Mume wangu hapendi ndugu zangu

Ww unashida moja umekuja na majibu yako kichwani ukiwa na shauku ya kupata sapoti ya mawazo yako......kuna watu kibao huko juu washakushauri muondoe huyo dogo hapo home ila bado unakaza fuvu....unaendelea kuuliza umpeleke wapi???😬😬😬mumeo alikuoa ww sio familia yako so kaa ukijua nyumba yenu ni yako...jamaa na watoto wenu wa kuwazaaa.....hao watu wengine ni nyongeza tu usilazimishe maisha ya kiswahiliswahili jaribu kubeba mzigo wako bila kutafuta kichaka cha kuonewa huruma.
Swali langu jingine,, wakati unamleta hapo huyo mdogo wako ulimshirikisha mwamba na unauwakika alikubali au ulifosi????inabidi utambue mwenzako anapenda kujitawala akiwa nyumbani kwake so jaribu kucope ukishindwa omba talaka ukiolewe na waswahili wenzako wanaopenda extended familiies....na ukiendelea kukaza fuzu huyo dogo atakupindua kwenye hiyo ndoa🤝dogo aende hosteli au utegemee mwamba kuna siku itaikula tu hiyo pisi kali.
 
Aiseee pole sana kwa changamoto. Lkin ki ukweli ukishamjua mtu hawezi kukupa shida. Huwezi kumbadilisha mtu kama yeye mwenyewe hajaamua kubadilika. Ila unaweza kucheza kwenye tune yake.

Kuna watu ni wabinafsi hata uonyeshe upendo wa kutoa roho yako kwa ajili yao kamwe hawewezi kujifunza.
Jiridhishe kwanza kama hakuna sababu ya msingi ya mume wako kumchukia mdogo wako,,kaa chini na wako ongea naye amekuja hapo kwa ajili yako. Yeye ndo anayekufahamu huyo bwana mmekutana ukubwani. Chochote atachosema au kumfokea mdogo wako uwe na kauli moja tu samahani ,,,usibishane wala usitake kumdhihirishia kuwa nani mkosaji na nani si mkosaji. Na akilalamika kujaa kwenye sofa acha wadogo zako wakae chini. Trust me fanya hivyo miezi kadhaaa utakuja kunishukuru.

Hakuna njia bora ya kumbadilisha zaidi ya kumpuuza. Na usipambane kuwaonesha ndugu zako kuwa mume ni bora,,acha ajipambanie mwenyewe kwa kufanya matendo mema.
 
Mawazo yake ni kwamba amekuoa wewe tu! Na sio umlete NDUGU uishi nae, akakae na NDUGU zake.
 
Hakuna cha maombi hapo...huyo kaomba K kanyimwa ndo maana kisirani

Unajisumbua bure ukweli ndo huo

Mhamishe mdogo ako hapo!
 
Maelezo mengi ila utambue jambo moja "UMEOLEWA WEWE NA SI NDUGU ZAKO"
 
Shukrani🤝🤝
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23]

Na kwanini unafoka foka?
 
Tabia zinatofautiana na kila binadamu ana mapungufu yake
Huyu wa kwako ni mbahili kupitiliza yaani anachukia hata hewa ya bure anayopumua hapo

Watu wa hivyo wapo ila usiumize roho ingawa wanawake mna roho ya huruma mda mwingi
Mwambie mdogo wako amchukulie kama alivyo ila jitahidi wewe kumsaidia zaidi mdogo wako kwa mambo madogo madogo

Asiwe mtu wa kukaa sitting room kila wakati hilo aepuke nalo pia amkwepe tu kila wakati
La kuachana kwa sababu hiyo sio uamuzi mzuri kwani sioni shida kubwa sana

Unajua madhaifu yake na ndugu waambie kama unavyotuambia sisi kuwa hawapendi na yeye mwambie kuwa ujumbe unaenda hivyo
Ikishindikana kabisa mdogo wako arudi kwenu tu
 
Swali la kujiuliza kama ilitokea mzazi na ndugu zenu Kuna baadhi hawakuwahi kuwapenda unafikir ni rahis mumeo ambae sio nduguyako kumpenda mdogowako??mtu kuwa na upendo Kwa watu wengine mara nying ni asili tu pia marachache mtu kuweza kubadilika,

kubali ndo tabia ya mumeo na kukwepa madhara ni kuongea na mumeo abadilike akishindwa mtoe mdogowako hapo..
 
Mimi nimeona watu wameshauri vitu Vingi lakin tayari una majibu yako kichwani ukitaka ushauri kubali kishauriwa japo wakat mwingine ushauri unaopewa unaweza kuwa mgumu kwako
Asante kwa kuniunga mkono
 
Haya ndio nionavyo Mimi

 Mosi, uwezo wa huyo mdogo wako kupanga chumba upo Ila unajisikia vibaya kwanini akapange na Hali wewe upo na anaweza kuishi kwako

Jibu ni rahisi mumeo hamtaki hapo kwake,Busara ni huyo kuhama hapo na mweleze ukweli mdogo wako kuwa inaonekana uwepo wako hapo mumeo hapendi na hujui sababu,hii itakusaidia mdogo wako kujua kuwa sio mapenzi yako yeye kuhama Ila Kero zimezidi toka Kwa mumeo.

 Pili, unapenda Sana mumeo aonekane ni mtu mzuri kwenu ndio maana unajitahidi kuficha upuuzi wake,Hilo ni Jambo zuri lakini wakati mwingine sio Sawa aonekane yeye ni Malaika,nahisi ndio maana unahisi mdogo wako alienda kupanga basi mumeo ataonekana sio mtu mzuri,Kwa mazingira hayo kuwa muwazi sema kweli kuwa mumeo hapendi uwepo wa mdogo wako pale.


Tatu, ambalo ndio kubwa na wanabodi wengi wamesema ni kuwa mumeo anataka kumla supu huyo mdogo wako,na hivyo mdogo wako amegoma kuliwa supu,hiyo ndio sababu kubwa Kwa sababu zifuatazo:

* Mumeo hamhudumii huyo binti Kwa nauli wala Karo ya chuo na mambo mengine,kwahiyo wala sio mzigo kwake hata kidogo useme labda Maisha magumu ndio maana hamtaki hapo

* Huyo binti Mda mwingi yupo chuoni sio kwamba anashinda hapo na kuwafanya msiwe huru na nyumba yenu .


* Kama unavyosema huyo binti ana Tabia njema hivyo naamini hajawahi kuvunja heshima ya nyumba yenu.


Kitu pekee ambacho kimebakia hapo ni kuliwa supu na huyo mumeo.

Raisi mstaafu aliwahi kutuambia akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Ushauri wangu,tafuta siku utoke out na mumeo sehemu nzuri nzuri hivi I mean sehemu yenye mandhari nzuri lakini pia itakayowapa nafasi ya kufurahia as if mna update penzi vile mkipiga mastori ya hapa na pale huku mkikumbushana kipindi cha ujana wenu, halafu kwa upole na unyenyekevu huku ukiwa huna chembe za kuonesha kulaumu ongea na mwamba kuhusu mdogo wako(amvumilie kwa mapungufu madogo anayoyaona kwa muda mfupi atakaokua hapo) natumaini atakuelewa.
Ikishindikana hapo nashauri uongee na wazazi wako huyo dogo apangishiwe chumba jirani na chuo ili amani iwepo kwenye familia yako.
 
Kujazana ndg ni tabia za kinyamwezi, kinyiramba na kirangi zaidi
 
Pole sana dadangu, mke mwema na mme mwema hutoka kwa Mungu, na kwa namna ulivyojieleza nimeona hapo Kuna tatizo!!! Ushauri wangu fanya mambo yafuatayo
1: mme wako ndiye baba wa familia na ndiye mwaamuzi wa mwisho, kaa naye faragha mwambie juu ya udhaifu wake huo wa kutowapenda ndugu zako, pamoja na mdogo wako huyo, na mwambie labda Kama yeye hataki ukae naye Basi umuondoe nyumbani hapo!!
2: yawezekana kweli mdogo wako huyo anakosea kweli katika hali ya kuonywa wewe unaona anaonewa kwa sababu sio ndugu yake( wanawake wengi wapo hivyo), jaribu kujithathimini pia kwa Hilo
3: mme wako ndiye mwenye maamuzi, usimpelekee taarifa mbali mpelekee maombi!!! Usipange ndugu zako kuja nyumbani alafu wewe ndo uende kumpa taarifa huku tiyari ulishawaambia ndugu zako wake siku Fulani, Hilo ni kosa, mme wako unatakiwa umuombe Kwanza juu ya Hilo akikukubalia ndo uende kuwapanga ndugu zako! Vinginevyo mme akikataa utasema amewakataa ndugu zako

4: mme wako ndiye mwenye familia akisema Hana hela Wala usimhukumu, vinginevyo mna mfuko mmoja wa kutunza pesa, Mara nyingi wanaume wakiwa na hela au kutokuwa na hela hawasemi Kama Wanahela! Alafu Wana mipango mingi tofauti na wewe mwanamke, hilo ni vyema ulijue, maana yeye mda wote atawajibika lakutokea likitokea nyumbani hapo yeye ndiye atakaye ulizwa! Wala sio wewe mpendwa!

6: mwanamke automatically ukishaolewa unaingia kwenye familia ya mwanaume, maana nyingine ndugu wa mwanaume ndiyo ndugu zako, ndo maana mpaka na jina mwanamke unabadilisha, hii maanake ni kwamba, mmeo bado ataendelea kuwasaidia ndugu zake zaidi, kuliko ndugu zako, wazazi wake zaidi kuliko wazazi wako, marafiki zake zaidi kuliko marafiki zako, hii ni kwa sababu wewe umeletwa kwenye familia, lakini wao bado wapo pale pale, hivyo basi ukishalijua Hilo mpendwa, unachotakiwa kukifanya ni wewe kupambana aidha Kama una kazi, au biashara kuwasaidia ndugu zako, lakini usitegemee hela ya mme wako kuwasaidia ndugu zako, maana hela ya mme wako ni familia yenu!! Ambayo wewe umejumuishwa pia,

7: ndoa ni ya mme na mke!! Nyie mkae mkubaliane mweleze tu kuwa unampenda na haupo tiyari kumkwaza kwa sababu ya ndugu zako, kama hawataki akuambie tu!!! Mm ninaamini ukikaa naye vzr ukamweleza Kama ni mtu mwenye akili atajirudi tu mpendwa!!! Maana hiyo ni tabia ya asili, lakini inarekebishika

8: ndoa inalindwa na maombi, mpendwa, Bwana Yesu akitawala ndoa Yenu hayo mambo yataondoka outomaticallly
Wagalatia 5:22
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

Wagalatia 5:23
upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

Wagalatia 5:24
Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.

Barikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…