mume wangu jamani


Usidanganywe na wanaokuambia "uende kwa Mungu". Hao viongozi wa dini ya mtu mmoja ukienda kwao hujaenda kwa Mungu bali umeenda kwenye makucha yao, nao hawana uwezo wala nia ya kukupeleka kwa Mungu bali nia yao na uwezo wao ni wa kukuopoa hela yako na kukufilisi kama walivyowafilisi wafuasi wao wengi. Hawa viongozo wa dini za vichochoroni na waganga wa kienyeji ni pande mbili za sarafu moja. Wote ni matapeli na ukienda kwao na tatizo hilo lako watakuvua chupi mara moja.
Tatizo ulilo nalo linatokana na jamii kulazimisha ndoa ya mume mmoja kwa mke mmoja, kinyume na maumbile, na baada ya muda mtu huchoka kula ugali kwa kisamvu kila siku. Kwa hiyo dawa yake utaijua. Labda unaweza kuzungumza na mumeo mkaelewana kuhusu hili ili lisiathiri familia yenu.
 
Ushauri umesimama, akiyashika haya , furaha ya ndoa itarejea
 
Hakika Ibilisi naye yuko kazini kuhakikisha matakwa yake yanakamilika. sidhani kama Michelle anapozungumzia Kumrudia BWANA MUNGU anamaanisha kukimbilia kwa viongozi wa dini kama wewe unavyodhani, akifanya hivyo hakika matatizo yake hayawezi kuisha maana imeandikwa '... Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana - Jeremiah 17:5’
 
Helw wana jf, tangu wiki mbili sasa nilikuwa nataka nirudi kuwashukuru kwa ushauri mlionipa kwenye thread yangu niliyoipa kichwa cha habari kama hiki hapo juu, kwa kweli napenda kutoa shukran kwanza kwa mwenyezi mungu kwa kutusaidia tatizo lile limeisha, najua ni mungu tu ndie aliyesaidia,jina la bwana lishukuriwe

Napenda kuwashukuru wale wote waliochangia thread yangu na kunipa ushauri mungu awabariki pia wale walionibeza mungu pia awazidishie walipopunguza pia shukrani za dhati ziwaendee wale walioenda mbele zaidi na kuguswa kwa namna moja au nyingine wakani pm na kunipa ushauri zaidi hawa si wengine ni Mu-sir, Fisherscom, Annony, jamal-tanga na kiraka nashukuru sana mungu awabariki sana ushauri wenu wote niliufanyia kazi kwa namna moja au nyingine.

Ilitokea tu amesafiri nje ya nchi aliporudi mambo yakawa poa na nilipomuuliza kafanya nini akaniambia hakuna alichofanya basi sijamuuliza mpaka leo. Nawashauri wote wenye tatizo kama langu, wasikate tamaa mungu yupo na anasaidia wote wenye kuelemewa na mizigo, mwisho kabisa nashukuru ile post ya michell ambayo watu wengi walicomment niifatilie pia na mimi niliipenda na kuifanyia kazi

Oooops at last am free now, nawapenda nyote, muendelee kuwa na upendo kwa wengine wote wenye matatizo, kwa kweli naipenda jf family, mungu ambariki mwanzilishi max na mods wote kwa kazi nzuri,kila siku inayoenda nazidi kufall in love nayo. ahsanteni.
 
Mshukuru Mungu kwa kila jambo. Afadhali kama ameondokana na hiyo adha
 
Mshukuru Mungu kwa kila jambo analotenda juu yako na ni vizuri zaidi ukazidi kumuomba kwa baraka zaidi kwani anasema palipo wawili mimi ni kati yenu sala ni muhimu sana ili kuepuka vikwazo mbali mbali na wote tuseme AMEN.
 
Mpe bwana utukufu na sifa kwani ni yeye anayestahili,zidisha sala hasa katika kipindi hiki cha kwaresma.
 
mshukuru mungu kwa kila jambo analotenda juu yako na ni vizuri zaidi ukazidi kumuomba kwa baraka zaidi kwani anasema palipo wawili mimi ni kati yenu sala ni muhimu sana ili kuepuka vikwazo mbali mbali na wote tuseme amen.

amen!!!
 

Ndaga mama
 
Mshukuru Mungu kwa kila jambo analotenda juu yako na ni vizuri zaidi ukazidi kumuomba kwa baraka zaidi kwani anasema palipo wawili mimi ni kati yenu sala ni muhimu sana ili kuepuka vikwazo mbali mbali na wote tuseme AMEN.

Namshukuru na nitaendelea kumshukuru ahsante The Finest
 
Mungu ni Mwema, mshukuru kwa kila jambo maana hakuna linaloshindikana mbele zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…