiaje? Mimi ningefanyiwa hivyo na hii akili yangu nisingekaa kuja kusahau
 
Kama mna uwezo kwanini msiruhusu huyo mdogo wako akapange, aishi mwenyewe.

Sio rahisi mtu kumkataa ndgu wa mke/mume lakini kikubwa ni mmoja kati yenu ajiongeze kulingana na dalili zinavoonekana.

Na tatizo hilo nahisi hata mdogo wako analijua coz mtu kama hakupendi mbona unaona tu huyu mtu ananichukia.
Mdogo wako asije akafeli kwa stress za hapo kwako kisa kukazania uonekane mwema kwa ndgu zako.

Tafuta njia mdogo wako akapange ila awe anakuja kuwasalimia mara kwa mara.

Kuna dalili mumeo kakataliwa kama wadau wanavosema. Huko kukaza kichwa ukiwatetea as if wewe ni mungu unaona hadi mawazo yao, sawa endelea kukaza.
Namuonea huruma kupanga na mimi sina uwezo wa kumpangia, hana kazi si ndo naenda kumuacha aingie kwenye mtego wa mababa wa mjini, ni mzuri so kusumbuliwa lazima ila akiwa chini yangu nammudu nimemwekea hadi mda wa kurudi. Hata kama anaenda sehemu lazima aage kwangu na kwa shemeji yake. Kama wametongozana nikijua ntapata busara kutokea hapo. Acha Mungu anioneshe najipunguzia stress za kuwaza hayo
 
Dar Kuna vyumba Hadi vya 10000,mdogo ongea na wazazi wako akae hostel au mpangishieni chumba ,amalize chuo
 
Kuhusu kuzaa wala sio kikwazo tuko vizuri. Namrudishaje nyumbani mtoto sasa nawaambiaje? Wakati mimi ndo nilishadadia aje akae huku karibu na chuo. Leo nasema arudi kwasababu gani.

Na kingine mdogo wangu anaweka mambo yake sawa atarudi tu nyumbani ila huo mda wa miezi kadhaa mbona ntakoma mimi. Maana mume kila siku anaibuka na jipya naumia
Kama mdogo wako Hana muda mrefu ataondoka basi huna budi kumvumilia.

Ila poleni Sana
 
Back
Top Bottom