Mume wangu hasimamishi, nifanyaje?!

Mume wangu hasimamishi, nifanyaje?!

Kuna mfanyakazi wa serikali alikuja mkoani kwetu, akadanganyiwa binti Mwenye kichaa. Kanisani walikuwa wanafahamu vizuri na pastor anafahamu kuwa huyo binti ana tatizo la afya ya akili na kila baada ya miezi mitatu huwa anaenda clinic ya vichaa pale Lutindi hospitalini.

Mwanaume akafungishwa ndoa na baada ya miezi 3 dawa anazotumia binti kwa Siri zikaisha, akanza kuonyesha dalili ya ukichaa. Ndipo mwanaume akawajuza wasimamizi wa ndoa, jibu alilipewa ni hili: NDIYO ALIVYO TOKA UTOTONI, MPELEKE HOSPITALINI ATAPATA NAFUU.

jamaa akataka ndoa ivunjwe akaambiwa ndoa ya Kanisani huwa haivunjwi kwa sababu ni Agano.

Je, mwanaume angepaswa kuchukua uamuzi gani?
Yesu weee
Kumbe alicholalamima huyu dada NI cha kweli jamaan
Kwanini lakini watoto wa Mungu wanateseka hivi kanisani??
Cc: Restless Hustler njoo SKILIZA majibu ya waenda Mbinguni
 
Akawafungulie mashitaka ahakikishe ushahidi upo na mashahidi wapo na vithibitisho vipo pia , akafungue kesi adai nafidia hiyo ndoa inavunjwa na mahakama za Jamuhuri ya nchi usika haraka iwezekanavyo na jamaa atalipwa fidia zake zote akitaka. Kuhusu hilo agano aliloingizwa la kitapeli hata yeye anaweza akalifuta baada ya mahakama kuvunja hiyo ndoa sawa sawa na imani yake kwa Mungu wake
Weee, kumbe inawezekana?!
 
Haya mje sasa
Naona kumekucha
Haya MALALAMIKO nimeyapata Kwa dada alieolewa miezi 6 iliopita, kaolewa huko Kwa walokole

Kisa kinaenda hivi

Mlokole: money penny me naumia Sana, huwezi amini tangu tuoane hatujawahi tembea pamoja kama MKE na mume

Money penny: nini mbaya mami??

Mlokole: mume hasimamishi nanii yake

Money penny: kivipi?

Mlokole: unajua Sisi kabla hamjaolewa hairuhusiwi kuzini wala kujuana sehemu zenu za siri, nikavumilia na kutii maagizo ya kanisa, lakini tulipoongea Tu yupo honey moon nikajuà mwanaume hasimamishi, sijui nafanyaje na huu NI mwezi wa 6

Money penny: umeenda kwa Mchungaji au wasimamizi WA ndoa wakasemaje?

Mlokole: wote wanasema ndoa haivunjwi kwasababu mwanaume hasimamishi kitakachovunja ndoa NI kifo Tu na Mungu wenyewe Sisi haturuhusiwi

Sasa nifanyaje??

Stori kamili: ipo YouTube channel yangu

Msaidieni binti WA watu afanyaje
Ndoa inaweza kuvunjwa endapo mwanaume au mwanamke hawezi kushiriki tendo la ndoa. Na endapo mmoja anaonesha kulalamikia suala hilo ndoa inavunjwa vizuri tu.
 
Kwenye Kanisa Katoliki Ndoa Iko hivi

Mkianza kunjunjana tuu hiyo ni ndoa lakini si takatifu. Mkiamua mnaenda kanisani Kuitakatifuza/kubariki ndoa.

Mkienda mbele ya Kanisa kwanza mbele ya mashahidi kabla hamjajuaa Kimwili mnafanya ndoa takatifu. Ndoa hii iliyoanzia kanisani hukamilishwa na tendo la ndoa baadae.
Tendo la Ndoa likishindikana Ndoa inabatilishwa.

Udanganyifu wowote ukigundulika pia Ndoa yaweza Kubatilishwa.
Mf.
Mmoja wa wanandoa kuwa na watoto kabla na kutowataja. Ikigundulika baadae Ndoa huweza kubatilishwa.
Mmoja wa wanandoa kugundulika na magonjwa kama ukichaa n.k.
Ahadi za Uongozi
Kushindwa kutii kiapo Cha ndoa ikiwapo Cha "shida na raha".
Kuongeza mwanamke/mwanaume. Maana mkataba ni mme Mmoja Mke mmoja.

Hivyo Ndoa Ya Kikatoliki huweza kubatilishwa pia pale Uvumilivu na Upendo unapofika Ukomo.
 
Back
Top Bottom